Unganishwa

Search the region

22491 stories

Uncategorized · The Ankole Times

IT STARTED FROM A LOCAL BAR TO SËX!! Suspects Narrate How Afrigo Band Legend Moses Matovu Was Killed , What Annoyed The Killer?

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

KAZEMBE AWATAKA VIJANA KUSHIRIKI MICHEZO KULINDA AFYA

Na Victor Masangu, Kibaha MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kibaha Mjini, Ramdhani Kazembe, amewataka vijana nchini kuwa wazalendo, kudumisha amani na kuachana na tabia ya kukaa vijiweni, badala yake wajitokeze kushiriki kikamilifu katika michezo na mazoezi kwa ajili ya kujenga afya zao. Kazembe ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Bonanza la Tangini Season One, lililofanyika Kibaha, kwa niaba ya Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Pwani, Alhaj Mussa Mansour. Amesema kushiriki katika michezo na mazoezi ni muhimu kwa vijana kwa kuwa husaidia kuimarisha afya ya mwili na akili, huku pia ikisaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa. Aidha, Kazembe amesema Alhaj Mansour ameahidi kushirikiana bega kwa bega na viongozi wa klabu za Jogging katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, ambapo amepanga kukutana nao kwa ajili ya kuweka mikakati madhubuti ya kuendeleza na kuunga mkono mchezo huo. Amesema ushirikiano huo pia utasaidia kuwawezesha vijana kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kwa ajili ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi. “Napenda kuwapongeza kwa dhati wanachama wa Tangini Jogging pamoja na vilabu vyote ambavyo vimeshiriki kikamilifu katika bonanza hili. Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Pwani amenituma kuja kumwakilisha na amesema yupo pamoja nanyi na ataendelea kushirikiana na vijana katika kuendeleza klabu za Jogging,” amesema Kazembe. Kwa upande wake, Mratibu wa Bonanza la Tangini Season One, Ally Gombati, amesema lengo la kuandaa bonanza hilo ni kuwakutanisha vilabu mbalimbali vya Jogging ili kufanya mazoezi kwa pamoja, kujenga na kuimarisha afya, sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuendeleza sekta ya michezo. Gombati amesema wameona umuhimu wa kuwaunganisha vijana kutoka maeneo mbalimbali ili kujenga misingi ya umoja na mshikamano, huku wakiwakumbusha umuhimu wa kulinda amani ya nchi na kufanya mazoezi kwa ajili ya afya zao. “Tumeamua kuandaa bonanza hili ambalo tumeliita Tangini Bonanza na tumeweza kuvishirikisha vilabu vya Jogging zaidi ya 30 kutoka maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha pamoja na maeneo mengine jirani ya Jiji la Dar es Salaam, ikiwemo E-FM Jogging, Clouds Jogging, Tangini Jogging pamoja na Jogging nyingine kutoka maeneo mbalimbali,” amesema Gombati. Nao baadhi ya wanachama wa Tangini Jogging Club wamesema bonanza hilo limewapa fursa ya kukutana na kufahamiana na watu kutoka maeneo mbalimbali, huku mazoezi hayo yakitarajiwa kuwasaidia kuimarisha afya zao na kupunguza hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa. “Kwa kweli tunapenda kutoa shukrani zetu za kipekee kwa uongozi wa Tangini kwa kuona umuhimu wa kuandaa bonanza hili ambalo limetukutanisha na wenzetu kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kibaha pamoja na Jiji la Dar es Salaam. Tumeweza kukimbia pamoja na kubadilishana mawazo mbalimbali kuhusu michezo na masuala ya maendeleo,” wamesema. Bonanza la Tangini Season One limewakutanisha wanamichezo kutoka klabu mbalimbali za Jogging za Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam, likiwa na lengo la kujenga urafiki, kudumisha umoja na mshikamano, kuimarisha afya na kujikinga na magonjwa yasiyoambukizwa.

Sat, 26 Sep 2026 16:38:16 +0000
Uncategorized · SoftPower News

She Cranes Crowned Africa Netball Champions After Beating South Africa

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

China, US agree to set up channel for AI safety incidents

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · SoftPower News

U.S. Unveils Uganda’s Roosevelt Africa Trail as First Trade Over Aid Deal

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Deux généraux de l’armée parmi les 17 victimes d’un crash aérien en RDC

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Yaga Burundi

Entreprendre au féminin au Burundi : les difficultés pour celles qui osent bousculer les codes

Manque de temps, méfiance des banques, pression familiale, voire hostilité du conjoint, entreprendre au féminin reste un parcours semé d’embûches au Burundi. Un atelier d’Enabel consacré à la dissémination de la Toolbox Entrepreneuriat Féminin a permis de mettre en lumière […] L’article Entreprendre au féminin au Burundi : les difficultés pour celles qui osent bousculer les codes est apparu en premier sur Yaga Burundi .

Sat, 26 Sep 2026 16:01:24 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

DKT. MWIGULU AIPONGEZA QATAR KWA KUTUMIA NISHATI SAFI USAFIRI WA UMMA

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba ameipongeza Serikali ya Qatar kwa kufanikiwa kuwa na matumizi makubwa ya teknolojia kwenye usafiri wa umma na hasa matumizi ya nishati safi. Ametoa pongezi hizo leo (Jumamosi, Septemba 26, 2026) jijini Doha, Qatar mara baada ya kupokea taarifa ya uendeshaji wa kampuni ya usafirishaji ya MOWASALAT kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdullah bin Mohammed Al Thani. Waziri Mkuu ambaye ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini humo, amesema ubunifu wao umesaidia kuondoa msongamano wa magari barabarani kwa sababu usafiri wa umma ni wa uhakika. "Nyumbani tunalo tatizo la msongamano wa magari na kupitia teknolojia mnazotumia, Tanzania inaweza kujifunza mbinu mlizotumia ili nasi tuweze kukabiliana nalo," amesema. Waziri amesema amefurahi kuona kampuni yao inatumia nishati safi kwa sehemu kubwa. "Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kinara wa nishati safi barani Afrika, na hii ni hatua nzuri kwetu. Tunatarajia kuwa wenyeji wa AFCON 2027, kwa hiyo itatufaa sana," amesema. Waziri Mkuu ameishukuru kampuni hiyo kwa kuwaajiri Watanzania 722 katika nafasi mbalimbali. "Ni fursa kwa vijana wetu kukuza ujuzi na kujifunza teknolojia mbalimbali." Mapema, Waziri wa Uchukuzi wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdullah bin Mohammed Al Thani alimweleza Dkt. Mwigulu kwamba kampuni hiyo inatoa huduma za usafiri wa abiria kwa kutumia mabasi, taxi, usafiri kwa wanafunzi, matukio binafsi, ya kitaifa na ya kimataifa. "Kwa mwaka 2025, kampuni yetu imetoa huduma kwa watu milioni 42. Tunayo magari 1,200 na njia za magari (routes) tulizonazo ni 128. Asilimia 70 ya magari yetu yanatumia umeme na kutokana na ubora na uhakika wa huduma zetu, tumeweza kuyatoa barabarani magari 12,363," alisema. Alisema kutokana na teknolojia walizonazo, magari yao yanakuwa yanakaguliwa kwa mfumo wa kielektroniki. Yamewekewa mfumo unaowezesha kubaini changamoto kwa haraka badala ya kusubiri kufanyiwa ukaguzi na mafundi," alisema.

Sat, 26 Sep 2026 15:57:31 +0000
Uncategorized · HabariLeo

CCM Iringa yamkabidhi Asas tuzo ya heshima

Read the full report from the original source.

Recently
National · Jamhuri Media

ACT WAZALENDO Yaiomba Serikali kukaa na Wamachinga kupata suluhu naomna upangaji wa Jiji

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Issa Michuzi

DKT MWINYI KUFUNGUA MAONYESHO YA MADINI GEITA - RC MNYETI

Na Mwandishi wetu, Geita MKUU wa Mkoa wa Geita Alexander Pastory Mnyeti amesema maonyesho ya tisa ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanatarajiwa kuzinduliwa kesho Septemba 27 mwaka 2026 na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ally Mwinyi na yanatarajiwa kufungwa Oktoba 3, mwaka 2026 na Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Lameck Nchemba. RC Mnyeti akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 26, 2026 amesema maandalizi yote yamekamilika kwa ajili ya ufunguzi na kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Madini ni Utajiri, Tuwajibike kwa Pamoja Kufikia Dira ya Taifa 2050.” Mkuu huyo wa mkoa amesema maonesho hayo yanakutanisha washiriki 765 kutoka sekta mbalimbali za umma na binafsi, wakiwamo wachimbaji, wajasiriamali, taasisi za fedha na wauzaji wa teknolojia na vifaa vya uchimbaji huku mataifa tisa yakishiriki. RC Mnyeti amesema washiriki hao wanatoka katika maeneo mbalimbali chini ya mnyororo wa thamani wa madini na sekta zinazofungamana na uchimbaji. Amesema washiriki hao ni pamoja na kampuni 15 za uchimbaji madini, taasisi 41 za umma, wajasiriamali 599, wachimbaji wadogo, vijana na watu wenye mahitaji maalum 52, taasisi saba za fedha na kampuni 11 zinazouza vifaa vya utafiti na uchimbaji. Pia wapo watoa huduma mbalimbali, wakiwamo watoa huduma za vyakula na vinywaji 29, kampuni tano za ulinzi, watoa huduma watano wa michezo na burudani kwa watoto pamoja na mwakilishi mmoja kutoka sekta ya wanyamapori. “Maonesho haya yamekusudia kuwaunganisha wadau wote katika mnyororo wa thamani wa madini, wakiwamo wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa teknolojia pamoja na wachimbaji, wachenjuaji na wafanyabiashara wa madini,” amesema RC Mnyeti. RC Mnyeti amesema maonesho hayo yanalenga kuongeza matumizi ya teknolojia katika shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini nchini, pamoja na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa. Malengo mengine ni kukuza matumizi sahihi ya teknolojia katika uchimbaji na uchenjuaji wa madini, kuwaunganisha wachimbaji na taasisi za Serikali, wizara, wadau wa madini na taasisi wezeshi, pamoja na kuwaunganisha wawekezaji wakubwa, wa kati na wadogo ili kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili. Lengo lingine ni kuwaunganisha wafanyabiashara wanaofanya shughuli katika mnyororo wa thamani wa madini na sekta zinazofungamana na madini.Maonesho hayo pia yanalenga kuifanya Tanzania kuwa mwenyeji wa maonesho bora ya teknolojia ya madini na sekta fungamanishi barani Afrika ifikapo mwaka 2035.

Sat, 26 Sep 2026 15:49:52 +0000
Business · Jamhuri Media

TBS Yazidi kufikisha elimu ya viwango na usalama wa bidhaa kwa wafanyabiashara

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

MAFUNZO YA UONGOZI NI MUHIMU KUKIIMARISHA CCM - ABDI

Na MWANDISHI WETU, Zanzibar NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Abdi Mahamoud Abdi, amesema mafunzo ya uongozi ni muhimu katika kuwawezesha viongozi na wanachama wa chama hicho kuwa wazalendo, pamoja na kuzingatia na kutekeleza sera, kanuni na taratibu za CCM. Abdi ameyasema hayo leo, Septemba 26, 2026, wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya Itikadi, Uenezi na kuongeza wanachama wapya wa CCM kwa awamu ya pili, yaliyofanyika Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja. Amesema CCM imekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo ya uongozi kwa wanachama wake kwa lengo la kuwaongezea uelewa na uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi na taratibu za chama. Amesema elimu inayotolewa kwa viongozi na wanachama kupitia mafunzo hayo itasaidia kukiimarisha CCM na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za chama, pamoja na kuchangia juhudi za kuleta maendeleo kwa ujumla. Aidha, Abdi amewataka washiriki kutumia fursa hiyo kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuongeza uelewa kuhusu Itikadi, Uenezi na misingi ya CCM ili elimu watakayoipata iweze kutumika ipasavyo katika utekelezaji wa majukumu yao. Amesisitiza kuwa uelewa mzuri wa misingi na taratibu za chama ni muhimu kwa viongozi na wanachama katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa kuzingatia malengo ya CCM.

Sat, 26 Sep 2026 15:45:47 +0000
Uncategorized · DW Rwanda

Trump rejects Iran proposal to reopen Strait of Hormuz

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

HEMED ASISITIZA MAKADA KUFAHAMU ITIKADI NA HISTORIA YA CCM

Na MWANDISHI WETU, Zanzibar MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amewataka makada wa chama hicho kuwa na uelewa mpana wa Itikadi, misingi na historia ya CCM ili waweze kutoa ufafanuzi sahihi kwa wananchi. Hemed ameyasema hayo leo, Septemba 26, 2026, wakati akifungua mafunzo ya Itikadi, Uenezi na kuongeza wanachama wapya wa CCM kwa awamu ya pili, yaliyofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Uongozi Dambwe, Tunguu, Zanzibar. Amesema sera za CCM zinalenga kuleta maendeleo na kuimarisha uchumi wa nchi, hivyo ni muhimu kwa makada kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu sera, misingi na historia ya chama hicho. Amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kujifunza na kupata tija, ikiwemo kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali zinazokikabili chama. Aidha, Hemed amesema CCM inapotoa ahadi kwa wananchi, inaendelea kuzitekeleza kwa vitendo, akieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa viongozi na wanachama wa chama. Katika hatua nyingine, amewataka makada hao kujifunza kwa kina historia ya CCM na kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu misingi na Itikadi ya chama ili waweze kueleza na kutetea kwa usahihi misimamo na sera zake wanapowahudumia wananchi. Zaidi ya makada na wanachama 380 wa CCM kutoka mikoa mbalimbali ya Unguja, Pemba na Tanzania Bara wanashiriki mafunzo hayo yanayolenga kuongeza uelewa kuhusu Itikadi na Uenezi, pamoja na kuimarisha uhai wa Chama Cha Mapinduzi.

Sat, 26 Sep 2026 09:00:00 +0000
Uncategorized · DW Rwanda

Trump rejects Iran proposal to reopen Strait of Hormuz

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Prime Minister Nsengiyumva meets Rwandans living around New York City

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Nigeria fight back as Gambia, Rwanda and Guinea-Bissau make winning starts to AFCON 2027 qualifiers

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Rwanda Foreign Minister exchanged with AU Commission Deputy Chairperson

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Watchdog Uganda

TOP NEWS: Here Are The Six Crucial Road Projects Set to Begin Soon by Works Ministry

Kampala: The Ministry of Works and Transport has ignited fresh optimism across Uganda as it begins the technical review of six major national road projects, a decisive step toward design…

Recently

Page 1031 of 1125 · 22491 stories