Search the region
22339 stories
TANZANIA, CAF WASAINI MKATABA WA HAKI ZA MATANGAZO KUELEKEA AFCON 2027
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), wamesainiana Mkataba wa Haki za Matangazo kuelekea Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, yatakayofanyika kwa pamoja nchini Tanzania, Kenya na Uganda. Mkataba huo umesainiwa jijini Dar es Salaam leo Novemba 25, 2026 na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi. Thereza Mugobi, kwa niaba ya Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii na Katibu Mkuu wa CAF Samson Adamu aliyewakilisha shirikisho hilo. Akizungumza kabla ya utiaji saini wa mkataba huo, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amesema hatua hiyo ina manufaa makubwa kwa Sekta ya Utalii na mnyororo mzima wa thamani katika sekta hiyo kwani itachochea ukuaji na maendeleo yake. “Utiaji saini wa mkataba huu ni faida kwa Sekta ya Utalii na mnyororo wote wa thamani katika sekta hiyo,” amesema Dkt. Kijaji. Ameongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imejipanga kuhakikisha Tanzania inanufaika na ujio wa michuano hiyo, akieleza kuwa AFCON 2027 ni fursa ya kipekee ya kuitangaza nchi pamoja na vivutio vyake vya utalii ndani na nje ya Tanzania. Aidha, amesema hatua hiyo inaweka historia na kuendelea kudhihirisha uzalendo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa akitambua na kuendeleza sekta mbalimbali nchini, zikiwemo Sekta ya Utalii na Michezo. Amesisitiza kuwa uongozi imara wa Rais Samia Suluhu Hassan umechangia kuifungua Tanzania kwa fursa mbalimbali za kimataifa, hivyo anastahili pongezi kwa juhudi hizo.Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda (Mb), amesema kuwa ujio wa michuano ya AFCON 2027 nchini ni fursa muhimu ya kiuchumi, kwani utaleta wageni wengi, kuchochea shughuli mbalimbali za kiuchumi na kuongeza kipato kwa wananchi.
Wed, 25 Nov 2026 13:54:14 +0000EU plans €50 billion tech equity fund to boost quantum technology
Read the full report from the original source.
RecentlyUganda’s growth forecast adjusted downwards – UDB report
Uganda’s economic growth forecast for the 2026/27 financial year has been revised downwards to 6 – 6.5 per cent from an earlier projection of 7–7.5…
RecentlyDeath by a Thousand Integrations: How Seamless Tech Left Companies Open to Cyberattack
Read the full report from the original source.
RecentlyDes formations nocturnes d’Imbonerakure à Mukinya inquiètent les habitants
Read the full report from the original source.
RecentlyEquity posts strong financial growth
Equity Group Holdings Plc has reported a 32 per cent increase in profit after tax to approximately Shs 2.32 trillion for the nine months ended…
RecentlyKWS launches rhino audit at Ol Pejeta after 17 deaths
The audit will verify the conservancy’s rhino population and assess monitoring practices following the deaths recorded between February and November
RecentlyGood News For HIV-Positive People As Ugandan Study Shows Injectable Treatment Works Better Than Daily Pills For Adolescents
Read the full report from the original source.
RecentlyMediheal gets more time to pay Sh245m or lose Eldoret property
Read the full report from the original source.
RecentlyWorld News in Brief: Vaccine crisis in Yemen, aid for Ukraine, another UNRWA staffer killed
Read the full report from the original source.
RecentlyUkraine: Industrial attacks and anger at Russia among Ukraine's allies
Read the full report from the original source.
RecentlyWoman charged over alleged attempt to steal Ksh.173,000 phone in hospital
Read the full report from the original source.
RecentlyTanzanian, AFD sign Euro 175m loan deals for water, fisheries, dairy farming projects in Mwanza and Tanga
Read the full report from the original source.
RecentlySERIKALI YAITAKA NBAA KUIMARISHA HATUA ZA KINIDHAMU KWA WAHASIBU WANAOKIUKA MAADILI
NAIBU Waziri wa Fedha, Laurent Luswetula, ameitaka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kuimarisha usimamizi wa maadili na hatua za kinidhamu dhidi ya Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu wanaokiuka maadili ya taaluma na taratibu za uandaaji wa taarifa za fedha. Akifungua Kongamano la 39 la Mwaka la Wahasibu, Novemba 25, 2026, Bunju, Dar es Salaam, Luswetula amesema usimamizi madhubuti wa uadilifu katika Taaluma ya Uhasibu ni muhimu katika kupunguza upotevu wa mapato na matumizi mabaya ya fedha za umma. Amesema Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha taarifa za fedha zinaandaliwa kwa usahihi, uwazi na kuzingatia viwango na taratibu za kitaaluma, ili kuimarisha uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali za umma na binafsi. Ameitaka NBAA kuhakikisha kuwa madai ya ukiukaji wa maadili yanashughulikiwa kwa haraka na bila upendeleo, akisisitiza kuwa hatua za kinidhamu zinapaswa kuzingatia uchunguzi wa kina, ushahidi na haki ya mtuhumiwa kujitetea kabla ya uamuzi kufikiwa. Luswetula amesema hatua hizo zinapaswa kuendana na uzito wa kosa lililothibitika, ili kulinda heshima ya Taaluma ya Uhasibu na kuimarisha imani ya umma kwa wahasibu na wakaguzi wa hesabu. Amesisitiza kuwa kuimarisha maadili na uwajibikaji katika Taaluma hiyo kutachangia kuboresha usimamizi wa fedha, kuongeza uaminifu katika taarifa za kifedha na kusaidia juhudi za Serikali za kudhibiti upotevu wa mapato na matumizi yasiyo sahihi ya fedha za umma. Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) akikabidhiwa tuzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia S. Temu wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa 39 wa mwaka 2026 wa Wahasibu na Wakaguzi. Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) akikabidhi tuzo kwa Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius A. Maneno kwa utendaji wake katika Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa 39 wa mwaka 2026 wa Wahasibu na Wakaguzi. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia S. Temu. Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Mtaafu, CPA Pius A. Maneno akipongezwa mara baada ya kupokea Tuzo ya heshima Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) akikabidhi tuzo kwa CPA Eustace Osler Katagira kwa kutunukiwa Uanachama wa Heshima kama Heshima Maalumu ya Kutambua Mchango wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa 39 wa mwaka 2026 wa Wahasibu na Wakaguzi. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia S. Temu. Naibu NaibuWaziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa 39 wa mwaka 2026 wa Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kufanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia S. Temu akizungumza kuhusu mikakati mbalimbali ya kusimamia Taaluma ya Uhasibu na Ukaguzi wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2026. Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Prof. Siasa Mzenzi akisoma hotuba kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa 39 wa mwaka 2026 wa Wahasibu na Wakaguzi uliofanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Mtaafu, CPA Pius A. Maneno akitoa salamu katika mkutano mkuu wa 39 wa mwaka 2026 wa Wahasibu na Wakaguzi. Baadhi ya wa wahasibu na wakaguzi wa Hesabu wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi NaibuWaziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb) aliyemwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2026 wa Wahasibu na Wakaguzi Picha za pamoja
Wed, 25 Nov 2026 13:26:28 +0000Nigeria: Umukinnyi wa filime w'inararibonye Pete Edochie yapfuye ku myaka 79
Read the full report from the original source.
RecentlyNTSA announces four-hour system maintenance
Services will be unavailable from 8pm to midnight on Wednesday as the authority steps up festive-season road safety operations
RecentlyMinister Ogwang, Afcon is our meal, do not let it get lost in the mill
As much as this article is addressed to Peter Ograng, the state minister for sport, it is dedicated to Shadow Sports minister Zambali Bulasio Mukasa,…
RecentlyTANZANIA NA ALGERIA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA NISHATI –MHE. SALOME MAKAMBA
Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amesema Tanzania na Algeria zinaendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta ya nishati kwa lengo la kukuza uwekezaji, kubadilishana uzoefu na kutekeleza miradi yenye manufaa kwa mataifa hayo mawili. Akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya miaka 72 ya Mapinduzi ya Uhuru wa Algeria, iliyofanyika Novemba 24, 2026, jijini Dar es Salaam, Mhe. Salome amesema sekta ya nishati ni miongoni mwa maeneo muhimu ya ushirikiano kati ya nchi hizo, akibainisha kuwa Tanzania inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo. Ameeleza kuwa uwekezaji huo unalenga kupanua upatikanaji wa nishati ya uhakika na nafuu kwa wananchi, kuendeleza matumizi ya nishati jadidifu pamoja na kuongeza matumizi ya suluhisho za nishati safi ya kupikia. Aidha, amesema ushirikiano wa Tanzania na Algeria katika sekta ya nishati unaendana na vipaumbele vya maendeleo ya Taifa, hivyo kuna fursa za kuuimarisha zaidi kupitia kubadilishana uzoefu na uwekezaji wenye manufaa kwa pande zote mbili. Katika hafla hiyo, Mhe. Salome pia aliwasilisha salamu na pongezi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Rais wa Algeria, Mhe. Abdelmadjid Tebboune, Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria. Kupitia salamu hizo, Rais Samia amewaasa wananchi wa Algeria kuendelea kudumisha amani, umoja, ustawi na maendeleo, huku akisisitiza dhamira ya Tanzania ya kuimarisha urafiki na ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili. Katika hafla hiyo, Mhe. Salome ameeleza kuwa vita vya ukombozi wa Algeria, vilivyoanza Novemba 1954, vilikuwa chanzo muhimu cha hamasa kwa mataifa mengi ya Afrika katika mapambano dhidi ya ukoloni na kudai uhuru. Amesisitiza kuwa historia hiyo inaendelea kuwa kumbukumbu muhimu ya mshikamano wa Afrika na umuhimu wa kuendeleza mahusiano ya kindugu, ushirikiano na maendeleo baina ya mataifa ya Afrika.
Wed, 25 Nov 2026 13:22:16 +0000Tanzania, Nigeria join forces to advance women’s health across Africa
Read the full report from the original source.
RecentlySpotify Streams for Sale: 4 Sites Worth Knowing in 2026
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 2 of 1117 · 22339 stories