Search the region
22483 stories
DUKA JIPYA LA YAS KUFUNGUA FURSA KWA WAKAZI WA KAHAMA
Wakazi na wafanyabiashara wa Kahama mkoani Shinyanga wanatarajiwa kunufaika na upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kifedha kwa urahisi zaidi, kufuatia Yas Tanzania kufungua duka jipya mjini humo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Mhe. Mataluma Kaniki alisema kuendelea kuongezeka kwa uwekezaji wa sekta binafsi ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza fursa za ajira katika Manispaa hiyo. “Kahama ni miongoni mwa maeneo yanayokua kwa kasi kiuchumi kutokana na shughuli za madini, kilimo na biashara. Tunapopata uwekezaji kama huu, tunaona matokeo yake si katika huduma pekee, bali pia katika ajira, biashara zinazozunguka uwekezaji huo na mchango wake katika uchumi wa Manispaa yetu. Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri yatakayovutia uwekezaji zaidi Kahama,” alisema Mhe. Kaniki. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Uendeshaji wa Yas Tanzania, Bi. Mwangaza Matotola, alisema duka hilo limefunguliwa ili kuwapa wateja wa Kahama sehemu ya kupata huduma na msaada wanaouhitaji kwa urahisi zaidi. “Tunataka mteja wa Kahama apate huduma anayoihitaji kwa urahisi na kwa wakati. Duka hili linatupa nafasi ya kuwa karibu zaidi na wateja wetu, kusikiliza mahitaji yao, kutatua changamoto zao na kuwapatia huduma za Yas na Mixx katika sehemu moja,” alisema Matotola. Alisema duka hilo ni sehemu ya mtandao wa zaidi ya maduka 556 ya Yas nchini, yanayowezesha wateja kupata huduma mbalimbali ikiwemo za laini, intaneti, vifaa vya mawasiliano na huduma za kifedha. Matotola alisema upanuzi wa maduka unaenda sambamba na uwekezaji wa zaidi ya Sh trilioni moja ambao Yas imefanya katika kupanua na kuboresha miundombinu na huduma zake nchini. Kwa mujibu wake, Yas kwa sasa ina zaidi ya minara 4,900, inayowezesha huduma za teknolojia za 4G na 5G katika maeneo mbalimbali, huku ikihudumia zaidi ya wateja milioni 33.2 Tanzania Bara na visiwani. Alisema uwekezaji katika mtandao na vituo vya huduma kwa wateja unalenga kuhakikisha ongezeko la matumizi ya huduma za kidijitali linaenda sambamba na upatikanaji wa msaada wa moja kwa moja kwa wateja. “Kadiri matumizi ya teknolojia yanavyoongezeka, ndivyo mahitaji ya wateja yanavyobadilika. Ndiyo maana tunaendelea kuwekeza si tu kwenye mtandao, bali pia kwenye maeneo ambayo mteja anaweza kufika, kuzungumza nasi na kupata suluhisho la mahitaji yake,” alisema Matotola. Mbali na kusogeza huduma karibu na wateja, kufunguliwa kwa duka hilo kumeongeza pia fursa za ajira kwa vijana wa Kahama, ikiwa ni sehemu ya manufaa ya uwekezaji huo kwa jamii.
Fri, 25 Sep 2026 05:30:00 +0000The Takeaway: UN General Assembly debate Day 3
Read the full report from the original source.
RecentlyAustralia urges global cooperation on climate, AI checks and international law
Read the full report from the original source.
RecentlyUNGA Day 4: Lebanese on deck after defiant Netanyahu speech
Read the full report from the original source.
RecentlyFrench DJ Phaphane to headline Don Julio tequila sundowner at Mediterraneo
Kampala — Tequila brand Don Julio and Kampala restaurant Mediterraneo will host the second edition of their tequila sundowner on Sunday, September 27, with French DJ Phaphane headlining the event. The...
RecentlyTARURA Kilosa yajiandaa kukabiliana na mvua, vikundi 17 vya CBRM vyaanza kazi
Read the full report from the original source.
RecentlyClimate experts call for early action, not disaster response
ARUSHA: TANZANIA and other countries in Africa and the Asia-Pacific have been urged to strengthen climate preparedness systems and shift…
RecentlyRed cards that could throw 2027 polls into uncertainty
Read the full report from the original source.
Recently‘Turn what we know into what we do,’ Barbados PM Mottley urges world leaders at UN
Read the full report from the original source.
RecentlyKRA issues new tax guidance for Kenyans living abroad with rental property
Read the full report from the original source.
RecentlyNoah Woods left playground through gap in fence, inquest hears Noah's mother tells parents to "hold their children a little tighter and cherish every moment".
Noah's mother tells parents to "hold their children a little tighter and cherish every moment".
RecentlyGovt urges Kenyans in flood-prone areas to relocate as preparations intensify
NATIONAL NEWS · 4 hours ago
RecentlyTanzania attends the GPE meeting to mobilize funding to global education systems
NEW YORK: THE Minister for Education, Science and Technology, Professor Adolf Mkenda, has participated in the GPE Multiplier Possibility meeting…
RecentlyNCIC urges Kenyans to reject ethnic politics and violence ahead of 2027
NATIONAL NEWS · Quick read
RecentlyItaly adopts 30pc cap on foreign pupils, sparking debate over integration policy
Latest · World
RecentlyTanzania reschedules 2026 national exams over El Niño rains
Read the full report from the original source.
RecentlyConseil de sécurité : qui soutient la candidature africaine?
Read the full report from the original source.
RecentlyMuteti recounts abduction ordeal Muteti said his alleged abductors questioned him about his activism during the ordeal.
Muteti said his alleged abductors questioned him about his activism during the ordeal.
RecentlyTanzania yatoa wito kwa nchi za Afrika kuweka mikakati endelevu kwenye mapambano dhidi ya malaria
Read the full report from the original source.
RecentlyUS-China rivalry remains frozen after Trump-Xi summit
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 1050 of 1125 · 22483 stories