Unganishwa

Search the region

22597 stories

Uncategorized · Iwacu

Mardi ne sera pas un mardi comme les autres !

Il y a des mardis qui passent comme des feuilles mortes, emportés par le vent, oubliés avant même d'avoir existé. Et puis, il y a ce mardi-là. Mardi 17 novembre 2026. À Bujumbura. Ce mardi-là, le Burundi ne jouera pas un match de football. Le Burundi vivra un rendez-vous avec son destin. Le Burundi regardera la Zambie dans les yeux, et lui dira : tu ne m'as pas tué à Ndola, tu ne me tueras pas ici.

Mon, 16 Nov 2026 07:14:48 +0000
Uncategorized · Iwacu

Le classement, ou le miroir d’un championnat amoureux

Regardez ce tableau, amis sportifs. Regardez-le bien. Car ce tableau ne dit pas seulement des chiffres. Il raconte des destins. Il raconte des amours naissantes, des gloires qui vacillent, des douleurs qui se taisent. Après douze journées, la Primus Ligue Burundi 2026-2027 a enfin montré son vrai visage. Un visage splendide, cruel, magnifique.

Mon, 16 Nov 2026 07:21:56 +0000
Uncategorized · Iwacu

Églises : entre unité spirituelle et divisions confessionnelles

Alors que les Églises sont appelées à promouvoir l'amour, la solidarité et la cohésion sociale, certaines pratiques confessionnelles semblent parfois favoriser l'exclusion et la discrimination. À Bujumbura, des fidèles témoignent de tensions liées à leur appartenance religieuse, notamment dans les relations sociales et les unions matrimoniales. Une sociologue rappelle que les confessions religieuses devraient être des espaces de rassemblement plutôt que de division.

Mon, 16 Nov 2026 14:18:56 +0000
Uncategorized · Iwacu

Plus de 30 jeunes Imbonerakure morts et plusieurs autres blessés dans un accident de roulage à Busoni

La commune Busoni dans la province de Butanyerera est en deuil, elle déplore la mort de 31 jeunes Imbonerakure dans un accident grave survenu dans la soirée de ce dimanche 15 novembre à Kabanga dans cette même commune du nord du Burundi. Ces jeunes avec leurs camarades militants du parti au pouvoir étaient à bord […]

Mon, 16 Nov 2026 18:54:05 +0000
Uncategorized · Iwacu

Réforme de l’Obuha : Le fiasco plane toujours

Lors des questions orales mercredi 28 octobre 2026 0 L’Assemblée nationale, Alain Ndikumana, ministre des Finances, a annoncé le retrait à l’Obuha de la construction des infrastructures publiques. La mission est désormais confiée aux départements communaux. Pour certains membres de la société civile, une telle réforme risque d’être comme un coup d’épée dans l’eau.

Tue, 17 Nov 2026 05:38:23 +0000
Uncategorized · Iwacu

La douzième journée, ou le week-end où le Burundi a battu comme un seul cœur

Il y a des week-ends qui passent, et il y a des week-ends qui restent. Car, du samedi 07 au dimanche 08 novembre 2026, la Primus Ligue Burundi n'a pas seulement offert des scores. Elle a offert des frissons, des larmes, des silences, des cris. Elle a offert ce que seul le football burundais sait offrir : une poésie brute, sincère, presque douloureuse.

Tue, 17 Nov 2026 06:23:30 +0000
Uncategorized · Iwacu

Programme REST-GLR 2027-2033 : le Burundi affine sa feuille de route pour faire du commerce transfrontalier un levier de paix durable

Réunis dans un atelier national de consultation, le Gouvernement burundais et le Programme des Nations-unies pour le Développement (PNUD) ont posé les jalons de la contribution nationale au programme régional REST-GLR. Cette initiative stratégique ambitionne de transformer les frontières burundaises en véritables écosystèmes économiques intégrés centrés sur l’économie bleue autour du lac Tanganyika, les corridors agroéconomiques autour de la Rusizi ainsi que le commerce résilient autour de Kobero et des autres postes frontières.

Tue, 17 Nov 2026 10:39:28 +0000
Uncategorized · Iwacu

Protocole d’accord Burundi/Gigawatt : Du développement des pôles agro-énergétiques au service de l’économie rurale

La société Gigawatt Burundi S.A. et le Gouvernement de la République du Burundi ont signé, samedi 14 novembre à Bujumbura, un protocole d’accord portant sur le développement des énergies renouvelables décentralisées, des mini-réseaux électriques, de l’électrification rurale et des usages productifs de l’énergie renouvelable au Burundi, dans le cadre du programme PURE Power Burundi. Ledit accord vise à faire de l’énergie un véritable moteur de transformation des économies rurales.

Tue, 17 Nov 2026 11:57:40 +0000
Uncategorized · Iwacu

Kirundo : Une assistance russe pour 40 mille vulnérables

De la farine de blé et du pois cassé, c’est le paquet d’un don que la Fédération de Russie a octroyé, ce mardi 17 novembre 2026, à Bujumbura, au Programme Alimentaire Mondial (PAM). Ces denrées ont une valeur de 2 millions de dollars américains.

Tue, 17 Nov 2026 15:10:03 +0000
Uncategorized · Iwacu

Raphaël Yaminyibuka, un parcours atypique au service du développement local

Dans la zone Gahabura, en commune Bukinanyana de la province de Bujumbura, Raphaël Yaminyibuka, surnommé Rwasa, est devenu un acteur important de l’économie locale. À travers son entreprise Coffee Quality Business, il emploie aujourd’hui 110 personnes et contribue à améliorer les conditions de vie de nombreux ménages. Son parcours, fait de revers et de persévérance, témoigne d’une reconversion réussie dans l’entrepreneuriat.

Wed, 18 Nov 2026 05:31:52 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

UMAHIRI WA EWURA WAWAVUTA WAGAMBIA KUJIFUNZA UDHIBITI

Na.Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM Umahiri wa utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) umewavutia wadhibiti wenza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati, Maji, Mawasiliano na Usafiri(PURA) kutoka nchini Gambia, ambao wameitembelea mamlaka hiyo kwa lengo la kujifunza mifumo na mbinu zinazotumiwa katika kutekeleza majukumu ya udhibiti kwa ufanisi. Ujumbe huo kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati, Maji, Mawasiliano na Usafiri (PURA) ya Gambia umeonesha nia ya kujifunza uzoefu wa EWURA katika usimamizi wa sekta zinazodhibitiwa, hususan mifumo ya utoaji leseni, ufuatiliaji wa watoa huduma na utatuzi wa malalamiko ya watumiaji wa huduma. Akizungumza wakati wa kuwakaribisha wajumbe wa Bodi ya PURA ya Gambia, Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Profesa Mark Mwandosya, alisema mafanikio ya mamlaka hiyo yanatokana na kuzingatia misingi imara ya utendaji inayojengwa katika utaalamu, uwazi na uhuru wa kufanya maamuzi ya kiudhibiti. Alisema EWURA katika kutekeleza majukumu yake huzingatia maslahi ya pande zote muhimu, wakiwemo watoa huduma, watumiaji wa huduma na Serikali, kwa lengo la kuhakikisha maamuzi yanayofanywa yanakuwa na tija na kuleta matokeo chanya katika sekta zinazodhibitiwa. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya PURA ya Gambia, Bibi Lucy Fye, alisema wamevutiwa na mifumo ya EWURA ya kushughulikia malalamiko ya wananchi, taratibu za utoaji wa leseni pamoja na namna mamlaka hiyo inavyofuatilia utendaji wa watoa huduma walio chini ya udhibiti wake. Aliongeza kuwa wamevutiwa pia na mfumo wa utawala na uendeshaji wa EWURA pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa leseni na vibali, hatua inayorahisisha utoaji wa huduma na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kiudhibiti. Ziara hiyo inatoa fursa ya kubadilishana uzoefu na maarifa kati ya taasisi hizo mbili za udhibiti, huku ikilenga kuimarisha ushirikiano katika kuboresha mifumo ya udhibiti na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mon, 16 Nov 2026 17:39:18 +0000
Health · Issa Michuzi

TIRA YAWEKA MSISITIZO BIMA YA AFYA KWA WOTE, YATOA ONYO KWA SKIMU ZA BIMA

*Yasisitiza wananchi kujiunga na skimu zilizosajiliwa, yataka uwazi wa vifurushi na huduma Na Said Mwishehe,Michuzi Blog MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imewataka Watanzania kujiunga na skimu za bima ya afya zinazotambulika kisheria ili kujikinga na gharama za matibabu, huku ikizionya kampuni na skimu zinazotoa huduma hizo kuhakikisha wananchi wanapewa taarifa sahihi kuhusu vifurushi na stahiki zao. Mamlaka hiyo imesema utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote ni hatua muhimu katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za matibabu wanapozihitaji bila kukabiliwa na vikwazo vya kifedha, lakini mafanikio yake yanategemea uwazi, uaminifu na usimamizi madhubuti wa watoa huduma. Akizungumza leo Novemba 16,2026 jijini Dar es Salaam katika kikao kilichoandaliwa na TIRA chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Kamishna Mkuu wa TIRA, Dk. Baghayo Saqware, amesema mamlaka hiyo ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ya mwaka 2023, ikiwamo kuhakikisha skimu za umma na binafsi zinatoa huduma kwa kuzingatia sheria na kulinda haki za wanachama. Amesema wananchi wanapaswa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) au kampuni binafsi za bima zilizosajiliwa na kusimamiwa na TIRA, akisisitiza kuwa bima ya afya ni kinga inayopaswa kununuliwa kabla ya mtu kuugua. “Bima ya afya ni utaratibu wa kununua kinga kabla ya ugonjwa ili uweze kupata matibabu unapougua. Huwezi kusubiri gari ipate ajali ndipo uanze kutafuta bima,” amesema. Dk. Saqware amesema wananchi wanaojiunga na NHIF au kampuni binafsi zilizosajiliwa wana haki ya kupata huduma kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa, huku TIRA ikiendelea kusimamia watoa huduma ili kuhakikisha wanatimiza wajibu wao. Amezitaka kampuni na skimu za bima kuhakikisha kabla ya mwananchi kujiunga, anapewa maelezo yanayoeleweka kuhusu huduma zinazolipiwa, zile ambazo hazijumuishwi, masharti ya matumizi ya bima na utaratibu wa kupata matibabu. Pia ameonya dhidi ya matumizi ya matangazo na ahadi zinazoweza kuwapotosha wananchi na kuwafanya kujiunga na vifurushi bila kuelewa huduma wanazostahili kupata. Aidha amezitaja skimu hizo kuweka wazi orodha ya hospitali, vituo vya afya na zahanati zinazotambuliwa katika utoaji wa huduma ili wananchi waweze kujua wanakoweza kupata matibabu kupitia bima zao. “Ni muhimu malalamiko ya wanachama kupokelewa, kuchunguzwa na kutatuliwa kwa wakati katika ngazi za kampuni na skimu husika, huku wananchi wanaoshindwa kupata suluhisho wakipewa nafasi ya kuwasilisha malalamiko yao TIRA kwa hatua zaidi za kiudhibiti.” Amefafanua jukumu la mamlaka hiyo si kuwa idara ya madai ya kampuni za bima, bali kuhakikisha watoa huduma wanatimiza wajibu wao na kulinda haki za wananchi. Kuhusu sekta ya bima kukua kwa kasi amesema mchango wake katika Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 1.68 mwaka 2021 hadi asilimia 2.11 mwaka 2025, huku mamlaka hiyo ikilenga kufikisha mchango huo asilimia tano ifikapo mwaka 2050. Amefafanua ongezeko hilo linaashiria kuimarika kwa matumizi ya huduma za bima nchini, ambapo idadi ya watumiaji imeongezeka kutoka milioni 5.6 mwaka 2021 hadi milioni 26.8 mwaka 2025. “Mafanikio hayo yanaonyesha kuongezeka kwa uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa bima katika kulinda mali, afya, biashara na uwekezaji dhidi ya vihatarishi mbalimbali. “Aidha ajira rasmi katika sekta hiyo zimeongezeka kutoka 3,777 mwaka 2021 hadi 15,568 mwaka 2025, huku matumizi ya huduma za bima kwa kila Mtanzania yakipanda kutoka Sh15,560 hadi Sh67,455 katika kipindi hicho.” Dkt. Saqware amesema ukubwa wa soko la bima nao umeongezeka, ambapo thamani ya ada za bima zilizokusanywa imepanda kutoka Sh bilioni 911 mwaka 2021 hadi Sh trilioni 2.55 mwaka 2025. Amesema mali za kampuni za bima zimeongezeka kutoka Sh bilioni 979 mwaka 2021 hadi Sh trilioni 2.2 mwaka 2025, huku thamani ya mali zilizowekewa kinga ya bima ikipanda kutoka Sh bilioni 367 hadi Sh trilioni 1.29. Ameongeza sekta hiyo imeendelea kuimarika katika ulipaji wa madai, ambapo takwimu za mamlaka zinaonyesha kuwa asilimia 95 ya madai hulipwa, huku changamoto zinazobaki zikihusishwa na masuala ya nyaraka na uchunguzi wa udanganyifu.

Mon, 16 Nov 2026 17:43:39 +0000
Health · Issa Michuzi

MCHENGERWA: ATAKA UCHUNGUZI UFANYIKE HOSPITALI YA WILAYA YA MAFIA

Na John Mapepele, Mafia Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa amemtaka Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Grace Magembe kuunda Kamati ya uchunguzi ili kuchunguza utolewaji wa huduma katika Hospitali ya  Wilaya ya Mafia ili kuboresha huduma katika hospitali hiyo. Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Novemba 16, 2026  baada ya kufanya ziara ya kikazi na kukagua maeneo mbalimbali ya Hospitali hiyo ambapo hakuridhishwa na utendaji kazi. Ninamuelekeza Katibu Mkuu kuunda timu kuja kufanya uchunguzi na kubaini changamoto ili kuja na suluhisho la maboresho ya kudumu katika hospitali Amesema dhamira ya Serikali kwa sasa  ni kuifanya hospitali hiyo kutoa huduma za afya kwa kiwango cha kisasa na kuachana na mazoea. amefafanua sababu za kuifanya Hospitali hiyo kutoa huduma kwa kiwango cha kisasa kuwa ni pamoja na sehemu ya kisiwa hicho  kuwa na Hifadhi ya Bahari ambayo huleta wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani. "Sote tunajua eneo hili la mafia ni eneo la kimkakati katika nchi yetu lina Hifadhi ya Bahari ambayo inatembelewa na watalii wengi hivyo pindi wanapopata shida za kiafya lazima tuwe na hospitali inayoweza kutoa huduma ya uhakika tofauti na sasa". Ameongeza Mhe. Mchengerwa Aidha, ameitaja sababu nyingine kuwa kisiwa cha Mafia kipo pembeni mwa Tanzania bara na bado hakuna usafiri wa uhakika hivyo ni muhimu kuwa na huduma zilizoboreka. Ametoa wiki mbili kwa uongozi wa hospitali hiyo kufunga mashine za kisasa  za  X-ray ambazo imepelekwa kwenye zahanati ya Chole. "Naelekeza ile X-ray Mashine ya kisasa ambayo haijafungwa kwenye zahanati ya Chole sasa ije ifungwe hapa kwa kuwa hapa kuna uhitaji zaidi kuliko kule." amesisitiza Mhe. Waziri Mchengerwa. Katika ziara hiyo ambayo aliambatana na Mkurugenzi wa Idara Kinga Dkt. Hamad Nyembea alipata fursa ya kuongea na wagonjwa waliofika kutibiwa.

Mon, 16 Nov 2026 17:50:52 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

WAFUGAJI KIBAHA WATAKIWA KUFUGA KISASA KUNASA SOKO LA NJE-MAGOGWA

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha WAFUGAJI katika Manispaa ya Kibaha mkoani Pwani wametakiwa kuboresha ufugaji kwa kuzingatia kanuni za kisasa ili kukidhi vigezo vya masoko ya nje na ndani ya nchi, ikiwemo kupanda majani ya malisho, kutoa chanjo kwa mifugo na kutumia mfumo wa ufugaji wa ndani (zero grazing). Hatua hiyo inalenga kuongeza ubora na uzalishaji wa mifugo, kudhibiti magonjwa pamoja na kupunguza migogoro kati ya wakulima na wafugaji. Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibaha, Moses Magogwa, Novemba 16, 2026, wakati akizindua awamu ya pili ya zoezi la chanjo na utambuzi wa mifugo kwa ruzuku, eneo la Mtakuja, Kata ya Pangani, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Fadhil Nkurlu. Magogwa alisema wafugaji wamekuwa wakikosa fursa za soko la nje kutokana na kutofikia vigezo vinavyohitajika, huku akitaja uwepo wa viwanda vya kuchakata nyama vya Tan Choice na Union Meat kuwa fursa inayopaswa kutumiwa na wafugaji wa eneo hilo. Alisema viwanda hivyo vimekuwa vikikabiliana kutopata mifugo inayokidhi mahitaji yake, hivyo ni muhimu wafugaji kuboresha mbinu za ufugaji ili kuongeza uzalishaji na ubora wa mifugo inayozalishwa. Alieleza kuwa Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuja na mpango wa chanjo na utambuzi wa mifugo kwa ruzuku ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali, ikiwemo homa ya mapafu kwa ng'ombe, pamoja na kuweka alama za utambulisho zitakazosaidia kudhibiti wizi wa mifugo. Aidha, Magogwa aliwataka wataalamu wa mifugo kuendelea kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu ufugaji wa kisasa, ikiwemo kuwatembelea katika shamba la mbegu za majani lililopo Vikuge, Kata ya Soga, ili kujifunza namna ya kupanda na kuzalisha malisho kwa ajili ya mifugo yao na hivyo kupunguza tabia ya kuhama hama kutafuta chakula. Kwa upande wake, mfugaji wa Mtaa wa Mtakuja, Twalibu Selemani, alisema mpango huo wa miaka mitano ni mkombozi kwao kwa kuwa utasaidia kukabiliana na changamoto ya vifo vya mifugo vinavyotokana na magonjwa pamoja na wizi unaochangiwa na kutokuwepo kwa alama za utambulisho. Naye Daktari wa Mifugo wa Manispaa ya Kibaha, Chiza Martin, alisema Serikali imetoa chanjo kwa ruzuku pamoja na kuweka miundombinu wezeshi kwa ajili ya kurahisisha utekelezaji wa zoezi hilo. Alisema kabla ya kuanza kwa mpango huo, wafugaji walikuwa wakichangia Sh 1,500 kwa chanjo ya ng'ombe, Sh 300 kwa mbuzi na kondoo, huku chanjo ya kuku ikitolewa bure. Alifafanua kuwa chanjo hizo zinalenga kukabiliana na magonjwa ya homa ya mapafu, sotoka na mdondo (kideli). Alisema Manispaa ya Kibaha ina jumla ya ng'ombe 85,000, mbuzi 65,000 na kuku 300,000, huku katika awamu hii Serikali ikiwa imeanza kutoa chanjo kwa ng'ombe 2,000, kuku 150,000 na mbuzi 1,500.

Mon, 16 Nov 2026 17:55:32 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

Krismasi Yazidi Kunoga! Kwa Wateja wa Meridianbet

MERIDIANBET imekuja na zawadi nyingine ya burudani kwa wapenzi wa michezo ya kasino kupitia Xmas Guardians Megaways, mchezo maalumu kutoka Pragmatic Play unaobeba mvuto wa sikukuu za Krismasi. Mchezo huu unawaalika wateja kuingia katika ulimwengu wa kipekee uliojaa mandhari ya sikukuu, ubunifu na msisimko wa kila mzunguko. Kupitia mchezo huu, wachezaji wanapata nafasi ya kuungana na Walinzi wa Krismasi katika safari inayochanganya burudani na mazingira ya kuvutia. Muonekano wake maalumu unaendana na furaha ya msimu wa sikukuu, na kuufanya kuwa chaguo la kipekee kwa wanaopenda michezo yenye mandhari tofauti. Moja ya vitu vinavyoongeza mvuto wa mchezo huu ni mfumo wa Megaways unaobadilisha idadi ya alama zinazoweza kuonekana katika kila mzunguko. Mfumo huu unaifanya kila spin kuwa na muundo tofauti, huku ukiwapa wachezaji uzoefu wa kipekee wanapoendelea kufurahia mchezo. Katika kipindi hiki maalumu, Meridianbet imewaandalia wateja wake fursa ya kufurahia Xmas Guardians Megaways kupitia michezo ya kasino . Ni sehemu ya burudani inayowaletea wapenzi wa michezo ya kasino chaguo jipya linaloendana na msimu wa Krismasi. Jambo la kuzingatia ni kwamba mchezo huu utapatikana kwa wateja wa Meridianbet pekee ndani ya kipindi maalumu cha promosheni. Hii inawapa wateja wa jukwaa hilo nafasi ya kipekee ya kujaribu mchezo huu kutoka Pragmatic Play na kujionea burudani yake. Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Walinzi wa Krismasi wanakuita, je, uko tayari kuungana nao? Tembelea Meridianbet, ingia kwenye sehemu ya kasino na ujaribu Xmas Guardians Megaways . Usikose burudani hii maalumu, cheza ufurahie ushindi. Jiunge na meridianbet leo ufurahie mzuka wa krismasi.

Tue, 17 Nov 2026 04:30:00 +0000
Sports · Issa Michuzi

Ushindi Mkubwa Unakusubiri Siku ya Leo

LEO hii unaweza ukaondoka na pesa ukibashiri mechi zako za ushindi, Kule Ulaya na huku Afrika mechi za Kimataifa bado zipo. Ingia kwenye akaunti yako na usuke jamvi lako sasa. Pesa ipo kwenye mechi ya Denmark dhidi ya Norway ambapo kwenye msimamo wa Kundi wanapishana pointi 3 pekee, hii ni mechi ambayo kila timu inahitaji ushindi ili kuweza kujiweka kwenye nafasi ya pili. Denmark ametoka kushinda mechi yake iliyopita hivyo anaingia kwenye mchezo huu akiwa na ari ya nguvu kabisa, halikadhalika kwa Norway naye amtoka kutoa dozi kubwa. Odds kubwa zipo kwenye mechi hii. Suka jamvi hapa. Timu zote zina wachezaji wakubwa na ambao wanacheza ligi kubwa wakiwemo kina Haaland, Hojlund, Odergaard na wengine wengi. Piga pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Mechi nyingine ya UEFA NATIONS ni hii inayowakutanisha kati ya Wales dhidi ya Ureno moja ya mechi ambayo itakuwa ikitazamwa sana kutoka na matokeo yao yaliyopita, ambapo timu hizi zote zimetoka kupoteza michezo yao iliyopita. Lakini kwa upande wa Ureno hali imekuwa mbaya zaidi baada ya kupokea kipigo kizito kabisa huku maneno yakiibuka kwamba kutokuwepo kwa Ronaldo pia imechangia hivyo timu hiyo chini ya kocha mkuu Jorge inabidi ijiangalie. Jisajili hapa. Vijana wa Bellamy, Wales wanahitaji matokeo mazuri katika mchezo huu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuepuka kushuka daraja, lakini wanakutana na Ureno yenye kikosi chenye uzoefu na ubora mkubwa. Wales imekuwa na wakati mgumu katika michezo ya hivi karibuni, ikipoteza mechi nne kati ya tano za Nations League. Hata hivyo, uwepo wa Harry Wilson, David Brooks na Brennan Johnson unaweza kuongeza makali katika safu yao ya ushambuliaji. Kwa upande wa Ureno, licha ya kupokea kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Denmark katika mchezo uliopita, wana wachezaji wenye uwezo wa kubadilisha matokeo kama Bruno Fernandes, João Félix na Gonçalo Ramos. Pia, Ureno itahitaji kujipanga upya katika safu ya ulinzi kutokana na kukosekana kwa Rúben Dias, huku Wales ikitafuta kutumia faida ya kucheza nyumbani kupata matokeo mazuri. Kule kwa wakali wa ubashiri Tanzania, Meridianbet wao wanampa nafasi kubwa ya kushinda Ureno. Je wewe beti yako unaiweka kwa nani siku ya leo?. Jisajili hapa. Lakini pia ile michuano ya kufuzu AFCON inaendelea kwa michezo mingi lakini sisi tutajikta na mchezo wa Tanzania dhidi ya Nigeria huku hii ikiwa ni mechi ya kisasi kwa wenyeji baada ya kupigika kwenye mechi ya kwanza walipokutana. Kwenye Kundi lao, Tanzania ambao ni moja ya wenyeji wa michuano hii 2027, wapo nafasi ya mwisho ambayo ni ya mwisho, huku Nigeria wao wakiwa nafasi ya 2 kwenye msimamo baada ya kujikusanyia pointi zao 6. Chini ya kocha mkuu Gamondi bado Stars haipewi nafasi ya kushinda mechi hii kutokana na ubora wa wachezaji ambao timu pinzani inayo, pia wengi wa wachezaji wao wanacheza kwenye ligi kubwa Duniani. Je hii ni mechi ya wenyeji kushinda?. Suka jamvi hapa.

Tue, 17 Nov 2026 06:00:00 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

Kampuni Mpya ya Betting Yazinduliwa, GBT Yasisitiza Uwajibikaji Kwa Jamii.

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) imezitaka kampuni za michezo ya kubahatisha (betting) na kasino, kuzingatia kikamilifu sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia sekta hiyo ili kulinda maadili na ustawi wa vijana, sambamba na kuongeza mchango wao katika maendeleo ya kijamii kupitia sekta za elimu, afya na michezo. Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa GBT, James Mbalwe, wakati akiongoza hafla ya uzinduzi wa kampuni mpya ya michezo ya kubashiri ya BetSasa, iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni maalumu ya kuwazawadia wateja zawadi mbalimbali, ikiwemo gari jipya aina ya Jetour. Akizungumza katika hafla hiyo, Mbalwe alisema ongezeko la kampuni zinazoendesha shughuli za michezo ya kubahatisha nchini linapaswa kwenda sambamba na manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa taifa, yakiwemo mapato ya Serikali na mchango katika kuboresha huduma za kijamii. “Tunawakaribisha BetSasa katika soko la Tanzania. Tumeona wameanza vizuri kwa kuja na kampeni hii inayolenga kuwazawadia wateja wao zawadi mbalimbali, ikiwemo gari jipya la kisasa. Hata hivyo, tunatoa wito kwao na kampuni nyingine katika sekta hii kuongeza tija ya shughuli zao kwa kuhakikisha wanarejesha kwa jamii kupitia kusaidia sekta za afya, elimu, michezo na maeneo mengine muhimu ya maendeleo,” alisema Mbalwe. Aidha, aliwataka washiriki wa michezo ya kubahatisha, hususan vijana, kushiriki kwa uwajibikaji na kwa kiasi, huku wakitambua umuhimu wa kutenga muda na rasilimali zao kwa ajili ya kazi, shughuli za uzalishaji na majukumu mengine ya kijamii. Akizungumzia kampeni hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa BetSasa, Jimmy Kenneth, alisema kampeni hiyo itadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja na inajulikana kwa jina la “Kusanya Point, Usepe na Jetour”, ikiwa na lengo la kuwapa wateja fursa ya kushinda zawadi mbalimbali, kuanzia fedha taslimu kila wiki hadi gari jipya aina ya Jetour. “Promosheni hii imeandaliwa mahususi kwa ajili ya wadau na wateja wetu. Kupitia kampeni hii, tutakuwa tukiwazawadia washindi 50 fedha taslimu kila wiki, huku zawadi kubwa ikiwa ni gari jipya aina ya Jetour litakalotolewa kila baada ya miezi mitatu,” alisema. Aliongeza kuwa BetSasa imejipanga kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia sheria, kanuni, masharti na miongozo ya mamlaka zinazosimamia sekta ya michezo ya kubahatisha nchini, sambamba na kutekeleza wajibu wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), James Mbalwe (wa kwanza kulia), akikagua gari jipya aina ya Jetour litakalotolewa kama zawadi kwa washindi wa kampeni ya BetSasa, kampuni mpya ya michezo ya kubashiri nchini. Kampeni hiyo inayojulikana kwa jina la “Kusanya Point, Usepe na Jetour” inawapa wateja fursa ya kushinda zawadi mbalimbali, zikiwemo fedha taslimu kwa washindi 50 kila wiki na gari jipya aina ya Jetour kila baada ya miezi mitatu. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi na Mmiliki wa BetSasa, Vakhtang Nikoleishvili (kushoto), pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Jimmy Kenneth (katikati) Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), James Mbalwe (kushoto), sambamba na Mkurugenzi na Mmiliki wa BetSasa, Vakhtang Nikoleishvili (katikati), pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Jimmy Kenneth (kulia) wakijipongeza wakati wakionyesha zawadi ya gari jipya aina ya Jetour litakalotolewa kama zawadi kwa washindi wa kampeni ya BetSasa, kampuni mpya ya michezo ya kubashiri nchini. Kampeni hiyo inayojulikana kwa jina la “Kusanya Point, Usepe na Jetour” inawapa wateja fursa ya kushinda zawadi mbalimbali, zikiwemo fedha taslimu kwa washindi 50 kila wiki na gari jipya aina ya Jetour kila baada ya miezi mitatu Akizungumzia kampeni hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa BetSasa, Jimmy Kenneth (alieshika mic) alisema kampeni hiyo itadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja na inajulikana kwa jina la “Kusanya Point, Usepe na Jetour”, ikiwa na lengo la kuwapa wateja fursa ya kushinda zawadi mbalimbali, kuanzia fedha taslimu kila wiki hadi gari jipya aina ya Jetour.

Tue, 17 Nov 2026 08:30:00 +0000
National · Issa Michuzi

WAZIRI MKUU AIPONGEZA WIZARA YA UCHUKUZI KWA UFANISI WA USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI, AITAKA KUONGEZA KASI KUELEKEA DIRA 2050

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ameipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa hatua zilizopigwa katika kuendeleza miundombinu na huduma za uchukuzi kupitia ushirikiano na sekta binafsi, huku akisisitiza kuongezwa kwa kasi, ufanisi na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 Dkt. Nchemba ametoa pongezi hizo Novemba 16, 2026, wakati akifungua Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza, akieleza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuongeza uwekezaji na kuboresha utoaji wa huduma za uchukuzi Amesisitiza kuwa pamoja na hatua zilizofikiwa, sekta hiyo inapaswa kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi, kuimarisha matengenezo ya miundombinu na usalama, pamoja na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto za upungufu wa fedha na ucheleweshaji wa miradi Akitoa salamu za Wizara, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema Serikali imeendelea kupiga hatua katika kuendeleza miundombinu ya reli, barabara, bandari na anga, sambamba na kuimarisha mifumo ya udhibiti na usimamizi wa sekta hiyo Amesema mkutano huo unaofanyika Novemba 16–18, 2026, wenye kaulimbiu ya “Kuharakisha Utoaji wa Huduma Jumuishi za Uchukuzi, Ufadhili Endelevu na Uwajibikaji wa Sekta kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050” ni jukwaa muhimu la kutathmini mafanikio, kubaini changamoto na kuweka mikakati ya kuongeza ufanisi wa sekta Awali, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Abubakar Assenga, ameipongeza Serikali kwa uwekezaji katika miundombinu ya uchukuzi na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa miradi ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi na taifa. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akionesha tuzo mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akimkabidhi tuzo Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na wadau mbalimbali wa Usafirishaji wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza. Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisoma hotuba pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) jijini Mwanza. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Abubakar Assenga akitoa salamu za Kamati ya Bunge wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 19 wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Uchukuzi (JTSR) Mkutano ukiendelea Picha za pamoja

Tue, 17 Nov 2026 14:16:48 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

TRA DODOMA YAANZA RASMI KAMPENI YA UKAGUZI WA BIDHAA NA KUTOA ELIMU KUHUSU STEMPU ZA KODI ZA KIELEKTRONIKI

Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Aubrey Silayo,akizungumza na waaandishi wa habari leo Novemba 17,2026 jijini Dodoma kuhusu matumizi ya mfumo wa Stempu za kodi za Kielektroniki kwenye vinywaji na bidhaa nyingine. Na.Mwandishi Wetu – DODOMA MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma imeanza rasmi kampeni ya ukaguzi wa bidhaa na kutoa elimu kwa umma kuhusu stempu za kodi za kielektroniki katika wilaya zote za Mkoa wa Dodoma. Kampeni hiyo inalenga kuhakikisha bidhaa zinazouzwa sokoni zinatumia stempu halali za kielektroniki, kudhibiti matumizi ya stempu bandia na bidhaa zisizolipiwa ushuru, pamoja na kuongeza uelewa kwa wafanyabiashara na wananchi kuhusu umuhimu wa kuhakiki stempu kabla ya kununua au kutumia bidhaa. Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 17, 2026 jijini Dodoma, Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Aubrey Silayo, amesema zoezi hilo litahusisha ukaguzi wa uhalali wa stempu zinazobandikwa kwenye bidhaa mbalimbali, zikiwemo vinywaji, bia, pombe kali, sigara na mvinyo, pamoja na kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi kuhusu umuhimu wa kuhakiki stempu kabla ya kununua au kutumia bidhaa. Silayo amesema matumizi ya stempu za kodi za kielektroniki ni sehemu ya jitihada za Serikali kuimarisha usimamizi wa kodi, kudhibiti bidhaa zisizo halali na kuhakikisha wafanyabiashara wote wanatekeleza wajibu wao wa kulipa ushuru kwa mujibu wa sheria. “Mfumo wa stempu za kodi ulianza kutumika nchini mwaka 1998, kabla ya Serikali kupitia TRA kuanzisha mfumo wa kisasa wa stempu za kielektroniki mwaka 2018, ambao umechukua nafasi ya stempu za karatasi zilizokuwa katika mazingira rahisi ya kughushiwa,” amesema Bw. Silayo. Ameeleza kuwa mfumo huo wa kidijitali unawezesha kila bidhaa kuwa na namba maalumu ya utambulisho pamoja na alama za kiusalama, zinazosaidia kutambua uhalali wa bidhaa na kutoa nafasi kwa watumiaji kufanya uhakiki kabla ya kuzitumia. Silayo amesema hatua hiyo siyo tu inalenga kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali, bali pia inalinda afya za wananchi dhidi ya bidhaa bandia au ambazo hazijathibitishwa ubora na usalama wake na mamlaka husika. “Wananchi wanaweza kutumia simu janja kupakua programu ya HAKIKI STEMPU, ambayo inawawezesha kuhakiki bidhaa wanazokusudia kununua au kutumia kwa kuchunguza uhalali wa stempu iliyobandikwa kwenye bidhaa husika,” amesisitiza. Ameongeza kuwa endapo mtumiaji atabaini bidhaa yenye stempu isiyothibitishwa au inayotia shaka, anaweza kutoa taarifa kupitia mfumo huo kwa kueleza eneo alilonunua bidhaa, aina ya bidhaa na kuambatanisha picha pamoja na taarifa nyingine zitakazosaidia TRA kufanya ufuatiliaji. Katika hatua nyingine, Silayo amewatahadharisha wafanyabiashara, watengenezaji na waagizaji wa bidhaa kuhakikisha wanatumia stempu sahihi za kielektroniki kabla ya kuingiza bidhaa sokoni, akisisitiza kuwa matumizi ya stempu bandia ni kosa linaloweza kuchukuliwa hatua za kisheria. Amesema TRA imeimarisha uwezo wa kubaini stempu za kughushi kwa kutumia mifumo ya kiintelijensia pamoja na skana maalumu, hivyo wahusika wanaojihusisha na udanganyifu huo watabainika na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria. Kwa mujibu wa Silayo, adhabu kwa watakaobainika kutumia vibaya stempu za kielektroniki ni faini isiyopungua Sh milioni tano na isiyozidi Sh milioni 50, au kifungo kisichozidi miaka mitatu, au adhabu zote mbili kwa pamoja. Amesisitiza kuwa jukumu la kuhakikisha bidhaa zinazotumika ni halali halipaswi kuachwa kwa TRA pekee, bali linahitaji ushirikiano wa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla, huku akiwataka kutoa ushirikiano kwa maafisa watakaotekeleza zoezi la ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo. Amesema matumizi sahihi ya stempu za kielektroniki yataimarisha ushindani wa haki katika biashara, kudhibiti ukwepaji wa kodi, kuongeza mapato ya Serikali na kulinda afya za wananchi. Hata hivyo, amewahimiza wananchi kujenga utamaduni wa kuhakiki stempu za kodi kabla ya kutumia bidhaa, akieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya uwajibikaji wa kila mmoja katika kulinda uchumi wa nchi na usalama wa jamii. HAKIKI STEMPU, TUMIA BIDHAA HALALI, LINDA AFYA YAKO! Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Aubrey Silayo,akizungumza na waaandishi wa habari leo Novemba 17,2026 jijini Dodoma kuhusu matumizi ya mfumo wa Stempu za kodi za Kielektroniki kwenye vinywaji na bidhaa nyingine.

Tue, 17 Nov 2026 14:19:27 +0000
National · Issa Michuzi

TANZANIA, IAEA NA EU KUIMARISHA USALAMA WA MIONZI KUPITIA MAFUNZO YA KIKANDA

NA MWANDISHI WETU - ARUSHA Serikali ya Tanzania imeendelea kuimarisha juhudi za kuhakikisha usalama wa mionzi kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu (IAEA) na Umoja wa Ulaya (EU), kupitia mafunzo ya kikanda yanayolenga kuwajengea uwezo wataalamu katika uandaaji wa viwango maalum vya usalama wa mionzi kwa vifaa vinavyokusudiwa kutumika tena, kuchakatwa au kutupwa. Mafunzo hayo ya siku tano, yanayofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 16 hadi 20 Novemba 2026, yanalenga kuimarisha uwezo wa nchi katika kufanya tathmini ya viwango vya mionzi kwenye vifaa mbalimbali ili kuhakikisha kuwa matumizi yake hayaleti madhara kwa afya za binadamu na mazingira. Akifungua mafunzo hayo leo, Novemba 16, 2026, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, Mkurugenzi Msaidizi wa Sayansi na Teknolojia, Dkt. Harun Makandi, amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa kitaalamu na mifumo ya udhibiti wa usalama wa mionzi, hususan katika kipindi ambacho matumizi ya teknolojia ya nyuklia na vyanzo vya mionzi yanaendelea kuongezeka katika sekta mbalimbali. Dkt. Makandi ameeleza kuwa uandaaji wa viwango maalum vya kuondoa vifaa kwenye udhibiti wa mionzi (Specific Clearance Levels) ni hatua muhimu inayowezesha kufanya maamuzi ya kitaalamu kuhusu vifaa vinavyoweza kutumika tena, kuchakatwa au kutupwa bila kuhatarisha usalama wa wananchi, wafanyakazi na mazingira. Katika mafunzo hayo, washiriki watajifunza masuala mbalimbali yakiwemo misingi ya ulinzi dhidi ya mionzi, taratibu za kuandaa viwango maalum vya usalama, tathmini ya athari zinazoweza kutokana na mionzi pamoja na matumizi ya mbinu za kitaalamu katika kufanya maamuzi kuhusu usimamizi wa vifaa vyenye mionzi. Aidha, mafunzo hayo yanatoa fursa kwa wataalamu kutoka nchi mbalimbali kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto na kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika kuhakikisha kuwa viwango vya usalama wa mionzi vinazingatiwa kwa mujibu wa miongozo na viwango vya kimataifa. Mafunzo hayo yanahusisha wataalamu kutoka Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu (IAEA), Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Nishati ya Nyuklia la Afrika Kusini (NECSA) pamoja na washiriki kutoka nchi mbalimbali, huku Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) ikiwa mwenyeji wa mafunzo hayo. Kupitia mafunzo hayo, Tanzania inaendelea kuimarisha nafasi yake katika usimamizi wa matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia na mionzi kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, sambamba na kulinda mazingira, wafanyakazi, wagonjwa na wananchi dhidi ya madhara ya mionzi.

Tue, 17 Nov 2026 14:20:37 +0000

Page 168 of 1130 · 22597 stories