Search the region
22486 stories
Maria Kiwanuka appointed Uganda National Mining Company boss
Former Finance minister Maria Kiwanuka has been appointed acting chairperson of the Uganda National Mining Company (UNMC), following a leadership shake-up at the state-owned mining…
RecentlyHRW alerte sur les frappes indiscriminées en Ethiopie
Read the full report from the original source.
RecentlyMoses Matovu murder: Prime suspect arrested
The prime suspect in the killing of Afrigo Band legend Moses Matovu has been arrested, police have confirmed. Vincent Nsamba, 41, a private security guard,…
RecentlyMIGOGORO YA ARDHI YAONGOZA MALALAMIKO, SERIKALI YAPANGA KUMARISHA MABARAZA
Na Janeth Raphael - MichuziTv Migogoro ya ardhi imeendelea kuwa miongoni mwa changamoto kubwa zinazowasilishwa na wananchi kupitia kipindi cha Sema na Waziri, hali ambayo imeifanya Serikali kuendelea kutathmini upya mfumo wa utatuzi wa migogoro hiyo ili kupata njia yenye ufanisi zaidi. Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Homera, amesema asilimia kubwa ya malalamiko yanayowasilishwa katika kipindi hicho yanahusu migogoro ya ardhi, akieleza kuwa Serikali inaendelea na uchambuzi wa kina wa sheria inayosimamia mabaraza ya ardhi nchini. Dkt. Homera amesema uchambuzi huo unalenga kubaini iwapo mabaraza hayo yanapaswa kuongezewa nguvu na mamlaka ili yaweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi, au endapo majukumu hayo yanaweza kuhamishiwa katika mfumo wa mahakama. Amesema kwa sasa mabaraza ya ardhi yamebaki zaidi katika jukumu la usuluhishi, hivyo Serikali inataka kutathmini namna bora ya kuimarisha utendaji wake ili yaweze kuwa na mchango mkubwa zaidi katika kutatua migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi. Kwa mujibu wa Dkt. Homera, hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha wananchi wanapata ufumbuzi wa changamoto zao kwa wakati, hususan migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikichukua muda mrefu na kuathiri maisha na shughuli za wananchi. Amesema hatua hiyo pia inatekelezwa kufuatia maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi zinapatiwa ufumbuzi na mifumo ya utoaji haki inaendelea kuimarishwa. Dkt. Homera ameyasema hayo leo Septemba 25, 2026, jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kipindi cha Sema na Waziri, ambapo ameeleza hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha mifumo ya haki na sheria nchini. Waziri huyo amejiwekea utaratibu huo wa kuzungumza na wananchi Moja kwa moja ( KUpitia simu) ili wananchi waeleze changamoto za kisheria zinazowakabili.
Fri, 25 Sep 2026 16:48:12 +0000C-CEOs FORUM KUWA CHACHU YA UTEKELEZAJI WA DIRA 2050
Na Mwandishi wa OTR - Arusha. Serikali imesema Mkutano wa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma (C-CEOs Forum) 2026, unaotarajiwa kuwakutanisha viongozi kutoka Mashirika zaidi ya 300 ya Umma, pamoja na wawakilishi wa Sekta Binafsi na washiriki wengine zaidi ya 700 kuanzia Septemba 28 hadi 30, 2026, utakuwa jukwaa muhimu la kuimarisha utendaji, tija na mchango wa Mashirika hayo katika utekelezaji wa Dira 2050. Forum hiyo, inayoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR), ni ya nne kufanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2023 na inalenga kuwakutanisha Wenyeviti wa Bodi, Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma na wadau mbalimbali kujadili namna ya kuongeza ufanisi wa taasisi hizo na kuhakikisha mipango na shughuli zao zinaendana na vipaumbele vya kitaifa vilivyoainishwa katika Dira 2050. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ijumaa, Septemba 25, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, alisema kuwakutanisha viongozi wa Mashirika ya Umma katika jukwaa moja kunatoa fursa ya kujenga uelewa wa pamoja, kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano kwa lengo la kuongeza tija na mchango wa Mashirika hayo katika maendeleo ya Taifa. Amesema ni muhimu Mashirika ya Umma kuhakikisha mipango na shughuli zao zinaendana na malengo ya Dira 2050, ili rasilimali na uwekezaji unaosimamiwa na Serikali uweze kuzalisha matokeo yenye thamani zaidi kwa uchumi na wananchi. “Tunataka mkutano huu uwe na manufaa yanayoonekana pia nje ya ukumbi wa mikutano, kwa kuwafungulia fursa wafanyabiashara, watoa huduma na wananchi wa Arusha,” alisema. Mhe. Makalla amesema Arusha ina uzoefu wa kuhudumia mikutano mikubwa ya kitaifa na kimataifa na kwamba Mkoa uko tayari kuwapokea washiriki wa C-CEOs Forum 2026, huku akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha mazingira ya usalama, utulivu na ukarimu kwa wageni. “Watakaohudumia wageni wawe wakarimu ili warudi tena,” amesema, akieleza kuwa ujio wa washiriki zaidi ya 700 utatoa fursa kwa sekta mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo hoteli, migahawa, usafiri, utalii, biashara na huduma nyingine. Kwa upande wake, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, alisema utekelezaji wa Dira 2050 unahitaji mabadiliko katika namna Mashirika ya Umma yanavyotazama utendaji wao, kutoka kwenye kuendesha taasisi na shughuli zake kwenda kwenye kuzalisha matokeo yanayopimika na yenye thamani kwa Taifa. Kwa mtazamo wake, ufanisi wa juu unapaswa kuonekana katika uwezo wa Mashirika kutumia rasilimali na uwekezaji waliokabidhiwa kwa tija, kujenga ushindani, kuimarisha uimara wa kifedha na kutoa huduma zenye ubora, huku yakichangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi. “Tunataka Mashirika ya Umma yenye ufanisi wa juu, shindani na imara katika kutekeleza Dira 2050,” alisema Mchechu. Bw. Mchechu alisema thamani ya uwekezaji wa Serikali katika Mashirika na kampuni zake imeongezeka kutoka Sh67.95 trilioni mwaka 2020/21 hadi Sh92.28 trilioni mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 35.8, hali inayoongeza umuhimu wa kuhakikisha uwekezaji huo unazalisha matokeo makubwa zaidi. Alisema matokeo hayo hayawezi kupimwa kwa gawio pekee, bali yanapaswa kuangaliwa kwa upana kupitia tija, ubora wa huduma, ufanisi wa matumizi ya rasilimali, uimara wa kifedha, ubunifu, matumizi ya teknolojia, uwezo wa kushindana na athari ya taasisi katika uchumi. Kwa mtazamo huo, alisema Mashirika ya Umma yanapaswa kujenga uwezo wa kubadilika kulingana na mazingira ya uchumi, teknolojia na mahitaji ya wananchi, huku uongozi na bodi zikibeba jukumu muhimu la kuweka mwelekeo wa utendaji na uwajibikaji. “C-CEOs Forum inalenga kuangalia kwa upana zaidi jinsi ya kubadilisha rasilimali na uwekezaji kuwa utendaji na matokeo yenye thamani zaidi,” alisema. Bw. Mchechu alisema ongezeko la mapato yasiyo ya kodi linalotokana na Mashirika na taasisi zinazochangia kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, linaonesha pia umuhimu wa kuendelea kuboresha utendaji wa taasisi hizo. Mapato hayo yameongezeka kutoka Sh637.7 bilioni mwaka 2020/21 hadi Sh1.327 trilioni mwaka 2025/26, sawa na ongezeko la asilimia 108.3. Alisema kwa hiyo, mjadala kuhusu Mashirika ya Umma haupaswi kuishia kwenye suala la kiasi cha fedha kinachowasilishwa Serikalini, bali unapaswa kuangalia thamani pana inayozalishwa na uwekezaji wa umma, ikiwemo huduma, ajira, uzalishaji, ubunifu, ushindani na mchango katika uchumi. Katika mtazamo wake, maeneo hayo yanahitaji uongozi wenye mwelekeo wa kimkakati, utawala bora, matumizi makubwa zaidi ya teknolojia za kidijitali na akili bandia, mifumo endelevu ya upatikanaji wa fedha, pamoja na ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi. Alisema pia Mashirika yanahitaji kuwekeza katika rasilimali watu na ujuzi wa baadaye ili yaweze kukabiliana na mabadiliko ya kiteknolojia, kiuchumi na kimazingira, sambamba na kuzingatia masuala ya mazingira, jamii na utawala bora.
Fri, 25 Sep 2026 16:50:30 +0000Mechi Kubwa za Kimataifa Kuchezwa Leo
MECHI Kubwa za Kimataifa zimewadia na safari hii kila timu inahitaji ushindi mnono. Je nani anaweza kuondoka kifua mbele baada ya dakika 90 za mwamuzi? Leo hii kutakuwa na mechi ya kukata na shoka kati ya Italia dhidi ya Ubelgiji, mechi ambayo inaenda kuamuliwa kwa uwezo wa wachezaji kwani zote hizi ni timu kubwa Duniani ambazo zina wachezaji wenye uwezo wa kufanana. Timu ya Taifa ya Italia chini ya kocha mkuu Roberto Mancini ni timu ambayo ina uwezo mkubwa wa kutawala mpira, kujenga mashambulizi huku wakitarajiwa kutumia nafasi ambazo wanazitengeneza, na wachezaji wa kufanya hayo yote wapo kikosini hapo. Licha ya kutoshiriki Kombe la Dunia kwa kutokufuzu, bado haiwapi wapinzani wao nafasi ya kuwabeza kwani bado wanajiamini na kujua kuwa wana nafasi ya kuondoka na ushindi leo. Kwa upande wa Ubelgiji ni timu ambayo ina uwezo mkubwa wa kujilinda na kufanya mashambulizi kwani wachezaji wenye kasi kwenda mbele kushambulia wapo wakiongozwa na Doku, Trossard, Ketelaere, lakini pia wana wachezaji wazuri kwenye eneo la kiungo wakiongozwa na De Bruyne. Timu hizi mara ya mwisho kukutana ilikuwa ni msimu wa 2024 ambapo Italia waliondoka na pointi 4. Mtanange mwingine ni huu wa Uturuki dhidi ya Ufaransa ambao ni mabingwa wa Kombe la Dunia 2018 kikiwa ni kikosi chenye wachezaji wenye uwezo mkubwa sana kikiongozwa na nahodha wao Kylian Mbappe. Ikumbukwe kuwa Ufaransa mpaka sasa ina kocha mpya ambaye ni Zinedine Zidane ambaye alichukua mikoba ya Deschamps amabye aliachia kazi ya kunoa kikosi icho la Bleus baada ya kumaliza nafasi ya 4 kwenye Kombe la Dunia. Kikosi hicho kina wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa kama vile, Olise, Thuram, Dembele, Mbappe, Maignan na wengine wengi ambao kwa pamoja wana uwezo mkubwa wa kuisaidia timu. Huku kwa Uturuki wao ni timu ambayo ina mchanganyiko wa wachezaji wenye uwezo tofauti tofauti ambao wengi wanacheza kwenye ligi ya Uturuki, lakini wachache ndio wapo kwenye ligi zingine kama vile kina Kenan Yildiz. Timu hizi zinatarajiwa kuchuana vikali kuwania pointi 3 muhimu kwenye mechi ya kwanza ya UEFA Nations League huku takwimu zikionesha kuwa mara ya mwisho kukutana ilikuwa ni 2019 ambapo hakuna aliyekuwa mbabe kati yao. Beti mechi hii. Vilevile ile michuano ya AFCON itaendelea ambapo Morocco itamenyana dhidi ya Gabon katika mchezo wa kwanza wa Kundi A kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat. Morocco inaingia ikiwa na faida ya kucheza nyumbani na ikiwa imefanya vizuri kwenye Kombe la Dunia 2026, ambako ilifika robo fainali. Simba wa Atlas ndiyo timu inayobeba presha kubwa zaidi kwenye mchezo huu. Ikiwa nyumbani, matarajio ni kuona wakitawala mpira, wakicheza kwa kasi kupitia pembeni na kuilazimisha Gabon kujilinda kwa muda mrefu. Lakini pia The Atlas ina kumbukumbu nzuri sana dhidi ya Gabon katika mechi zao za hivi karibuni. Iliifunga Gabon 4-1 nyumbani mwaka 2024 kabla ya kushinda tena 5-1 ugenini. Vilevile kwa upande wa Gabon wao ni timu ambayo haiwezi kudharauliwa. Ina wachezaji wenye uwezo wa kubadilisha mchezo kupitia mashambulizi ya haraka, lakini tatizo kubwa litakuwa namna ya kuhimili Morocco ikiwa wenyeji wataanza kulisukuma eneo lao.
Fri, 25 Sep 2026 16:51:19 +0000Who Killed Muhammad Kirumira? Renewed Inquiry Puts 2018 Shocking Assassination Under Scrutiny
Read the full report from the original source.
RecentlyGovernor Achani rallies Kwale residents behind Ruto re-election bid
Read the full report from the original source.
RecentlyCCM YARIDHISHWA NA UHAI WA CHAMA TANGA, SAMIA ATOA BILIONI 35 KWA MRADI WA MAJI
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimeridhishwa na uhai wa chama na utekelezaji wa shughuli zake katika Mkoa wa Tanga, kikieleza kuwa ushirikiano mzuri kati ya chama na Serikali umewezesha kurahisisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi. Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, wakati akiendelea na ziara mkoani Tanga yenye lengo la kukagua uhai wa chama pamoja na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2025–2030. Kihongosi amesema miongoni mwa changamoto kubwa zinazowakabili wananchi wa Wilaya ya Mkinga ni upatikanaji wa maji, akieleza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetenga Sh35 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji katika eneo hilo. “Changamoto kubwa inayowakabili wananchi hapa ni suala la maji, lakini Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta Sh35 bilioni kwa ajili ya mradi wa maji,” amesema Kihongosi. Kihongosi ameyasema hayo leo Septemba 25,2026 wakati akizindua Shina Namba 6 lililopo Mbuyuni, Kata ya Manza, ambapo amesema wananchi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za maji, afya na elimu. Amesema Serikali inayoongozwa na CCM chini ya Rais Samia imeendelea kuchukua hatua kuhakikisha changamoto hizo zinapatiwa ufumbuzi na wananchi wanapata huduma muhimu pamoja na mazingira bora ya maendeleo. Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya CCM na Serikali ni muhimu katika kuhakikisha ilani ya chama inatekelezwa na ahadi zinazotolewa kwa wananchi zinatimizwa.
Fri, 25 Sep 2026 16:45:34 +0000Des relations au plus bas entre l'Allemagne et la Russie
Read the full report from the original source.
RecentlyRaundi Moja Kutoa Split Mpya, Forever Split Megaways Inatikisa
MERIDIANBET imeongeza moto kwenye kasino kwa ujio wa Forever Split Megaways, mchezo mpya kutoka Pragmatic Play unaokuja na burudani ya aina yake. Kama wewe ni mpenzi wa reels zinazozunguka, alama zinazobadilika na sapraizi zinazoweza kujitokeza wakati wowote, basi mchezo huu una sababu ya kuingia kwenye orodha yako ya kujaribu. Mara tu raundi inapoanza, macho yanaelekezwa kwenye reels kusubiri kuona kinachofuata. Kinachovutia zaidi ni mfumo wa splits, ambao unaweza kufanya reels zibadilike na kufungua mchanganyiko mpya wa alama. Hii ndiyo sehemu inayoongeza msisimko, kwa sababu kila raundi inaweza kuleta mpangilio tofauti na kufanya safari ya mchezo iwe hai zaidi. Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Forever Split Megaways imewasili Meridianbet ikiwa kwenye kipindi maalum cha ufunguzi wa muda mfupi hadi Oktoba 1, 2026. Hii ni fursa kwa wachezaji kuingia mapema na kuutambua mchezo huu mpya kutoka Pragmatic Play. Badala ya kusubiri mchezo upate nafasi yake, sasa unaweza kuufungua na kuona mwenyewe namna mfumo wake wa mgawanyiko unavyofanya kazi. Kwa kila mzunguko wa mchezo, kuna jambo jipya la kufuatilia. Mchezo huu umeundwa kwa mtindo unaoweka msisitizo kwenye mabadiliko na burudani, hivyo kila mzunguko unaweza kuwa mwanzo wa tukio jingine. Hapo ndipo Forever Split Megaways inapopata ladha yake na kuwafanya wachezaji kutaka kuona kinachofuata. Ukiwa tayari kwa burudani mpya, Forever Split Megaways inakusubiri Meridianbet kasino . Ingia, cheza na ugundue mfumo huu bora ulioletwa na Pragmatic Play.
Fri, 25 Sep 2026 16:40:48 +0000ITANGAZO RYA CYAMUNARA Y’UMUTUNGO UTIMUKANWA
Read the full report from the original source.
RecentlyTaRL Yaleta Matumaini Kumaliza Changamoto ya KKK
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv ZAIDI ya watoto 4,200 kati ya 25,617 waliofanyiwa tathmini katika Halmashauri ya Jiji la Tanga wamebainika kuwa na changamoto katika stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK), hali iliyosababisha kuanza kutumika kwa mbinu ya Teaching at the Right Level (TaRL) ili kuwasaidia kumudu stadi hizo. Mratibu wa Mradi wa TaRL, Alex Sigalla, amesema baada ya watoto hao kufundishwa kwa kutumia mbinu hiyo, kati ya asilimia 80 na 85 waliweza kumudu stadi za msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu. Sigala amesema hayo wakati kando ya Mkutano wa Sita wa African Curriculum Association (ACA), uliofanyika Dar es Salaam, akieleza kuwa mradi huo unaotekelezwa katika shule zote 87 za Halmashauri ya Jiji la Tanga unalenga kuhakikisha hakuna mtoto anayevuka kwenda darasa la tatu bila kumudu stadi hizo. Amesema TaRL haimwangalii mtoto kwa kuzingatia umri au darasa analosoma, bali kiwango chake cha uelewa. Hivyo, mtoto mwenye changamoto huwekwa katika kundi linalolingana na uwezo wake na kufundishwa kwa kutumia mbinu shirikishi. “Unaweza ukaona mtoto yuko darasa la sita lakini ana changamoto za mwambatano. Huyu katika ngazi ya uelewa ana changamoto ya silabi sawasawa na yule mtoto aliyeko darasa la awali, la kwanza au la pili,” amesema. Amesema katika utekelezaji wa mradi huo, walimu 176 tayari wamejengewa uwezo wa kutumia mbinu ya TaRL, huku lengo likiwa kuwafikia walimu 261 katika Halmashauri ya Jiji la Tanga. Kwa mujibu wa Sigala, mafanikio yaliyopatikana Tanga yamewafanya kuendelea kuhimiza matumizi ya TaRL katika shule zote nchini, akisema mbinu hiyo inaweza kusaidia kukabiliana na changamoto ya watoto kushindwa kumudu stadi za msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu. Amesema Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanza kushirikiana katika hatua za kuangalia namna mbinu hiyo inaweza kusambazwa zaidi nchini. “Kwa maana hii, tayari Wizara ya Elimu imeshakuwa tayari ni mdau mkubwa ambaye tayari anataka kuona watoto kufikia darasa la pili kwenda la tatu, hakuna mtoto atavuka kama atakuwa na changamoto za KKK,” amesema. Kwa upande wake, Mwalimu Baturi Msuya wa Shule ya Msingi Tanga amesema TaRL imekuwa rahisi kutumia kwa kuwa inamshirikisha mtoto kupitia michezo, nyimbo na ubunifu mbalimbali. Amesema shule zote 87 za Halmashauri ya Jiji la Tanga zimepata mafunzo hayo, huku kila shule ikiwa na walimu wawili wanaotumia mbinu hiyo kuwasaidia watoto wenye changamoto za KKK. Msuya amesema vifaa vinavyotumika katika utekelezaji wa mbinu hiyo ni rahisi kupatikana, kwa kuwa baadhi yake hutengenezwa kwa kutumia vifaa vinavyopatikana katika mazingira ya kawaida, ikiwamo maboksi, makuti, vifuu vya nazi na karatasi. Amesema matumizi ya TaRL yameongeza uwezo wa watoto katika KKK, akieleza kuwa kwa sasa zaidi ya asilimia 96 ya watoto wa darasa la pili wanaweza kusoma, kuandika na kuhesabu. “Mbinu ambayo mtoto ndiye kitovu cha ujifunzaji. Maana yake hata ukiwa haupo, ukiacha darasa liko hivi, wanacheza wenyewe na wanajifunza wenyewe kwa wenyewe,” amesema. Msuya amewataka walimu wa mikoa mingine kuipokea mbinu hiyo, akisema inamwezesha mtoto kujifunza kwa kushiriki moja kwa moja katika mchakato wa ujifunzaji.
Fri, 25 Sep 2026 16:35:38 +0000Rwanda urged to adopt dedicated law for organic farming
Read the full report from the original source.
RecentlyKASI YA AI YAWEKA SERA ZA TANZANIA KWENYE MIZANI
KASI ya ukuaji wa Teknolojia ya Akili Unde (AI) imeibua mjadala kuhusu uwezo wa sera, taasisi na mifumo ya uongozi nchini kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia hiyo. Hoja hiyo imeibuliwa katika Mkutano wa Tatu wa Vyuo Vikuu Vitano (5UCC) unaofanyika katika Taasisi ya Nelson Mandela African Institution of Science and Technology (NM-AIST), Arusha, kuanzia Septemba 23 hadi 25, 2026. Akifungua mkutano huo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, amesema mjadala kuhusu AI haupaswi kuangalia uwezo wa teknolojia hiyo pekee, bali pia namna taasisi, sera na mifumo ya uongozi inavyopaswa kuitikia fursa na changamoto zake. “Huu ndio hasa aina ya mjadala tunaouhitaji, si kuhusu tu kile ambacho teknolojia inaweza kufanya, bali pia namna taasisi zetu, sera zetu na mifumo yetu ya uongozi inavyopaswa kuitikia fursa na changamoto zinazoletwa na teknolojia hiyo,” amesema. Katika mkutano huo, Dkt. Philbert Nyinondi, mhadhiri na mtafiti wa mawasiliano ya sayansi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), amewasilisha utafiti unaochunguza uwezo wa miongozo ya AI kwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya teknolojia hiyo katika elimu ya juu. Utafiti huo umechambua National Guidelines for AI in Education (NGAIE) na National Digital Education Guidelines for Universities (NDEGU), zote za mwaka 2025, na kubaini kuwa Tanzania tayari ina msingi wa kisera unaotambua ufuatiliaji, mrejesho na maboresho ya sera. Hata hivyo, Dkt. Nyinondi amesema bado kuna mapungufu, ikiwamo kutokuwepo kwa vichocheo vilivyoainishwa wazi vya kufanya mapitio ya haraka ya sera, muda wa kushughulikia changamoto za dharura, mfumo wa tahadhari za awali kuhusu teknolojia zinazoibuka na utaratibu wa wazi wa kuunganisha taarifa za ufuatiliaji na maamuzi ya kisera. Amesema kadiri AI inavyoendelea kubadilika, matumizi yake katika elimu ya juu yanaweza kuleta changamoto ambazo hazikutarajiwa wakati miongozo hiyo ilipoandaliwa, hivyo mifumo ya kisera inahitaji kuwa na uwezo wa kutambua mabadiliko hayo na kuchukua hatua kwa wakati. Dkt. Nyinondi amesema hoja si kwamba Tanzania haiwezi kubadilisha sera, bali ni kama mifumo iliyopo inaweza kufanya mabadiliko hayo kwa kasi inayolingana na maendeleo ya AI. Kwa upande wake, Profesa Raffaella Cagliano wa Politecnico di Milano, Italia, amesema maendeleo ya teknolojia yanapaswa kuendana na mahitaji na mazingira ya kijamii na kiuchumi ya watu. “Hatuwezi kutenganisha uendelezaji wa teknolojia na uhalisia wa mazingira na mifumo ya kijamii,” amesema. Naye Profesa Tushar Shinde wa IIT Madras Zanzibar amesema AI haipaswi kupimwa kwa ukubwa wa mifumo pekee, bali pia kwa ufanisi, upatikanaji na gharama yake. “Lengo si kujenga mfumo mkubwa zaidi. Lengo ni kuufanya mfumo uwe mdogo, wa haraka na wa gharama nafuu,” amesema. Amesema mustakabali wa AI unapaswa kupimwa kwa kiwango cha athari inayozalisha, huku akisisitiza umuhimu wa kujenga teknolojia inayoweza kuwafikia watu wengi zaidi. Mijadala hiyo imeonesha umuhimu wa kujiandaa kwa matumizi ya AI katika ufundishaji, ujifunzaji, tathmini, utafiti na huduma za kitaaluma, sambamba na kuimarisha uwezo wa mifumo ya kitaifa kukusanya ushahidi, kufanya maamuzi na kurekebisha sera kwa wakati.
Fri, 25 Sep 2026 16:28:53 +0000Wetangula fires back at Uhuru over 2022 poll remarks: ‘Why is he wailing more than the bereaved?’
Read the full report from the original source.
RecentlyEL NIÑO YASOGEZA RATIBA YA MITIHANI YA TAIFA
Na Karama Kenyunko Michuzi tv SERIKALI imebadilisha ratiba ya Upimaji na Mitihani ya Taifa ya mwaka 2026, kwa kurudisha nyuma mitihani hiyo kutoka Novemba hadi Oktoba, kutokana na utabiri wa mvua kubwa za El Niño unaotarajiwa kuathiri maeneo mbalimbali nchini. Hatua hiyo imetangazwa leo Septemba 25, 2026, huku Serikali ikieleza kuwa hatua hiyo imelenga kulinda usalama wa wanafunzi, walimu, wasimamizi na maofisa wengine, pamoja na mitihani, vifaa na nyaraka zake. Akizungumza na waandishi wa Habari, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Amneir, amesema Serikali imechukua hatua hiyo baada ya kuzingatia uwezekano wa mvua kubwa kunyesha mwezi Novemba 2026, kipindi ambacho baadhi ya mitihani ilikuwa imepangwa kufanyika. Amesema kwa mujibu wa utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wa Agosti 18, 2026, kuna uwezekano wa kutokea kwa El Niño yenye nguvu, inayotarajiwa kuathiri mvua za Vuli kuanzia Oktoba hadi Desemba 2026 na kuendelea hadi Januari 2027. “Kwa mujibu wa utabiri huo, mvua hizo zinatarajiwa kuanza mwezi Oktoba 2026, huku mwezi Novemba 2026 ukitarajiwa kuwa na mvua nyingi zaidi,” amesema Amesema Serikali, kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), imeona umuhimu wa kufanya marekebisho ya ratiba ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo. Wanu amesema mvua kubwa zinaweza kusababisha mafuriko, kuathiri barabara na usafiri, hali ambayo inaweza kuchelewesha au kuzuia ufikishaji wa mitihani, vifaa na nyaraka katika vituo vya mitihani. Amesema pia mvua hizo zinaweza kusababisha wanafunzi, wasimamizi na maofisa wengine kushindwa kufika vituoni kwa wakati, huku kukatika kwa umeme na kuathirika kwa mawasiliano kukiwa ni changamoto nyingine inayoweza kujitokeza. Aidha, amesema mvua na unyevunyevu vinaweza kuathiri mazingira ya afya na usafi katika baadhi ya vituo vya mitihani, hususan maeneo yenye changamoto katika mifumo ya maji, vyoo na taka. Amesema Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Pili unahusisha shule 21,353, huku wa Darasa la Nne ukihusisha shule 21,008, hivyo athari za mvua katika vituo vya upimaji zinaweza kuwakabili wanafunzi wengi. Amesema wanafunzi wanaofanya upimaji huo wengi wao wana umri wa chini ya miaka 11, hivyo wanahitaji mazingira salama na rafiki wakati wa kufika na kushiriki katika upimaji. Wanu ametoa wito kwa Kamati za Mitihani za Mikoa na Halmashauri pamoja na Wakuu wa Shule kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na NECTA katika kutekeleza maelekezo yatakayotolewa. Pia amewataka wanafunzi, wazazi na walezi kuendelea kufuatilia taarifa rasmi zitakazotolewa na Wizara na NECTA kuhusu ratiba na maelekezo ya uendeshaji wa Upimaji na Mitihani ya Taifa kwa mwaka 2026. Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohamed, Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne ambao awali ulipangwa kufanyika Oktoba 21 na 22, sasa utafanyika Oktoba 5 na 6, 2026. Amesema Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Pili uliokuwa ufanyike Novemba 17 na 18, sasa utafanyika Oktoba 7 na 8, 2026. Aidha, Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili uliopangwa kufanyika Novemba 2 hadi 13, sasa utafanyika Oktoba 12 hadi 23, 2026. Kwa upande wa Mtihani wa Kidato cha Nne, ambao awali ulipangwa kuanza Novemba 9 hadi 27, sasa utaanza Oktoba 19 na kukamilika Novemba 6, 2026. Profesa Said amesema marekebisho hayo yanalenga kuhakikisha kalenda ya mitihani na mihula katika sekta ya elimu haiathiriki, huku wanafunzi wakifanya mitihani katika mazingira salama. “Uamuzi huu umezingatia zaidi usalama wa watoto, usalama wa mitihani na kuunga mkono juhudi za Serikali kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño, hasa mwezi Novemba ambao unatabiriwa kuwa na mvua nyingi zaidi,” amesema.
Fri, 25 Sep 2026 16:24:49 +0000Sudan’s farmers are ready to return – private investment could get them there
Read the full report from the original source.
RecentlyBurundi : Banki Nkuru ivuga ko yibwe ama euro arenga ibihumbi 814
BRB yabwiye BBC ko ubwo busuma bwakozwe hakoreshejwe ubuhinga bwo kwinjira mu buryo bwa mudasobwa ata ruhusha, buzwi nka cyberattaque
Recently'Act Now!' Ugandan lawyer urges Ruto to use diplomatic channels for Besigye's release
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 1046 of 1125 · 22486 stories