Unganishwa

Search the region

22391 stories

Uncategorized · Yaga Burundi

article comment count is: 0

Il est venu de Kamenge, armé de son flow, de sa foi et d’une énergie débordante. Face à plus de 600 candidats, Double D s’est hissé jusqu’à la deuxième place de NeXstar 2026. Retour sur le parcours d’un jeune rappeur […]

Recently
Uncategorized · Yaga Burundi

Stève Cédric Bizimana

Une nouvelle réforme du système éducatif est annoncée par le gouvernement burundais pour 2026-2027. Sur le terrain, le constat est sans appel : plus d’une décennie après l’instauration de l’École fondamentale, la qualité

Recently
Uncategorized · Yaga Burundi

article comment count is: 0

Une nouvelle réforme du système éducatif est annoncée par le gouvernement burundais pour 2026-2027. Sur le terrain, le constat est sans appel : plus d’une décennie après l’instauration de l’École fondamentale, la qualité

Recently
Uncategorized · Yaga Burundi

article comment count is: 0

Elle est maman, chanteuse et désormais troisième de NeXstar. Derrière la voix douce de Ka Kelly se cache une femme qui a dû se battre contre les préjugés et les doutes pour atteindre la lumière. Son parcours, de ses prem

Recently
Uncategorized · HabariLeo

Wizara ya Nishati yatwaa Tuzo Utendaji MEL 2026

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

WATU NANE WAFARIKI AJALI YA COASTER NA SCANIA RUFIJI

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani WATU nane wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa baada ya gari la abiria aina ya Toyota Coaster kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania katika eneo la Chumbi, Kata ya Chumbi, Tarafa ya Mohoro wilayani Rufiji mkoani Pwani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rufiji, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Protas Mutayoba, amesema ajali hiyo ilitokea Septemba 22, 2026, saa 9:15 mchana katika barabara kuu ya Lindi–Dar es Salaam. Amesema ajali hiyo ilihusisha Toyota Coaster yenye namba za usajili T930 ERF, iliyokuwa ikiendeshwa na Halifan Cosmas Madodo (44), na lori aina ya Scania lenye namba za usajili T511 EPS, likiwa na tela namba T469 EPL, lililokuwa likiendeshwa na Hassan Salum Goro (30). Kwa mujibu wa Mutayoba, watu wanane waliokuwa ndani ya Toyota Coaster walifariki dunia, huku wengine 12 wakijeruhiwa katika ajali hiyo. Ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Coaster, ambaye alishindwa kulimudu gari lake na kusababisha kuhamia upande wa kulia wa barabara, ambako liligongana uso kwa uso na lori hilo. Mutayoba amesema majeruhi wamepelekwa katika Kituo cha Afya Mohoro kwa ajili ya matibabu, huku baadhi yao wakitarajiwa kuhamishiwa katika hospitali kubwa kwa uchunguzi na matibabu zaidi. Ametoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kusababisha vifo, majeraha na uharibifu wa mali.

Wed, 23 Sep 2026 14:14:00 +0000
National · Citizen Digital

KPA boss William Ruto given 14 days to respond to petition on term expiry

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

WAZEE CCM RUKWA WATAKIWA KUHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA MWENGE

Na Jane Mwakyoma, Rukwa MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Rukwa, Silafu Maufi, amewataka wajumbe wa Baraza la Wazee wa chama hicho mkoani humo kuendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, kinachotarajiwa kufanyika mkoani Rukwa Oktoba 14, mwaka huu. Maufi ametoa rai hiyo leo wakati alipokutana na kuzungumza na wajumbe wa Baraza hilo kuhusu maandalizi ya mapokezi na kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, akisisitiza umuhimu wa wazee kushiriki kikamilifu katika maandalizi na kuhamasisha jamii kujitokeza katika shughuli hiyo ya kitaifa. Aidha, amesema kilele hicho kitaambatana na Wiki ya Vijana, ambapo vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini wataonesha shughuli za maendeleo wanazozifanya. Maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa Oktoba 8, mwaka huu. Kwa upande wao, wajumbe wa Baraza la Wazee la CCM Mkoa wa Rukwa wameahidi kutoa ushirikiano katika kufanikisha shughuli zote za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru na kilele chake, pamoja na kuendelea kuelimisha makundi mbalimbali ya jamii kuhusu umuhimu wa Mwenge wa Uhuru kitaifa.

Wed, 23 Sep 2026 14:08:37 +0000
Business · Issa Michuzi

DKT. SAADA: WHI IONGEZE ELIMU YA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Ikulu) anayesimamia Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, ametembelea banda la Watumishi Housing Investments (WHI) lililopo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wakaguzi wa Ndani unaofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 21 hadi 25 Septemba, 2026. Akiwa katika banda la WHI, Mhe. Dkt. Saada alipata maelezo kuhusu huduma na fursa mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo, ikiwemo uwekezaji kupitia Faida Fund, huduma ya e-Wekeza pamoja na fursa mbalimbali za kumiliki nyumba. Aidha, alipata nafasi ya kufahamu baadhi ya miradi ambayo WHI imeisimamia na kuitekeleza katika nafasi yake kama Mshauri Elekezi na Mkandarasi wa Ujenzi Daraja la Kwanza. Baada ya kupokea maelezo hayo, Mhe. Dkt. Saada aliipongeza WHI kwa kazi nzuri inayofanya, huku akisisitiza umuhimu wa taasisi kuendelea kuongeza juhudi za kujitangaza na kutoa elimu kwa umma ili huduma na fursa hizo ziweze kuwafikia wananchi wengi zaidi. Alisisitiza zaidi umuhimu wa wananchi kuendelea kufikiwa na elimu kuhusu fursa za uwekezaji, hususan kupitia Faida Fund, ili waweze kufahamu namna wanavyoweza kuwekeza na kunufaika na fursa zilizopo. WHI inaendelea kutumia majukwaa mbalimbali kuwafikia wananchi, kutoa elimu kuhusu huduma zake na kutangaza fursa za uwekezaji, umiliki wa nyumba pamoja na huduma zake za ujenzi na ushauri elekezi.

Wed, 23 Sep 2026 14:10:28 +0000
Health · Issa Michuzi

MSD YAINGIZA SHEHENA YA KWANZA YA DAWA YA KUDHIBITI URAIBU WA POMBE

Na Mwandishi Wetu BOHARI ya Dawa (MSD) imefanikiwa kuingiza nchini shehena ya kwanza ya dawa ya Naltrexone , inayotumika katika matibabu ya uraibu wa pombe. Hatua hiyo ni matokeo ya ushirikiano wa kimkakati kati ya MSD na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe , katika kuimarisha huduma za matibabu ya uraibu wa pombe nchini. Akizungumza kupitia taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa MSD, Etty Kusiluka , amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa makubaliano ya kuimarisha huduma kati ya MSD na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, hususan katika kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za kudhibiti uraibu wa pombe. “Dawa ya Naltrexone itapatikana na kuratibiwa na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, huku ikiwa ni bidhaa itakayoendelea kununuliwa na MSD kwa ajili ya taasisi hiyo,” amesema. Amesema mapema mwezi huu, wakati wa mafunzo kuhusu matumizi ya dawa hiyo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe , aliiagiza MSD kuharakisha upatikanaji wa vidonge hivyo. Kusiluka ameongeza kuwa kupokelewa na kuingizwa nchini kwa shehena hiyo ni hatua muhimu katika kuimarisha huduma za afya ya akili na tiba ya uraibu wa pombe. Amesema mafanikio hayo yanaonesha juhudi za Serikali kupitia MSD na wadau wa sekta ya afya kuhakikisha bidhaa muhimu na za kimkakati za afya zinapatikana nchini kwa wakati.

Wed, 23 Sep 2026 14:05:45 +0000
National · Citizen Digital

NCIC summons Didmus Barasa over ‘dismiss Kikuyu job seekers’ remarks

Read the full report from the original source.

Recently
National · Capital FM

KMA warns of rough seas, strong winds along Kenya coast through December

Latest · Kenya

Recently
National · Daily News

Dr Mwinyi opens 3rd Zanzibar Organic Festival, pledges to continue bolstering agricultural products

ZANZIBAR: PRESIDENT of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council, Dr Hussein Ali Mwinyi, said his government will continue investing…

Recently
Business · Issa Michuzi

BALOZI MATINYI ATEMBELEA WAZALISHAJI MASHINE ZA BIDHAA ZA KILIMO ALGERIA

Na Mwandishi Wetu BALOZI wa Tanzania nchini Algeria, Mobhare Matinyi, leo Septemba 23, 2026, amefanya ziara katika kiwanda cha kampuni ya CAM SARL kilichoko nje kidogo ya jiji la Algiers, kinachotengeneza mashine za kusindika na kufungasha mazao ya kilimo na dawa za tiba. Katika ziara hiyo, Balozi Matinyi alifanya majadiliano na timu ya menejimenti ya kampuni hiyo iliyoongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu Bouzid Belhadj, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha Abderraouf Belhadj, na Mkurugenzi wa Uendeshaji Alaaeddine Belhadj. Lengo la majadiliano hayo lilikuwa kuangalia uwezekano wa kampuni hiyo kutengeneza mashine mahsusi kwa ajili ya kusindika na kufungasha mazao yanayolimwa nchini. Balozi Matinyi aliielezea kampuni ya CAM kwamba Serikali ya Tanzania imeweka sera na mikakati ya kuhakikisha bidhaa za kilimo za Tanzania zinaongezewa thamani kabla ya kuuzwa kwenye soko la kimataifa. Akitoa mifano ya mazao ya chakula yanayolimwa nchini, kama matunda, mbogamboga, viungo, nafaka, korosho, karanga na hata alizeti, chai na kahawa, Balozi Matinyi alielezea matumaini yake kwamba ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Algeria utaiwezesha kampuni hiyo kutoa mchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya kilimo nchini. Mtendaji Mkuu wa CAM, Belhadj, alimshukuru Balozi Matinyi kwa ziara hiyo na kuahidi kuendeleza ushirikiano na Tanzania pamoja na kufanya ziara nchini ili kujionea fursa na mahitaji yaliyopo. Kampuni ya CAM hutumia wataalamu wa Algeria kutengeneza mashine hizo kwa kutumia teknolojia ya nchi za Ujerumani, Italia na Hispania, na tayari imeshaanza kuingia katika masoko ya nchi jirani na Algeria ikiwemo Tunisia. Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare Matinyi, akiagana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya CAM SARL, Bouzid Belhad, ambayo hutengeneza mashine za kusindika na kufungasha dawa na mazao ya kilimo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa CAM, Abderraouf Belhadj, na kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji, Alaaeddine Belhadj.

Wed, 23 Sep 2026 13:58:55 +0000
Business · Issa Michuzi

CHANZO MGOGORO MIGODI YA INK,MAYOMBA CHATAJWA

Na George Maziku, Mbogwe CHANZO cha mgogoro baina ya mgodi wa INK na Mayombya Gold Mine iliyopo kata ya Lugunga, wilayani Mbogwe, mkoa wa Geita, kimewekwa hadharani. Mgogoro huo umesababisha Serikali kuifunga migodi hiyo kwa muda mwisho wa wiki iliyopita ili kupisha uchunguzi, unadaiwa kuchochewa na kampuni ya Dwasi Simon Company Limited, inayomiliki duara namba F1 iliyopo ndani ya leseni ya Mayombya Gold Mine. Akitoa ufafanuzi kuhusu mgogoro huo, Meneja Mkuu wa mgodi wa Mayombya Gold Mine Majuto Manyilizu alisema uongozi wa mgodi wake hauwatambui wachimbaji wa kigeni kutoka China, bali unamtambua na umeingia mkataba na mwekezaji mtanzania aitwaye Dwasi Simon Company Limited anaemiliki duara namba F1. “Kwenye leseni yangu sina wachimbaji wachina, siwatambui wala sijaingia mkataba na wachina,nimeingia mkataba na mwekezaji anayeitwa Dwasi Simon Company Limited ambaye anamiliki duara namba F1, huyu ndiye ninamtambua kama mwekezaji kwenye leseni yangu”, alifafanua Manyilizu. Hata hivyo, Manyilizu alikiri kufahamu uwepo wa raia hao wa kigeni kutoka China, wanaofanya kazi ya uchimbaji kwenye kitalu kinachomilikiwa na Dwasi Simon Company Limited. Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo mgogoro baina ya migodi hiyo miwili inayohusu kuingiliana kwa mipaka pamoja na matumizi ya milipuko mikubwa inaayodaiwa kufanywa na mgodi wa Mayombya ambayo inaathiri shughuli za uchimbaji katika mgodi wa INK. Mgogoro huo ulichukua sura mpya Ijumaa, wiki iliyopita, baada ya uamuzi wa Tume ya Madini nchini kusitisha shughuli za uchimbaji katika migodi yote miwili ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na wataalamu wa tume hiyo. Kiini cha mgogoro huo kinadaiwa kuwa ni vitendo vya wachimbaji wa kichina kuendesha shughuli za uchimbaji bila kuzingatia kwanza mipaka baina ya mgodi wa Mayombya na mgodi jirani wa INK, ambapo inadaiwa wamevuka mpaka na kuingia eneo la leseni la mgodi wa INK. “Mojawapo ya changamoto zilizozalisha mgogoro huu ni shughuli za kichimbaji za daraja la kati zinazoendeshwa katika leseni ya jirani zetu kwa kutumia raia wa kigeni ambazo zinaambatana na milipuko mikubwa ambayo zimeleta athari kubwa katika maduara yanayomilikiwa na wachimbaji wadogo kwenye mgodi wetu… “Uchunguzi wa awali unaashiria hatari kubwa kama hatua za haraka hazitachukuliwa kunaweza kutokea ajali kubwa na kusababisha mauaji ya wachimbaji wengi”, alisisitiza Meneja Mkuu wa mgodi wa INK Farid Lugwisha. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Dwasi Simon Company Limited , Dwasi Simon alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi wa mgogoro huo hakuwa tayari kuzungumza kwa madai alikuwa msibani wilayani Bariadi, mkoani Simiyu, hivyo akimtaka mwandishi kusubiri hadi atakaporejea Mbogwe.

Wed, 23 Sep 2026 14:02:37 +0000
National · Capital FM

Kindiki: Kenya Kwanza implementing manifesto ‘project by project’

Kenya · 3 hours ago

Recently
National · Capital FM

Kakuzi birdwatching tour ends in triumph as Japanese royalty sights rare migratory birds

Latest · Kenya

Recently
Business · The Star Kenya

Dramatic eviction of woman aged 87 highlights Spain's housing shortage Maricarmen's father first rented the property in 1956 and she continued as the tenant after her parents died

Maricarmen's father first rented the property in 1956 and she continued as the tenant after her parents died

Recently
National · Daily News

REA pledges to complete distribution of power in all rural hamlets by 2030

DODOMA: THE Tanzanian government is committed to completing electricity distribution projects in all rural hamlets by 2030, a move expected…

Recently
World · DW Rwanda

UN General Assembly: Syria's al-Sharaa kicks of Day 2

Read the full report from the original source.

Recently

Page 1093 of 1120 · 22391 stories