Unganishwa

Search the region

22499 stories

Uncategorized · Issa Michuzi

TAARIFA YA MABADILIKO YA MAKATIBU WA CCM WA MIKOA NA SEMINA ELEKEZI

Sun, 27 Sep 2026 13:10:45 +0000
Uncategorized · The Star Kenya

Traders oppose bid to raise minimum smoking age The Kisumu traders questioned the motive of the proposal, adding that it was unclear

The Kisumu traders questioned the motive of the proposal, adding that it was unclear

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

India news: SRFTI students violently attacked in Kolkata

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Ten climbers missing after avalanche hits Himalayan base camp Poor weather has hampered rescue efforts, with rescue teams unable to reach the site

Poor weather has hampered rescue efforts, with rescue teams unable to reach the site

Recently
Business · HabariLeo

Gofu yafungua milango ya ushirikiano wa biashara

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Issa Michuzi

WAZIRI MKUU: SEKTA BINAFSI NI MUHIMU KUFIKIA UCHUMI WA DOLA TRILIONI MOJA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema ushirikishwaji wa sekta binafsi ni muhimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya Tanzania, hasa azma ya kufikisha thamani ya uchumi wa Taifa hadi dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050. Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo, Jumapili, Septemba 27, 2026, jijini Doha, Qatar, alipokutana na Makamu wa Kwanza wa Chama cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda cha Qatar (QCCI), Bw. Mohammed bin Ahmed bin Twar Al Kuwari, pamoja na ujumbe wake katika kikao kilichofanyika katika Hoteli ya Kempinski. Waziri Mkuu amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuwa akisisitiza umuhimu wa kuishirikisha sekta binafsi katika mipango ya maendeleo ya nchi, kupitia Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050. “Tunaamini kwamba Serikali peke yake haiwezi kufanikiwa katika uwekezaji huo bila kushirikisha wawekezaji wa ndani au wa nje. Ndiyo maana Serikali imeweka vivutio vya kiuwekezaji ili kuvutia mitaji,” amesema Dkt. Mwigulu. Katika kikao hicho, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya uchumi na uwekezaji, pamoja na kuainisha fursa zilizopo Tanzania na Qatar, pamoja na fursa zinazotokana na ushiriki wa nchi hizo katika jumuiya za kikanda za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Baraza la Ushirikiano la Nchi za Kiarabu za Ghuba (GCC). Aidha, kikao hicho kimekubaliana kuhusu umuhimu wa kuwakutanisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Qatar kupitia taasisi zao za uwakilishi, zikiwemo QCCI, TPSF na TCCIA, kwa lengo la kujadili kwa kina maeneo ya ushirikiano wa kimkakati, biashara na uwekezaji. Kikao hicho kiliwashirikisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga; Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe; Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji; Wabunge pamoja na watendaji wengine wa Serikali.

Sun, 27 Sep 2026 12:50:50 +0000
Uncategorized · KBC

Xi invokes centuries of China-US ties, urges new chapter in bilateral relations

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

WATCH LIVE: Governor Wanga, Nyanza leaders attend fundraising service at St. Francis Catholic Church Rangenya - Kisumu

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Issa Michuzi

VODACOM TANZANIA YAUNGANA NA VIONGOZI WA SEKTA YA BIASHARA KATIKA CEO GOLF TOURNAMENT 2026

Vodacom Tanzania plc imeendelea kutumia mchezo wa golf kama jukwaa la kuunganisha viongozi wa biashara na makampuni, watoa maamuzi na wadau wa sekta mbalimbali, kupitia ushiriki na udhamini wake katika CEO Golf Tournament 2026, iliyofanyika Septemba 26 katika viwanja vya hotel Sea Cliff Golf Course, Zanzibar. Mashindano hayo yamewakutanisha viongozi wa makampuni, maafisa watendaji wakuu (CEO’s), wanadiplomasia na wachezaji wa golf kutoka hapa nchini na mataifa mbalimbali ya Afrika ikiwemo Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, Afrika Kusini na Nigeria, huku yakishirikisha zaidi ya wachezaji 80 kutoka mataifa hayo. Wachezaji wa golf kutoka Kenya, Thomas Mwangi na Caroline Muigai, wametwaa ubingwa wa jumla kwa wanaume na wanawake mtawalia katika mashindano ya hayo yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania Plc. Mwangi alitwaa ubingwa wa jumla kwa wanaume baada ya kukusanya pointi 40, huku Muigai akiibuka kinara kwa wanawake kwa pointi 41 katika mashindano yaliyochezwa kwa mfumo wa Stableford kwenye mashimo 18. Katika Division A, Patrick O’Rourke alitwaa nafasi ya kwanza, huku Ernest Sengeu akimaliza wa pili kwa pointi 31. Thagaran Govender alishinda Division B kwa pointi 39, akifuatiwa na Gregory Eayrs aliyepata pointi 38. Katika Division C, Abbas Simkoko alitwaa ushindi kwa pointi 40, akifuatiwa na Joseph Sayi aliyepata pointi 37. Kwa upande wa wanawake, Salome Gakere alishinda kwa pointi 36, huku Vicky Elias akimaliza nafasi ya pili baada ya kufungana pointi 35 na Maryanne Mugo na kuamua kwa mfumo wa countback. Ushiriki wa Vodacom Tanzania katika mashindano hayo umeenda zaidi ya mchezo wa golf na kuwa sehemu ya namna kampuni inavyotumia majukwaa ya michezo kujenga mahusiano na jumuiya ya biashara, huku ikiunganisha teknolojia na huduma za kidijitali katika mahusiano hayo kwa lengo la kuchochea ukuaji wa biashara. Akizungumza wakati wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando, alisema kampuni hiyo inajivunia kuunga mkono mashindano yanayounganisha michezo na jamii ya wafanyabiashara. “Tunafurahi kudhamini na kushiriki mashindano ya CEO Golf Tournament kwa sababu gofu si mchezo pekee, bali ni jukwaa linalowakutanisha watu, mawazo na fursa,” alisema Kamando. Alisema mashindano hayo yanatoa mazingira rafiki kwa viongozi wa biashara kutoka sekta mbalimbali kukutana na kujenga mahusiano ya kikazi. Kamando pia alihusisha mashindano hayo na juhudi za kukuza utalii visiwani Zanzibar, akisema matukio ya kimataifa ya michezo yanaitangza Zanzibar kwa wageni ambao wanaweza kurejea kwa ajili ya utalii au shughuli za kibiashara. “Tunajivunia kushiriki katika kuitangaza Zanzibar kama kituo cha biashara, utalii na michezo. Matukio kama haya yanaongeza thamani si kwa washiriki pekee, bali pia kwa uchumi kiujumla,”alisema. Hivyo, ushiriki katika majukwaa kama CEO Golf Tournament unaipa Vodacom Tanzania nafasi ya kukutana na viongozi wanaofanya maamuzi katika sekta ya biashara, kusikiliza mahitaji yao na kuendeleza mazungumzo kuhusu namna teknolojia inavyoweza kusaidia biashara kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Kwa Vodacom Tanzania, ushiriki katika majukwaa ya golf unaendelea kuwa sehemu ya kujenga mahusiano na viongozi wa makampuni ya biashara, kubadilishana mawazo na kuendeleza fursa za ushirikiano katika dunia ya biashara inayozidi kuunganishwa na teknolojia. Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (Kulia) akikabidhi zawadi kwa mshindi wa jumla kwa upande wa wanaume Thomas Mwangi (kushoto) katika mashindano ya CEO Golf Tournament 2026, iliyofanyika Septemba 26, 2026 katika viwanja vya Sea Cliff Golf Course visiwani Zanzibar. Mashindano hayo yaliwakutanisha viongozi wa biashara, Maafisa Watendaji wakuu (CEOs), wanadiplomasia na wadau mbalimbali kutoka Tanzania na mataifa mengine ya Afrika, huku Vodacom Tanzania Plc ikiwa mdhamini mkuu wa tukio hilo lililolenga kuimarisha uhusiano, kujenga mitandao ya kibiashara na kukuza ushirikiano miongoni mwa viongozi wa sekta mbalimbali. Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando akishiriki katika mashindano ya CEO Golf Tournament, iliyofanyika Septemba 26, 2026 katika viwanja vya Sea Cliff Golf Course visiwani Zanzibar. Mashindano hayo yaliwakutanisha viongozi wa biashara, Maafisa Watendaji wakuu (CEOs), wanadiplomasia na wadau mbalimbali kutoka Tanzania na mataifa mengine ya Afrika, huku Vodacom Tanzania Plc ikiwa mdhamini mkuu wa shindano hilo lililolenga kuimarisha uhusiano, kujenga mitandao ya kibiashara na kukuza ushirikiano miongoni mwa viongozi wa sekta mbalimbali. Mkuu wa idara ya Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Business katika kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Joseph Sayi (kulia) akimkabidhi zawadi mshindi wa pili wa divisheni A katika Mashindano ya CEO Golf Tournament 2026, Ernest Sengeu (kushoto). Mashindano hayo yaliwakutanisha viongozi wa biashara, Maafisa Watendaji wakuu (CEOs), wanadiplomasia na wadau mbalimbali kutoka Tanzania na mataifa mengine ya Afrika, huku Vodacom Tanzania Plc ikiwa mdhamini mkuu wa shindano hilo lililolenga kuimarisha uhusiano, kujenga mitandao ya kibiashara na kukuza ushirikiano miongoni mwa viongozi wa sekta mbalimbali. Mkuu wa Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Business wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Joseph Sayi (kulia) akikabidhiwa zawadi na afisa masoko wa kampuni hiyo Chelsea Njau, baada ya kuibuka mshindi wa Pili wa Mashindano ya CEO Golf Tournament 2026. Mkuu wa Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Business katika kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Joseph Sayi akishiriki katika mashindano ya CEO Golf Tournament. Mashindano hayo yaliwakutanisha viongozi wa biashara, Maafisa Watendaji wakuu (CEOs), wanadiplomasia na wadau mbalimbali kutoka Tanzania na mataifa mengine ya Afrika, huku Vodacom Tanzania Plc ikiwa mdhamini mkuu wa shindano hilo lililolenga kuimarisha uhusiano, kujenga mitandao ya kibiashara na kukuza ushirikiano miongoni mwa viongozi wa sekta mbalimbali.

Sun, 27 Sep 2026 07:00:00 +0000
Uncategorized · The Standard

Lamu community sets conditions for Sh2 trillion Dangote oil refinery project

Lamu's Bajuni community leader has said that they will reject the oil refinery project if they are not fully involved, and guaranteed benefits agreed for the host community.

Sun, 27 Sep 2026 15:34:31 +0300
Uncategorized · The Star Kenya

Kaluma projects over 60% Luo vote for Ruto Kaluma projects that the four Luo Nyanza counties will register over 4 million voters

Kaluma projects that the four Luo Nyanza counties will register over 4 million voters

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

SIKU YA UTALII DUNIANI, NGORONGORO SI PAKUJA PEKE YAKO, NJOO NA MPENZI WAKO

Leo ni siku ya Utalii Duniani ambapo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inaungana na wadau wengine duniani kusherehekea sikukuu hii ikiwa imejipanga kuendeela kuhudumia watalii kwa viwango vya kimataifa na kuendelea kuwahimiza wapendanao kuja kushuhudia maajabu ya dunia katika bustani ya Eden. Kutokana na upekee wa Ngorongoro ambapo hadithi, fikra na mtazamo wako unakutana na uhalisia ukija bila mpenzi wako utapata tabu ya kumsimulia mwenzako kutokana na utakayoyaona kwani ni hifadhi iliyojaa kila aina ya vivutio ambavyo si  fahari ya Tanzania pekee bali dunia nzima Akizungumzia kuhusu maajabu ya Ngorongoro kamishna Msaidizi Mwandamizi anayesimamia huduma za utalii na Masoko Mariam Kobelo amesema kwamba Hifadhi ya Ngorongoro ni urithi uliotukuka ambao unahitaji  kulindwa kwa wivu mkubwa kwa maslahi ya vizazi vijavyo. Kobelo anaeleza kuwa katika kuadhimisha Siku ya Utalii Duniani 2026, Mamlaka inawashukuru kwa  dhati  wageni waendeshaji wa utalii, mawakala wa safari, washirika ,wawekezaji, waongoza watalii, wadau wa sekta ya utalii na jamii  kwa mchango mkubwa katika utalii. “Tunapoelekea katika mustakabali mpya wa utalii, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro inaendelea kufanya maboresho mbalimbali katika huduma za kidijitali na matumizi ya Akili Unde (Artificial Intelligence - AI) ili kuongeza ufanisi, kuboresha uzoefu wa wageni na kutoa huduma zinazokidhi viwango vya kimataifa, huku tukizingatia msingi wetu mkuu wa uhifadhi na utalii endelevu” amesisitiza kamishna Kobelo Ameongeza kuwa Ngorongoro si eneo la kutembelea tu bali ni urithi wa dunia unaopaswa kuishi kwa faida ya vizazi na vizazi kuendelea kujifunza kutokana na historia ya asili iliyofunikwa na tabasamu la uhifadhi endelevu.  Ngorongoro inathamini utamaduni wetu, tunahifadhi maliasili zote kwa kutambua kuwa maendeleo ya utalii yanaenda sambamba na wajibu wa kulinda mazingira na kuhifadhi urithi wetu kwa ajili ya vizazi vijavyo ‘Katika siku hii muhimu, ninawaalika wote kuendelea kuwa sehemu ya safari hii, Tuitembelee Ngorongoro, Tuiheshimu Ngorongoro, Tuilinde Ngorongoro, Tuiache Ngorongoro ikiwa bora kwa vizazi vya sasa na vijavyo na kuhakikisha tunaenda sambamba na kauli mbiu yam waka huu isemayo  “Ajenda ya Kidijitali na Akili Bandia Kubuni Upya Sekta ya Utalii,” Heri ya Siku ya Utalii Duniani 2026.

Sun, 27 Sep 2026 12:28:13 +0000
Business · Issa Michuzi

ZANZIBAR MAGAZINE YAZINDULIWA NEW YORK, YAANGAZIA MAONO YA MAMA MARIAM MWINYI KATIKA UCHUMI WA BULUU

Jarida la Zanzibar Magazine limezinduliwa pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA 81), jijini New York, Septemba 2026 likiwa na makala maalum inayoangazia kazi zinazofanywa na Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) pamoja na maono ya Mama Mariam Mwinyi katika kuendeleza Uchumi wa Buluu Zanzibar. Makala hiyo, inayoanzia ukurasa wa 12, inaangazia umuhimu wa kuwa na mtazamo shirikishi na jumuishi katika kuendeleza Uchumi wa Buluu, hususan katika sekta ya kilimo cha mwani, kwa kuzingatia nafasi na mchango wa wanawake na vijana. Aidha, makala hiyo inaeleza juhudi zinazofanywa na Serikali pamoja na wadau mbalimbali katika kuwawezesha wanawake na vijana kunufaika na fursa za Uchumi wa Buluu, na kuibadilisha shughuli ya kilimo cha mwani kutoka uzalishaji wa kujikimu na kuwa shughuli endelevu na yenye tija kiuchumi. Uzinduzi wa jarida hilo unaendelea kutoa fursa ya kuonesha juhudi, mafanikio na fursa zilizopo Zanzibar katika kuwawezesha wananchi, hususan wanawake na vijana, kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Uchumi wa Buluu.

Sun, 27 Sep 2026 12:22:32 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

SIKU YA UTALII DUNIANI; WONDERS ARE CALLING

Na Mwandishi wetu, Urithi Geopark Karatu Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mhe. Dkt. Lameck Karanga, ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kufuatia jitihada zinazofanywa na Mamlaka hiyo kutumia teknolojia za kidijitali kutangaza maajabu ya vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro ambapo matumizi ya teknolojia hiyo yanasaidia kuwaita watalii mbalimbali duniani. Dkt. Karanga alitoa pongezi hiyo tarehe 27 Septemba, 2026, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani yaliyofanyika katika jengo la Makumbusho ya Urithi Geopark, Wilayani Karatu mkoani Arusha yakiongozwa na kauli mbiu isemayo “ Ajenda ya Kidijitali na Akili Bandia katika Kubuni upya Utalii,” Mhe. Karanga ameongeza kuwa matumizi ya teknolojia katika utalii yamekuwa muhimu katika kuwafikia watalii kwa urahisi zaidi, hususan katika kipindi ambacho teknolojia imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku. “Tunapoadhimisha siku hii tumepata nafasi ya kujionea jinsi ambavyo Ngorongoro mnatumia teknolojia kutangaza vivutio vya utalii, pamoja na vitu vingine tumeona matumizi ya QR codes kupata taarifa za vivutio vya utalii, tumeona matumizi ya Visual reality ambayo ni jitihada kubwa ya mapinduzi ya kutangaza utalii kisasa” ,alisema Dk. Karanga Naibu Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA Joas Makwati, amebainisha kuwa Ngorongoro inaendelea kuimarisha matumizi ya teknolojia za kidijitali katika kutangaza utalii wa wanyamapori, malikale, urithi wa utamaduni, jiolojia, kuibua mazao mapya ya utalii sambamba na kuboresha huduma kwa wateja kupitia miumo wa kisasa wa malipo na kuingia na kutoka ndani ya hifadhi wa Vipenyo Smart Gates (VGS). Ngorongoro imefanya maadhimisho hayo kwa kushirikisha wadau kufanya mbio fupi (Fun Run) na michezo kwa lengo la kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za utalii na michezo, pamoja na kuelimisha kuhusu umuhimu wa utalii katika kuchochea maendeleo ya jamii.

Sun, 27 Sep 2026 12:25:26 +0000
Uncategorized · The Star Kenya

Atellah: I am bringing the fight for doctors to Lang’ata Atellah said he has spent years standing with doctors in street protests

Atellah said he has spent years standing with doctors in street protests

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Pope to bishops: Root out "scourge" of sexual abuse A 2021 inquiry found that clergy or lay members of the Church had abused about 330,000

A 2021 inquiry found that clergy or lay members of the Church had abused about 330,000

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Switzerland: Voters reject stricter view of neutrality

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Pope decries 'scourge' of sexual abuse during France visit

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

How to use contact lenses safely Thin lenses placed directly on the eyes to help improve vision

Thin lenses placed directly on the eyes to help improve vision

Recently
Uncategorized · Burundi Forum

Burundi / Économie : Bigirimana Jean publie un nouvel ouvrage sur la souveraineté économique

Après des ouvrages consacrés au développement du Burundi et à l’unité politique africaine, Bigirimana Jean consacre son troisième livre à la reconquête de la souveraineté économique. Une somme de près de 570 pages, qui va de la mémoire productive du Burundi ancien...

Sun, 27 Sep 2026 11:45:52 +0000

Page 1022 of 1125 · 22499 stories