Search the region
22720 stories
Banki Nkuru y'u Rwanda izaniye umwihariko abana b'abakobwa
Read the full report from the original source.
RecentlyJab by jab, house by house, Nigeria slowly rolls out malaria vaccine
Read the full report from the original source.
RecentlyOPM renews Five-Year Partnership with GiveDirectly to support Vulnerable Communities
Read the full report from the original source.
RecentlySifuna more popular than Gachagua among Mt Kenya, DCP supporters – TIFA poll
Latest · Politics
RecentlyDKT. MWIGULU AHIMIZA MAANDALIZI YA ELIMU 2028
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wadau wa elimu wajadili namna ya kuimarisha upatikanaji wa mapato ya ndani ambayo yataboresha uwezo wa nchi kutekeleza vipaumbele vya kitaifa. Amesema kwenye suala la elimu, upatikanaji wa fedha unapaswa kuwa endelevu na unaoambatana na mipango ya uhakika, utoaji wa fedha kwa wakati, manunuzi sahihi, uwazi kwenye matumizi ya fedha na matokeo yanayoweza kupimika Ametoa wito huo leo (Alhamisi, Novemba 12, 2026) wakati akifungua Mkutano wa Sita wa Kimataifa wa Ubora wa Elimu katika ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu amesema katika kupanga matumizi ya fedha zinazopelekwa kwenye sekta ya elimu, hawapaswi kuangalia tu mgao wa fedha hizo, bali wahoji endapo zinafika kwenye shule zilikopangiwa na zinatumiwa na wanafunzi wanaozihitaji zaidi. “Lazima tuimarishe utekelezaji wa bajeti zinazopelekwa, tupunguze uzembe, tuboreshe uratibu baina ya taasisi za kitaifa na za kwenye maeneo yetu na tutumie takwimu za kuaminika katika kufanya maamuzi. Kila shilingi iliyowekezwa kwenye elimu inapaswa kuchangia ufundishaji bora, matokeo bora na fursa za sawa,” amesema. Amesema wanajadili suala upatikanaji wa fedha na ubora wa elimu, maamuzi yatakayofikiwa yanapaswa kuzingatia usawa na ujumuishi kwa wanafunzi. “Rasilimali zitakazopatikana zinapaswa kujibu mahitaji ya wanafunzi wa kike, wanafunzi wenye mahitaji maalum ya elimu, watoto walioathiriwa na umaskini, wale walio katika jamii ambazo hazijahudumiwa na wanafunzi wote wanaokabiliwa na vizuizi vya kielimu.” “Hakuna mtoto anapaswa kuachwa kwenye mfumo wa elimu yetu kwa sababu ya mahali anapoishi au mazingira yanayomzunguka. Tunapaswa tuhakikishe kuwa shule ziko salama, zinafikika na zina mazingira ambayo kila mwanafunzi anaweza kushiriki.” Akielezea kuhusu maandalizi ya mfumo wa kupokea makundi mawili ya wahitimu ifikapo mwaka 2028 kutokana na mabadiliko ya mfumo wa elimu kupitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023, pamoja na mitaala iliyoboreshwa, Waziri Mkuu amesema kipindi hiki cha mpito kinahitaji maandalizi yaliyoratibiwa baina ya taasisi za Serikali na wadau wa elimu. Waziri Mkuu amesema lengo la mabadiliko hayo ni kuongeza elimu ya lazima, kuimarisha ujuzi wa vitendo na kuwawezesha wanafunzi kuingia kwenye ajira au kujiajiri. “Hakuna wizara moja, taasisi, au shule inayoweza kusimamia mahitaji kama haya peke yake. Lazima tupange kwa pamoja, tutarajie kutakuwa na ongezeko la mahitaji ya walimu, madarasa, vifaa vya kujifunzia, fedha na tuhakikishe utekelezaji unalenga mahitaji ya wanafunzi,” amesisitiza. Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda alisema mkutano huo unafanyika katika wakati sahihi ambapo Serikali inasimamia mageuzi katika sekta ya elimu, mageuzi ambayo yana kalenda ya ukalimishaji na tayari safari imeshaanza. “Mageuzi haya yanalenga kuongeza ujuzi katika elimu ili isiwe ya mafundisho tu ya kinadharia bali impe mwanafunzi uwezo wa kujiajiri. Hapa tuna mkondo wa elimu ya amali na mkondo wa elimu jumla,” alisema. Akielezea mabadiliko hayo, Prof. Mkenda alisema elimu ya sasa itatoka miaka saba hadi 10 na itakuwa ni ya lazima kwa kila mtoto wa Kitanzania. Watoto lazima wasome hadi kidato cha nne, wazazi lazima wawasimamie watoto. Kwa hiyo, elimu ya msingi itakuwa ya miaka sita, na baada ya hapo inabidi waende kidato cha kwanza,” alisema. Alisema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alishawapa Wakuu wote wa Mikoa kipimo cha utekelezaji wa agizo lake kuhusiana na maandalizi ya kuanza kwa mfumo huo mpya na kwamba hivi sasa nguvu kubwa inapaswa ielekezwe kwenye suala hilo. “Kalenda ya utekelezaji imeshatoka na ifikapo Januari, 2028 tutakuwa na wahitimu wa darasa la sita na darasa la saba ambao wote kwa pamoja wataingia kidato cha kwanza. Katika hili hakuna kufeli wala hakuna kurudi nyuma,” alisisitiza. Alitumia fursa hiyo kuwaalika wadau wa elimu nchini waangalie fursa zilizopo na wapi wanaweza kusaidiana na serikali kufanikisha lengo hilo. “Tunaalika wadau kwa sababu bado tunahitaji shule zaidi. Tunahitaji taasisi za dini na sekta binafsi zituunge mkono.”
Thu, 12 Nov 2026 12:53:44 +0000Pavage des routes dans les quartiers urbains : le premier ministre encourage les autorités administratives à sensibiliser la population
Read the full report from the original source.
RecentlyLe pari perdu de Kigali : comment l’aventure congolaise de Kagame précipite le Rwanda dans la crise économique et l’isolement diplomatique
Longtemps présenté comme le « chouchou » des bailleurs occidentaux, le Rwanda de Paul Kagame traverse aujourd’hui la tempête la plus violente de son histoire post-génocide. Sanctions américaines, gel de l’aide britannique, dette asphyxiante et jeunesse sacrifiée sur les collines du Kivu...
Thu, 12 Nov 2026 12:48:28 +0000New York: Brooklyn building collapse death toll climbs to 8
Read the full report from the original source.
RecentlyNgo nde...Muhozi, Perezida? Turabyanze - impaka zavutse i Bugande
Read the full report from the original source.
RecentlyTanzania’s food security needs more than chemical-based agricultural solutions
MBEYA: Farmers often associate good harvests with improved seeds and fertilisers. But what happens when traditional seeds disappear and the…
RecentlyKAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA WAMI/RUVU KWA UHIFADHI WA MAZINGIRA NA UFUATILIAJI WA RASILIMALI ZA MAJI
Katika kuimarisha usimamizi na uhifadhi wa rasilimali za maji nchini, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeendelea na ziara ya kutembelea na kukagua vituo vya ufuatiliaji wa mwenendo wa maji katika mito vinavyosimamiwa na Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu. Katika ziara hiyo, wajumbe wa Kamati wametembelea kituo cha kupima hali ya wingi wa maji katika Mto Ruvu, kilichopo eneo la Ruvu Kibungo, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, ambapo wamepata maelezo kuhusu namna kituo hicho kinavyofanya kazi katika kukusanya na kutoa takwimu za mwenendo wa maji mtoni. Vituo hivyo vina umuhimu mkubwa katika usimamizi wa rasilimali za maji kwani huwezesha Bodi kupata takwimu sahihi na za uhakika kuhusu kiasi cha maji kinachopita katika mito kwa nyakati tofauti. Taarifa hizo hutumika katika kupanga na kusimamia matumizi ya maji, kufanya maamuzi sahihi kuhusu ugawaji wa rasilimali hiyo, kutambua mabadiliko ya mwenendo wa maji pamoja na kutoa tahadhari mapema dhidi ya vihatarishi vinavyoweza kusababisha mafuriko au upungufu wa maji. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Patrick Mwalunenge (Mb), ameipongeza Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa juhudi zinazofanyika katika kusimamia na kuhifadhi mazingira, akieleza kuwa hatua hizo ni muhimu katika kulinda vyanzo vya maji na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa rasilimali hiyo kwa matumizi ya sasa na vizazi vijavyo. Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa Kamati hiyo kukagua utekelezaji wa miradi na shughuli mbalimbali za usimamizi, uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za maji zinazotekelezwa na Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu.
Thu, 12 Nov 2026 12:47:05 +0000BUNIFU ZA KISAYANSI KULENGA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv TAFITI na bunifu za kisayansi zinazolenga kutatua changamoto za wananchi zinatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya maadhimisho ya miaka 40 ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), yatakayofikia kilele Novemba 18, 2026, jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa bunifu zilizooneshwa ni mkanda maalumu wa kusaidia kudhibiti upotevu wa damu kwa mama baada ya kujifungua, chanjo ya samaki inayolenga kukabiliana na magonjwa yanayoathiri ufugaji wa samaki pamoja na teknolojia ya kuzalisha gesi kwa kutenganisha hidrojeni na oksijeni kutoka kwenye maji. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema bunifu hizo ni sehemu ya mchango wa sayansi, teknolojia na utafiti katika kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi. mesema maonesho ya tafiti, teknolojia na bunifu yatafanyika Novemba 17 na 18 katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, huku kilele cha maadhimisho hayo kikitarajiwa kufungwa na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, Novemba 18. Kuhusu ubunifu wa kuzalisha gesi kwa kutenganisha hidrojeni na oksijeni kutoka kwenye maji, Prof. Mkenda amesema ameagiza wataalamu kuchunguza usalama wa teknolojia hiyo pamoja na uwezekano wa kuitumia kiuchumi na kibiashara. Katika eneo la afya, amesisitiza umuhimu wa vyuo vikuu na taasisi za utafiti kufanya uchunguzi wa kisayansi kuhusu mimea inayotumika kutibu magonjwa, ili kubaini ufanisi wake, kiwango sahihi cha matumizi na madhara yanayoweza kujitokeza. Amesema pia ni muhimu kuimarisha uwezo wa kufanya majaribio ya awali ya dawa nchini kabla ya kufikia hatua ya kuzijaribu kwa binadamu, hatua itakayoongeza nafasi ya watafiti wa Tanzania kushiriki katika maendeleo ya tiba. Prof. Mkenda ameeleza kuwa maadhimisho hayo pia ni fursa ya kutathmini mchango wa COSTECH katika maendeleo ya nchi na kuweka msukumo mpya wa matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Amebainisha kuwa matumizi ya teknolojia na tafiti yanapaswa kuimarishwa katika sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi na uchimbaji wa madini ili kuongeza tija na kuwezesha rasilimali za nchi kutumika kwa manufaa ya wananchi. Amesema katika kilimo, tafiti zinapaswa kuelekezwa katika kuongeza uzalishaji katika eneo linalolimwa, kupunguza umaskini wa wakulima na kuchangia upatikanaji wa chakula kwa gharama nafuu. Aidha, amezitaja jitihada za ufadhili wa masomo kupitia Samia Scholarship, utoaji wa tuzo kwa watafiti na Mfuko wa Samia wa Ubunifu kuwa miongoni mwa hatua zinazolenga kuendeleza wataalamu na kuwawezesha wabunifu nchini. Ameeleza kuwa kabla ya kufikia kilele hicho, shughuli mbalimbali zimefanyika zikiwemo kliniki ya ubunifu wakati wa maonesho ya Nanenane, maonesho katika viunga vya Bunge na mikutano ya wadau wa sayansi na utafiti. Amewakaribisha wananchi, waandishi wa habari na wadau mbalimbali kutembelea maonesho hayo ili kujionea tafiti, teknolojia na bunifu zinazolenga kuchangia maendeleo ya Tanzania.
Thu, 12 Nov 2026 12:47:36 +0000Airtel Yafanya Ziara Maalum kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi
Dodoma, Novemba 10, 2026 KAMPUNI ya Airtel Tanzania imesema itaendelea kuimarisha mifumo ya ulinzi wa taarifa binafsi za wateja wake ili kuendelea kutoa huduma bora na kuhakikisha usalama wa huduma zake za kidijitali. Dhamira hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto, wakati wa ziara ya heshima katika Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), ambapo alikutana na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Dkt. Emmanuel Lameck Mkilia, pamoja na viongozi wengine. Katika ziara hiyo, Kamoto aliishukuru Tume kwa mwongozo na ushirikiano iliowapatia katika kuendana na mfumo wa ulinzi wa taarifa binafsi, akieleza kuwa mafunzo na miongozo yaliyotolewa kwa wafanyakazi wa Airtel yamekuwa muhimu katika kuongeza uelewa wa namna sahihi ya kuchakata, kuhifadhi na kushughulikia taarifa za wateja. Alisema ulinzi wa taarifa binafsi haupaswi kuonekana kama suala la kutimiza matakwa ya kisheria pekee, bali ni sehemu muhimu ya uendeshaji wa biashara na kujenga uhusiano wa muda mrefu na wateja. “Kwa Airtel Tanzania, kulinda taarifa binafsi si wajibu wa kutimiza matakwa ya kisheria pekee, bali ni jukumu la msingi na sehemu muhimu ya namna tunavyoendesha biashara yetu. Kulinda taarifa za wateja ni muhimu katika kujenga na kudumisha imani pamoja na mahusiano ya muda mrefu,” alisema Kamoto. Aliongeza kuwa kampuni hiyo inaendelea kuwekeza katika mafunzo na programu za uhamasishaji kwa wafanyakazi, pamoja na kuweka sera na mifumo ya ndani inayolenga kuhakikisha kuwa ulinzi wa taarifa binafsi unazingatiwa katika shughuli zake za kila siku. Kamoto alisema hatua hizo ni muhimu zaidi wakati kampuni ikiendelea kupanua huduma zake za kidijitali na mipango ya ujumuishaji wa huduma za kifedha, hali inayoongeza umuhimu wa kutunza vyema taarifa za wateja ipasavyo. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Dkt. Emmanuel Lameck Mkilia, aliipongeza Airtel Tanzania kwa kutembelea ofisi za Tume na kutambua umuhimu wa ushirikiano kati ya Tume na sekta binafsi. Alisisitiza pia umuhimu wa makampuni mbalimbali kuelewa dhamira ya Tume, hususan katika kuhakikisha kuwa biashara zinaweka mifumo imara ya kulinda na kuhifadhi taarifa binafsi za wateja wao. “Naipongeza Airtel Tanzania kwa utayari wake wa kushirikiana na Tume katika kuunga mkono utekelezaji wa malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hususan katika kuendeleza safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kidijitali na kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wananufaika na fursa za kidijitali,” alisema Dkt. Mkilia. Airtel Tanzania inathamini ushirikiano wake na Tume na inaendelea kujizatiti kuimarisha uhusiano huo katika kukuza usimamizi na utunzaji sahihi wa taarifa binafsi kwa lengo la kukuza na kujenga mazingira salama ya kidijitali nchini.
Thu, 12 Nov 2026 12:50:28 +0000La commune Bukinanyana plaide pour l’accès à l’eau potable, au profit des zones Buganda et Ndava
Read the full report from the original source.
RecentlyMarché de Mukenke : des toilettes fermées, un risque sanitaire croissant
Read the full report from the original source.
RecentlyDore umuganga ushinjwa gutoranya abarwayi bagombaga kwicwa muri Jenoside
Read the full report from the original source.
RecentlyKenyan scholars, political leaders weigh lessons from China’s governance model
Read the full report from the original source.
RecentlyBishops to MPs: Don't tamper with laws ahead of 2027 polls
They want Parliament to reject divisive proposals and urge IEBC to strengthen election preparedness ahead of the 2027 General Election.
RecentlyTanzania awards EDTCO a tender to construct 92.3km, 33kv power project from Mtwara to Tandahimba
MTWARA: THE Tanzanian government has awarded a tender to Electrical Transmission and, Distribution Construction Maintenance Company (EDTCO), to build a…
RecentlyPM calls for increased investment in education to drive innovation
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 218 of 1136 · 22720 stories