Search the region
22553 stories
Archbishop Muheria threatens to sack church officials over politicians
News · 4 hours ago
RecentlyWhy Bafana Bafana do not want to play Harambee Stars again
Football · 4 hours ago
RecentlyCMA approves Africa Eats cross-listing and new dividend ETF on NSE
Latest · Markets
RecentlyDorita Macharia eulogised as a strong family pillar
The Jamaican-born entrepreneur was remembered for her resilience, patience, love of fine living and unwavering commitment to her children and grandchildren.
RecentlyHISTORIA YAANDIKWA; KITABU CHA HAKIMU WA KWANZA MWANAMKE MTANZANIA CHAZINDULIWA
· Chazinduliwa na Jaji Mkuu Masaju · Chaeleza historia na mchango wa Jaji Mstaafu Eusebia Nicholas Munuo Na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma Tarehe 17 Novemba, 2026 itabaki kuwa katika historia ya Mhimili wa Mahakama na Taifa la Tanzania kwa ujumla kufuatia tukio la uzinduzi wa Kitabu cha Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo aliyekuwa Mwanamke wa kwanza Mtanzania kuwa Hakimu na Jaji wa Mahakama ya Rufani. Katika kusherehekea mchango mkubwa wa Jaji Mstaafu huyo almaarufu kwa jina la Mama Munuo/Jaji Munuo, Mahakama ya Tanzania kupitia aliyekuwa Jaji Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma iliona umuhimu wa kuwa na kitabu kitakachoeleza historia yake, hivyo, walikieleza Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto kuandika Kitabu cha Historia ya Mwanamama huyo mahiri kufuatia historia yake nzuri na utumishi wa umma uliotukuka kwa Mahakama na Taifa kwa ujumla. Wazo la kuandika kitabu hicho lililozaliwa tarehe 20 Machi, 2024 limezaa matunda na kuja na Kitabu kiitwacho ‘JUSTICE EUSEBIA MUNUO: A Trailblazer in the Legal Profession in Tanzania,’ ambacho kimezinduliwa na Mgeni Rasmi wa hafla ambaye alikuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Mhe. Masaju amesema kuwa, Kitabu hicho ni hazina mpya na dira muhimu ya kisheria na kimaadili kwa kizazi cha sasa na kijacho na kinasalia kuwa funzo kwa Majaji, Mahakimu, Wanasheria, Wanafunzi wa Sheria na kila Mtanzania kuwa mafanikio ya kweli hujengwa kwa maono, uwezo, ujasiri, nidhamu, uadilifu na moyo wa dhati wa kuitumikia jamii. Akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua Kitabu hicho, Mhe. Masaju amesema kuwa, uzinduzi wa kitabu hicho unadhihirisha kwa mara nyingine tena umahiri, ujasiri na alama isiyofutika iliyoachwa na Jaji Mstaafu, Mhe. Munuo katika utumishi wake uliotukuka uliodumu kwa miongo kadhaa, ukiwa ni kielelezo cha umahiri wa kipekee na utetezi thabiti wa misingi ya haki, usawa na utawala wa sheria nchini Tanzania. Jaji Mkuu amekiri kufurahishwa na tukio hilo na kusema kuwa, kwake ni faraja na anamshukuru Mungu kwa kumpa fursa hiyo ya kuzindua kitabu hicho, ambapo amesema, “nina furaha kubwa kushiriki tukio hili lenye umuhimu mkubwa kwa Mahakama ya Tanzania,Taaluma ya sheria, masuala ya jinsia na Taifa letu kwa ujumla, kwani leo hatuzindui kitabu tu, tunazindua kumbukumbu ya historia, tunatambua mchango wa mtumishi aliyejitolea maisha yake katika utumishi wa haki na tunahifadhi utetezi wa taaluma kwa ajili ya kizazi hiki na vizazi vijavyo.” Amesema, tukio hilo ni la uhusishaji wa maarifa, uhusishaji wa hekima na akili, lakini na maadili katika utumishi na jamii ya watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba Mahakama itaendeleza matukio hayo ya uandishi wa vitabu kwa Majaji na watumishi wengine wa Mahakama waliostaafu, kama sehemu na mkakati wa kuhifadhi maarifa, Hekima, akili na maadili ya wenzetu. Mhe. Masaju amesema kitabu hicho kitabu hicho kina umuhimu unaozidi maelezo ya maisha ya mtu mmoja na kwamba ni nyaraka ya kihistoria ya mageuzi ya Mahakama ya Tanzania; ni kumbukumbu ya juhudi za wanawake katika taaluma ya sheria; ni ushahidi wa mabadiliko ya nafasi ya mwanamke katika uongozi wa kitaifa na kimataifa; na zaidi ya yote, ni somo kuhusu namna mtu mmoja anavyoweza kuacha alama katika taasisi na jamii nzima. “Kwa kusoma kitabu hiki, ndipo tunaweza kujua kujifunza mambo mengi yaliyofanywa na Mhe. Munuo alipokuwa katika utumishi wa umma katika Mhimili huu wa Mahakama,” ameeleza Jaji Mkuu. Kadhalika, Mhe. Masaju amesema kuwa, Jaji Eusebia Nicholas Munuo si sehemu tu ya historia ya Mahakama ya Tanzania bali ni miongoni mwa watu walioisaidia historia hiyo kubadilika katika Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kufuatia historia ya Jaji Munuo, Jaji Mkuu amesema, kuna haja ya kuangalia maisha yake si kwa kuhesabu tu vyeo alivyowahi kushika, bali kuangalia milango aliyofungua, taasisi alizojenga, watu aliowainua, kanuni za haki alizozisimamia na kizazi cha wataalam alichokipa ujasiri wa kuamini kwamba nacho kinaweza kufika mbali. Aidha, Mhe. Masaju amekipongeza Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa kulitekeleza jukumu la kuandika kitabu hicho kwa ufanisi ipasavyo mara tu walipoelekezwa na aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa wakati huo, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma pamoja na wote walioshiriki kuandika na kuweka mada zao ndani ya kitabu hicho. Ametoa rai kwa Uongozi wa Mahakama, bado kuna haja na deni kubwa la kuendelea kuandika vitabu kwa Majaji wengine na hasa ambao bado wako hai. Miongoni mwao ameshauri uangaliwe uwezekano wa kuandika mapema iwezekanavyo kitabu kinachohusu sifa za maisha ya Jaji Damian Lubuva. Akizungumzia maisha na safari ya uongozi wa Mhe. Munuo, Jaji Mkuu amesema kwamba, ni kielelezo cha pekee cha uvumilivu, uwezo mkubwa, na utumishi uliotukuka uliovunja vizuizi vya kijinsia na kuweka msingi thabiti katika mfumo wa sheria na utoaji haki nchini Tanzania. Amesema, safari ya Jaji Munuo ndani ya Mhimili wa Mahakama ni ushahidi thabiti kuwa, uwezo hauna jinsia. Alianza kazi yake akiwa na umri wa miaka 24 na kuvunja rekodi katika kila ngazi aliyopitia ambazo ni pamoja na kuwa Hakimu Mkazi wa Kwanza Mwanamke Tanzania aliajiriwa rasmi tarehe 01 Julai, 1970 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Dar es Salaam, Hakimu Mkazi Mfawidhi katika Vituo vya Mwanza na Tabora, akiongoza shughuli za kimahakama, ugawaji wa mashauri, na usimamizi wa watumishi. Nafasi nyingine alizowahi kushika Jaji Munuo ni pamoja na Hakimu Mkazi mwenye Mamlaka ya Ziada (1984), Jaji wa Mahakama Kuu (1987): alipandishwa cheo na kuhudumu katika kanda mbalimbali zikiwemo Mbeya, Songea, Moshi, na Dar es Salaam, Jaji wa Mahakama ya Rufani (2002), alikuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuingia katika Mahakama ya juu ya Nchi. Mhe. Masaju amesema kuwa, Jaji Munuo aliwahi pia kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania ambapo alikabidhiwa dhamana ya kuiongoza Mahakama nzima ya Tanzania katika vipindi mbalimbali. Mbali na vyeo hivyo, Jaji Mkuu ameeleza kuwa, Mhe. Munuo alienda zaidi ya hukumu na kuwa Mwalimu, Mlezi na Mjenzi wa Taasisi. Amesema, “Jaji Munuo hakuwa tu mtoa maamuzi ya kisheria, bali alikuwa mchango hai katika kujenga uwezo wa kitaaluma na taasisi imara nchini.” Kwa upande wa Elimu na Mafunzo, Mhe. Masaju amesema kuwa, Jaji Munuo aliwahi kuwa Mhadhiri katika Chuo cha Usimamizi wa Maendeleo Mzumbe (IDM), akiandaa Maofisa Mahakama na Mahakimu. Alikuwa mtoa mada mkuu katika maadili ya Mahakama, haki za binadamu, usawa wa kijinsia, na kupambana na vitendo vya rushwa ya ngono (sextortion). Vilevile, Jaji Munuo alifanya Utumishi wa Kitaifa Nje ya Mahakama ambapo aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Regional Housing Tribunal, Arusha (1984 - 1987), Mwenyekiti wa Regional Local Government Election Committee, Kamishna wa Law Reform Commission of Tanzania (1984 - 1990), akishiriki katika uchunguzi wa mfumo wa haki jinai, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Majaji (2007–2012) na Mwenyekiti wa National Parole Board of Tanzania (2013–2016). Katika hatua nyingine, Jaji Mkuu amesema kuwa, ili kuhakikisha kuwa mafanikio yake hayabaki kuwa ya pekee yake, Jaji Munuo aliongoza juhudi za kuanzisha Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) mwaka 2000, akihudumu kama Mwanzilishi na Mwenyekiti wake wa kwanza ili kuwajengea uwezo, kuwaunganisha, na kuwalinda wanawake na watoto kisheria. “Ushawishi wake ulivuka mipaka ya nchi hadi kufikia kuongoza International Association of Women Judges (IAWJ) kama Rais wa Kimataifa (2012 - 2014). Chini ya uongozi wake, Tanzania iliweka historia ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 12 wa Kimataifa wa IAWJ uliofanyika Arusha mwezi Mei, 2014,” amesema Mhe. Masaju. Kwa upande wa Maamuzi muhimu ya Kimahakama yaliyounda Sheria, Jaji Mkuu amesema kupitia maamuzi yake makuu ya kimahakama, Jaji Munuo alisaidia kuimarisha misingi ya kisheria na utawala bora nchini. Mhe. Masaju amesema mchango wa Jaji Munuo ulitambuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Desemba, 2012 alipotunukiwa nishani ya heshima ya kitaifa ya Nishani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daraja la Pili (Order of the United Republic of Tanzania, Second Class Medal) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa wakati huo, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na tuzo nyingine za kitaifa na kimataifa. Mhe. Eusebia Munuo alizaliwa tarehe 01 Septemba, 21946 katika Kijiji cha Njari, Uru Kaskazini Moshi mkoani Kilimanjaro. Hafla ya uzinduzi wa Kitabu hicho iliyoratibiwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto imehudhuriwa na Majaji wa Mahakama ya Rufani, baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Antony Jingu, Msajili Mkuu wa Mahakama, Mhe. Eva Kiaki Nkya, Wasajili wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu, Naibu Wasajili, Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama na ya IJA pamoja na Watumishi wa Mahakama Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju akizindua Kitabu cha historia ya Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo kinachoitwa ‘JUSTICE EUSEBIA MUNUO: A Trailblazer in the Legal Profession in Tanzania’ tarehe 17 Novemba, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania-Dodoma. Wanaoshuhudia zoezi hilo kushoto ni, Jaji Mstaafu, Mhe. Munuo na kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Mary Levira. Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akimkabidhi Jaji Munuo nakala za vitabu vya JUSTICE EUSEBIA MUNUO: A Trailblazer In The Legal Profession in Tanzania mara baada ya kukizindua tarehe 17 Novemba, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mhe. George Masaju akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Histioria ya Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Eusebia Munuo kinachoitwa JUSTICE
Wed, 18 Nov 2026 11:04:46 +0000Elgeyo Marakwet: Youth leaders call for support to stop drug abuse
Read the full report from the original source.
RecentlyMcCarthy brushes off fan criticism after Harambee Stars loss to South Africa
Read the full report from the original source.
RecentlyMABADILIKO CHANYA KATIKA JAMII HAYALETWI KWA KUPIGANA, BALI KWA KUSHIRIKIANA; JAJI MSTAAFU MUNUO
Na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma Jaji Mstaafu na Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo amesisitiza kuwa, juhudi zote za kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii, ikiwemo kulinda haki za wanawake na watoto, zinapaswa kuendeshwa kwa pamoja kupitia elimu, mafunzo, na maandishi badala ya migogoro na mabishano. Akitoa neno la shukrani tarehe 17 Novemba, 2026 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kitabu maalum kinachomuenzi kinachoitwa ‘JUSTICE EUSEBIA MUNUO: A Trailblazer in the Legal Profession in Tanzania,’ kilichoandaliwa chini ya uratibu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Jaji Munuo almaarufu kwa jina la Mama Munuo alieleza kuwa nguvu ya kalamu na maarifa husafiri kila kona na kuleta mageuzi ya kudumu kuliko kutumia nguvu. Katika hotuba yake iliyojaa hisia na kumbukumbu za safari yake ndefu ya utumishi, Jaji Munuo ameishukuru Mahakama ya Tanzania pamoja na Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto kwa hatua waliochukua ya kuona umuhimu wa kuwa na kitabu hicho. Kadhalika, Jaji Mstaafu huyo, alikumbushia mchango wa Mwanazuoni na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Prof. Ruth Meena, ambaye wamefanya naye kazi kwa karibu miongo kadhaa. Alisimulia namna ushirikiano wao ulivyosaidia kufungua milango ya kimataifa, ikiwemo safari yake ya kwanza mwaka 1996 kuhudhuria mkutano wa Chama cha Kimataifa cha Majaji Wanawake (IAWJ) mjini Ottawa, Canada, kwa msaada wa mtandao huo na Ford Foundation. Aliongeza kuwa, jitihada za pamoja zilizofanywa kupitia asasi za kiraia na mashirika ya kimataifa kama ‘UN Women’ zimesaidia kupiga vita vitendo vya rushwa ya ngono (sextortion), kiasi kwamba leo hii elimu hiyo imefika hadi vijijini na kuongeza uelewa mpana kwa jamii. Akizungumzia uanzishwaji wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), Jaji Munuo alibainisha kuwa mafanikio ya chama hicho hayakujengwa na wanawake pekee, bali yalitokana na ushirikiano thabiti wa Mahakama na Majaji wa kiume (akiwataja viongozi kama aliyekuwa Jaji Mkuu, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, Jaji Ignas Kitusi na Mhe. Masati. Alieleza kuwa, uwepo wa Majaji wa kiume katika mafunzo yaliyotolewa vijijini uliimarisha uaminifu (credibility) kwa jamii, kwani wananchi waligundua kuwa lengo kuu lilikuwa ni maendeleo ya familia nzima na usalama wa watoto, badala ya mgawanyiko wa kijinsia. Jaji Munuo alihitimisha kwa kutoa rai kwa Majaji, Mahakimu na Wanasheria vijana kwamba, Uongozi wa kimahakama unavuka mipaka ya kusikiliza mashauri mahakamani pekee, bali watumishi wa sheria wanapaswa kujitokeza kama Viongozi na waelezi wazuri katika jamii ili kuhakikisha kuna amani, upendo katika familia na taifa kwa ujumla. Kitabu hicho kipya kinatazamwa kama hazina kubwa na kifungua macho (eye opener) kitakachonufaisha vizazi vya sasa na vijavyo katika kuimarisha misingi ya utawala wa sheria nchini Tanzania na kimataifa. Awali akitoa neno la utangulizi wakati wa uzinduzi wa Kitabu hicho kilichozinduliwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju, Hakimu Mkazi Mkuu na Mkurugenzi wa Mafunzo-Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Patricia Kisinda alisema siku hiyo si ya kuzindua kitabu pekee; bali pia ni siku ya kutambua historia, kuenzi utumishi uliotukuka na kuthamini mchango wa kipekee katika maendeleo ya haki na utawala wa sheria nchini Tanzania wa Jaji Mstaafu, Mhe. Eusebia Munuo. “Tukio hili la leo lina umuhimu wa kipekee kwakuwa linaakisi historia ya Jaji Munuo, Mwanamke aliyefungua njia katika taaluma ya sheria Nchini,” alisisitiza Mhe. Dkt. Kisinda. Aliongeza kuwa, historia ya Jaji Mstaafu, Mhe. Munuo ni fahari ya Mahakama na Nchi kwa ujumla kwakuwa mafanikio yake ni somo la na urithi wa utumishi wake wa umma uliotukuka ni mwongozo wa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. Jaji Mstaafu na Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo akitoa neno la shukrani wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Jaji Munuo kiitwacho ‘JUSTICE EUSEBIA MUNUO: A Trailblazer in the Legal Profession in Tanzania, kilichozinduliwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju tarehe 17 Novemba, 2026 kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Baadhi ya Majaji, Viongozi, Watumishi wa Mahakama pamoja na Wageni waalikwa walioshiriki katika Hafla ya Uzinduzi wa Kitabu ‘JUSTICE EUSEBIA MUNUO: A Trailblazer in the Legal Profession in Tanzania, kilichozinduliwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju tarehe 17 Novemba, 2026 kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kushoto) akiwa pamoja na Hakimu Mkazi Mkuu na Mkurugenzi wa Mafunzo - Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Patricia Kisinda wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha Jaji Mstaafu, Mhe. Eusebia Munuo kiitwacho ‘JUSTICE EUSEBIA MUNUO: A Trailblazer in the Legal Profession in Tanzania.'
Wed, 18 Nov 2026 11:00:36 +0000Abadepite banenze imiburanishirize y'urubanza ruregwamo Moise Katumbi
Abadepite bo mu Ntara ya Haut-Katanga bahagarariye ishyaka Ensemble pour la République banenze imigendekere y’urubanza Moïse Katumbi aregwamo na murumuna we Raphaël Katebe Katoto mu Rukiko rw’Ikirenga rwa Repubulika Iharanira Demokarasi ya Congo (RDC). Bavuze ko hari amategeko n’imiburanishirize bitubahirijwe kandi rwahinduwe urwa politiki.
Wed, 18 Nov 2026 12:41:57 +0200Nigeria approves law allowing states to run their own police
But critics fear that governors could use the forces to intimidate political opponents, suppress dissent or influence elections.
RecentlyRegina Re's daughter charged with murder of grandmother as DPP opposes bail
An 18-year-old daughter of former television actress Regina Re has been charged with murdering her 86-year-old grandmother in a case that has shocked the family.
Wed, 18 Nov 2026 12:56:00 +0300Nairobi–Thika highway motorists to pay tolls under proposed Sh100bn road project
Latest · Economy
RecentlyINGINGO Z'INGENZI Z'IMPAMVU YO GUSABA GUHINDUZA AMAZINA
Wed, 18 Nov 2026 12:37:33 +0200General Muhoozi Will Continue Giving Ugandans the Freedom They Are Enjoying Currently
Read the full report from the original source.
RecentlyGhana's new $60m presidential jet sparks outrage
The government says the purchase is justified, arguing that Ghana's improving economy makes it affordable and is needed to replace an ageing presidential jet
RecentlyRAIS DKT. MWINYI AZINDUA JUKWAA LA UWEKEZAJI WA MWANI, ATOA WITO WA KUONGEZA THAMANI YA ZAO HIL
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amefungua Jukwaa la Uwekezaji la Zao la Mwani Zanzibar 2026 leo tarehe 18 Novemba 2026 katika Hoteli ya Golden Tulip Mkoa wa Mjini Magharibi, akisisitiza umuhimu wa kuimarisha usarifu wa mwani na uzalishaji wa bidhaa zenye thamani kubwa ili kuongeza kipato cha wakulima, ajira na kuchochea ukuaji wa Uchumi wa Buluu. Amesema Serikali imeweka sekta ya Uchumi wa Buluu katika nafasi muhimu ya mageuzi ya uchumi wa Zanzibar, hivyo itaendelea kuwekeza katika teknolojia za kisasa, kilimo cha mwani katika kina kirefu cha bahari, upatikanaji wa mbegu bora na tafiti za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Aidha, Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya ukaushaji, uhifadhi, ukusanyaji na usarifu wa mwani ili kuongeza ubora wa zao hilo, kupunguza upotevu baada ya mavuno na kuwawezesha wakulima kunufaika zaidi na shughuli zao. Rais Dkt. Mwinyi amewakaribisha wawekezaji wenye mitaji, teknolojia na utaalamu kuwekeza katika sekta hiyo, akisisitiza umuhimu wa uwekezaji utakaowezesha upatikanaji wa masoko ya uhakika, kuongeza ajira kwa vijana na kuwashirikisha wananchi katika mnyororo mzima wa thamani wa zao la mwani. Katika hafla hiyo, Rais Dkt. Mwinyi amezindua Zanzibar Seaweed Investment Promotion Deal Book, inayobainisha fursa za uwekezaji katika uzalishaji wa mbegu bora, teknolojia za kilimo, ukaushaji, uhifadhi, usarifu wa viwandani na utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na mwani kwa matumizi ya vyakula, vipodozi, dawa na kilimo. Viongozi mbalimbali wamehudhuria wakiwemo wa Serikali, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, wawekezaji, taasisi za fedha, washirika wa maendeleo, watafiti, sekta binafsi, wakulima na wadau mbalimbali wa zao la mwani kutoka ndani na nje ya nchi.
Wed, 18 Nov 2026 10:32:09 +0000U Rwanda rwahaye Liberia ibitekerezo ku kubaka amahoro arambye
Read the full report from the original source.
RecentlyHigh ARV Sales Push Quality Chemical Revenue to UGX195 Billion, Profit Drops to UGX15.6 Billion
Read the full report from the original source.
RecentlyNew Child-Protection System: Is Government Planning to Take Children Away From ‘Irresponsible’ Parents?
Read the full report from the original source.
RecentlyGov’t lifts NGO ban, but tightens political leash
The meeting between Uganda’s minister of Internal Affairs and civil society organizations ended last week on an unexpectedly hopeful note. Prof Ephraim Kamuntu, newly appointed…
RecentlyPage 150 of 1128 · 22553 stories