Search the region
22529 stories
Ukraine: Civilian casualties in 2026 already far exceed previous years’ tolls
Read the full report from the original source.
RecentlyRuto: I’ve delivered, give me second term
President William Ruto has used his State of the Nation Address to defend his administration’s performance and make a case for another term
RecentlyPWANI YAPONGEZA UZINDUZI KITAMBULISHO KIPYA CHA TAIFA
Na Said Mwishehe,Michuzi Blog MKUU wa Mkoa wa Pwani, Stanlaus Nyongo, ameipongeza Serikali kwa maboresho ya huduma za usajili na utambuzi wa watu kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), akisema teknolojia mpya ya uzalishaji wa vitambulisho itaimarisha usalama, ubora na ufanisi wa huduma hizo. Amesema uzinduzi wa kitambulisho kipya cha taifa pamoja na teknolojia mpya ya uzalishaji wake ni hatua muhimu katika kuboresha mfumo wa utambulisho wa wananchi na kurahisisha upatikanaji wa huduma za NIDA. Nyongo aliyasema hayo leo Novemba 18,2026 wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitambulisho kipya cha taifa na teknolojia mpya ya uzalishaji wa vitambulisho, iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, akiwa mgeni rasmi.Uzinduzi huo umefanyika Kibaha Pwani Amesema wakazi wa Mkoa wa Pwani wana furaha kubwa kuwa wenyeji wa tukio hilo la kitaifa, akibainisha kuwa wamepata fursa ya kuwa miongoni mwa wananchi wa kwanza kunufaika na huduma zilizoboreshwa za NIDA, zikiwemo huduma zinazolenga kupunguza foleni. Amefafanua maboresho hayo yatasaidia wananchi wengi zaidi kupata vitambulisho vya taifa kwa urahisi na kwa muda mfupi, hivyo kuondoa changamoto zinazoweza kujitokeza katika upatikanaji wa huduma hizo. Pia ameishukuru Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na NIDA kwa kuuchagua Mkoa wa Pwani kuwa mwenyeji wa uzinduzi huo. Nyongo amesema mafanikio ya shughuli za usajili na utambuzi wa watu yanategemea ushirikiano wa karibu kati ya NIDA na Serikali za Mitaa, akisisitiza umuhimu wa viongozi wa wilaya, kata, vijiji, mitaa na vitongoji katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma hizo. Amesema viongozi hao wana nafasi muhimu kwa kuwa wako karibu na wananchi na wana uwezo wa kuratibu shughuli za usajili na kuwafikia wananchi katika maeneo yao. Ameongeza kuwa uongozi wa Mkoa wa Pwani utaendelea kushirikiana na NIDA kuhakikisha shughuli za usajili na utambuzi wa watu zinatekelezwa kwa ufanisi na kuwafikia wananchi wengi zaidi. Katika hatua nyingine, Nyongo amesema mkoa huo uko salama na wananchi wanaendelea na shughuli zao za kijamii na kiuchumi, licha ya baadhi ya maeneo kukumbwa na athari za mvua. Amesema Serikali ya mkoa inaendelea kufuatilia na kusimamia athari hizo ili kuhakikisha zinadhibitiwa na hazisababishi madhara zaidi kwa wananchi. Aidha, amemuomba Waziri Mkuu kufikisha salamu za upendo na shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan, akisema wakazi wa Pwani wanamthamini, wanamuombea afya njema na kuendelea kuongoza nchi katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Wed, 18 Nov 2026 19:02:06 +0000KOKA AMLILIA WAZIRI MKUU MAJI, BARABARA NJIA NANE KIBAHA
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Kibaha MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini mkoani Pwani Silvester Koka, ameiomba Serikali kuharakisha utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya maji na barabara katika Manispaa ya Kibaha, akieleza kuwa baadhi ya miradi hiyo imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na kusababisha usumbufu kwa wananchi. Amesema miongoni mwa miradi inayotia wasiwasi ni ujenzi wa tenki la maji la Pangani, ambao licha ya kusainiwa kwa mkataba takribani miaka mitatu iliyopita, umefikia asilimia 13 pekee ya utekelezaji. Akizungumza leo Novemba 18,2026 mbele ya Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, Koka amesema mradi huo ni muhimu kwa wakazi wa Kata ya Pangani na maeneo jirani ambayo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama. Ametaja maeneo yanayohitaji huduma hiyo kuwa ni Mpapa, Pangani, Mdeja, Majimoto na Lulanzi, akisema wananchi wake wameendelea kuhangaika kutafuta maji licha ya mradi huo kuanza kutekelezwa Amesema hali hiyo inahitaji uingiliaji wa Serikali ili mkandarasi aharakishe kazi na kuhakikisha wananchi wananufaika na uwekezaji huo badala ya kuendelea kusubiri huduma muhimu. Katika hatua nyingine, mbunge huyo ameiomba Serikali kuongeza kasi ya upanuzi wa barabara ya Morogoro, akieleza kuwa eneo la Kibaha limekuwa likikabiliwa na msongamano mkubwa wa magari kutokana na shughuli za kiuchumi na usafiri kuelekea mikoa ya Magharibi. Ameongeza magari mengi yanayoingia na kutoka Dar es Salaam yanapita katika eneo hilo, huku sehemu kubwa ya msongamano ikijitokeza kati ya Kibaha na Chalinze, hali inayopoteza muda na kuongeza gharama za usafirishaji. Koka amesema barabara hiyo ni miongoni mwa miundombinu muhimu zaidi kiuchumi nchini, hivyo Serikali inapaswa kuipa kipaumbele katika utekelezaji wa miradi ya upanuzi. Pia ameeleza kusuasua kwa mradi wa barabara ya Chang’ombe–Mapinga yenye urefu wa takribani kilomita 25, akisema hadi sasa ni kilomita 10 pekee zilizojengwa. Ameongeza kuchelewa kukamilika kwa miradi ya aina hiyo kunachelewesha manufaa yaliyokusudiwa na kuongeza gharama za utekelezaji, hivyo akaiomba Serikali kuingilia kati ili kuhakikisha mradi huo unakamilika Kuhusu usafiri wa umma, Koka amesema wananchi wa Kibaha Mjini bado hawajanufaika na huduma ya mwendokasi licha ya miundombinu ya barabara kujengwa na kuwepo kwa mazingira ya kuanza kwa huduma hiyo. Ameiomba Serikali kuharakisha maandalizi na kuweka utaratibu utakaowezesha wananchi kuanza kutumia usafiri huo, akisema utasaidia kupunguza adha ya usafiri kati ya Kibaha na Dar es Salaam. “Barabara hizo zina umuhimu mkubwa katika kufungua fursa za biashara, uwekezaji na usafirishaji wa bidhaa, hasa kutokana na matarajio ya kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.” Aidha, ameelezachangamoto ya daraja la Lunguki linalopita Mto Mpiji na kuunganisha Kata ya Pangani na maeneo ya Mkamba, Maringota pamoja na Wilaya ya Mkuranga. Amefafanua daraja hilo limekuwa likikumbwa na changamoto ya mabadiliko ya mkondo wa mto, hali inayosababisha wananchi kushindwa kuvuka kwa urahisi, huku watoto wakipata wakati mgumu kufika shuleni na wafugaji wakikabiliwa na changamoto ya kuvusha mifugo. Ameiomba Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mkuranga kutafuta suluhisho la kudumu la ujenzi wa daraja hilo ili kurahisisha mawasiliano na shughuli za kiuchumi. Pamoja na changamoto hizo, Koka ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji katika maendeleo ya Manispaa ya Kibaha, akisema hatua mbalimbali zimeongeza kasi ya utoaji wa huduma za kijamii. Pia amesema Halmashauri imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, ambapo katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2026/27 ilikuwa imekusanya takribani Shilingi milioni 18, sawa na asilimia 55.5 ya makadirio ya kipindi hicho. Ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2026/27, takribani Shilingi milioni 600 zimetumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya huduma za jamii. Katika sekta ya elimu, amesema Serikali imejenga shule mpya za msingi 12 na sekondari 10, huku ujenzi wa madarasa na maabara ukiendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji. Ameongeza hatua hizo zimechangia kuongezeka kwa ufaulu, kiasi cha shule za sekondari za kata kuanza kushindana na shule binafsi katika matokeo ya mitihani. Kuhusu afya, amesema Halmashauri imeendelea kuboresha huduma kwa kujenga vituo vya afya na zahanati, huku upatikanaji wa dawa ukiongezeka ikilinganishwa na hali ya awali. Serikali pia imeendelea kuwekeza katika miundombinu ya barabara, maji na umeme, akitaja utekelezaji wa miradi ya maji yenye thamani ya Shilingi milioni 700.5 na ujenzi wa miundombinu mingine ya kusogeza huduma karibu na wananchi. Koka alihitimisha kwa kuiomba Serikali kuyafanyia kazi maombi yaliyowasilishwa, akisema kukamilika kwa miradi hiyo kutafungua fursa za uwekezaji, kuongeza shughuli za kiuchumi na kuboresha maisha ya wakazi wa Kibaha Mjini.
Wed, 18 Nov 2026 18:58:55 +0000TUME YA TAIFA YA MIPANGO, UNFPA KUDUMISHA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA DIRA 2050
Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam. Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Bw. Mark Bryan Schreiner, leo Novemba 18, 2026, jijini Dar es Salaam. Viongozi hao, wamefanya tathmini ya ushirikiano baina ya taasisi zao kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na maendeleo baina ya baina ya nchi. Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu amemshukuru Bw. Schreiner kwa mchango wake katika kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na UNFPA, hususan katika masuala ya idadi ya watu na mipango ya maendeleo. Dkt. Kida amesisitiza umuhimu wa kuzingatia mwenendo wa idadi ya watu, uwekezaji kwa vijana na maendeleo ya rasilimali watu katika utekelezaji wa Dira 2050 na Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano. Aidha, amesisitiza kuwekeza kwa vijana, kuimarisha rasilimali watu na kukabiliana na changamoto za umaskini, mimba za utotoni na ukatili wa kijinsia ili Taifa liweze kunufaika na fursa za idadi kubwa ya vijana. Aidha, viongozi hao wamekubaliana kukamilisha mapitio ya Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu na kuandaa programu mpya ya ushirikiano inayoakisi vipaumbele vya Dira 2050. Kwa upande wake, Bw. Schreiner amethibitisha dhamira ya UNFPA kuendeleza ushirikiano huo, ikiwemo kutoa msaada wa kitaalamu katika uchambuzi wa takwimu na mwenendo wa idadi ya watu.
Wed, 18 Nov 2026 18:55:09 +0000Pochettino arrives at Man Utd to start work
Read the full report from the original source.
RecentlyWaunifor–Flax road opens new economic frontiers for rural communities
Read the full report from the original source.
RecentlyThe Diplomacy Beneath the Veto: Tanzania, Russia, and the Mechanics of Multilateral Leverage: Stratgic Non-Alignment and Executive Realism in Modern Geopolitics
Western foreign policy establishments are sleepwalking into a multipolar reality they refuse to name. While Washington and Brussels obsess over…
RecentlyDKT. MWIGULU AZINDUA KITAMBULISHO CHA TAIFA KILICHOBORESHWA
▪️ Serikali yawekeza zaidi ya Sh. bilioni 30 katika kadi na mashine za uzalishaji ▪️ Asisitiza wananchi kupata vitambulisho bila usumbufu ▪️ Vitambulisho vya awali vinaendelea kutumika WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua kitambulisho cha Taifa kilichoboreshwa, toleo la mwaka 2026, akisisitiza kuwa uwekezaji huo unapaswa kurahisisha upatikanaji wa huduma na kupunguza usumbufu kwa wananchi. Katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya Zamani ya Mailimoja, Kibaha, mkoani Pwani, Waziri Mkuu pia amezindua teknolojia mpya ya uzalishaji wa vitambulisho, programu tumizi ya NIDA Wallet na magari 10 ya huduma za usajili. Amesema maboresho hayo yanafungua fursa ya kuunganisha huduma mbalimbali kupitia utambulisho mmoja, hivyo kupunguza ulazima wa wananchi kubeba vitambulisho vingi katika shughuli zao za kila siku. “Lengo la Serikali ni kuhakikisha uwekezaji huu unaleta matokeo yanayoonekana katika maisha ya kila siku ya Mtanzania,” amesema. Dkt. Mwigulu amesisitiza kuwa kila Mtanzania anayestahili kupata kitambulisho cha Taifa anapaswa kukipata kwa wakati, bila usumbufu wala urasimu. Amempongeza Rais Dkt. Samia kwa kuwezesha uwekezaji huo, akisema matumizi ya teknolojia yanapaswa kuboresha huduma, kuimarisha utawala bora na kupanua fursa za wananchi katika shughuli za kiuchumi. Akifafanua maboresho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), James Kaji, amesema Serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 30 katika ununuzi wa kadi mpya na mashine tano za kisasa zenye uwezo wa pamoja wa kuzalisha vitambulisho 2,800 kwa saa. Amesema mashine hizo zinatumia teknolojia ya kuchora taarifa na picha kwa mionzi ya leza ndani ya tabaka za kadi, badala ya kuzichapisha kwa wino juu ya uso wake. Hatua hiyo inalenga kuongeza uimara wa kitambulisho na kupunguza uwezekano wa kughushi. Aidha, amesema nafasi za programu za kidijitali zinazoweza kuunganishwa kwenye kadi zimeongezwa kutoka nne hadi nane, ili kuwezesha matumizi mapana zaidi ya kitambulisho hicho katika huduma mbalimbali. Ameeleza kuwa uunganishaji wa huduma, zikiwemo bima ya afya, leseni za udereva na usafiri, utafanyika kwa hatua kulingana na utayari wa mifumo, makubaliano ya taasisi husika na matakwa ya kisheria. “Lengo si kuongeza teknolojia kwa ajili ya teknolojia, bali ni kumwezesha mwananchi kutumia utambulisho wake katika huduma mbalimbali kwa usalama na urahisi zaidi,” amesema Kaji. Kuhusu NIDA Wallet, amesema ni programu tumizi inayowezesha mwananchi kuwa na utambulisho wake wa kidijitali kwenye simu na kuutumia kuthibitisha taarifa zake wakati wa kupata huduma, kadiri mifumo ya taasisi husika itakavyounganishwa. Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesisitiza kuwa uzinduzi huo hauondoi uhalali wa vitambulisho vya awali, hivyo wananchi hawalazimiki kubadilisha vitambulisho visivyo na dosari. “Hauna sababu ya kwenda kubadilisha kitambulisho chako cha zamani kwenda kupata kipya kama hakuna sababu yoyote ya msingi,” amesema. Katambi pia amewahimiza wananchi kuchukua vitambulisho vilivyo tayari katika maeneo walikojisajili. Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Paschal Inyasi Chinyele, amepongeza maboresho hayo, huku akisisitiza ulinzi wa taarifa binafsi za wananchi, ushirikiano baina ya NIDA na taasisi nyingine na uendelevu wa teknolojia inayotumika.
Wed, 18 Nov 2026 18:37:38 +0000DKT. MWIGULU: MSITWAE ARDHI ZA WANANCHI BILA FIDIA
▪️︎ Akemea matumizi mabaya ya mamlaka kuwatisha wamiliki wa maeneo ▪️︎ Ataka uwekezaji uwanufaishe pia wananchi wanaopisha miradi WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka maafisa wa ardhi kuzingatia sheria na kuhakikisha wananchi wanaopisha miradi ya maendeleo na uwekezaji wanalipwa fidia, akisisitiza kuwa matumizi ya maeneo hayo kwa manufaa ya umma hayapaswi kupuuza haki za wamiliki. Amesema katika maeneo mbalimbali amekutana na malalamiko ya wananchi ambao mashamba yao yametumika kujenga shule, vituo vya afya na kutekeleza miradi mingine, lakini hawajalipwa fidia licha ya huduma kuanza kutolewa. “Tuache kutumia vibaya sheria. Tuache kutumia vibaya mamlaka,” amesema. Dkt. Mwigulu ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi katika viwanja vya Stendi ya Zamani ya Mailimoja, Kibaha, mkoani Pwani, baada ya kuzindua kitambulisho cha Taifa kilichoboreshwa. Ameeleza kuwa Serikali inapohitaji ardhi kwa ajili ya miradi yenye maslahi mapana ya Taifa, wahusika wanapaswa kuzingatia masharti ya sheria na kulinda haki za wanaopisha maeneo hayo. Amesema kuwepo kwa shule au kituo cha afya kinachotoa huduma hakuondoi wajibu wa kuzingatia haki ya mwananchi aliyekuwa akimiliki eneo hilo, likiwemo shamba la urithi wa familia. Waziri Mkuu pia amekemea tabia ya baadhi ya maafisa kuwataka wananchi kurejesha hati zao kwa ahadi ya kupatiwa maeneo mengine, kisha maeneo hayo kuuzwa bila haki za wamiliki kuzingatiwa. Amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuunga mkono uwekezaji kwa sababu unaongeza ajira, uzalishaji na mapato ya nchi. Hata hivyo, amesema manufaa hayo yanapaswa kuwafikia pia wananchi wanaopisha miradi. Dkt. Mwigulu amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia malipo ya fidia, akisema alipokuwa Waziri wa Fedha alishuhudia Serikali ikilipa madai ambayo baadhi yake yalikuwa yamedumu kwa miaka mingi. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameeleza kuwa Serikali imetanguliza malipo ya miradi ambayo wakandarasi walikuwa wamesimamisha kazi, ikifuatiwa na malipo ya awali kwa miradi yenye mikataba, kabla ya kusaini mikataba mipya iliyokamilisha taratibu za manunuzi. Amewataka wakandarasi waliopokea fedha kurejea kazini na kuongeza kasi ya utekelezaji ili wananchi wapate huduma zilizokusudiwa. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Stephen Chaya, amesema Serikali imeandaa utaratibu wa kulipa kwa awamu wananchi wanaodai fidia katika eneo maalumu la uwekezaji la Bagamoyo. Amesema hatua hiyo inafuatia maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi hao wanalipwa. Naye Waziri wa Maji, Juma Aweso, ameelekeza madai ya mkandarasi wa mradi wa maji Pangani ya shilingi milioni 700 yalipwe kabla ya mwezi huu kuisha ili kuharakisha utekelezaji. Pia, ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuanza utaratibu wa kuwapatia wananchi wa Pangani maji bila kusubiri ujenzi wa tenki ukamilike.
Wed, 18 Nov 2026 18:39:49 +0000Duale: Over 33m Kenyans registered with SHA
Duale commended Nairobi County for training 923 health workers and 1,598 Community Health Promoters (CHPs) as part of the response
RecentlyQuel rôle pour l'Afrique dans la COP31 ?
Read the full report from the original source.
RecentlyIsrael launches new ground operation in Gaza
Read the full report from the original source.
RecentlyStanbic freezes Vodacom’s Sh9bn over Safaricom sale
Read the full report from the original source.
RecentlyUganda Digital Society elects new secretariat
The Uganda Digital Society (UDS) has elected a new Secretariat led by President-elect Rhoda Musiima, as the country accelerates efforts to expand digital connectivity, strengthen…
RecentlyMubende Hospital Opens Level 3 Neonatal Unit to Boost Newborn Survival
Read the full report from the original source.
RecentlyDuale reaffirms commitment to health reforms, accountability
Read the full report from the original source.
RecentlyCheza Mizunguko 100, Upate Mizunguko 50 Ya Bure
MERIDIANBET kwa kushirikiana na Expanse Studios imekuja na ofa maalumu kwa wapenzi wa michezo ya kasino kupitia mchezo wa Wild White Whale, ambapo wachezaji wanapata nafasi ya kutuzwa mizunguko 50 ya bure baada ya kucheza mizunguko 100 katika mchezo huo. Ofa hii inalenga kuongeza burudani na kuwapa wateja uzoefu zaidi wanapofurahia michezo ya kasino ndani ya Meridianbet . Kupitia promosheni hii, mchezaji anatakiwa kucheza jumla ya mizunguko 100 katika mchezo wa Wild White Whale ili kustahili kupata zawadi ya mizunguko 50 ya bure siku inayofuata. Kinachofanya ofa hii kuwa ya kipekee ni kwamba zawadi hiyo hutolewa bila kujali kama mchezaji ameshinda au amepoteza katika mizunguko yake 100 ya mwanzo. Wild White Whale ni mchezo unaopatikana ndani ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet, ukiwapa wachezaji nafasi ya kufurahia burudani ya kidijitali kupitia mfumo wake wa uchezaji. Kupitia ofa hii, wapenzi wa kasino wanaweza kuufurahia mchezo huku wakipata fursa ya kuongezewa mizunguko mingine 50 ya bure kwa mujibu wa masharti ya promosheni. Ni muhimu kufahamu kuwa mizunguko hiyo ya bure inatumika katika mchezo wa Wild White Whale pekee. Ofa hii ni halali kwa mtumiaji mmoja, Meridianbet pia inahifadhi haki ya kubadilisha au kusitisha promosheni wakati wowote, huku washiriki wakitakiwa kuzingatia vigezo na masharti ya kampuni. Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Usipitwe na ofa hii maalumu! Tembelea Meridianbet, soma vigezo na masharti ya promosheni, kisha furahia mchezo wa Wild White Whale . Kumbuka furaha ya krismas imeambana na meridianbet msimu huu. Jiunge na meridianbet ufurahie mizunguko ya bure.
Wed, 18 Nov 2026 06:06:00 +0000Je Pochettino Kuikomboa Man United?
KLABU ya Manchester United sasa imeamua kufanya mabadiliko kwa kumleta kocha mpya klabuni kwao ambaye ni Mauricio Pochettino akichukua nafasi ya Carick. Je kocha huyo ataifikisha wapi? Klabu ya Manchester United bado inapitia wakati mgumu msimu huu baada ya mfululizo wa matokeo mabaya kwenye mashindano yote ambapo klabu imelazimika kuachana na aliyekuwa kocha wao Michael Carrick na kuleta kocha mpya ambaye ni Pochettino. Carrick ameiacha klabu ikiwa nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi, yaani nafasi ya 3 kutoka chini kwenye kushuka daraja baada ya kucheza mechi 10 hadi sasa huku mara ya mwisho kushinda kwenye ligi ilikuwa ni mwezi Agosti wakiwa wameshinda mechi moja pekee. Tatizo la United si matokeo pekee, bali pia kushindwa kupata mwendelezo mzuri wa mchezo. Katika mechi zake za hivi karibuni, ilipoteza dhidi ya Bournemouth kwa mabao 3-0 na Chelsea kwa mabao 2-0, kabla ya kutoka sare ya mabao 4-4 dhidi ya Aston Villa. Licha ya uwezo wa Bruno Fernandes na Bryan Mbeumo kuchangia mabao, timu imekuwa ikishindwa kulinda matokeo na kuzuia wapinzani kupata nafasi za kufunga. Jisajili hapa. Nafasi ya ushindi ipo kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno , Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Na kwenye michuano ya Uefa pia bado hali ni mbaya ambapo United imerejea kushiriki michuano hiyo baada ya misimu miwili, lakini bado mwenendo wao hauridhishi kwani mpaka sasa inashika nafasi ya 17 wakiwa na pointi 6 pekee hadi sasa kwenye mechi 4 ambazo wamecheza. Mchezo ujao wanatarajiwa kukipiga dhidi ya Sporting CP utakuwa mtihani muhimu kwa kikosi hicho, hasa ikizingatiwa kuwa kinahitaji kuboresha matokeo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele. Kutokana na mwenendo huo, klabu iliamua kumuondoa Michael Carrick kwenye nafasi ya kocha mkuu Novemba 12. Carrick alikuwa amepewa nafasi hiyo baada ya kuondoka kwa Ruben Amorim, na aliwahi kuiongoza United kumaliza nafasi ya tatu kwenye EPL msimu uliopita na kufuzu Champions League. Hata hivyo, mwanzo mbaya wa msimu mpya, ukiwemo mfululizo wa mechi bila ushindi, ulifanya uongozi wa klabu kuchukua uamuzi wa kubadilisha benchi la ufundi. Na sasa kibarua kizito amekabidhiwa Mauricio Pochettino ambaye amepewa makataba utakaodumu hadi mwaka 2029. Kocha huyo an uzoefu mkbwa na ligi hiyo ambapo tayari ameonoa vilabu kama Tottenham Spurs pamoja na Chelsea kabla ya kwenda kuinoa timu taTaifa ya Marekani. Pochettino ataanza mtihani wake wa kwanza na mechi dhidi ya Liverpool kule Anfield, moja ya mechi ngumu sana kwa upande wa Mashetani Wekundu na hapo baadae atasafiri kwenda kule Ureno kusaka ushindi dhidi ya Sporting CP. Je kocha huyo ataanza vipi mechi hizo?. Beti sasa . Wadau mbalimbali wanasema kuwa klabu hiyo kwa ujumla inahitaji zaidi ya kubadilisha kocha inahitaji kurekebisha mfumo wa uchezaji, kuongeza uimara wa ulinzi na kurejesha ushindani. Pochettino ana kazi kubwa ya kuifanya timu iondoke kwenye eneo la hatari la kushuka daraja na kuanza kupigania nafasi za juu, huku akihakikisha safari yake ya Champions League haiishii mapema.
Wed, 18 Nov 2026 06:02:00 +0000IRDP YATAKA WAHITIMU KUTUMIA ELIMU KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII.
Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) kimewataka wahitimu wa chuo hicho kutumia elimu, ujuzi na maarifa waliyoyapata kutatua changamoto za jamii, kujiajiri na kuajiri wengine badala ya kutegemea vyeti pekee kupata ajira, kikieleza kuwa elimu inapaswa kuwa na matokeo yanayoonekana katika maisha ya wahitimu na jamii kwa ujumla. Akizungumza Novemba 18, 2026, jijini Dodoma katika Siku ya Masajili (Convocation) ya chuo hicho, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi, Joseph Kuzilwa, amesema wahitimu wanapaswa kutumia elimu yao kwa namna inayochangia maendeleo ya taifa kuelekea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2050, akisisitiza kuwa cheti si mwisho wa elimu bali ni msingi wa kutumia maarifa kujenga maisha, kujiendeleza kielimu na kuisaidia jamii. Kuzilwa amesisitiza matumizi sahihi ya akili mnemba (AI) katika elimu, akieleza kuwa teknolojia hiyo inaweza kusaidia ufundishaji na ujifunzaji lakini pia inaweza kudhoofisha uwezo wa mtu kufikiri ikiwa itatumika vibaya, amesema matumizi yake yanapaswa kuwa jumuishi kwa kuchanganya na uwezo wao binafsi wa kitaaluma ili kupata manufaa zaidi. Pia amewataka wahitimu waliopo kwenye maeneo ya kazi kushirikiana na chuo kwa kutoa nafasi za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi, kuwafanyia mentorship na kuwasaidia kupata uzoefu wa mazingira halisi ya kazi, huku waajiri wakitoa mrejesho utakaosaidia kuboresha mitaala na kuendana na mahitaji ya soko la ajira. Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, amesema chuo kimepiga hatua katika ukuaji na utoaji wa elimu, kutoka kuwa na wanafunzi 14 na watumishi takribani 13 hadi kufikia wanafunzi zaidi ya 15,000 na watumishi 495, akieleza kuwa mafanikio hayo ni sehemu ya juhudi za chuo kuimarisha mchango wake katika maendeleo ya taifa. Mayaya amesema chuo kinaendelea kuimarisha kituo cha ujasiriamali na ubunifu MEI (Mipango Entrepreneurship and Innovation Centre) kwa ajili ya kuwajengea wanafunzi ujuzi wa ziada wa kujiajiri na kuajiriwa, huku kikitarajia kujenga kituo kikubwa cha ubunifu katika Kampasi ya Furaha iliyopo Mjini Dodoma kupitia mradi unaotajwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 2.6, utakaowezesha wanafunzi na wadau wengine kupata fursa za ubunifu. Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Prof. Dimoso, amesema kituo cha ubunifu na ujasiriamali kimeanza kuonesha matokeo kupitia wanafunzi watano wa Diploma ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) waliobuni mfumo wa kidijitali wa kupanga foleni hospitalini, unaomwezesha mgonjwa kujisajili na kupata taarifa ya namba yake pamoja na muda anaotarajiwa kumuona daktari. Amesema mfumo huo utasaidia kupunguza muda wa wagonjwa kusubiri huduma hospitalini, kwa kuwa wanaweza kuendelea na shughuli zao nyingine wakati wakisubiri muda wa kwenda kumuona daktari, huku akieleza kuwa chuo kimeendelea kuimarisha matumizi ya teknolojia na akili mnemba katika ufundishaji na ujifunzaji na ufaulu wa wanafunzi umeongezeka ikilinganishwa na mwaka uliopita. Katika Siku hiyo ya Masajili, chuo pia kimetambua wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo na wahadhiri waliofanya vizuri katika utafiti na machapisho ya kitaaluma, hatua inayolenga kuhamasisha ubora wa elimu, ubunifu, tafiti na matumizi ya maarifa katika kutatua changamoto za jamii.
Wed, 18 Nov 2026 18:02:25 +0000Page 138 of 1127 · 22529 stories