Unganishwa

Search the region

22505 stories

Uncategorized · Issa Michuzi

MWENYEKITI CCM KIBAHA MJINI ATOA TAHADHARI YA MVUA ZA EL-NINO

Na Victor Masangu, Kibaha MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini, Mwalimu Mwajuma Nyamka, amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa na mabalozi kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya mvua kubwa za El-Nino zinazotarajiwa kunyesha katika baadhi ya maeneo nchini. Mwalimu Nyamka amewataka viongozi hao kuhakikisha wananchi wanaacha tabia ya kutupa taka hovyo na badala yake kushiriki katika usafi wa mazingira, ikiwemo kusafisha mifereji na kuzibua mitaro ili kuepusha maji kukwama na kusababisha mafuriko. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maandalizi ya mvua hizo, Mwenyekiti Nyamka amesema CCM Wilaya ya Kibaha Mjini imekutana na viongozi mbalimbali, wakiwemo wenyeviti wa serikali za mitaa na mabalozi, kwa lengo la kuweka mipango na mikakati ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza. “Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) hivi karibuni ilitoa taarifa kuhusu mvua hizi kubwa za El-Nino. Sisi kama chama tukaona ni vema tukutane na viongozi wetu kuanzia ngazi za chini ili kupeana maelekezo na majukumu yanayopaswa kufanyika katika kipindi hiki,” amesema. Amesema viongozi hao wamehimizwa kuwasisitiza wananchi kutotupa taka hovyo, kuzibua mitaro na kusafisha mifereji ili kuhakikisha maji ya mvua yanapita kwa urahisi na kupunguza uwezekano wa kutokea kwa mafuriko. Mwenyekiti Nyamka amesema taarifa iliyotolewa na TMA imepokelewa kwa tahadhari kubwa na kwamba CCM pamoja na Halmashauri ya Mji wa Kibaha wamezingatia maelekezo yanayotolewa na mamlaka husika ili kuhakikisha wananchi wanajiandaa mapema na kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo. Aidha, amewataka wananchi kuacha tabia ya kutupa taka hovyo na kusisitiza kuwa watakaobainika kukiuka taratibu za usafi wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ili kuwa fundisho kwa wengine. Katika hatua nyingine, Mwenyekiti Nyamka amezitaka mamlaka zinazohusika, ikiwemo Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kuhakikisha zinachukua hatua za mapema kukarabati madaraja na makalavati yaliyo katika hali hatarishi. Amesema hatua hiyo ni muhimu hasa katika maeneo yanayokumbwa na changamoto wakati wa mvua, ikiwemo Kata za Muheza, Mwanalugali na maeneo mengine yenye changamoto ya miundombinu. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kuhusu uwezekano wa kunyesha kwa mvua kubwa katika baadhi ya maeneo nchini, hali ambayo inawataka wananchi na mamlaka husika kuchukua hatua za mapema ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza, ikiwemo mafuriko.

Mon, 28 Sep 2026 16:13:45 +0000
Uncategorized · Daily News

TZ tourism firm brings Tesla, drives green tourism

MOSHI: TANZANIAN tour operator Altezza Travel has bought a Tesla electric vehicle as it steps up efforts to reduce the…

Recently
Uncategorized · SoftPower News

Chinese phone maker Xiaomi launches REDMI Note 17 series

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

'My record as MP proves I can run Nairobi,' Babu Owino defends bid to unseat Governor Sakaja

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

DKT. MWIGULU ATEMBELEA MAKTABA YA TAIFA YA QATAR

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Jumapili, Septemba 27, 2026, ametembelea Maktaba ya Taifa ya Qatar (Qatar National Library) jijini Doha, Qatar. Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu amepokelewa na Rais wa Maktaba hiyo, Dkt. Mohamed Bin Ahmed Bin Twar Al Kuwari, na kupata fursa ya kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo katika kuhifadhi, kukuza na kuwezesha upatikanaji wa maarifa na urithi wa kiutamaduni. Ziara hiyo ni sehemu ya ratiba ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akiwa nchini Qatar kwa ziara ya kikazi.

Mon, 28 Sep 2026 16:07:29 +0000
Health · Issa Michuzi

Jamii Yahimizwa Kupima Seli Mundu Kabla ya Ndoa

Dkt. Yonazi Charles, Mkurugenzi Mtendaji wa Masaki Wellspring Hub, ambao ni waandaaji wa Masaki Health Expo ( wa nne kushoto mwenye miwani) akiongea na baadhi ya wadau muhimu katika maonesho hayo yaliyofanyika Masaki, jijini Dar es Salaam Mmoja wa wananchi akifanyiwa vipimo wakati wa maonesho ya Afya ya Masaki ( Masaki Health Expo 2026) katika jitihada za kupambana na ugonjwa wa Seli Mundu Na Mwandishi Wetu JAMII imetakiwa kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara, ikiwemo kupima ugonjwa wa seli mundu (sickle cell), huku vijana wakihimizwa kupima vinasaba vya ugonjwa huo kabla ya kuingia kwenye ndoa ili kupunguza uwezekano wa kupata watoto wanaozaliwa na ugonjwa huo. Akizungumza jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa matembezi na maonesho yaliyolenga kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa seli mundu, Mratibu wa Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza mkoani humo, Dkt. Living Dennis Nyaki, amesema seli mundu ni ugonjwa wa kurithi unaoweza kumpata mtoto pale wazazi wote wawili wanapokuwa na vinasaba vinavyosababisha ugonjwa huo. Dkt. Nyaki amesema vijana wanapaswa kupima na kufahamu hali zao za vinasaba kabla ya kuingia kwenye ndoa, ili waweze kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya na uzazi. Pia amesisitiza umuhimu wa kuwapeleka watoto kupima ili kutambua hali zao mapema na kuwawezesha kupata huduma stahiki. “Ni muhimu vijana kupima kabla ya kuingia kwenye ndoa ili kujua kama wana vinasaba vya seli mundu. Hii itasaidia kuongeza uelewa na kuchukua hatua sahihi za kiafya kabla ya kupata watoto,” amesema. Aidha, Dkt. Nyaki ameitaka jamii kubadili mfumo wa maisha ili kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa kufanya mazoezi mara kwa mara, kuzingatia ulaji salama na kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Masaki Wellspring Hub, Dkt. Yonazi Charles Senkondo, ambao ni waandaaji wa matembezi na maonesho hayo kwa kushirikiana na Ruge Mutahaba Foundation, amesema shughuli hiyo imelenga kuhamasisha jamii kuwa na uelewa kuhusu seli mundu na umuhimu wa kupima, sambamba na kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi na ugonjwa huo. Naye Dkt. RhobiJeremiah Zakaria kutoka Ruge Mutahaba Foundation amesema inakadiriwa kuwa kati ya watoto 11,000 na 14,000 huzaliwa kila mwaka wakiwa na ugonjwa wa seli mundu, akisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za mapema kupitia elimu na upimaji. Katika kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kupima, Balozi wa Seli Mundu na Miss Universe Tanzania 2026, Queen Elizabeth, amesema kuwa yeye anaishi na changamoto hiyo na ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kupima afya na kufahamu hali zao za vinasaba kabla ya kuingia kwenye mahusiano na ndoa. “Mimi ni mama wa mtoto mwenye changamoto hiyo, hivyo ni ugonjwa ambao nimekuwa nikiishi nao. Naiasa jamii kuwa na utamaduni wa kupima afya na kujua vinasaba vyetu tunapokutana na wenza wetu. Ni muhimu kupima,” amesema. Queen Elizabeth amesema ugonjwa wa seli mundu unaweza kuwa na gharama kubwa za matibabu, akieleza kuwa baadhi ya matibabu yanaweza kugharimu kiasi kikubwa ambacho familia nyingi haziwezi kumudu. Amesema Serikali inatoa huduma ya upandikizaji wa uboho katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, lakini gharama ya huduma hiyo, inayokadiriwa kufikia takribani Sh milioni 75, bado ni changamoto kwa watu wengi, huku akieleza kuwa ni watu wachache tu wameweza kupata huduma hiyo hadi sasa. “Katika uhalisia wa maisha ya kawaida, kwa Watanzania zaidi ya milioni 60, watu wengi hawawezi kumudu gharama hizi. Hivyo ni muhimu kupima mapema ili ujue kama unabeba kinasaba na kuchukua hatua ili kuzuia mtoto kuzaliwa akiwa na ugonjwa huo,” amesema. Queen Elizabeth ameipongeza Wellspring Hub Masaki Health Expo kwa kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchukua hatua za mapema dhidi ya seli mundu, huku akiwataka Watanzania kuendelea kupima afya zao na kuchukua hatua stahiki. Hii ni mara ya tatu kwa Masaki Health Expo kuandaa uko hilo ili kuongeza uelewa , kuima na ktoa ushauri juu ya magonjwa yasiyoambukiza Wadau waliounga mkono tukio hilo mwaka huu ni pamoja na Kanisa la Waadventista wa Sabato Masaki, Elveth Group, Choplife Foundation na Fortune Management Consulting.

Mon, 28 Sep 2026 16:09:52 +0000
Uncategorized · Burundi Forum

18 officiers Zambiens en visite d’échange au Burundi

Bujumbura, 28 septembre 2026 — Une délégation de 18 officiers de l’École supérieure de commandement et d’état-major de Zambie séjourne au Burundi depuis le 27 septembre et ce, jusqu’au 2 octobre 2026. Cette visite s’inscrit dans le cadre du programme d’échange d’expériences...

Mon, 28 Sep 2026 16:07:05 +0000
Uncategorized · SoftPower News

Hoima Emyooga Beneficiaries Link Clean Environment to Health, Wealth

Read the full report from the original source.

Recently
National · Jamhuri Media

Makamu wa Rais aagiza milango ifunguliwe kwa vijana 10,000

Read the full report from the original source.

Recently
Sports · Issa Michuzi

Ubelgiji, Ufaransa Kukipiga Uefa Nations League

KARIBU Meridianbet ambapo Kipindi hiki ambacho timu za taifa kutoka maeneo mbalimbali duniani zipo kwenye majukumu yao, kuna michezo mikubwa inayosubiriwa na mashabiki, ikiwemo UEFA Nations League, mechi za kufuzu AFCON 2027 na michezo mingine ya kimataifa Bila kusahau Odds kubwa na machaguzi kibao kwenyekila mchezo. Timu ya Taifa ya Ubelgiji itakuwa mwenyeji wa Ufaransa katika mchezo wa UEFA Nations League 2026/27 , utakaochezwa usiku wa leo Jumatatu, Septemba 28, 2026, katika Uwanja wa King Baudouin, Brussels. Mchezo huo wa Kundi A1 utaanza kutimua vumbi saa 21:45 usiku. Ubelgiji inaingia kwenye mchezo huo ikiwa imepangwa pamoja na Ufaransa, Italia na Türkiye katika Kundi A1. Timu hiyo chini ya kocha Mark van Bommel imejumuisha nyota kadhaa wenye uzoefu, akiwemo Kevin De Bruyne, Romelu Lukaku, Youri Tielemans, Leandro Trossard na Lois Openda . Kwa upande wa Ufaransa, mchezo huo utakuwa sehemu ya mwanzo wa enzi mpya chini ya kocha Zinedine Zidane, ambaye amechukua nafasi ya Didier Deschamps. Zidane ameendelea kumtegemea Kylian Mbappé kama nahodha, huku kikosi kikiwa na wachezaji mbalimbali kama Ousmane Dembélé, Michael Olise, Eduardo Camavinga na Ibrahima Konaté . Ufaransa inaanza kampeni yake kwa mchezo dhidi ya Türkiye Septemba 25, kabla ya kusafiri kwenda Brussels kukutana na Ubelgiji siku tatu baadaye. Kwa Ubelgiji, mchezo huo pia ni wa pili kwenye ratiba ya kundi hilo baada ya kuanza kampeni dhidi ya Italia Septemba 25. Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa wachezaji kutoka pande zote mbili. Ubelgiji itakuwa na faida ya kucheza nyumbani mbele ya mashabiki wake, wakati Ufaransa itatafuta kuonyesha uwezo wake chini ya Zidane katika moja ya michezo yake ya kwanza kwenye mashindano haya. Kwa ujumla, Ubelgiji na Ufaransa zinakutana katika kipindi muhimu cha hatua ya ligi ya Nations League , huku kila timu ikihitaji matokeo mazuri ili kujiweka katika nafasi nzuri ndani ya Kundi A1. Macho yatakuwa pia kwa Mbappé, De Bruyne na nyota wengine wakubwa ambao wanaweza kuwa na ushawishi mkubwa katika mchezo huo.

Mon, 28 Sep 2026 03:54:00 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

BoT YAWATAKA WANAOTAKA KUANZISHA TAASISI NDOGO ZA FEDHA KUFUATA SHERIA

Mkoa wa Geita ukiwa ni miongoni mwa maeneo yenye shughuli kubwa za madini nchini, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeeleza kuwa uwepo wa shughuli hizo unaendana na mzunguko mkubwa wa fedha, hivyo ni muhimu kwa wananchi na watoa huduma za fedha kuhakikisha fedha hizo zinawekwa na kuzunguka kupitia mifumo na taasisi za fedha zilizo salama na zinazotambuliwa kisheria. Akizungumza na Michuzi TV Septemba 28, 2026 katika mwendelezo wa Maonesho ya 9 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, Afisa Mkuu Mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Mwile Kauzeli, amesema mtu anayetaka kufanya shughuli za huduma ndogo za fedha anapaswa kufika Benki Kuu kwa ajili ya kupata maelekezo na kutimiza utaratibu wa kupata leseni. Amesema mwombaji wa leseni anatakiwa kuwa na namba ya mlipa kodi TIN, Tax Clearance, jina la biashara lililosajiliwa BRELA lenye kuhusisha shughuli za microfinance, finance, credit au microcredit, pamoja na mtaji wa kuanzia wa Shilingi milioni 20. Kauzeli amesema mwombaji anatakiwa pia kuwasilisha ushahidi wa chanzo cha mtaji huo, picha mbili za passport size, NIDA au cheti cha kuzaliwa, CV pamoja na Credit Reference Report, kabla ya kuwasilisha maombi ya leseni kwa Gavana wa Benki Kuu Amesema kufanya shughuli za huduma ndogo za fedha bila leseni ni kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha Na. 16, hivyo wananchi wanaofanya shughuli hizo wanapaswa kuhakikisha wanapata leseni kabla ya kuanza kutoa huduma. Kwa upande mwingine, Kauzeli amewataka wananchi kutoa taarifa kwa Benki Kuu endapo watabaini taasisi inayofanya shughuli za huduma ndogo za fedha bila kuwa na leseni, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa. Amesema Benki Kuu imeweka orodha ya taasisi zilizopewa leseni kwenye tovuti yake, pamoja na taarifa za Mabenki, taasisi ndogo za fedha, ili wananchi waweze kupata taarifa hizo. Kwa mujibu wa Kauzeli, hadi Septemba 25, 2026, Benki Kuu ya Tanzania imesajili jumla ya leseni 3,355 za taasisi ndogo za fedha. Aidha, amewakaribisha wananchi wanaofika kwenye Maonesho ya 9 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita kutembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania ili kupata elimu na maelekezo kuhusu huduma za fedha na masuala mbalimbali yanayosimamiwa na Benki Kuu.

Mon, 28 Sep 2026 16:03:15 +0000
Uncategorized · Capital FM

County billions: Tracking the journey from allocation to service delivery

Latest · Business

Recently
Science · Issa Michuzi

Planet Power Slots Kukupeleka Angani Kufuata Mkwanja

KAMA bado umekaa magetoni ukisubiri bahati ikufuate yenyewe, basi huenda safari ya kuitafuta ikaanza sasa kupitia Planet Power Slots, mchezo mpya unaopatikana Meridianbet kasino . Hapa si suala la kukaa tu na kusubiri mambo yaje, bali ni kuingia kwenye safari yenye burudani ya kipekee, huku kila raundi ikibeba msisimko wa kile kinachoweza kutokea sekunde inayofuata. Planet Power Slots imebuniwa kwa mandhari ya anga za mbali, ikichanganya burudani na mazingira yanayokuweka kwenye hali ya kuendelea kutazama kila kinachoendelea kwenye skrini. Mchezo huu kutoka Expanse Studios umejengwa kwa picha zenye mvuto mkubwa, huku sayari zinazong'aa zikitoa hisia kama uko ndani ya misheni maalumu ya kutafuta utajiri katikati ya anga. Kila unapocheza, mwonekano wake unakufanya ufuatilie hatua kwa hatua huku ukisubiri kuona kama raundi inayofuata italeta tukio kubwa. Ni safari ambayo haishii kwenye muonekano pekee, kwa sababu kila hatua inaweza kuleta jambo jipya na kuongeza hamasa ya kuendelea na mchezo. Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Kinachoongeza ladha zaidi ni uwepo wa vizidishi vinavyoweza kufika hadi mara 1000, jambo linalofanya kila raundi kuwa na msisimko wake. Kwa dau linalochezwa, uwepo wa kizidishi kikubwa unaweza kubadilisha kabisa thamani ya ushindi unaoweza kupatikana. Hapo ndipo Planet Power Slots inapoanza kuonyesha sura yake nyingine, kwa sababu haujui ni wakati gani raundi inaweza kukuletea kizidishi kitakachofanya safari yako ya anga kuwa tamu zaidi. Lakini safari haishii hapo, kwani Planet Power Slots pia ina bonasi zinazoweza kukupa nafasi zaidi za kuendelea kucheza bila kuongeza dau jipya katika kila hatua. Hii inaifanya kila raundi kuwa na matarajio mapya, huku wachezaji wakisubiri kuona kama bonasi nyingine itafunguka. Kadri mchezo unavyoendelea, ndivyo hamasa inavyopanda, hasa unapokuwa ukifuatilia alama na matukio yanayoweza kukusogeza karibu na zawadi kubwa. Na sasa, macho yote yaelekezwe kwenye sayari ya njano. Ikionekana, ni ishara kwamba mchezo unaweza kuingia kwenye hatua yenye bonasi na kusogeza jackpot karibu zaidi. Hapo ndipo msisimko unapopanda na kila kinachotokea kwenye skrini kinakuwa na uzito wake. Planet Power Slots inakusubiri Meridianbet , ikiwa na safari ya anga iliyojaa burudani, bonasi na nafasi za ushindi.

Mon, 28 Sep 2026 04:00:00 +0000
Uncategorized · BBC Rwanda

Umucamanza wo mu Bwongereza yategetse ushinjwa jenoside yo mu Rwanda kuriha £100,000 y'ingwate kugira ngo arekurwe by'agateganyo

Brown ashinjwa "kwica, kuyobora cyangwa gushishikariza" impfu z'Abatutsi mu Rwanda. Ahakana avuga ko nta cyaha yakoze.

Recently
Uncategorized · Capital FM

African Marketers Conference to Explore AI’s Growing Role in Marketing

Latest · NATIONAL NEWS

Recently
Uncategorized · Capital FM

Samsung Galaxy S26 FE Launch: The “Fan Edition”

Latest · Editors Pick

Recently
Business · Jamhuri Media

Tanzania yafungua milango kwa uwekezaji wa madini ya kimkakati, yalenga kujenga viwanda badals ya kuuza malighafi

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

TRAMEPRO YATOA WITO WA KULINDA UADILIFU WA TAARIFA KWA AJILI YA UMOJA, AMANI NA MAENDELEO

Dar es Salaam, Septemba 28, 2026 — Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania (TRAMEPRO) limetoa wito kwa wananchi, viongozi, waandishi wa habari na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuhakikisha wanahakiki taarifa kabla ya kuzisambaza, likisisitiza kuwa taarifa sahihi ni msingi wa kujenga umoja, amani na maendeleo ya Taifa. Wito huo umetolewa leo, Septemba 28, 2026, wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa (International Day for Universal Access to Information). TRAMEPRO imesema maadhimisho hayo yanapaswa kuwa fursa ya kutafakari umuhimu wa wananchi kupata taarifa sahihi, za kuaminika, kwa wakati na zinazoweza kufikiwa, sambamba na wajibu wa kila mmoja kuzihakiki na kuzitumia kwa uadilifu. TRAMEPRO imesema maendeleo ya teknolojia za kidijitali, mitandao ya kijamii na zana za akili bandia yameongeza kasi ya uzalishaji na usambazaji wa taarifa, hivyo kuna umuhimu wa kujenga utamaduni wa kuhakiki taarifa kabla ya kuzisambaza. Kwa mujibu wa shirika hilo, taarifa sahihi zina nafasi muhimu katika kujenga uelewa, kuimarisha uwajibikaji, kulinda afya ya jamii, kuhifadhi mazingira na kuimarisha umoja, amani na mshikamano wa Taifa. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inalenga “Kulinda Uadilifu wa Taarifa katika Enzi ya Kidijitali: Nafasi ya Upatikanaji wa Taarifa katika Kukabiliana na Mkanganyiko wa Taarifa.” Wito kwa Waandishi wa Habari TRAMEPRO imewasihi waandishi wa habari kuendelea kuzingatia weledi, maadili na ukweli katika utekelezaji wa majukumu yao, huku wakifanya uhakiki wa taarifa kabla ya kuzichapisha. Shirika hilo limesema vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kujenga uelewa wa jamii na kutoa taarifa zinazoweza kusaidia kuimarisha umoja, amani na mshikamano. Aidha, limewataka viongozi na taasisi za umma kutoa taarifa kwa wananchi kwa uwazi, usahihi, kwa wakati na kwa lugha inayoeleweka. Shirika hilo pia limeonya kuhusu taarifa zisizo sahihi zinazohusu afya, dawa na tiba, likisisitiza kuwa taarifa hizo zinaweza kuwa na madhara kwa afya na maisha ya wananchi. Changamoto nyingine zilizotajwa ni pamoja na upatikanaji usio sawa wa teknolojia, gharama za intaneti, ujuzi mdogo wa kidijitali na changamoto ya kutambua maudhui yaliyotengenezwa au kubadilishwa kwa kutumia teknolojia za akili bandia. TRAMEPRO imewataka wananchi na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa na utamaduni wa kuhakiki taarifa kabla ya kuzisambaza, ili kuzuia taarifa zisizo sahihi kuwa chanzo cha hofu, migawanyiko au madhara kwa jamii. Shirika hilo pia limewataka wataalamu wa tiba asili kuzingatia usalama, ushahidi, maadili na uwajibikaji wanapotoa taarifa kuhusu dawa na tiba asili, na kuepuka madai ya kitabibu ambayo hayawezi kuthibitishwa. TRAMEPRO imesema Tanzania yenye umoja na amani inahitaji utamaduni wa mawasiliano unaoheshimu ukweli na utu wa kila mwananchi. “Taarifa sahihi hujenga uaminifu. Uaminifu hujenga uelewa. huimarisha Umoja na Amani. Kwa mujibu wa shirika hilo, taarifa sahihi zinaweza kusaidia kuelimisha jamii kuhusu afya, kumsaidia mkulima, kumlinda mtumiaji wa dawa, kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kumwezesha mwananchi kushiriki katika maendeleo ya Taifa. Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa huadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Septemba, ikiwa na lengo la kuhamasisha upatikanaji wa taarifa, uwazi, uwajibikaji na mazingira yanayomwezesha mwananchi kupata taarifa muhimu kwa maisha na maendeleo yake. Taarifa hii imetolewa na Boniventura Mwalongo, Katibu Mkuu wa Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania (TRAMEPRO).

Mon, 28 Sep 2026 15:48:31 +0000
Uncategorized · TechCabal East Africa

How Nigeria’s overlapping data rules affect fintechs and banks

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

6.4 million older Kenyans by 2045: Are systems ready? Experts says Kenya needed to prepare its systems for longer lives while ensuring older persons remain healthy

Experts says Kenya needed to prepare its systems for longer lives while ensuring older persons remain healthy

Recently

Page 1001 of 1126 · 22505 stories