Search the region
22471 stories
Whose drugs? Burning questions as Murkomen leads Sh8.2b drug haul destruction
Read the full report from the original source.
RecentlyAfrigo Band Legend Moses Matovu Left No Verifiable Fortune, Net Worth
Read the full report from the original source.
RecentlyNSSF’s 22.53% Interest Rate: What It Means for Savers
Read the full report from the original source.
RecentlyRelying too much on AI impedes growth of skills essential for effective communication
DAR ES SALAAM: IN a previous discussion published in the Daily News, concerns were raised about what Tanzania needs to…
RecentlyGovt tells universities to commercialise research
DAR ES SALAAM: THE government is stepping up efforts to turn university research into commercial products and investment opportunities, seeking…
RecentlySpecialist camp saves 2bn/- in overseas treatment costs
ARUSHA: THE government has saved more than 2bn/- in overseas medical expenses after more than 300 patients received specialist and…
RecentlyPost-harvest losses open investment opportunities
THE government has called for greater adoption of good agronomic practices to reduce post-harvest losses, while urging the private sector…
RecentlyGen. Muhoozi commends security agencies for arresting Moses Matovu murder prime suspect
Chief of Defence Forces (CDF) Gen Muhoozi Kainerugaba has commended Uganda’s security forces for the swift arrest of a prime suspect in the murder of legendary Afrigo Band musician Moses…
RecentlyISAIAH KATUMWA: Tribute to Moses Matovu
I received the news of Moses Matovu's passing with a very heavy heart. To me, Moses was far more than one of Uganda's greatest musicians. He was a pioneer, a…
RecentlyWhy Trump gave Xi an ornate bald eagle statue at the state dinner
News · Quick read
RecentlyThe ‘Lupita Effect’: What Oscar-winning actress’ investment in NCT portends for Kenyan sports
Latest · Basketball
RecentlyMEYA KIBAHA ATOA WITO VIWANDA KUBORESHA MIFUMO YA MAJITAKA KABLA YA EL NIÑO
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani MANISPAA ya Kibaha imeendelea kusimamia utekelezaji wa maagizo ya utunzaji wa mazingira kwa viwanda, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa mvua za El Niño zinazotarajiwa. Meya wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Nicas Mawazo, ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda kuboresha mifumo ya kuchuja na kutiririsha maji taka, ili kuzuia maji hayo kusambaa katika maeneo ya wananchi na kusababisha madhara kwa jamii na mazingira. Dkt. Mawazo ametoa wito huo wakati akikagua kiwanda cha kutengeneza karatasi cha Fortune, kilichopo Misugusugu, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Manispaa kuhusu utunzaji wa mazingira. Amesema kiwanda hicho awali kilikuwa na mashimo manne makubwa yaliyotumika kutiririsha maji taka, hali iliyokuwa ikihatarisha wananchi wanaoishi maeneo ya jirani, lakini katika ukaguzi huo amebaini kuwa maagizo ya Manispaa yametekelezwa kwa mashimo hayo kufukiwa na mfumo wa majitaka kuboreshwa. Meya Mawazo amesema Serikali inaendelea kushirikiana na wawekezaji kwa kuwa viwanda vinachangia pato la Serikali na kutoa ajira, huku akiwataka kuzingatia sheria na miongozo ya utunzaji wa mazingira. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Saeni, Edward Kitale, amesema wananchi walikuwa wakikabiliwa na kero ya harufu mbaya pamoja na maji taka kuelekea mashambani, lakini hali hiyo imeanza kuimarika baada ya mashimo hayo kufukiwa. Naye Ofisa Mazingira wa kiwanda hicho, Daudi Tito, amesema wamepokea maelekezo ya Serikali na Manispaa na wataendelea kuzingatia sheria na miongozo ya mazingira ili changamoto hiyo isijitokeze tena. Meneja Biashara wa kiwanda hicho, Colin Tang, amesema kiwanda kimeboresha mifumo yake kwa kujenga mitambo ya kisasa ya kuchuja maji taka, hatua inayolenga kuzuia madhara kwa wananchi na mazingira. Katika ziara hiyo ya ukaguzi, Meya Dkt. Mawazo pia amekagua kiwanda cha kutengeneza mabati na bidhaa za chuma cha Kinglion, pamoja na Shule ya Sekondari na Shule ya Msingi Misugusugu.
Fri, 25 Sep 2026 07:13:43 +0000It’s now a Bongo-flavoured Africa in “Pawa”-like hits
DAR ES SALAAM: IT’S “Pawa IV” by Mbosso featuring Darassa, Billnass, and Gnako that shakes music airwaves in many parts…
RecentlyZ’bar urged to preserve culture, expand creative economy
ZANZIBAR: ZANZIBAR’S Minister for Information, Arts, Culture and Sports, Dr Riziki Pembe Juma, has called on the public to protect…
RecentlyNetanyahu defends Israeli military action as delegates walk out before UN speech
Latest · News
RecentlyINADES YAZITAKA NGO's KUWA NA VYANZO MBALIMBALI VYA MAPATO.
Mkurugenzi wa Shirika la INADES Formation Tanzania, Jacqueline Nicodemus, amesema mashirika yasiyo ya kiserikali yanapaswa kuweka mikakati ya kuwa na vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuhakikisha yanaendelea kutekeleza shughuli zake bila kutegemea zaidi fedha kutoka kwa wafadhili. Akizungumza leo Septemba 24, 2026, jijini Dodoma kwenye Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Dodoma, amesema ushiriki wao katika jukwaa hilo ulianza katika ngazi za wilaya, ambapo walishiriki katika majukwaa yaliyofanyika katika wilaya tano kabla ya kufikia ngazi ya mkoa. Amesema ajenda kubwa iliyojadiliwa ni uendelevu wa mashirika yasiyo ya kiserikali, hususan changamoto ya kuwa na vyanzo vya kutosha vya mapato ili kupunguza utegemezi wa fedha kutoka kwa wafadhili. Aidha, amesema mashirika yanaweza kutumia fursa zilizopo kuendeleza bidhaa na huduma mbalimbali zinazoweza kuzalisha mapato, hatua ambayo itasaidia kupanua wigo wa mapato na kuimarisha utekelezaji wa shughuli zao. Kwa upande mwingine, amesema kupitia majukwaa hayo, wadau wameweza kujadili na kuweka mikakati ya kuhakikisha mashirika yanapata fursa zaidi za mapato na kuwa na uwezo wa kujiendesha kwa uendelevu. Ameongeza kuwa mjadala huo utaendelea katika ngazi ya kitaifa mwezi Oktoba, ambapo mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka maeneo mbalimbali Nchini yataendelea kutoa mchango kuhusu namna ya kujenga uendelevu wa sekta hiyo nchini Tanzania. Naye Rajab A. Rajab, ambaye ni mjumbe wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali NACONGO, kutoka Wilaya ya Kondoa, ameeleza kuwa INADES Formation Tanzania imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo, ikiwemo mazingira, kilimo, ufugaji, elimu na uwezeshaji wananchi kiuchumi. Amesema kupitia shughuli za mazingira, shirika hilo limefanikiwa kupanda zaidi ya miti 80,000 katika mkoa wa Dodoma, huku likiendelea kuwafikia wakulima na wafugaji kwa kutoa elimu na kuwawezesha kushiriki katika shughuli za maendeleo. Aidha, amesema katika maeneo ambayo shirika halifiki moja kwa moja, hutumia njia mbalimbali kuwafikishia wananchi elimu na taarifa muhimu, ikiwemo tafiti na machapisho yanayowasaidia wakulima kupata uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo. Ameeleza pia kuwa matokeo ya shughuli za shirika yanaonesha kuwa zaidi ya vikundi saba vinaendelea kutekeleza shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii vijijini, huku vikifikia zaidi ya watu 150,000. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Khatibu Kazungu, amezitaka mashirika yasiyo ya kiserikali kuzingatia masharti ya sheria, kushiriki mikutano na vikao vya wadau, kuwasilisha kwa wakati taarifa za robo mwaka na mwaka pamoja na kulipa ada kwa wakati. Kazungu pia amesisitiza mashirika hayo kulinda maslahi ya nchi, kuheshimu mila, desturi, utamaduni na maadili, kuhakikisha wanufaika wanashirikishwa katika utekelezaji wa miradi na kuzingatia mipango na vipaumbele vya Serikali, hususan Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050. Kwa upande wake, Patrick Mafuru, akizungumza kwa niaba ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalumu, amesisitiza mashirika kufanya kazi kwa ushirikiano na kuzingatia sheria, taratibu na kanuni zinazowaongoza, akieleza kuwa lengo kuu linapaswa kuwa kuisaidia Serikali kufikisha huduma kwa jamii katika maeneo ambayo bado haijafika.
Fri, 25 Sep 2026 07:10:11 +0000'My home away from home': Gachagua takes Wamunyoro spirit to Dallas as he meets Kenyans
Read the full report from the original source.
RecentlyProtest survivor shot three times appeals for Ksh.500K medical support
Read the full report from the original source.
RecentlyStakeholders call for sustained blue economy gains
TANGA: STAKEHOLDERS in the blue economy sector have called for concerted efforts to sustain gains made under the Regenerative Seascapes…
RecentlyTANZANIA YATOA WITO KWA DUNIA KUFANYA KWA VITENDO AHADI YA KUKABILI ATHARI ZA KUPANDA KWA KINA CHA BAHARI
Tanzania imetoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuongeza kasi ya upatikanaji wa fedha za mabadiliko ya tabianchi, teknolojia na mifumo madhubuti ya tahadhari za mapema ili kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na athari zinazoongezeka za kupanda kwa kina cha bahari. Akihutubia Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu kupanda kwa kina cha Bahari mjini New York, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi, amesema tatizo hilo si tishio la siku zijazo tena, bali tayari linaathiri maisha ya watu, uchumi na mifumo ya ikolojia duniani. Kwa Tanzania, athari hizo ni kubwa kutokana na ukanda wake wa pwani ya Bahari ya Hindi, Zanzibar na visiwa vingine ambavyo vinategemewa na mamilioni ya watu kupitia uvuvi, utalii na biashara. Mmomonyoko wa fukwe, kuingia kwa maji ya chumvi katika vyanzo vya maji baridi na mafuriko vinatajwa kuwa miongoni mwa vitisho kwa wananchi, miundombinu na mafanikio ya maendeleo ya nchi. Makamu wa Rais ameeleza kuwa, Tanzania tayari inachukua hatua kwa kuimarisha ulinzi wa pwani, kurejesha mikoko na mifumo ya ikolojia, kuimarisha usalama wa maji na kuendeleza mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi inayoongozwa na jamii. Hata hivyo, Makamu wa Rais amesisitiza kuwa juhudi za nchi moja moja hazitoshi, akitaka fedha za tabianchi kuwa za kutosha, za uhakika na zinazopatikana kwa urahisi zaidi kwa nchi zinazoendelea na jamii za pwani zilizo katika mazingira hatarishi. Mkutano huo wa Septemba 24, 2026, umezikutanisha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Viongozi, Wataalamu na Wadau wengine kuweka msimamo wa pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa dhidi ya tishio la kupanda kwa kina cha bahari. Mkutano huo unafanyika ikiwa ni mwendelezo wa Mkutano wa Ngazi ya Juu wa mwaka 2024 uliolifanya suala hilo kuwa ajenda muhimu ya kimataifa. Miongoni mwa maeneo ya msingi yanayopewa uzito ni ulinzi wa maisha na shughuli za kiuchumi katika maeneo ya pwani, mifumo ya tahadhari za mapema, takwimu za tabianchi, miundombinu himilivu, teknolojia, suluhisho zinazotegemea mazingira asilia pamoja na kuongeza uwezo wa nchi zilizo hatarini kukabiliana na athari zisizoepukika. Mkutano huo unatarajiwa kufikia Azimio la pamoja lenye mwelekeo wa utekelezaji, likilenga kuimarisha hatua za kimataifa, ustahimilivu na uwezo wa kukabiliana na kupanda kwa kina cha bahari. Tanzania imeunga mkono kupitishwa kwa Azimio hilo kwa makubaliano ya pamoja, huku ikisisitiza umuhimu wa dunia kuhamisha mjadala kutoka katika ahadi kwenda kwenye utekelezaji wenye matokeo. Kwa Tanzania, utekelezaji wa dhamira hizo unaweza kufungua fursa zaidi za ushirikiano wa kimataifa katika rasilimali za tabianchi, teknolojia, mifumo ya tahadhari za mapema na ujenzi wa miundombinu himilivu, hatua zenye umuhimu mkubwa katika kulinda jamii za pwani hususani Zanzibar, sekta ya utalii, uvuvi na shughuli nyingine za uchumi wa buluu. Akihitimisha ujumbe wake, Makamu wa Rais ametoa mwito wenye msisitizo kwa jumuiya ya kimataifa: “Bahari inatuunganisha. Hivyo basi, kupanda kwa kina cha maji yake kunapaswa pia kutuunganisha katika kuchukua hatua za pamoja.” Makamu wa Rais yuko New York nchini Marekani, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenye Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Fri, 25 Sep 2026 07:03:59 +0000Page 1058 of 1124 · 22471 stories