Search the region
22544 stories
Ruto announces Sh15bn coffee payout, Sh1.2bn sugar bonus
Ruto says coffee prices have risen to Sh130 per kilogram, with Sh15bn paid to farmers and a Sh1.2bn sugarcane bonus set to begin next week
RecentlyAkiba za wanachama PCCB Saccos zafikia bil 31.8/-
Read the full report from the original source.
RecentlyZILIZOBAMBA MITANDAONI | Wachambuzi Muro, Juma Abdul watamani kumuona Domayo akirejea uwanjani
ZILIZOBAMBA MITANDAONI: Wachambuzi @godlisten_muro7 na @juma_abdul_12 wanasema kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Frank Domayo anafaa kuwa kocha mchezaji ndani ya kikosi hicho. Juma Abdul anasema ufanisi wa Domayo unahitajika ndani ya kikosi cha Kagera Sugar huku ‘akijimwagia maua’ kwamba yeye pia bado anahitajika kwenda kutoa darasa kwa vijana kuhusu namna ya kupiga krosi. Ni #Zilizobamba kupitia kipindi cha #Viwanjani #Viwanjani
2026-11-18T13:10:37+00:00Uganda Airlines has launched daily direct flights between Entebbe and Kigali
Read the full report from the original source.
RecentlyRuto: Increased education funding has eased burden on parents
The President cited increased funding, the recruitment of 100,000 teachers and construction of classrooms as evidence of his administration's education reforms.
RecentlyNairobi health facilities triple revenue to Sh2.6bn as county expands access
Capital Health · Quick read
RecentlyCitizen TV named Superbrand as it marks 25 years on air
Read the full report from the original source.
RecentlyLinda Mwananchi sets Ksh.5,000 lifetime membership fee
Read the full report from the original source.
RecentlyRuto announces Ksh.1.2B bonus for sugarcane farmers, payments to begin next week
Read the full report from the original source.
RecentlyTanzania eyes bigger share of lucrative global MICE tourism market
ARUSHA: IMAGINE thousands of delegates arriving in Arusha from across the globe, gathering under one roof to negotiate investment deals,…
RecentlySHIVYAWATA YAOMBA SERIKALI KUANDAA WATUMISHI WENYE UJUZI WA KUTUMIA LUGHA YA ALAMA
Na Jane Mwakyoma Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Mkoa wa Rukwa limeiomba Serikali kutoa elimu ya lugha ya alama kwa watumishi wa taasisi za umma ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu wa kusikia. Ombi hilo limetolewa katika kikao cha kujadili masuala mbalimbali yanayohusu ustawi na maendeleo ya watu wenye ulemavu kilichofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, ambapo wameeleza kukumbana na changamoto ya mawasiliano wanapohitaji huduma katika ofisi za Serikali. Wamesema changamoto hiyo imekuwa ikikwamisha upatikanaji wa huduma na utatuzi wa matatizo yao kutokana na baadhi ya watumishi kutokuwa na uelewa wa lugha ya alama. “Tunapokwenda ofisini tukiwa na shida, kwa mfano mimi ni mlemavu wa kutokusikia, suala la kupata huduma linakuwa gumu kutokana na mtumishi kutokujua namna ya kunielewesha. Hali hii inatuletea ukakasi,” walisema. Aidha, wameiomba Serikali kuhakikisha katika ofisi za umma, hususan ofisi za wakurugenzi wa halmashauri, kunakuwa na angalau mtumishi mmoja anayefahamu lugha ya alama ili kuwasaidia watu wenye ulemavu wa kusikia kupata huduma na kuelewa maelekezo kwa urahisi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Mkoa wa Rukwa, Elina John, amesema licha ya Serikali ya Awamu ya Sita kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu, bado kuna mahitaji mbalimbali yanayopaswa kushughulikiwa, ikiwemo uelewa wa jamii kuhusu uwezo wa watu wenye ulemavu. Ameiomba jamii kuwapa fursa na kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika shughuli za kijamii, kisiasa na kiuchumi, akisisitiza kuwa wana uwezo wa kutekeleza majukumu mbalimbali kama watu wengine. Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga, Nassir Kirusha, amesema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya huduma kwa watu wenye ulemavu katika sekta mbalimbali, ikiwemo elimu na afya, kwa kujenga miundombinu inayozingatia mahitaji yao, kama vyoo maalumu na njia za kupita. Aidha, amewataka wazazi na walezi wenye watoto wenye mahitaji maalumu kutowaficha majumbani, bali kuwapeleka shuleni na kuhakikisha wanaandikishwa ili wapate haki ya elimu na kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali.
Wed, 18 Nov 2026 13:20:12 +0000Absa’s StanChart acquisition: Can it challenge Centenary and Stanbic’s dominance?
Read the full report from the original source.
RecentlyMPs chant 'Pawa' as Oburu arrives in Parliament
National Assembly Speaker Moses Wetang’ula acknowledged his presence, describing him as the ODM youth leader who also serves as the party leader
RecentlyWAZIRI MKUU: SAYANSI NA TEKNOLOJIA NGUZO YA UCHUMI SHINDANI
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Tanzania inaendelea kutambua sayansi, teknolojia na ubunifu kama nguzo muhimu za mabadiliko ya kiuchumi na kijamii. Amesema kuwa katika kuelekea uchumi shindani unaotegemea maarifa, Serikali imeweka mazingira wezeshi ya kuimarisha tafiti, ukuzaji wa teknolojia na ubunifu. Amesema hayo leo (Jumatano, Novemba 18, 2026) kwenye maadhimisho ya kilele cha miaka 40 ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City. Akielezea kuhusu mifumo ya data na uratibu, Waziri Mkuu amesema katika dunia ya leo, maendeleo ya sayansi na teknolojia hayawezi kufanikiwa pasipo uwepo wa mifumo madhubuti ya ukusanyaji, uchambuzi, uhifadhi na matumizi ya taarifa. “Ninaipongeza COSTECH kwa kuanzisha na kuendeleza Mfumo wa Taifa wa Taarifa za Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (NISSTI), ambao unaimarisha uratibu wa tafiti za kisayansi nchini na kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi kwa ajili ya kufanya maamuzi.” Amesisitiza kuwa mfumo huu unaweka msingi wa kuunganisha watafiti, taasisi za elimu ya juu, wabunifu, watunga sera na wadau wengine katika jukwaa moja la kitaifa. “Kupitia mfumo huu, Tanzania inajenga hazina ya maarifa itakayosaidia kupanga maendeleo kwa misingi ya ushahidi na takwimu sahihi.” Akitolea mfano, Dkt. Mwigulu alisema zipo bunifu zilizofanywa na vijana ambazo zinatumika kukausha mazao bila kukata miti. “Kwa COSTECH, hii ni miaka 40 ya mafanikio yenye kuleta ufumbuzi kwenye maisha ya kila siku ya Watanzania.” “Katika maeneo ya vijijini hivi sasa wanatumia mbegu zilizofanyiwa utafiti na pia wananchi wanatumia mbolea, jambo ambalo zamani lisingeweza kufanyika. Mheshimiwa Rais Dkt. Samia mwenyewe ameweka msisitizo kwenye matumizi ya sayansi na teknolojia ambapo ameanzisha Mfuko wa Samia wa Ubiasharishaji Ubunifu ili kuhakikisha matokeo ya tafiti na ubunifu yanageuzwa kuwa bidhaa, huduma na biashara zinazoweza kuleta ajira, kuongeza mapato na kukuza uchumi wa Taifa.” Aidha, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wadau wote waendelee kujenga ubia imara utakaowezesha ubunifu wa Watanzania kufikia masoko ya ndani na nje ya nchi. Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, alisema kuwa na teknolojia bila sayansi ni sawa na kumiliki shamba lakini huwezi kulilima; badala yake unategemea mtu aje alime, avune na kisha aje akugawie. Pia, Prof. Mkenda amefafanua kuwa Tanzania inapaswa kuwa na vijana wabobezi wa sayansi na teknolojia watakaotumia ujuzi wao kwenye sekta za madini, uchukuzi, miundombinu, afya na kilimo. Akiwasilisha Maazimio ya Wadau wa Sayansi na Teknolojia kuelekea utekelezaji wa Dira 2050, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonaz, alisema wadau wamekubaliana vipaumbele vya utafiti viendane na mahitaji ya Taifa, uzalishaji, maendeleo ya watu na changamoto za jamii. “Tanzania ielekeze nguvu na rasilimali katika maeneo machache ya tafiti na teknolojia yenye manufaa makubwa kwa uchumi na wananchi. Fedha za utafiti zisaidie kutatua matatizo yanayowakabili wakulima, wazalishaji na wafanyabiashara.” Amesisitiza kuwa Dira ya 2050 itafikiwa pale maarifa na teknolojia zitakapoongeza uzalishaji, kufungua ajira na kuboresha maisha ya wananchi.
Wed, 18 Nov 2026 13:11:05 +0000Qualcomm Yahitimisha Programu ya Make in Africa na Kutangaza Mshindi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Matokeo ya Kijamii
Qualcomm Technologies, Inc. leo imetangaza kuhitimishwa kwa programu yake ya nne ya kila mwaka ya ‘Qualcomm Make in Africa Startup Mentorship Program’ , iliyofikia kilele chake kupitia hafla ya kwanza iliyofanyika ana kwa ana katika maonyesho ya ‘Africa Tech Festival’ jijini Cape Town. Qualcomm pia imetangaza mshindi wa Mfuko wa Uwekezaji wenye Matokeo kwa Kijamii wa ‘Qualcomm for Good Social Impact Fund’ wa mwaka 2026. Mambo muhimu: Programu ya mwaka 2026 ilisaidia kampuni changa kumi (startups) kutoka nchi tisa za Afrika (kampuni ya SafeSip ya Tanzania inayotoa suluhisho la maji salama linalotumia teknolojia janja kwa maeneo ya mijini na pembezoni mwa miji ilikuwa miongoni mwao), zinazotengeneza suluhisho zinazotumia akili mnemba (AI) inayounganishwa na mifumo halisi (embodied AI) na teknolojia ya kompyuta inayochakata taarifa karibu na chanzo chake (edge computing), katika sekta za kilimo, ufugaji wa samaki, usafiri wa kielektroniki, usafishaji wa maji na upatikanaji wa huduma kwa watu wenye mahitaji maalum. Qualikeeper Investments Ltd (Zambia) imechaguliwa kuwa mshindi wa Mfuko wa Uwekezaji wenye Matokeo ya Kijamii wa ‘Qualcomm for Good Social Impact Fund’ wa mwaka 2026 , kwa kutambua mfumo wake wa bei nafuu wa kidijitali unaounganisha akili mnemba na vifaa vya intaneti ya vitu (Edge-AIoT) kwa ajili ya ufuatiliaji na usimamizi wa mifugo, unaojulikana kama ‘StocKeeper’. Maombi ya kujiunga na programu ya Qualcomm Make in Africa ya mwaka 2027 yamefunguliwa. Waombaji wanaweza kutembelea tovuti ya Qualcomm ili kutuma maombi. Kilele cha Hafla hiyo kiliwakutanisha washiriki wa programu ya mwaka 2026 jijini Cape Town, ambapo waanzilishi wa kampuni hizo kutoka maeneo mbalimbali barani Afrika waliwasilisha kazi zao kama hitimisho la programu hiyo. Suluhisho zao zinahusisha teknolojia za ‘embodied AI’ na ‘edge computing’, zilizotengenezwa kwa kutumia teknolojia za Qualcomm na jukwaa la maendeleo la Arduino. Programu hii, ambayo haihitaji washiriki kutoa hisa za kampuni zao, inalenga kusaidia kampuni changa za teknolojia barani Afrika kupitia mafunzo ya biashara, msaada wa kiuhandisi na mwongozo kuhusu haki miliki. Washiriki wa mwaka 2026 walifanya kazi kwa kutumia teknolojia za Qualcomm® na jukwaa la maendeleo la Arduino®, ikiwemo Arduino® UNO™ Q. Kupitia L2Pro Africa na ushauri wa kitaalamu kutoka Adams & Adams, washiriki walipata msaada wa vitendo katika kulinda na kufanya ubunifu wao kuwa bidhaa au huduma zinazoweza kuuzwa kibiashara. Baada ya kukamilika kwa programu, kampuni hizo pia zitapokea fedha za kusaidia shughuli zao kiasi cha dola za Marekani 5,000, pamoja na kurejeshewa gharama za mpaka dola za Marekani 5,000 kwa ajili ya maombi kamili ya mara moja ya cheti cha matumizi (utility patent). “Programu ya Qualcomm Make in Africa inaakisi utabiti wa mifumo ya ubunifu na uvumbuzi inayokua barani Afrika, pamoja na uwezo mkubwa na mafanikio ya kipekee ya wajasiriamali wake,” alisema Wassim Chourbaji, Makamu wa Rais Mwandamizi na Rais wa Qualcomm kwa Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika (EMEA), Qualcomm France S.A.R.L. “Kwa kuwapatia fursa ya kutumia teknolojia za Qualcomm, jukwaa la maendeleo la Arduino, ushauri na msaada kutoka katika mfumo wa wadau wa teknolojia na ubunifu, tunawasaidia waanzilishi wa kampuni kubadilisha mawazo bunifu na yenye maono makubwa kuwa suluhisho zinazounganishwa na mifumo halisi zinazoweza kupanuliwa na kuleta matokeo halisi kwa jamii, kwa ufanisi na gharama nafuu za matumizi ya nishati. Kupitia Mfuko wa Uwekezaji wenye Matokeo kwa Kijamii, tunajivunia kuunga mkono kampuni changa ambayo ubunifu wake unaonesha uwezo mkubwa wa kuboresha maisha na kuleta manufaa endelevu kwa kijamii na kiuchumi barani Afrika.” “Kampuni changa kumi zilizoshiriki katika programu ya Qualcomm Make in Africa ya mwaka huu zinaonesha namna kujifunza mashine na teknolojia halisi zinavyoweza kutumika kutatua changamoto kwa vitendo katika sekta mbalimbali,” alisema Sudeepto Roy, Makamu wa Rais wa Uhandisi, Qualcomm Incorporated. “Katika kipindi chote cha programu, kampuni hizo zimeendeleza mifumo yao ya majaribio huku zikijenga uelewa mpana zaidi kuhusu haki miliki na hatua zinazohitajika kuanzia uvumbuzi mpaka kufanikisha biashara. Maendeleo yao ni mfano wa kutia moyo unaoonesha vipaji vya kiteknolojia na ari ya ujasiriamali vinavyoibuka katika maeneo mbalimbali ya Afrika.” Washirika kutoka serikalini na sekta binafsi pia walisisitiza umuhimu wa programu hiyo katika kuendeleza upatikanaji wa mawasiliano na uvumbuzi wa ndani barani Afrika. “Kupitia Azimio la Abuja la mwaka 2026 kuhusu Upatikanaji wa Mawasiliano Yenye Tija kwa Afrika (2026 Abuja Declaration on Meaningful Connectivity for Africa), nchi wanachama wa Umoja wa Mawasiliano wa Afrika (ATU) zimethibitisha tena dhamira yao ya pamoja ya kuharakisha ujumuishaji wa kidijitali na kuhakikisha kuwa Waafrika wote wanapata fursa ya kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali. “Wabunifu waliochaguliwa kushiriki katika programu ya Qualcomm Make in Africa ya mwaka huu wanaonesha jinsi dira hii inavyoweza kutafsiriwa kuwa matokeo halisi, kwa kutumia akili mnemba, mawasiliano ya kisasa na teknolojia nyingine zinazoibuka kutengeneza suluhisho zinazokidhi mahitaji ya ndani, zinazoshughulikia changamoto halisi na kuboresha maisha ya jamii za Afrika,” alisema Martial Dhossa, Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Redio, Umoja wa Mawasiliano wa Afrika (African Telecommunications Union – ATU). Mshindi wa Mfuko wa Uwekezaji wenye Matokeo ya Kijamii wa Qualcomm for Good Social Impact Fund Mfuko wa Uwekezaji wenye Matoke ya Kijamii wa Qualcomm for Good hutoa ruzuku kwa kampuni moja changa kutoka kila kundi la washiriki wa Qualcomm Make in Africa, ili kusaidia suluhisho lenye uwezo mkubwa wa kuleta manufaa ya kijamii. Ruzuku hiyo husaidia kampuni kuendeleza na kusambaza suluhisho lake, kupima athari zake na kuongeza wigo wa utekelezaji wake. Qualikeeper imetangazwa kuwa mshindi wa Mfuko wa Uwekezaji wenye Matokeo ya Kijamii wa Qualcomm for Good wa mwaka 2026. Kampuni hiyo itapokea ruzuku ya dola za Marekani 75,000 (zaidi ya Shilingi milioni 190 za Kitanzania) ambayo haihitaji kutoa hisa za kampuni, pamoja na msaada maalum wa kiufundi ili kusaidia kupanua suluhisho lake na kuongeza manufaa yake. “ Qualikeeper imechaguliwa kwa kutambua maono yake, ubunifu na dhamira yake ya kuimarisha afya ya mifugo na maisha ya wafugaji katika jamii zinazotegemea mifugo, hususan katika mazingira yenye rasilimali chache. “Kwa kuunganisha ubunifu wa kiteknolojia na msisitizo wa kuleta matokeo halisi, timu hiyo inaonesha uwezo wa ujasiriamali wa Afrika katika kushughulikia changamoto muhimu na kuleta thamani endelevu kwa jamii,” alisema Erica Ciaraldi, Meneja wa Masuala ya Serikali, Qualcomm Incorporated. “Tunafurahi kutambua mafanikio yao kupitia Mfuko wa Uwekezaji wenye Matokeo ya Kijamii wa Qualcomm for Good. Tunatarajia kuona namna watakavyoendelea kukuza mfumo wao wa teknolojia jumuishi wa akili mnemba (AIoT) wa ufuatiliaji wa mifugo, kufikia jamii mpya na kupanua manufaa yao barani Afrika na maeneo mengine duniani.” Mwelekeo wa Baadaye: Programu ya Qualcomm Make in Africa Startup Mentorship Program 2027 Kwa kuendeleza mafanikio ya programu hiyo, maombi ya kujiunga na Qualcomm Make in Africa Startup Mentorship Program ya mwaka 2027 sasa yamefunguliwa. Taarifa zaidi na maelezo ya namna ya kutuma maombi yanapatikana kupitia: https://www.qualcomm.com/company/locations/africa/qualcomm-make-in-africa Kuhusu Qualcomm Qualcomm inaendelea kufanya ubunifu wa kiteknolojia kwa lengo la kuwezesha mifumo ya kompyuta erevu kutumika kila mahali, kusaidia dunia kukabiliana na baadhi ya changamoto zake muhimu zaidi. Kwa kuendeleza uzoefu wake wa miaka 40 katika uongozi wa teknolojia na kuleta ubunifu unaobadilisha zama, kampuni inatoa wigo mpana wa suluhisho zinazotumia teknolojia zake za kisasa za akili mnemba, mifumo ya kompyuta yenye utendaji wa juu na matumizi madogo ya nishati, pamoja na uwezo wa kipekee wa mawasiliano. Majukwaa ya Snapdragon® yanawezesha uzoefu wa kipekee kwa watumiaji, huku bidhaa za Qualcomm Dragonwing™ zikisaidia biashara na sekta mbalimbali kufikia viwango vipya vya ukuaji na mafanikio. Kwa kushirikiana na wadau wake katika mfumo wa teknolojia, Qualcomm inawezesha mabadiliko ya kidijitali ya kizazi kijacho ili kuboresha maisha, kuimarisha biashara na kuendeleza jamii. Qualcomm Incorporated inajumuisha biashara yake ya utoaji leseni, QTL, pamoja na sehemu kubwa ya jukwaa lake la haki miliki. Qualcomm Technologies, Inc., kampuni tanzu ya Qualcomm Incorporated, pamoja na kampuni zake tanzu, husimamia takribani shughuli zote za uhandisi na utafiti na maendeleo, pamoja na sehemu kubwa ya biashara zake za bidhaa na huduma, ikiwemo biashara ya semikondakta ya QCT. Bidhaa zenye chapa ya Snapdragon na Qualcomm ni bidhaa za Qualcomm Technologies, Inc. na/au kampuni zake tanzu. Teknolojia zilizo na cheti cha matumizi za Qualcomm zinatolewa kwa leseni na Qualcomm Incorporated. Qualcomm na Wireless Reach ni chapa za biashara au chapa za biashara zilizosajiliwa za Qualcomm Incorporated. Qualcomm, Snapdragon na Qualcomm Dragonwing ni chapa za biashara au chapa za biashara zilizosajiliwa za Qualcomm Incorporated. Arduino ni chapa ya biashara au chapa ya biashara iliyosajiliwa ya Arduino S.r.l. QualiKeeper Investments Ltd. ikipokea ruzuku ya Dola za Marekani 75,000 kupitia Mfuko wa Uwekezaji wenye Matokeo kwa Kijamii wa ‘Qualcomm for Good Social Impact Fund’. Ruzuku hiyo ilikabidhiwa wakati wa hafla ya kilele cha programu ya Qualcomm Make in Africa (QMIA) 2026, iliyofanyika katika Africa Tech Festival jijini Cape Town, Afrika Kusini, tarehe 17 Novemba 2026. Katika picha (kutoka kushoto kwenda kulia): Martial Dhossa (Umoja wa Mawasiliano wa Afrika – African Telecommunications Union), Erica Ciaraldi (Qualcomm International, Inc.), Elijah Chileshe (QualiKeeper Investments Ltd.), Nicholas Katanekwa (QualiKeeper Investments Ltd.), na Elizabeth Migwalla (Qualcomm International, Inc.).
Wed, 18 Nov 2026 13:14:12 +0000Rwanda and five EU Member States are jointly exploring the possibility of establishing a return hub in Rwanda
Read the full report from the original source.
Recently‘I Don’t Need School Anymore!’ MUBS Fresher Quits After Winning Shs355 Million
Read the full report from the original source.
RecentlyRegina Re, brother freed on Sh200,000 bail over mother’s murder
Latest · News
RecentlyFinancial institutions urged to expand access to women and youth
DAR ES SALAAM: FINANCIAL institutions in the country have been urged to develop affordable and accessible financial products that address…
RecentlyAskofu Bagonza: Nimemjua aliyenitishia kunipoteza
Soma zaidi...
RecentlyPage 146 of 1128 · 22544 stories