Unganishwa

Search the region

22448 stories

World · DW Afrique

La guerre dans le Tigré, un problème pour la sous-région

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

UJENZI WA UWANJA WA NDEGE MSALATO WAFIKIA 89%, KUKAMILIKA NOVEMBA 2026

Na Janeth Raphael - MichuziTv Mradi wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato jijini Dodoma umefikia asilimia 89.02 kwa upande wa ujenzi wa miundombinu, huku kazi za ujenzi wa majengo zikifikia asilimia 78.37, na Serikali ikieleza kuwa mradi huo unatarajiwa kuanza kukamilika katika hatua zake kuu kuanzia Novemba hadi Desemba 2026. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta, amesema Package 1 inayohusisha ujenzi wa miundombinu imepiga hatua kubwa, ambapo ujenzi wa njia ya kurukia na kutua ndege umefikia asilimia 98, taxiways asilimia 99 na apron asilimia 99. Aidha, barabara za kuingia kiwanjani, barabara za ndani na maegesho ya magari zimefikia asilimia 75, mfumo wa maji asilimia 89, uzio na mageti asilimia 76, huku kazi za umeme na vifaa vya kuongozea ndege zikifikia asilimia 90. Mhandisi Besta amesema kazi zilizobaki katika Package 1 ni pamoja na upandaji wa nyasi katika maeneo ya usalama ya runway na taxiways, ufungaji wa taa za kuongozea ndege ardhini na taa za barabarani, mabomba na tanki la maji la chini ya ardhi, kukamilisha uzio na mageti pamoja na kufunga mifumo ya mawasiliano ya ndege ikiwemo ILS na DVOR, ambayo tayari imewasili katika eneo la mradi. Kwa upande wa Package 2 unaohusisha ujenzi wa majengo, amesema utekelezaji umefikia asilimia 78.37, ambapo jengo la abiria limefikia asilimia 81, mnara wa kuongozea ndege asilimia 74, kituo cha huduma za zimamoto asilimia 88, kituo kikuu na vituo vidogo vya umeme asilimia 71 na jengo la huduma za hali ya hewa (MTO) asilimia 87. Kazi zinazoendelea ni pamoja na umaliziaji wa majengo, mifumo ya mitambo, umeme na mabomba, TEHAMA na mawasiliano, mashine za ukaguzi wa mizigo, madaraja ya kupandia abiria, vifaa vya hali ya hewa na magari ya zimamoto. Amesema kwa mujibu wa mpango wa utekelezaji, ujenzi wa miundombinu unatarajiwa kukamilika ifikapo Novemba 27, 2026, huku ujenzi wa majengo ukitarajiwa kukamilika Desemba 30, 2026, huku TANROADS ikiendelea kufuatilia kwa karibu ratiba za kazi, upatikanaji na ufungaji wa vifaa, uratibu wa wakandarasi pamoja na utekelezaji wa kazi zinazotegemeana ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati. Aidha, Mhandisi Besta amesema mradi huo tayari umetoa ajira 9,059 kwa Watanzania, ambapo ajira 3,571 zimetolewa kupitia Package 1 na ajira 5,488 kupitia Package 2, huku wafanyakazi wa kigeni wakiwa 47. Amewataka Watanzania, hususan wakazi wa Dodoma, kutumia fursa zitakazotokana na uwanja huo kukuza biashara na uchumi, ikiwemo usafirishaji wa bidhaa zinazohitaji kufika sokoni kwa haraka kama matunda, mboga mboga, samaki, kuku na maua, pamoja na kutumia fursa hiyo kukuza sekta ya utalii.

Thu, 24 Sep 2026 15:23:40 +0000
National · Issa Michuzi

WANANCHI KITETE WAILILIA ARDHI, DC SHAKA AINGIA ENEO LA MGOGORO WA MIAKA

Na Farida Mangube MGOGORO wa ardhi unaodaiwa kudumu kwa miaka kadhaa kati ya wananchi wa Kijiji cha Kitete Msindazi, Kata ya Ruhembe wilayani Kilosa, Mkoani Morogoro na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi umechukua sura mpya baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, kufika katika eneo linalolalamikiwa na kuahidi kuanza upya mchakato wa kutafuta suluhu. Wananchi wa kijiji hicho wamekuwa wakidai utekelezaji wa maamuzi yaliyowahi kufikiwa na Serikali katika kushughulikia migogoro ya ardhi kati ya vijiji vinavyopakana na hifadhi, wakisema pamoja na baadhi ya vijiji kunufaika na hatua zilizochukuliwa, wao bado hawajaona utekelezaji wa jambo hilo katika eneo lao. Wananchi hao wanasema changamoto hiyo imewaacha bila maeneo ya kutosha ya kilimo, huku eneo linalohusishwa na mgogoro likiwa halitumiki rasmi na wananchi, lakini likiendelea kulindwa na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi. Kwa mujibu wa wananchi hao, miongoni mwa maeneo yaliyowahi kufanyiwa uhakiki ni Kijiji cha Kitete Msindazi, ambapo wanadai takribani hekta 4,972 zilihusishwa na eneo la hifadhi na kwamba hatua zilizofuata zilipaswa kuweka wazi hatima ya eneo hilo na matumizi yake. Athuman Abdi Kihombe, ambaye alijitambulisha kuwa aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi wa Kijiji hicho na Mratibu wa Mbunge wa Mikumi wa wakati huo, Abdulsalaam Suleiman Ameir maarufu kama SAS amesema suala hilo limefuatiliwa kwa muda mrefu katika ngazi mbalimbali bila wananchi kupata utekelezaji waliokuwa wakiutarajia. Kihombe alikwenda na nyaraka alizozisoma mbele ya Mkuu wa Wilaya, akieleza kuwa mwaka 2011 Waziri wa Maliasili na Utalii wa wakati huo, Ezekiel Maige, alitoa majibu Bungeni kuhusu mipaka ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi baada ya swali la Mbunge wa Mikumi wa wakati huo, SAS. Kihombe amesema baada ya wananchi kuona utekelezaji wa maamuzi hayo unasuasua, walimfuata aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi,na kupitia timu ya mawaziri nane wa kushughulikia migogoro ya ardhi kati ya wananchi na maeneo ya hifadhi, timu maalum iliundwa katika wilaya hiyo kwa kushirikisha wananchi, wataalamu wa ardhi na wawakilishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, ambapo uhakiki wa mipaka ulifanyika na alama zikawekwa katika maeneo yaliyohusika. Cloud Petter, mkazi wa Kitete Msindazi, amesema changamoto kubwa kwa sasa ni uhaba wa maeneo ya kulima wakati kuna eneo ambalo wananchi wanaamini lilipaswa kufanyiwa uamuzi wa mwisho badala yake wanaona maeneo hayo yanalindwa na askari wa hifadhi bila wananchi wanaotegemea kilimo kwa maisha yao wakishindwa kuyatumia. Cloud katika mkutano wa hadhara wa Kijiji, akamuomba mkuu wa Wilaya ya Kilosa kwenda eneo linalolalamikiwa na kujionea hali halisi ili kupata picha halisi ya changamoto inayowakabili wananchi. Kwa upande wake, Ismail Ngwale, mkazi wa Kitete Msindazi, amesema wananchi wamekuwa wakisubiri majibu ya Serikali kwa muda mrefu na kwamba suala hilo linahitaji hatua inayoweza kuleta utulivu wa kudumu katika kijiji hicho. Wananchi waliohudhuria mkutano huo walionyesha matumaini baada ya Mkuu wa Wilaya kukubali kwenda katika eneo walilokuwa wakilalamikia, huku baadhi yao wakisema hatua hiyo imewapa picha kwamba Serikali italifanyia kazi shauri hilo kwa kuwa umeona uhalisia Baadhi ya wananchi walionekana kushangilia huku wengine wakijilaza mbele yake kama ishara ya kumshukuru kwa kukubali kusikiliza kilio chao na kwenda kujionea hali halisi, huku wengine wakicheza muziki kwa Furaha. Aliporudi eneo la mkutano, Mkuu huyo wa wilaya alitaka kwanza kusikia sauti za wananchi ambapo Mwenyekiti mstaafu wa Kijiji cha Kitete Msindazi, Timilai Lunyungu, amesema baada ya kufika eneo hilo wamejiridhisha kuwa suala hilo linahitaji utulivu na hatua za Serikali badala ya wananchi kuendelea kuingia katika maeneo yenye mgogoro hivyo kuwasihi wananchi watulivu wakati Serikali ikiendelea na mchakato kulishughulikia suala hilo. Naye Diwani wa Kata ya Ruhembe, Frank Hamis , akasema wananchi wanapaswa kuendelea kuwa watulivu ili Serikali iweze kupata nafasi ya kulishughulikia suala hilo kwa utaratibu. Hata hivyo diwani huyo ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuruhusu mazao ambayo tayari yamepandwa katika eneo linalolalamikiwa, hasa mahindi yaliyokuwa karibu kuvunwa, yaachwe yakomae na kuvunwa badala ya kuondolewa mara moja. Aidha akaomba wananchi waliokamatwa au wanaokabiliwa na mashauri kutokana na mgogoro huo waangaliwe kwa jicho la huruma na ikiwezekana mashauri yao yaondolewe kwenye vyombo vya Dola. Akijibu ombi hilo, Shaka amesema Serikali imepokea hoja hiyo na itaishughulikia baada ya kushauriana na mamlaka husika, badala ya kutoa uamuzi wa moja kwa moja kuhusu mashauri yaliyo kwenye vyombo vya Dola. Akawataka wananchi kutokwenda katika maeneo yenye mgogoro kufanya shughuli mpya za kilimo, ujenzi au maendeleo mengine wakati Serikali ikiendelea na mchakato wa kutafuta suluhu baada ya kuundwa kwa timu ya maridhiano itakayoshirikisha wawakilishi wa Wananchi, wataalamu,na wadau wengine. Amesema Serikali ya wilaya imeona mgogoro huo unahusu maisha ya wananchi na kwamba haupaswi kuendelea bila kutafutiwa ufumbuzi. “Mgogoro huu sio mkubwa kama ulivyokuwa ukitengenezwa. Sisi wenyewe Serikali ya wilaya tunaweza kuumaliza. Rais ametupa nyenzo zote za kufanyia kazi, tukishindwa hata kwa hili dogo tunamwangusha,” alisema Shaka. Shaka amesema baadhi ya watu wamekuwa wakiufanya mgogoro huo uonekane mkubwa kuliko ulivyo, huku akisisitiza kuwa Serikali sasa inalenga kuufanyia kazi kwa hatua na taratibu ili pande zote ziwe salama, ziiishi kwa amani na utulivu na shughuli za uzalishaji ziendelee kama kawaida. “Ufunguo wa suluhisho tunao, lakini tunataka utatuzi ufuate hatua na taratibu zote. La msingi na kubwa ni kuwa watulivu wakati suala hili linashughulikiwa,” akaongeza Katika hatua nyingine, Shaka aliwapa muda wa mwezi mmoja wananchi wenye mazao yaliyopo katika eneo lenye mgogoro kuyaondoa, huku akisisitiza kuwa Serikali haitaruhusu watu wengine kuingia katika eneo hilo kwa ajili ya kuanzisha shughuli mpya na watakaokwenda kinyume watambue hawatafumbiwa macho na wataonekana ni wasiotaka mchakato wa kutafuta suluhu.

Thu, 24 Sep 2026 15:27:14 +0000
National · Watchdog Uganda

Minister Babalanda Holds Thanksgiving in Buyende, Lauds President Museveni for Transforming Her Life and Championing Development

BUYENDE, UGANDA — The Minister for the Presidency and Member of Parliament for Budiope West Constituency, Hon. Babirye Milly Babalanda, on Wednesday, 23 September, held a colourful Thanksgiving ceremony at…

Recently
Entertainment · Watchdog Uganda

Alhaji Kirunda Mourns Afrigo Band’s Moses Matovu, Hails Musical Legacy

The Special Presidential Assistant–Press and Mobilisation and Deputy Press Secretary to H.E the President, Alhaji Faruk Kirunda, has mourned the death of veteran musician Moses Matovu, describing him as an…

Recently
National · The Star Kenya

Rider arrested in probe into Mbobu’s killing Police said the rider was arrested in Nairobi as detectives pursued further leads in the September 2025 killing

Police said the rider was arrested in Nairobi as detectives pursued further leads in the September 2025 killing

Recently
Uncategorized · Capital FM

EU commits Sh7.38bn to help Africa eradicate livestock disease

Latest · Africa

Recently
Uncategorized · Daily News

Taifa Stars’ AFCON 2027 campaign gets 500m/- boost as NBC hands over new bus

DAR ES SALAAM: A national football team cannot prepare effectively for major international competitions if basic logistical needs remain unresolved.…

Recently
Uncategorized · DW Afrique

ONU : ce que des dirigeants africains ont dit à la tribune

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Tobacco Bill: Businesses push back against new licences Stakeholders say the proposed rules could raise business costs and fuel illicit trade.

Stakeholders say the proposed rules could raise business costs and fuel illicit trade.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

UNGA81: Rwanda highlighted the importance of investing in skills and digital infrastructure

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Senate Vice President welcomes the new Clerk of the Senate

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · UBC

Uganda, Denmark explore Cooperation on Firefighting and Emergency response

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Observer Uganda

Preps for maternal health marathon pick up tempo

The race for a healthier Uganda will take on a deeper meaning on October 4 when the Independence Marathon brings together runners, fitness enthusiasts and corporate partners in a drive to help save mothers’ lives. Last S

Recently
Uncategorized · BBC Afrique

"Je ne savais pas que mon partenaire me violait pendant mon sommeil."

Adelle Overton était en couple avec Steven Uden depuis 13 ans lorsqu'elle a découvert qu'il la violait.

Recently
Uncategorized · The Observer Uganda

Matovu was not intended target, says ‘girlfriend’

Afrigo Band icon Moses Matovu may not have been the intended target in the fatal attack that followed a confrontation involving his alleged girlfriend and…

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Winnie Odinga to youth: Question leaders, think independently Winnie says even admired leaders should remain open to scrutiny, reflecting on her late father Raila Odinga’s legacy

Winnie says even admired leaders should remain open to scrutiny, reflecting on her late father Raila Odinga’s legacy

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

BMH YAWEKA BAYANA WAJIBU, HAKI 10 ZA MGONJWA KATIKA HUDUMA ZA AFYA

Na Janeth Raphael - MichuziTv Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Dodoma imewataka wagonjwa kuwa sehemu ya mchakato wa matibabu kwa kufahamu haki zao na kushiriki kikamilifu katika maamuzi yanayohusu afya zao, ikiwa ni pamoja na kupewa taarifa sahihi, kuheshimiwa na kupata huduma salama kwa wakati. Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Usalama wa Mgonjwa yaliyofanyika hospitalini hapo leo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dk. Abdalah Baja, amesema mgonjwa ana haki ya kupata huduma bora na salama kulingana na mahitaji yake, kushirikishwa katika maamuzi ya matibabu, kupata maoni ya pili ya kitabibu na kuhakikishiwa faragha wakati wa kupatiwa huduma. Dkte. Baja amesema haki nyingine ni kuheshimiwa utu wa mgonjwa, kulindwa kwa usiri wa taarifa zake za kiafya, kupewa nafasi ya kueleza changamoto zake na kusikilizwa, kuhudumiwa kwa wakati pamoja na kupata taarifa zilizo wazi kuhusu gharama, huduma anazohitaji na maendeleo ya matibabu yake. Dk. Baja alisisitiza kuwa utoaji wa taarifa sahihi humwezesha mgonjwa kuelewa huduma anayopewa na kushiriki ipasavyo katika maamuzi ya matibabu. Pia Dkt. Baja, amesema usalama wa mgonjwa unaweza kuathiriwa na changamoto mbalimbali, ikiwamo baadhi ya wagonjwa kuchelewa kufika hospitalini katika muda waliopangiwa, kutomuona daktari au kutofanyiwa vipimo walivyoelekezwa, pamoja na changamoto za miundombinu. Amesema hali hizo zinaweza kuongeza hatari ya madhara kwa mgonjwa, ikiwamo matumizi yasiyo sahihi ya dawa. Kwa upande wake, Daktari  bingwa wa Upasuaji toka BMH Kakorongo Mugisha amesema BMH inaendelea kuimarisha usalama wa wagonjwa kwa kuwajengea uwezo wataalamu wa afya na kuhakikisha huduma zinatolewa kwa kuzingatia taratibu za kitaalamu. Alisema pia wagonjwa wana haki ya kuamua iwapo wanataka wanafunzi washiriki wakati wa huduma zao, huku hospitali ikiendelea kutoa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi kwa kuzingatia ridhaa ya mgonjwa na usalama wake. Aidha, alisema muda wa kupata majibu ya vipimo hutegemea aina ya kipimo, ambapo baadhi ya vipimo vya kawaida vinaweza kutoa majibu ndani ya saa tatu, huku vipimo kama CT Scan na MRI vikitarajiwa kutoa majibu ndani ya saa 24 kulingana na taratibu za huduma. Nao Baadhi ya wagonjwa waliopatiwa huduma BMH wameeleza kuridhishwa na huduma wanazopata, huku wakitoa mapendekezo ya maboresho. Omary Namganda, mkazi wa Kigoma Mjini, aliwapongeza wataalamu wa afya kwa huduma wanazowapatia wagonjwa, wakati Jasery Zacharia wa Kahama, Shinyanga, alisema amepata huduma na ufuatiliaji katika matibabu ya tatizo la figo lililohusisha mawe. Kwa upande wake, Sospiter Chibanila aliitaka hospitali kuendelea kuboresha kasi ya upatikanaji wa majibu ya vipimo vinavyohitaji muda mrefu ili kuwawezesha wagonjwa kupata huduma kwa wakati.

Thu, 24 Sep 2026 14:48:19 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

RAIS SAMIA AONGOZA DHAMIRA YA AFRIKA KUTOKOMEZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepongezwa kwa uongozi wake mahiri katika kusukuma mbele ajenda ya Afrika ya kutokomeza vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama na mtoto, huku bara hilo likikabiliwa na karibu asilimia 70 ya vifo vya akina mama duniani na takribani theluthi mbili ya vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano. Akiwa Kinara wa Umoja wa Afrika katika Afya ya Mama na Mtoto, Rais Samia anaongoza ajenda ya “Malengo Matatu ya Sifuri” (Three Zeros) inayolenga kufikia sifuri ya kujifungulia nyumbani, sifuri ya vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama na mtoto mchanga, pamoja na sifuri ya watoto wasiopata chanjo. Ajenda hiyo imepewa msukumo katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Wakuu wa Nchi kuhusu Afya ya Mama, Mtoto Mchanga na Mtoto, iliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81), ukiwakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali, viongozi wa taasisi za Umoja wa Afrika, mashirika ya kimataifa ya afya na washirika wa maendeleo. Akiwasilisha ujumbe wa Rais Samia katika mkutano huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema ukubwa wa changamoto unahitaji Afrika kutoka kwenye ahadi na kuelekea katika hatua madhubuti zinazoweza kupimwa kwa maisha ya wanawake na watoto yanayookolewa. Amesema, pamoja na hatua ambazo Bara la Afrika limepiga, Afrika bado inachangia karibu asilimia 70 ya vifo vya akina mama duniani na takribani theluthi mbili ya vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano, huku sehemu kubwa ya vifo hivyo ikiwa inaweza kuzuilika. Makamu wa Rais amesema msukumo wa Rais Samia unalenga kuimarisha mifumo ya afya ya nchi za Afrika, kuongeza ufadhili wa ndani, kuboresha huduma za dharura na mifumo ya rufaa, kuongeza upatikanaji wa wahudumu wa afya wenye ujuzi na kuhakikisha takwimu zinatumika kufuatilia matokeo na kubaini maeneo yanayohitaji hatua zaidi. Akielezea uzoefu wa Tanzania, Makamu wa Rais amesema uwekezaji katika huduma za afya ya msingi na za dharura kwa mama na mtoto mchanga, pamoja na kuimarishwa kwa mifumo ya rufaa ikiwemo M-Mama, unaonesha namna uongozi wa kisiasa, teknolojia na utoaji wa huduma kwa wananchi vinavyoweza kuunganishwa katika kuokoa maisha. Hatua hizo zimekwenda sambamba na kuongezeka kwa wanawake wanaojifungulia katika vituo vya afya kutoka asilimia 51 mwaka 2015 hadi asilimia 81 mwaka 2022, mafanikio yanayoonesha uwezekano wa kubadili mwenendo wa vifo vya mama na mtoto pale uwekezaji unapounganishwa na utekelezaji katika ngazi ya jamii. Makamu wa Rais alisema ajenda anayoiongoza Rais Samia pia inatoa uzito kwa suala la Afrika kujitegemea katika afya, akisisitiza kuwa mafanikio hayapaswi kupimwa pekee kwa uwezo wa bara kugharamia, kuzalisha au kununua mahitaji yake, bali pia kwa uwezo wa kuhakikisha huduma muhimu zinamfikia kila mama na mtoto kwa wakati na mahali wanapozihitaji. Katika kufanikisha hilo, nchi za Afrika zimehimizwa kuimarisha uwajibikaji wa kisiasa, kuongeza uwekezaji wa ndani katika huduma zinazookoa maisha na kuhakikisha rasilimali zinafika hadi katika ngazi ya utoaji huduma. “Dhamira ni kuhakikisha hakuna mama anayepoteza maisha kwa kukosa usafiri, damu, mhudumu mwenye ujuzi au huduma ya dharura; hakuna mtoto mchanga anayefariki kwa kukosa huduma inayoweza kuokoa maisha yake, na hakuna mtoto anayebaki bila chanjo kwa sababu mfumo wa afya haukuweza kuifikia familia yake,” amesema Mhe. Ndejembi. Makamu wa Rais amesema kulinda uhai wa mama na mtoto si suala la afya pekee, bali ni uwekezaji katika rasilimali watu, uchumi na mustakabali wa Afrika, pamoja na kuwa sehemu muhimu ya utekelezaji wa Ajenda 2063 ya Bara la Afrika. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Africa CDC, Dkt. Jean Kaseya, alipongeza uongozi wa Rais Samia na kueleza dhamira ya Taasisi hiyo kuendelea kumuunga mkono katika jukumu lake la Kinara wa Umoja wa Afrika katika Afya ya Mama na Mtoto, huku akitaja hatua zilizopigwa na Tanzania kama mfano wa mafanikio yanayoweza kupatikana barani Afrika. Takwimu za Africa CDC zinaonesha kuwa Tanzania imepunguza uwiano wa vifo vya uzazi kwa takribani asilimia 80, kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2016 hadi 104 mwaka 2022, hatua inayohusishwa na kuimarishwa kwa huduma za dharura za uzazi na watoto wachanga, mifumo ya rufaa, ongezeko la wahudumu wa afya pamoja na ufuatiliaji wa vifo vya mama na watoto. Dkt. Kaseya alisema Africa CDC itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kusukuma mbele ajenda hiyo, akisisitiza umuhimu wa uongozi wa kisiasa, uwekezaji na mifumo imara ya afya katika kulinda uhai na ustawi wa mama na mtoto barani Afrika. Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Dkt. Adhanom Ghebreyesus amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuandaa mkutano huo na kuwa kinara wa Umoja wa Mataifa wa Afya ya Mama na Mtoto. Amesema katika kipindi cha miaka sita pekee, Tanzania imepunguza kiwango cha vifo vya kina mama kwa asilimia 81. Amesema kwa kuzindua mpango mkakati huo wa sifuri tatu (Three Zeros), Tanzania inaongoza kwa mfano na inapaswa kuungwa mkono. Amesema Shirika la Afya Duniani limejidhatiti kusaidia kila nchi mwanachama kulingana na mazingira yake na kufikia malengo yake kwa kuimarisha viwango vya huduma za kitabibu vinavyotumiwa na wahudumu walio mstari wa mbele kuokoa maisha ya kina mama na watoto wachanga. Kupitia nafasi yake kama Kinara wa Umoja wa Afrika katika Afya ya Mama na Mtoto, Rais Samia anasukuma dhamira ya kulifanya bara hilo kufikia hatua ambayo vifo vinavyoweza kuzuilika havitachukuliwa tena kuwa jambo lisiloepukika, huku kaulimbiu ya “Jiongeze, Tuwavushe Salama” ikibeba wito wa Afrika kwenda hatua ya ziada kwa ajili ya kila mama, mtoto mchanga, mtoto na kijana balehe. Mkutano huo, umehudhuriwa na Viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Dkt. Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) Dkt. Jean Kaseya, Mwenza wa Rais wa Benin Bi. Nathalie Vilette Wadagni, Wadau wa Maendeleo wakiwemo, Gates Foundation, Global Fund, Gavi, UNFPA, Unicef, Suzan Thompson Buffett Foundation, Beginning Fund pamoja na Viongozi kutoka Umoja wa Afrika (AU).

Thu, 24 Sep 2026 14:52:24 +0000
Uncategorized · The Standard

Mvurya says Sh15.27 billion disbursed through Youth Enterprise Development Fund

Read the full report from the original source.

Recently

Page 1068 of 1123 · 22448 stories