Search the region
22397 stories
Five judges have selected the top finalists of the Radiate Rwanda Awards
Read the full report from the original source.
RecentlyKRA intercepts 52,607 smuggled smartphones at Eldoret airport
Read the full report from the original source.
RecentlyNACADA seizes 4,248 liquor bottles, arrests two in Kapsabet The seized consignment was secured as evidence pending further legal processes.
The seized consignment was secured as evidence pending further legal processes.
RecentlyKahiga questions night-time use of county vehicle
Read the full report from the original source.
RecentlyUganda bets Shs180bn on PET scans
A cancer diagnosis can depend not only on whether a patient reaches a hospital, but on whether doctors have the technology to see where the…
RecentlyDk Saada aipongeza WHI kwa kutoa fursa za uwekezaji
Read the full report from the original source.
RecentlyVIJANA WAJENGEWA UWEZO WA KUZALISHA VIFARANGA BORA VYA SAMAKI
Farida Mangube Morogoro Zaidi ya vijana 60 kutoka mikoa mbalimbali nchini wamepewa mafunzo ya kuzalisha vifaranga bora vya samaki, ikiwa ni fursa ya kuwawezesha kuongeza kipato kupitia ufugaji na kujenga ujuzi katika sekta ya ufugaji wa samaki. Mafunzo hayo ya siku nne yanatolewa kwa vijana na wajasiriamali wanaojishughulisha na ufugaji wa samaki, kwa lengo la kuwapa ujuzi wa kuzalisha vifaranga bora na hatimaye kuvisambaza kwa wafugaji wengine. Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Janeth Rukanda, amesema Serikali imeamua kuwawezesha vijana kwa kuwa ongezeko la shughuli za ufugaji wa samaki limeongeza mahitaji ya vifaranga bora nchini. Amesema mafunzo hayo yatawasaidia vijana kufanya ufugaji kwa tija, kuongeza kipato na kuwa wazalishaji wa vifaranga watakaoweza kuwahudumia wafugaji wengine katika maeneo mbalimbali. “Lengo la Serikali ni kuwajengea uwezo vijana wengi zaidi juu ya uzalishaji wa vifaranga bora,” amesema Rukanda. Kwa mujibu wa Rukanda, tafiti za mwaka 2020 hadi 2025 zinaonyesha kuwa uzalishaji wa vifaranga umeongezeka, lakini ongezeko la mahitaji limeendelea kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa katika sekta ya ufugaji wa samaki. Makamu Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Samaki (FETA), Makao Makuu, Mezia Mparazo, amewataka vijana hao kuzingatia mafunzo wanayopewa ili waweze kutumia ujuzi huo katika shughuli zao za uzalishaji. “Msipokuwa makini na kuwasikiliza ipasavyo wakufunzi, mtaondoka bila kupata maarifa ya kutosha. Hili litakuwa hasara kwenu na kwa Serikali, kwa sababu mafunzo kama haya yanatumia gharama kubwa,” alisema Mparazo. Kwa upande wao, Gojo Muhammed na Radhia Suleiman, ambao ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo, wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kupata ujuzi wa uzalishaji wa vifaranga bora vya samaki. Wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuongeza ujuzi, kuboresha shughuli zao za ufugaji na kutengeneza fursa zaidi za kiuchumi kupitia uzalishaji wa vifaranga vya samaki.
Wed, 23 Sep 2026 15:53:38 +0000Le sénat évalue les réalisations communales et la mise en œuvre de la politique de décentralisation
Read the full report from the original source.
RecentlyLa CEJP appelle à mettre fin à l’écocide par le développement durable
Read the full report from the original source.
RecentlyOver 340 petitions: Which MPs will survive
Ugandans cast their ballots months ago. But in hundreds of electoral contests, the final word may now come not from the polling station but from…
RecentlyNindie asisitiza usimamizi wa vihatarishi kukabiliana na changamoto katika taasisi
Read the full report from the original source.
Recently‘MAJIBU YENU YATAWEKA MSINGI MPYA WA SHERIA YA UHAINI’ — LISSU
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV DAR ES SALAAM — Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameiambia Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, kuwa shauri la uhaini linalomkabili ni la kwanza katika historia ya Tanzania ambapo mshtakiwa ni mmoja na shtaka hilo halihusiani na kumuua Rais wala kuipindua Serikali. Lissu ameyasema hayo wakati akiendelea kutoa majumuisho yake ya mwisho mbele ya jopo la majaji watatu, wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akisaidiwa na Jaji James Karayemaha na Jaji Ferdinand Kiwonde. Amesema kesi hiyo ni ya tatu ya uhaini katika historia ya Tanzania, akitaja kesi za Grey Likungu Mataka na wenzake ya mwaka 1970 na Khatibu Ghandi na wenzake ya mwaka 1983. Kwa mujibu wa Lissu, kesi hizo mbili zilizotangulia zilihusu madai ya mipango ya kumuua Rais na kuipindua Serikali kwa kutumia silaha, tofauti na kesi inayomkabili ambayo imefunguliwa chini ya kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, kinachohusu uhaini kwa kuitishia Serikali. “Tofauti na hizo kesi mbili za mwanzo, hii ya kwangu imefunguliwa chini ya kifungu cha 39(2)(d) na uhaini wa hapa ni wa kuitishia Serikali. Hakuna kumuua Rais wala kuipindua Serikali. Hii ni kesi ya kwanza,” amesema Lissu. Amesema uamuzi utakaotolewa na Mahakama katika shauri hilo utaweka msingi wa kisheria kuhusu dhana ya uhaini kwa kuitishia Serikali na unaweza kuwa rejea katika kesi zijazo. “Vyovyote vile mtakavyoamua, mtaweka msingi wa kisheria kuhusu uhaini wa kuitishia Serikali. Waheshimiwa Majaji, mtaweka precedent ambayo itaongoza Mahakama zetu kwa miaka mingi ijayo,” amesema. Lissu amesema majaji hawataamua tu hatma ya mshtakiwa mmoja, bali pia wataweka msingi wa kisheria utakaoweza kutumika katika kuamua masuala kama hayo kwa miaka ijayo. “Kwahiyo Majaji, hamtahukumu mtu mmoja, kwahiyo mtaweka utaratibu wa kisheria utakaofuatwa miaka mingi ijayo. Waheshimiwa Majaji wangu, sihitaji kuwakumbusha uzito wa huo mzigo mliobebeshwa. Hamuamui guilt ya mtu mmoja, bali mzigo wa kisheria kwa masuala haya for many years to come,” amesema. Lissu amesema utetezi wake tangu mwanzo haukuwa wa kukanusha maneno aliyoyasema, bali ulikuwa ukilenga kuieleza Mahakama msingi wa kisheria kwamba, kwa mtazamo wake, kauli za kisiasa hazijawahi kutengeneza kosa la uhaini. Akiifafanua dhana hiyo ya kisheria, Lissu ametaja hoja sita anazodai zinapaswa kuthibitishwa ili kosa hilo liweze kutengenezwa, ikiwemo kuwepo kwa nia madhubuti (mens rea), uchochezi unaolenga mtu au kundi maalumu la watu, pamoja na matokeo yanayoonekana kwa mujibu wa kifungu cha 10(2) cha Kanuni ya Adhabu. Amedai kuwa pale sheria inapohitaji kuwepo kwa nia katika kosa, ni lazima matokeo ya nia hiyo yaonekane na kuthibitika. Kwa mtazamo wake, iwapo hakuna matokeo yaliyotokea, maana yake ni kwamba nia hiyo haikutimia na hivyo kosa la uhaini haliwezi kuwepo. Aidha, Lissu amesema baada ya Mahakama kusikiliza mashahidi 17 wa upande wa mashtaka na kupokea vielelezo 16 vya utetezi, bila kuwepo kwa kielelezo cha Jamhuri, kesi ya Serikali imekuwa dhaifu zaidi ikilinganishwa na ilivyokuwa wakati ilipowasilishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). Katika hatua nyingine ya majumuisho yake, Lissu ameiomba Mahakama kutathmini iwapo yeye ndiye aliyeitisha mkutano huo na kuwaalika wanahabari, pamoja na iwapo alikuwa na nia ya kuchochea kundi la watu kuzuia uchaguzi kwa lengo la kuitishia Serikali. Kesi hiyo bado inaendelea, huku Lissu akiendelea kuwasilisha majumuisho yake ya mwisho mbele ya Mahakama.
Wed, 23 Sep 2026 15:47:57 +0000TFS YATOA MADAWATI 50, YAOKOA WANAFUNZI 150 KUKAA CHINI KILOSA
Farida Mangube, Kilosa Morogoro Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Mashariki, kupitia Ofisi ya Mhifadhi Misitu Wilaya ya Kilosa, imekabidhi madawati 50 yenye thamani ya Sh milioni 12 kwa Shule ya Msingi Mazinyungu, ikiwa ni sehemu ya mpango wa taasisi hiyo kurejesha kwa jamii. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo kwa niaba ya Kamanda wa TFS Kanda ya Mashariki, SACC Nethew Ntilicha, Mhifadhi Misitu wa TFS Wilaya za Kinondoni na Ubungo Dotto Ndumbikwa amesema msaada huo ni sehemu ya utaratibu wa TFS kurudisha kwa jamii huku akiwataka wakazi wa Kilosa kuendelea kutunza misitu kwa kuwa faida zinazotokana na uhifadhi wake ndizo zinazowezesha shughuli za kijamii kama utoaji wa msaada huo. Ndumbikwa amesema TFS inaendelea kushirikiana na wadau katika kulinda na kuhifadhi rasilimali za misitu, huku akisisitiza kuwa jamii ina nafasi kubwa katika kuhakikisha misitu inalindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, ameishukuru TFS kwa msaada huo akisema umefika wakati muafaka kutokana na ongezeko la idadi ya watoto wanaojiunga na shule. Amesema serikali haiwezi kufanya kila kitu bila ushirikiano wa wadau, hivyo akaitaka TFS kuendelea kuifikia shule nyingine zenye mahitaji pia amesisitiza umuhimu wa jamii kupanda na kutunza miti, akisema Kilosa haitakiwi kuwa jangwa, huku akibainisha kuwa walimu wana nafasi muhimu kuwafundisha watoto umuhimu wa uhifadhi ili ujumbe huo usambae katika jamii. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mazinyungu Kajika Gallani amesema msaada huo umepunguza changamoto ya upungufu wa madawati na kuwawezesha wanafunzi 150 waliokuwa wakikaa chini kupata sehemu za kukaa hata hivyo amesema shule hiyo bado ina upungufu wa madawati 50 na kuomba wadau wengine kuiga mfano wa TFS. Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi Kaka Mkuu wa shule hiyo, Marco Ng’ondya, mwanafunzi wa Darasa la Sita, ameishukuru TFS kwa msaada huo akisema awali baadhi ya wanafunzi walilazimika kukaa chini, hali iliyowafanya kupata changamoto katika kuandika, kuchafua sare na kushindwa kumfuatilia mwalimu kwa umakini. Aliahidi kuwa wanafunzi wataitumia fursa hiyo kusoma kwa bidii na kufanya vizuri katika masomo, huku akiomba wadau wengine kuendelea kusaidia shule hiyo kukamilisha mahitaji yaliyopo.
Wed, 23 Sep 2026 15:51:11 +0000Ces Africains exploités dans les centres d'arnaques en Asie
Read the full report from the original source.
RecentlyVers l’exemption de visa pour des titulaires de passeports diplomatiques et de service
Read the full report from the original source.
RecentlyHuit abris ingénieux pour la faune sauvage à travers le monde
D'un abri pour chauves-souris dans la campagne britannique à un refuge multispécifique dans les Catskills, voici huit havres de paix pour la faune sauvage conçus avec ingéniosité.
RecentlyLa sécurité du marché moderne de Bugenyuzi sera renforcée
Read the full report from the original source.
RecentlyGermany news: Call to scrap once-a-day gas price rises
Read the full report from the original source.
RecentlyAline Ishimwe turned a dream into a tourism destination business
When Aline Ishimwe looks at her journey in hospitality, she does not only see the growth of a tourism business. She sees a process of
RecentlyMulwa family to take plea in Dr Victoria Mutiso murder case next week
News · Quick read
RecentlyPage 1090 of 1120 · 22397 stories