Unganishwa

Search the region

22505 stories

National · Issa Michuzi

SH.90M ZATENGWA KUWAKINGA WATU WENYE UALBINO

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv SERIKALI imetenga Sh milioni 90 kwa ajili ya ununuzi wa mafuta kinga dhidi ya saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino, huku ikiagiza wadau wote kuhakikisha Mpango Kazi wa Taifa wa Haki na Ustawi wa Watu wenye Ualbino (MTHUWWU) unatekelezwa kwa vitendo na kwa wakati. Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Joy Maongezi, amesema fedha hizo zimetengwa katika mwaka wa fedha 2025/26 kwa ajili ya ununuzi wa mafuta hayo kupitia Bohari ya Dawa (MSD). Amesema tayari chupa 339 za mafuta hayo zimesambazwa katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kwa kushirikiana na wadau. Maongezi amesema Serikali pia ina wataalamu takribani 403 wa ngozi katika halmashauri pamoja na madaktari bingwa wa ngozi 98 katika hospitali za kanda na rufaa za mikoa. Akizungumza leo, Septemba 28, 2026, wakati akifungua Jukwaa la Kitaifa la Uratibu na Utekelezaji wa MTHUWWU jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu), Profesa Palamagamba Kabudi, amesema hatua hizo zinapaswa kuambatana na utekelezaji wa mpango huo katika maeneo yote yanayohusu haki na ustawi wa watu wenye ualbino. Kabudi amesema Serikali na wadau wana wajibu kuhakikisha mpango huo hautabaki kwenye nyaraka, bali utekelezwe kwa vitendo, ukipewa rasilimali na kutekelezwa kwa wakati. “Ni muhimu kuweka mipango madhubuti ya utekelezaji wa mpango na kuhakikisha kuwa mikakati na afua zilizoainishwa katika mpango zinapatiwa rasilimali na kutekelezwa kwa wakati,” amesema. Amesema shughuli zilizopangwa zinapaswa kutekelezwa na taarifa zake kutolewa kwa wakati ili kuwezesha Serikali na wadau kufuatilia maendeleo, kubaini changamoto, kupima matokeo na kuchukua hatua za kuboresha utekelezaji. Kabudi amesema mpango huo una nguzo nne ambazo ni ulinzi, kinga, usawa na kutobagua pamoja na uwajibikaji, huku mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ukitakiwa kufanya kazi kuanzia ngazi ya Taifa hadi Mkoa, Halmashauri, kata, kijiji na mtaa. Amesema jukwaa hilo la siku tatu linapaswa kwenda zaidi ya kutathmini yaliyofanyika, bali kubaini mambo yanayotakiwa kutekelezwa, maeneo yenye upungufu na hatua mahsusi za kuziba mapengo hayo. Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Watu Wenye Ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wambura Kizito, amesema sasa ni wakati wa kutoka katika hatua ya kuwa na mpango kazi na kuingia kwenye utekelezaji unaopimika, unaoratibiwa na wenye uwajibikaji. Amesema masuala ya watu wenye ualbino ni mtambuka na hayawezi kutekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu au taasisi moja pekee, bali yanahitaji ushirikiano wa sekta za afya, elimu, ajira, haki na ulinzi, ustawi wa jamii, uwezeshaji wa kiuchumi, ulinzi wa mtoto na usalama. Amesema jukwaa hilo litabaini shughuli zilizotekelezwa, zinazoendelea na ambazo hazijatekelezwa pamoja na sababu zake, taasisi zinazohusika, rasilimali zinazohitajika na changamoto zinazokwamisha utekelezaji. Mwenyekiti wa Jukwaa la Kitaifa la Uratibu na Utekelezaji wa MTHUWWU, Yohana Sali, amesema jukwaa hilo litatoa nafasi kwa Serikali na wadau kujadili mafanikio, changamoto, fursa na vipaumbele vya utekelezaji wa mpango huo. Amesema siku ya kwanza itajikita katika kujenga uelewa wa pamoja kuhusu mpango huo, historia yake, maudhui na hali ya utekelezaji, huku siku ya tatu ikijikita katika uratibu, masuala mtambuka na maandalizi ya mpango wa utekelezaji. Kabudi amesema Serikali pia inaendelea kuboresha mifumo ya taarifa za watu wenye ulemavu hadi ngazi ya kijiji na mtaa. Amesema kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Tanzania Bara ina watu wenye ualbino 71,631, wakiwemo wanaume 41,203 na wanawake 30,428. Amesema taarifa hizo zinaisaidia Serikali kufahamu idadi na maeneo wanakoishi watu wenye ualbino ili kupanga huduma kwa kuzingatia mazingira na mahitaji yao.

Mon, 28 Sep 2026 17:13:52 +0000
National · Issa Michuzi

MANYARA YAJIPANGA KUKABILIANA NA MADHARA YA EI NINO

Na Mwandishi Wetu-Manyara Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Martine Shigela leo Septemba 28, 2026 ameongoza Kikao Kazi cha Kujadili Utekelezaji wa Maelekezo yaliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu) kwa Mikoa kuhusu Kujiandaa na Kukabiliana na Madhara ya El Niño. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa Manyara kikiwa na lengo la kutathmini na kufuatilia kiwango cha utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa kwa mikoa pamoja na kuimarisha utayari na uwezo wa mkoa katika kujiandaa kukabiliana na madhara yanayoweza kusababishwa na hali ya El Niño. Akizungumza katika kikao hicho kwa niaba ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa (Sehemu ya Utafiti) kutoka ofisi hiyo Bw. Vonyvaco Luvanda amesema, Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu-SBUU ilitoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Kamati za Usimamizi wa Maafa katika ngazi zote kushirikiana na wadau waliopo katika maeneo yao kuchukua hatua za kujiandaa na El Nino ili kuzuia au kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza na hivyo kuokoa maisha na mali. Akieleza kuhusu baadhi ya maelekezo hayo Bw. Luvanda amebainisha kuwa, “Wizara, Taasisi, Mikoa na wadau wengine wanaohusika na miundombinu wafanye ukaguzi wa miundombinu muhimu na kuhakikisha inaimarishwa na kusafishwa ikiwemo madaraja, makalvati na mitaro, hali itakayosaidia upatikanaji wa huduma muhimu kabla, wakati na hata baada ya maafa kutokea ikiwemo usafirishaji, maji na umeme” Aidha, Bw. Luvanda ametoa rai kwa Kamati za Usimamizi wa Maafa kuhimiza wananchi kuendelea kufuatilia taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa kila siku lakini pia kutoa taarifa mbalimbali kwa kina kupitia vyombo vya habari vya jamii ili kuchukua hatua stahiki. Katika kikao hicho taarifa ya jumla ya mkoa na taarifa za kisekta kutoka (TMA, TANROADS, TARURA, TANESCO, RUWASA Mamlaka za Bonde, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji) kuhusu hatua za utekelezaji ziliwasilishwa ili kujua hatua zilizochukuliwa na zinazotarajiwa kuchukuliwa kabla, wakati na baada ya maafa kutokea ambapo kila taasisi imejipanga ipasavyo katika kukabiliana na madhara hayo. Mbali na hayo Bw. Luvanda amemkabidhi Mkuu wa Mkoa vitendea kazi ikiwemo Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya El Nino, vipeperushi vya kujiandaa na El Nino vya kawaida na vya Wenye Ulemavu.

Mon, 28 Sep 2026 17:13:59 +0000
Uncategorized · DW Afrique

Nix : du rap à l'empire créatif

Read the full report from the original source.

Recently
National · The Star Kenya

Court declines to stop Lamu refinery launch The applicants had sought orders stopping the planned groundbreaking and development of the refinery

The applicants had sought orders stopping the planned groundbreaking and development of the refinery

Recently
Uncategorized · DW Afrique

DW Fact-checking : reconnaître la propagande

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Court allows Lamu Refinery plans to proceed The applicants had sought orders stopping the planned groundbreaking and development of the refinery

The applicants had sought orders stopping the planned groundbreaking and development of the refinery

Recently
Uncategorized · UN News Burundi

The Takeaway: UN General Assembly debate Day 1

Read the full report from the original source.

Recently
National · Jamhuri Media

Pwani ni ‘nchi’ yenye rasilimali tatu ambazo hazipo mkoa wowote Tanzania

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UKWEPAJI KODI KWA UDANGANYIFU WA TAARIFA ZA MAGARI

Mon, 28 Sep 2026 08:00:00 +0000
National · The Star Kenya

Kalonzo visits Martha Karua to mourn her father Kalonzo shared the moment with the family as they remembered the late Mwalimu Karua

Kalonzo shared the moment with the family as they remembered the late Mwalimu Karua

Recently
National · Issa Michuzi

CP KOMBO AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA HABARI WA JESHI LA POLISI.

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Kombo Khamis Kombo amewataka Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi kuendelea kuwa nguzo imara katika kuelimisha na kuhabarisha umma kuhusu masuala ya ulinzi na usalama. Hayo amezungumza Septemba 28, 2026 wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu kwa Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi wa Makao Makuu ya Polisi, Mikoa, Vikosi na Vyuo vya Polisi katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) Moshi Mkoa wa Kilimanjaro. CP Kombo amehimiza nafasi ya Maafisa Habari katika kujenga na kuimarisha mahusiano mazuri kati ya Jeshi la Polisi na jamii, huku akiwataka kutumia taaluma yao kuhakikisha umma unapata elimu na taarifa sahihi na kwa wakati zinazohusu Jeshi la Polisi ikiwemo kazi na mafanikio. "Ninyi ni kiungo muhimu sana kati ya Jeshi la Polisi na jamii, kazi yenu sio tu kutoa taarifa bali kuwajengea uelewa wananchi kuhusu majukumu ya Jeshi la Polisi, changamoto zake, mafanikio yanayopatikana na hatua zinazochukuliwa katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao" alisema CP Kombo Naye, Kamishna wa Polisi Jamii CP Alex Mkama amesema kuwa kitengo cha habari na uhusiano ndani ya Jeshi la Polisi kimekuwa na mchango mkubwa katika kuzuia na kutanzua uhalifu kwani jamii imekuwa ikihabarishwa na kujengewa uwezo wa kubaini, kuzuia na kupambana na uhalifu kabla haujatokea katika maeneo yao. CP Mkama aliongeza kuwa, Maafisa Habari wa Mikoa wamekuwa msaada mkubwa sana kufikisha kwa umma elimu ya Polisi Jamii inayotolewa na Maafisa Polisi Jamii wa Mikoa, Wilaya na Polisi Kata na kuahidi kuendelea kushirikiana nao ili kuongeza chachu zaidi na kupata mafanikio zaidi katika kuzuia na kutanzua uhalifu. Akitoa neno la utangulizi katika hafla ya ufunguzi wa kikao kazi hicho, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime amesema kuwa Afisa Habari wa Jeshi la Polisi amekuwa ni mtu muhimu katika kuandaa na kusambaza maudhui sahihi ya kuelimisha na kutangaza mafanikio na majukumu ya Jeshi la Polisi. DCP Misime aliongeza kuwa, utendaji kazi wa Maafisa habari wa Polisi umeleta matokeo chanya katika jamii kwani wameendelea kuwa kiungo muhimu kati ya Jeshi la Polisi na wananchi, wamekuwa chachu katika uandaaji na utoaji wa taarifa kwa wakati, upigaji picha za kihabari na kuandaa maudhui ya uelimishaji jamii na kuainisha hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu nchini. Kikao kazi cha Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi nchini kimelenga kuwajengea uwezo, uelewa Maafisa habari wa Polisi na kuimarisha mahusiano mazuri kati yao na vyombo vya habari nchini katika kuhabarisha umma kwa kutumia njia za kidigitali na kujenga taswira chanya ya Jeshi la Polisi Tanzania kwa wananchi.

Mon, 28 Sep 2026 16:33:07 +0000
National · Issa Michuzi

WATANZANIA 8,408 WAUNGANISHWA NA AJIRA NJE YA NCHI

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv WATANZANIA 8,408 wameunganishwa na fursa za ajira nje ya nchi kuanzia Januari mwaka huu hadi sasa, huku jumla ya Watanzania 15,715 wakinufaika na fursa hizo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Deus Sangu, alisema Septemba 28,2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Sangu alisema Tanzania imeingia mikataba na nchi mbalimbali, zikiwemo za Ghuba, kwa ajili ya kuongeza fursa za ajira katika fani za kilimo, mifugo, udaktari, ujenzi, uhandisi, ufundi mchundo, udereva, upishi na huduma za majumbani. Alisema kwa sasa Watanzania wameanza kupata ajira za kitaalamu katika nchi za nje, zikiwemo za walimu wa vyuo vikuu, madaktari na wahandisi, tofauti na hapo nyuma ambapo wengi waliokwenda katika nchi za Kiarabu walifanya zaidi kazi za majumbani. “Hivi karibuni tutatangaza fursa za ajira kwa mainjinia 650, ma-engineer na ma-technician, ambazo ni fursa tuliyoenda kuzungumza nao wenzetu na wakatupatia hizo fursa,” alisema. Alisema kampuni kubwa ya ujenzi nchini Qatar, Holding Power, inatarajia kutoa fursa za ajira zipatazo 4,500 kwa Watanzania. Aidha, alisema Serikali imeendelea kuwaunganisha vijana na fursa katika nchi za Ulaya, zikiwemo Poland, Sweden, Norway na Ujerumani, huku baadhi yao wakiwa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) katika fani za kilimo na mifugo. Sangu alisema Serikali imeweka mifumo ya kuhakikisha vijana wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi wanalindwa dhidi ya changamoto zilizokuwa zikijitokeza hapo nyuma, ikiwemo unyanyasaji na kunyang’anywa pasipoti. Alisema kwa sasa hakuna wakala binafsi anayeweza kumkusanyisha mfanyakazi kwenda kufanya kazi nje ya nchi bila kupitia mifumo ya Serikali. “Tumehakikisha kwamba wote wanaoenda kufanya kazi nje ya nchi wanapewa mikataba, na mikataba hiyo itakuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano,” alisema. Alisema mikataba hiyo inalenga kulinda haki za wafanyakazi, ikiwemo kuhakikisha ujira na kiwango cha malipo vinaendana na kazi anayokwenda kufanya mfanyakazi. Sangu alisema Serikali pia inashirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia balozi zake, huku mwajiri akitakiwa kuwa na mawasiliano na ubalozi. “Tumehakikisha kwamba balozi wetu anakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na mwajiri. Na hii imepunguza sana changamoto ya vijana wetu kunyanyaswa, kunyang’anywa paspoti, na kwa kipindi hiki kuanzia mwezi Januari mpaka sasa hatuna kesi yoyote iliyoripotiwa kwamba kuna unyanyasaji,” alisema. Alisema Serikali imeweka pia utaratibu wa kuwaaga vijana kabla hawajaondoka nchini kupitia Special Departure Day, ambapo hupewa maelekezo kuhusu mazingira ya kazi na namna ya kupata msaada wanapokutana na changamoto. Aidha, Serikali imeweka kanzidata ya wafanyakazi wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi, na hakuna mfanyakazi anayekwenda kufanya kazi nje bila kupitia kanzidata hiyo. Sangu alisema fursa nyingine zipo kwa manesi kutoka Saudi Arabia, huku Qatar ikitarajiwa kutoa nafasi nyingine kwa manesi zitakazotangazwa hivi karibuni. “Fursa za nje zikipatikana ni jukumu letu Serikali kupitia Wizara ya Kazi na Ajira kuhakikisha tunawalinda vijana wetu na kuwaunganisha na fursa za ajira,” alisema.

Mon, 28 Sep 2026 16:33:11 +0000
National · The Observer Uganda

Activist Aloikin charged, remanded over using another person’s SIM card

27-year-old human rights activist and lawyer Aloikin Praise Opoloje has been remanded to Luzira Prison by the Buganda Road Chief Magistrate’s court on charges of…

Recently
World · DW Rwanda

Why diesel prices are soaring and what it means for Europe

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Seoul summons Ukraine envoy over prisoner-of-war row President Lee Jae Myung called the disclosure "greatly disappointing"

President Lee Jae Myung called the disclosure "greatly disappointing"

Recently
Uncategorized · Jamhuri Media

Rais Mwinyi akagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya mji wa michezo Zanzibar

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

TASAC: Sensa ya Vyombo vya Majini Kusaidia Mipango Endelevu ya Sekta

Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa Shirika hilo Nahson Sigalla wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) akifungua mafunzo kwa mawakala wa Sensa ya Vyombo vya Majini yaliyofanyika mjini Bagamoyo. Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo kwa ajili ya kuendesha Sensa ya Vyombo vya Majini Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema kufanyika kwa Sensa ya Vyombo vya Usafiri Majini kutaiwezesha Serikali na wadau wa sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji kupanga mipango endelevu ya maendeleo ya sekta hiyo. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa TASAC, Nahson Sigalla, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya Vyombo vya Usafiri Majini inayofanyika nchini kote. Sigalla amesema Sensa iliyofanyika mwaka 2021 ilikuwa na mafanikio, ambapo jumla ya vyombo 52,800 vya usafiri majini vilibainika, huku Sensa ya mwaka 2026 ikilenga kutoa hali halisi ya idadi na mwenendo wa vyombo hivyo nchini. Amesema taarifa zitakazopatikana kupitia sensa hiyo zitasaidia Serikali kupata picha ya mahitaji ya sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji na kuweka mikakati inayolenga kutekeleza dhamira ya Serikali ya kukuza uchumi wa buluu. “Sensa hii itatoa picha halisi ya hali ya vyombo vya usafiri majini na mahitaji yaliyopo katika sekta, jambo litakalosaidia Serikali na wadau kupanga mipango inayokidhi mahitaji hayo,” amesema Sigalla. Ameongeza kuwa, mbali na kuhesabu vyombo vya usafiri majini, TASAC inalenga kukusanya taarifa kuhusu maeneo muhimu yanayohusika na ujenzi wa vyombo hivyo, ikiwa ni pamoja na kubaini idadi ya wataalamu wanaohusika na uzalishaji wake. Kwa mujibu wa Sigalla, taarifa hizo zitasaidia kuhakikisha vyombo vinavyozalishwa vinazingatia viwango vinavyotakiwa vya usalama na mahitaji ya sekta ya usafirishaji majini. Amesema Sensa hiyo pia itasaidia kutoa picha ya hatua iliyofikiwa kuelekea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 katika sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji. Mshiriki wa Mafunzo hayo Afisa Uvuvi Mkoa wa Lindi, Abdallah Kawambwa, amesema alishiriki Sensa ya Vyombo vya Usafiri Majini iliyofanyika mwaka 2021 na kwamba zoezi la mwaka 2026 linatarajiwa kuwa na ufanisi zaidi kutokana na maboresho yaliyofanyika na changamoto zilizobainika katika zoezi lililopita. Baadhi ya maafisa kutoka sekta ya uvuvi walioshiriki mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yatawawezesha kutekeleza zoezi la sensa kwa weledi na usahihi, hatua ambayo itasaidia kuboresha huduma kwa jamii. Mafunzo hayo yamewakutanisha wataalamu kutoka taasisi na idara mbalimbali, zikiwemo Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), sekta ya Uvuvi na Mifugo, TASAC pamoja na Ofisi ya Rais–Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Picha za makundi za matukio mbalimbali ya Mgeni rasmi na washiriki wa mafunzo wataondesha Sensa ya Vyombo vya Usafiri majini.

Mon, 28 Sep 2026 16:20:00 +0000
Uncategorized · Capital FM

Kilifi pastor jailed 30 years for defiling 15-year-old cousin

Latest · NATIONAL NEWS

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

15 countries with lowest average meal prices The cost to eat out

The cost to eat out

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

RAIS DKT. MWINYI AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MJI WA MICHEZO ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 28 Septemba 2026, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mji wa Michezo Zanzibar (AFCON), Fumba, Wilaya ya Magharibi “B”, Unguja. Rais Dkt. Mwinyi amekagua miundombinu mbalimbali ikiwemo uwanja wa mpira wa miguu, viwanja vya mazoezi, mabwawa ya kuogelea na Diving Pool, Fan Zone yenye uwezo wa watu 4,000, pamoja na bandari kwa ajili ya boti ndogo na kubwa. Awamu ya kwanza ya mradi inatarajiwa kukamilika Desemba 31, 2026, ikiwa ni hatua muhimu kuelekea Zanzibar kuwa miongoni mwa wenyeji wa mashindano ya AFCON.

Mon, 28 Sep 2026 16:11:25 +0000

Page 1000 of 1126 · 22505 stories