Unganishwa

Search the region

22526 stories

Uncategorized · Daily News

Tanzania launches e-prescription to monitor the sale, use of prescription-only medicines

DODOMA: THE Tanzanian government has warned that it will take strict action against traders selling medicines in violation of regulations,…

Recently
Uncategorized · Daily News

Yas year-end campaign to benefit customers

DAR ES SALAAM: YAS Tanzania has said continued investment in telecommunications infrastructure is essential to improving connectivity reliability, expanding access…

Recently
Uncategorized · KBC

Humanising the police: IPOA hails senior police officer’s street dance with children

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Afrique

Destruction des points d'eau, quel impact sur la santé des enfants ?

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Le Mali valide son billet pour la CAN 2027 après une victoire contre le Rwanda

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Spending on development projects (Sh bn)

The Q1 2026/2027 outlay marks a sharp increase compared to previous financial years recorded over a seven-year period.

Recently
Uncategorized · Daily News

High Commissioner Kaganda invites Tanzanian entrepreneurs to participate in  Zimbabwe’s ZITF

ZIMBABWE: Tanzania’s High Commissioner to Zimbabwe, Suzan Kaganda, has received a delegation from the Parliamentary Standing Committee on Justice, Ethics…

Recently
World · Daily News

Tanzania, Finland commit to cement ties in diplomacy,conflict mediation in Great Lakes

DAR ES SALAAM: TANZANIA and Finland have expressed their commitment to strengthening cooperation in diplomacy, mediation and conflict prevention, particularly…

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

THBUB, DIHR KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA ULINZI WA HAKI ZA BINADAMU

NA MWANDISHI WETU TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesema ushirikiano wake na Taasisi ya Haki za Binadamu ya Denmark (DIHR) umechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha juhudi za kukuza na kulinda haki za binadamu nchini, hususan katika masuala ya biashara na haki za binadamu pamoja na usimamizi wa rasilimali za bahari. Mwenyekiti wa THBUB, Wakili Dunford George Mpelumbe, amesema hayo alipokutana na ujumbe wa DIHR jijini Dar es Salaam, akieleza kuwa ushirikiano huo ulioanza mwaka 2017 umewezesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali, ikiwemo tathmini ya hali ya biashara na haki za binadamu, kuandaa Mpango Kazi wa Taifa wa Biashara na Haki za Binadamu na kujenga uwezo wa watumishi. Amesema Tume pia imefanya uchambuzi kuhusu haki za wavuvi wadogo na upatikanaji wa rasilimali za baharini kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu, hatua iliyosaidia kuongeza uelewa wa jamii za pwani kuhusu haki zao na ushiriki katika maamuzi. Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuharakisha kupitishwa na kutekelezwa kwa Mpango Kazi wa Taifa wa Biashara na Haki za Binadamu, kuimarisha mifumo ya kushughulikia malalamiko na kuhakikisha haki za binadamu na mazingira zinazingatiwa katika sekta mbalimbali za uchumi. Kwa upande wake, Mshauri wa Haki za Binadamu, Biashara na Teknolojia wa DIHR, Bernard Ochieng, ameishukuru THBUB kwa ushirikiano mzuri na kuahidi kuendeleza mahusiano hayo yenye tija.

Thu, 19 Nov 2026 09:14:12 +0000
Uncategorized · The Citizen

23 US Peace Corps volunteers begin two-year assignments in Tanzania

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Citizen

Concern as Tanzania airlines still face EU safety ban

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Parliamentary leaders meet Auditor General to strengthen institutional cooperation

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Rwanda Agriculture Minister received new IFAD Country Director

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · SoftPower News

Minister Santa Alum Visit Exposes Inactive Emyooga SACCOs, Extortion and Staffing gaps in Karamoja

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

KEBS seizes 54 bales of maize flour over licensing breach

The agency urged consumers to exercise caution when purchasing packaged products and verify that they have been certified by the regulator

Recently
Uncategorized · Daily News

Tanzania hailed for successful Military-Civilian Cooperation Week

DAR ES SALAAM: TANZANIA has been commended for successfully hosting the Sixth East African Community (EAC) Military-Civilian Cooperation Week, held…

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Dozens missing after boat carrying 100 migrants sinks off Senegal

Initial reports said that one person had died, but some local media have reported that at least four bodies have been recovered. Dozens of people still missing

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

TIRA YATAKIWA KUDUMISHA VIWANGO VYA KIMATAIFA VYA UBORA WA HUDUMA

Na. Joseph Mahumi, WF, Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, ameitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa upatikanaji wa Cheti cha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora ISO 9001:2015 unakuwa chachu ya kuimarisha uwajibikaji, ufanisi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi na wadau wa sekta ya bima nchini. Ametoa msisitizo huo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Cheti cha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora ISO 9001:2015 kwa TIRA, iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Bima House, Njedengwa jijini Dodoma, ambapo alisema kupata cheti hicho si mwisho wa safari ya ubora, bali ni mwanzo wa hatua nyingine ya kuimarisha utendaji wa taasisi hiyo kwa kuzingatia viwango vinavyotambulika kimataifa. Dkt. Mwamba alisema mafanikio hayo yanaonesha dhamira ya TIRA katika kuimarisha mifumo yake ya kiutendaji, kuzingatia taratibu na viwango vya ubora, pamoja na kuongeza uwezo wa taasisi katika kutekeleza majukumu yake ya kusimamia na kuendeleza sekta ya bima nchini. “Cheti hiki kisiwe pambo la ofisi au nyaraka ya kutunzwa kwenye mafaili pekee, bali kiwe kielelezo cha utamaduni wetu wa kazi na dhamira yetu ya kutoa huduma bora kila siku,” alisisitiza Dkt. Mwamba Aidha alieleza kuwa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora (ISO 9001:2015) una umuhimu mkubwa katika kuimarisha michakato ya kazi, ufuatiliaji wa utekelezaji wa majukumu, utatuzi wa changamoto na matumizi ya maoni ya wadau kama nyenzo ya kuboresha huduma zinazotolewa na taasisi. Dkt. Mwamba alisema mafanikio ya TIRA katika kupata cheti hicho yanaendana na mwelekeo wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayosisitiza mageuzi ya kitaasisi na uimarishaji wa mifumo ya utoaji huduma ili kujenga taasisi imara, zenye ufanisi na zinazoweza kuchochea maendeleo endelevu ya Taifa. Akizungumzia mchango wa sekta ya bima katika uchumi wa Taifa, Dkt. Mwamba aliipongeza TIRA kwa juhudi za kusimamia sekta hiyo, kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma za bima na kuendeleza mazingira bora ya ukuaji wa soko la bima nchini ambapo mwaka 2025 ilichangia asilimia 2.11 ya Pato la Taifa. “Natoa rai kwenu kuendelea kuzihimiza kampuni za bima nchini kuwekeza katika mifumo ya usimamizi wa ubora ili kuimarisha ushindani, kuongeza uaminifu wa wateja na kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakidhi viwango vinavyotambulika kimataifa” alisema Dkt Mwamba. Alilipongeza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa utaalamu, mwongozo na ushirikiano uliowezesha TIRA kufikia hatua hiyo, huku akilihimiza shirika hilo kuendelea kusaidia taasisi nyingine nchini kuimarisha mifumo yao ya usimamizi wa ubora. Kwa upande wake Kamishna wa Bima nchini ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware, alisema kuwa Mamlaka hiyo inalenga kuhakikisha kuwa ofisi zake zote nchini zinafikia viwango hivyo ifikapo mwaka 2028. Dkt. Saqware alisema kuwa katika kufikia azma hiyo, TIRA itaendelea kuimarisha maeneo mbalimbali ya utoaji huduma ikiwemo miundombinu na majengo ya ofisi, uwezo wa watumishi pamoja na michakato ya kiutendaji inayotumika katika kutoa huduma kwa wananchi na wadau wa sekta ya bima. “TIRA itaendelea kuboresha mazingira ya kazi na mifumo ya utoaji huduma ili kuhakikisha kuwa wadau wote, wakiwemo wananchi, Serikali, kampuni za bima, watumishi na watoa huduma, wanapata huduma zinazokidhi viwango vinavyotakiwa” alisema Dkt. Saqware. Naye, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Ubora, wa Shirika la Ubora Tanzania -TBS, Mhandisi Abdallah Kileo, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TBS, alisema kuwa kupata Cheti cha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora ISO 9001:2015 kwa TIRA ni hatua muhimu inayoonesha dhamira ya Mamlaka hiyo katika kuimarisha mifumo ya usimamizi, kuongeza ufanisi na kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa wananchi na wadau wa sekta ya bima zinakidhi viwango vinavyotambulika kimataifa. Alisema kuwa uthibitisho huo unahusisha ofisi tano za TIRA, zikiwemo Makao Makuu ya Dodoma, Ofisi ya Zanzibar, Ofisi ya Dar es Salaam pamoja na Ofisi za Kanda ya Mashariki na maeneo mengine yaliyohusika katika utekelezaji wa mfumo huo. “Mfumo huu wa ISO 9001:2015 unatoa mwongozo wa kuimarisha taratibu za usimamizi wa ubora, uwajibikaji na ufuatiliaji wa michakato ya kiutendaji, huku ukilenga kuhakikisha taasisi zinakidhi mahitaji ya wateja na kufanya maboresho endelevu ya huduma” alisema Mhandisi Kileo. Aliongeza kuwa umuhimu wa mfumo huo kwa TIRA unatokana na ukubwa wa majukumu yake, yakiwemo kutoa leseni kwa kampuni na wadau wa sekta ya bima, kusimamia ushindani wa haki, kulinda maslahi ya wateja, kudhibiti shughuli za bima na kusimamia biashara za bima zinazovuka mipaka ya nchi, ambazo zinahitaji mifumo madhubuti ya usimamizi na uzingatiaji wa viwango vya ndani na kimataifa. Alieleza kuwa TBS itaendelea kutoa huduma za upimaji, uthibitishaji na tathmini ya mifumo ya usimamizi wa ubora kwa taasisi za Serikali na sekta binafsi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ubora, ufanisi na ushindani wa huduma na bidhaa nchini. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, akizungumza jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Cheti cha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora ISO 9001:2015 iliyotolewa kwa TIRA, na Shirika la Ubora Tanzania -TBS, iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Bima House, Njedengwa jijini Dodoma, ambapo aliitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa upatikanaji wa vyeti hivyo inakuwa chachu ya kuimarisha uwajibikaji, ufanisi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi na wadau wa sekta ya bima nchini. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (Katikati), akipokea Cheti cha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora ISO 9001:2015 iliyotolewa kwa TIRA, na Shirika la Ubora Tanzania -TBS, wakati wa hafla ya makabidhiano ya Vyeti vya Ubora iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Bima House, Njedengwa jijini Dodoma. Anayemkabidhi cheti hicho ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Ubora, wa Shirika la Ubora Tanzania -TBS, Mhandisi Abdallah Kileo (kulia), na kushoto ni Kamishna wa Bima nchini ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (kulia), akikabidhiwa Tuzo ya kutambua mchango wake katika Tasnia ya Bima, kutoka kwa Kamishna wa Bima nchini ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware, wakati wa hafla ya makabidhiano ya Cheti cha Mfumo wa Usimamizi wa Ubora ISO 9001:2015 iliyotolewa kwa TIRA, na Shirika la Ubora Tanzania -TBS, iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Bima House, Njedengwa jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma )

Thu, 19 Nov 2026 09:03:43 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

KAMPENI YA UGAWAJI WA VYANDARUA RUVUMA YAZINDULIWA RASMI

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed amezindua rasmi kampeni ya usambazaji na ugawaji wa vyandarua bure kwa wananchi wa mkoa huo, ikiwa ni mkakati wa kufikia lengo la kutokomeza malaria nchini (Zero Malaria) ifikapo mwaka 2030. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Brigedia Jenerali Ahmed amesema kiwango cha maambukizi ya malaria mkoani Ruvuma bado kiko juu ya wastani wa kitaifa, hali inayolazimu kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo. Pamoja na mambo mengine, RC Ahmed amekemea tabia ya baadhi ya wananchi kutumia vyandarua kinyume na malengo, ikiwemo kuvitumia kuvulia samaki na kuzungushia bustani za mbogamboga. Pia, ametoa wito kwa wananchi wa maeneo ya mijini na vijijini kuzingatia usafi wa mazingira, kudhibiti mazalia ya mbu kwa kutumia viuatilifu vya kuua viluilui, pamoja na kuacha matumizi holela ya dawa bila kupima ili kujua ugonjwa halisi. Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Wakili Mary Makondo, amesema kulinda afya za wananchi ni msingi muhimu wa kuwa na nguvu kazi imara itakayochangia ukuaji wa pato la kaya na taifa kwa ujumla. Kwa upande wake, Mwakilishi wa Bohari ya Dawa (MSD), Mboyi Wishega, amesema vyandarua 901,336 vitasambazwa katika vituo 888 vya kutolea huduma kwenye halmashauri tano za mkoa huo ambazo ni Madaba, Namtumbo, Nyasa, Songea Vijijini na Tunduru. Kwa upande mwingine, Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Peter Gitanya, amesisitiza umuhimu wa kudhibiti vyandarua hivyo visichepushwe kwenda nchi jirani ili malengo ya kitaifa ya kutokomeza malaria yaweze kutimia. Akitoa Takwimu za ugonjwa wa Malaria za mkoa wa Ruvuma, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Louis Chomboko, amesema mkoa umefanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria kutoka asilimia 26 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 8.3 sasa. Mkazi wa Manispaa ya Songea, Jacob Lwambano, ameishukuru serikali kwa kujali afya za wananchi na kuahidi kuwa watavitunza vyandarua hivyo na kuvitumia kwa lengo lililokusudiwa

Thu, 19 Nov 2026 09:05:09 +0000
Uncategorized · The Standard

Isiolo residents cautioned over floodwaters

Read the full report from the original source.

Recently

Page 127 of 1127 · 22526 stories