Search the region
22662 stories
Taifa Stars must rise to AFCON 2027 challenge
DAR ES SALAAM: TANZANIA’S ambition for the 2027 Africa Cup of Nations (AFCON) must go beyond hosting the tournament. The…
RecentlyFINLAND KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA KATIKA TEKNOLOJIA
Na. Peter Haule, WF, Dar es Salaam Finland imeeleza nia ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Tanzania kwa kuongeza uwekezaji na shughuli za maendeleo katika sekta za teknolojia ya kidijitali, mawasiliano, misitu na madini. Hayo yamebainishwa na Balozi wa Finland nchini, Mhe. Anna Merrifield wakati wa Mkutano na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, uliofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam. Mhe. Balozi Merrifield amesema nia ya nchi yake ni kuongeza ushirikiano kutoka katika mfumo wa kawaida wa ushirikiano wa maendeleo na kuelekea katika ushirikiano zaidi unaohusisha pia sekta binafsi, uwekezaji na matumizi ya teknolojia katika kukuza uchumi. “Finland ina uzoefu mkubwa katika sekta ya teknolojia na ubunifu, hususan katika maeneo ya huduma za kidijitali na mawasiliano, ambayo yanaweza kusaidia Tanzania kufikia malengo yake ya maendeleo”, alisema Mhe. Balozi Merrifield. Amebainisha kuwa teknolojia ya kidijitali na mawasiliano ni muhimu katika kufanikisha azma ya Tanzania ya kujenga uchumi wa dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050, akisisitiza kuwa maendeleo hayo hayawezi kufikiwa bila matumizi ya teknolojia katika sekta mbalimbali za uchumi. Kuhusu ushirikiano na sekta binafsi, amesema Finland inataka kuimarisha uhusiano kati ya miradi ya maendeleo na uwekezaji wa kampuni binafsi, ili kutumia utaalamu wa kampuni za Finland kutatua changamoto za maendeleo nchini Tanzania. Amesema mkazo utawekwa katika miradi yenye manufaa ya kijamii na kiuchumi ambayo huenda isiweze kujiendesha kibiashara kwa faida ya moja kwa moja, lakini inaweza kuleta matokeo chanya kwa wananchi na kusaidia maendeleo ya Tanzania. Ameongeza kuwa miradi hiyo inapaswa kuzingatia mahitaji na vipaumbele vya maendeleo vya Tanzania, huku ikitumia utaalamu na uwezo wa kampuni za Finland kwa manufaa ya pande zote mbili. Akizungumza awali Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba, amesema anafurahishwa na mfumo mpya wa ushirikiano wa uwekezaji katika sekta ya umma (Public Sector Investment Framework – PIF), unaowezesha Tanzania kupata mikopo yenye masharti nafuu inayofadhiliwa kwa ruzuku na Serikali ya Finland kwa ajili ya kutekeleza miradi iliyokubaliwa. Amefafanua kuwa mfumo huo unalenga kusaidia miradi ya umma yenye manufaa makubwa ya kiuchumi, kijamii na kimazingira, ambayo inaweza kukabiliwa na changamoto za upatikanaji wa fedha kupitia mifumo ya kawaida ya kibiashara. Akizungumzia utekelezaji wa mfumo huo, alisema mradi wa awali unaotarajiwa kutekelezwa ni Awamu ya Tano ya upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB), utakaotekelezwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), kwa kushirikiana na kampuni ya Nokia ya Finland. Amesisitiza kuwa Wizara ya Fedha itaendelea kufuatilia kwa karibu maandalizi ya mradi huo ili kuhakikisha hatua zinazohitajika zinakamilishwa kwa wakati, akibainisha kuwa nyaraka za mradi huo zinafanyiwa mapitio na Tume ya Taifa ya Mipango. Dkt. Mwamba ameipongeza Serikali ya Finland kwa ushirikiano wake na kumshukuru Balozi mstaafu wa Finland nchini Tanzania, Theresa Zitting, kwa mchango wake katika kuimarisha mahusiano ya nchi hizo, hususan katika kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miradi ya kimkakati. Mkutano huo ulihudhuliwa pia na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha na Ushirikiano na Sekta Binafsi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland, Bi. Emmi Oikari, Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Nokia, Bw. Amouneu Lopy na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Melckizedeck Mbise. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba akiongoza mkutano kati yake na Balozi wa Finland nchini, Mhe. Anna Merrifield, uliofanyika katika Ofisi ya Katibu Mkuu, Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba, akiagana na Balozi wa Finland nchini, Mhe. Anna Merrifield, baada ya Mkutano wao kuhusu ushirikiano wa maendeleo, uliofanyika katika Ofisi ya Katibu Mkuu, Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba, Balozi wa Finland nchini, Mhe. Anna Merrifield (wa nne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha na Finland, baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao, uliofanyika katika Ofisi ya Katibu Mkuu, Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Dar es Salaam)
Fri, 13 Nov 2026 07:29:28 +0000Christiano Ronaldo agiye kwerekeza muri Turkiya
Read the full report from the original source.
RecentlyAVEVA named finalist in Microsoft’s 2026 sustainability awards
Latest · Technology
RecentlyPCCB intervention lifts hospital revenue to 35m/-
SIMIYU: MONTHLY revenue at Itilima District Hospital has surged from 500,000/- to 35m/- following efforts by the Prevention and Combating…
RecentlyIndia news: Sonam Wangchuk says he is under house arrest in Ladakh
Read the full report from the original source.
RecentlyFDLR we! Rekura abantu bacu waheranye muri Congo, turabashaka ari bataraga
Read the full report from the original source.
RecentlyState secures 293,600 jobs for Kenyans in Saudi Arabia
The jobs cut across healthcare, construction, hospitality, education, transport, manufacturing, finance, oil and gas, and domestic work.
RecentlyBMH nurses urged to embrace innovation to improve patient care
DODOMA: NURSES have been urged to embrace innovative approaches, strengthen communication and promote teamwork to improve patient care and reduce…
RecentlyBedroom slaughter: Night killers crept in, broke through window and killed college principal
Gerishom Wafula Manases brutal death is either being linked to marital problems, a love triangle, a land deal gone sour or work-related disagreements.
Fri, 13 Nov 2026 10:20:00 +0300From Shs119 Billion To Shs982 Billion! The Shocking State House Budget Explosion
Read the full report from the original source.
RecentlyTrade for Jobs Uganda Partners with Sweden’s DeLaval to Advance Dairy Productivity and Competitiveness
Read the full report from the original source.
RecentlyPresident Museveni challenges African Content Creators to Champion Five Historical Missions for Africa’s Transformation
Read the full report from the original source.
RecentlyMbazira Challenges Judiciary to Drive Uganda’s Constitutional Transformation Through Judicial Power
Read the full report from the original source.
RecentlyIringa mourns 23 victims of deadly road crash
IRINGA: GRIEF has engulfed Kiponzelo Division in Iringa Region following a devastating road accident that claimed 23 lives, with the…
RecentlyAs banks in Tanzania grow richer, are customers getting a fair deal?
Read the full report from the original source.
RecentlyMicrosoft says attempts to fix global outage not going 'as expected'
Microsoft says the outage is not caused by a cyber-security incident.
RecentlyPM calls for sustainable education financing
Read the full report from the original source.
RecentlyTanzania’s banks grow richer, but are customers getting a fair deal?
Read the full report from the original source.
RecentlyTZ leads clean cooking drive
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 200 of 1134 · 22662 stories