Unganishwa

Search the region

22775 stories

Science · UBC

UN chief urges world leaders to tackle fossil fuels at COP31

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Acquitted 'China spy' tells BBC: I was fall guy for security services but also naive

The former researcher, has shared more than 6,000 messages with us revealing how a Chinese official sought information on sensitive poilitical matters in the UK

Recently
National · Issa Michuzi

TANZANIA YATAJWA MIONGONI MWA NCHI ZILIZOFUNGA MILANGO YA MAHAKAMA YA AFRIKA KWA WANANCHI

Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Arusha TANZANIA imetajwa kuwa miongoni mwa nchi nne za Afrika zilizoondoa utaratibu uliokuwa ukiwaruhusu wananchi wake kufikisha mashauri moja kwa moja katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR), hali inayotajwa kuwa miongoni mwa changamoto zinazoathiri upatikanaji wa haki kupitia taasisi hiyo inayotimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake. Wakili Bahame Tom Nyanduga kutoka Dar es Salaam, Tanzania, amesema hatua hiyo pamoja na changamoto za upungufu wa rasilimali watu na fedha ni miongoni mwa vikwazo vinavyoweza kudhoofisha uwezo wa mahakama hiyo kutekeleza majukumu yake ya kulinda haki za binadamu barani Afrika. Akizungumza katika kongamano la maadhimisho ya miaka 20 ya mahakama hiyo lililofanyika Arusha, Nyanduga amesema licha ya taasisi hiyo kufanikiwa kuwepo kwa kipindi hicho, bado inahitaji ushirikiano wa dhati kutoka kwa nchi wanachama ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Amesema katika kipindi cha miaka mitano hadi kumi ya mwanzo wa uendeshaji wa mahakama hiyo, kati ya nchi 34 zilizokuwa zimeridhia mkataba wake, ni nchi 10 pekee zilizokuwa zimekubali wananchi wake kuwasilisha mashauri moja kwa moja mahakamani hapo. Ameeleza kuwa hali hiyo ilikuwa changamoto kubwa ikizingatiwa kuwa bara la Afrika lina nchi 55, hivyo ushiriki mdogo wa nchi wanachama katika kuruhusu wananchi kutumia mahakama hiyo uliathiri wigo wa upatikanaji wa haki. Nyanduga amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi nne zilizoondoa tamko maalumu lililokuwa likiruhusu wananchi na taasisi zisizo za kiserikali kuwasilisha mashauri moja kwa moja mahakamani hapo, huku nyingine zikiwa ni Rwanda, Tunisia na Ivory Coast. Amesema msingi wa kuanzishwa kwa mahakama hiyo ulikuwa ni kuhakikisha wananchi wa Afrika wanapata fursa ya kutafuta haki katika ngazi ya bara pale wanaposhindwa kupata suluhisho kupitia mifumo ya mahakama za ndani ya nchi zao. Hata hivyo, pamoja na changamoto hizo, Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu imeendelea kupata mafanikio katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006, ikiwa ni pamoja na kupokea zaidi ya mashauri 350 yaliyohusu ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi mbalimbali za Afrika. Akizungumza katika kongamano hilo, Rais mstaafu wa mahakama hiyo, Jaji Imani Aboud, amesema taasisi hiyo imepiga hatua kubwa katika kipindi hicho, hususan katika kupokea na kushughulikia mashauri yanayohusu ukiukwaji wa haki za msingi za wananchi. Jaji Aboud amesema kati ya mashauri zaidi ya 350 yaliyowasilishwa mahakamani hapo, takribani 200 tayari yamefanyiwa maamuzi, huku mengine yakiendelea kushughulikiwa, hatua inayoonesha mchango wa taasisi hiyo katika kuimarisha mifumo ya haki barani Afrika. Amesema mahakama hiyo ilipoanza kazi ilikuwa na nchi 12 zilizokuwa zimekubali kutambua mamlaka yake kupitia matamko maalumu yaliyowezesha wananchi kupata haki moja kwa moja katika mahakama hiyo. Ameongeza kuwa licha ya baadhi ya nchi kuondoa matamko hayo, mahakama inaendelea kutekeleza wajibu wake kwa kupokea mashauri yanayowasilishwa kwa mujibu wa taratibu na mamlaka iliyowekwa kisheria. Kwa upande wake, Msajili wa mahakama hiyo, Dkt. Robert Eno, amesema taasisi hiyo imepata mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka 20, licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa watumishi. Dkt. Eno amesema tathmini ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa mwaka 2021 hadi 2025 imeonesha ongezeko la asilimia 27 la mashauri yaliyokamilishwa, jambo linaloonesha kuimarika kwa uwezo wa mahakama katika kushughulikia mashauri yanayofikishwa mbele yake. Amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano kati ya majaji, watumishi wa Ofisi ya Usajili, nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, asasi za kiraia, taasisi za kitaaluma na washirika wa maendeleo. Ameeleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2026 hadi 2030, mahakama hiyo imejipanga kuongeza upatikanaji wa haki, kuimarisha matumizi ya teknolojia, kujenga uwezo wa kitaasisi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na wadau wa sekta ya sheria. Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano hilo, Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Blaise Tchikaya, amesema ana imani na mustakabali wa taasisi hiyo, akieleza kuwa uwezo wa Afrika kuweka na kutekeleza malengo yake ni msingi muhimu wa kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu katika bara hilo. Jaji Tchikaya amesema anaamini mahakama hiyo itaendelea kufanya kazi kwa mafanikio katika miaka 40 ijayo na kufikisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006. Amesema kongamano hilo si maadhimisho ya kawaida pekee, bali ni fursa kwa majaji, wataalamu wa sheria, viongozi wa taasisi na wadau mbalimbali kutathmini mafanikio yaliyopatikana, kujadili changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu na watu barani Afrika.

Wed, 11 Nov 2026 13:08:17 +0000
Uncategorized · BBC Afrique

Claude Shannon, le brillant mathématicien qui a inventé l'ère numérique (et qui s'est ensuite retiré dans sa « salle de jeux »)

Vos empreintes digitales se trouvent sur tous les appareils électroniques que nous possédons, sur tous les écrans d'ordinateur que nous regardons, sur tous les supports numériques.

Recently
Uncategorized · Jamhuri Media

Makamu wa Rais aagiza kubadilishwa kwa meneja wa mradi wa umeme Songea – Tunduru- Masasi- Mahumbika

Read the full report from the original source.

Recently
Sports · Issa Michuzi

Morocco Vs Niger: Moto wa Kufuzu Afcon Wawaka!

MASHABIKI wa soka wanatarajia kushuhudia burudani nyingine ya kimataifa wakati Morocco itakapokutana na Niger katika mchezo wa Kundi A wa kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Ni pambano linalobeba ushindani, presha na umuhimu wa kila pointi katika safari ya kuelekea hatua inayofuata ya mashindano hayo. Morocco itaingia uwanjani ikiwa na dhamira ya kutumia vyema faida ya kucheza mbele ya mashabiki wake na kuonyesha ubora wake wa soka. Kikosi hicho kinahitaji nidhamu, kasi ya mashambulizi na umakini katika kutumia nafasi za kufunga ili kupata matokeo yatakayokiweka katika nafasi nzuri kwenye kundi hilo. Kwa upande wa Niger, mchezo huo ni nafasi muhimu ya kujaribu kuzuia kasi ya Morocco na kutafuta matokeo chanya ugenini. Niger italazimika kuwa makini katika safu ya ulinzi, kutumia vizuri mashambulizi ya kushtukiza na kupambana katika kila eneo la uwanja ili kuifanya Morocco ipate wakati mgumu. Kuelekea mchezo huo, Morocco inaingia ikiwa kileleni mwa Kundi A ikiwa na pointi sita baada ya kushinda michezo yake miwili ya awali dhidi ya Gabon na Lesotho. Kikosi cha kocha Mohamed Ouahbi pia kimeimarishwa na kurejea kwa mshambuliaji Youssef En-Nesyri pamoja na kuitwa kwa mara ya kwanza kwa winga Ayoub Oufkir. Kwa habari na taarifa mbalimbali za michezo usisite kutembelea meridianbet ili upate mambo yote yanayotokea na kuendelea kwenye ulimwengu wakimichezo, ikiwemo michuano mikubwa ya Africa, Ulaya na ile ya falme za kiaarabu zote zinapatikana hapa. Kwa hiyo, macho yataelekezwa kwa nyota wa Morocco kama Achraf Hakimi, Brahim Diaz na Youssef En-Nesyri, ambao wanaweza kuwa sehemu muhimu ya mipango ya ushambuliaji. Hata hivyo, Niger haitakiwi kudharauliwa kwani nayo inahitaji matokeo yatakayoipa nafasi ya kuendelea kushindana katika kundi hilo. Ni mchezo unaoahidi ushindani na burudani ya soka la kimataifa, huku kila timu ikiwa na sababu ya kupigania ushindi. Je, Morocco itaendeleza rekodi yake nzuri na kuimarisha uongozi wa Kundi A, au Niger itaibuka na matokeo yatakayozua mjadala? Usikose kufuatilia kila dakika ya pambano hili!

Wed, 11 Nov 2026 04:00:00 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

DKT. MWIGULU AAGIZA MAPITIO YA GHARAMA ZA PEMBEJEO

▪️ Awataka mawaziri watatu kupitia muundo wa tozo ▪️ Aagiza usanifu wa barabara Ushetu uharakishwe ili kuwahi bajeti ▪️ Aitaka TANESCO kuunganisha umeme vijijini kwa sh. 27,000 WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewaelekeza mawaziri wenye dhamana ya TAMISEMI, Fedha na Kilimo kupitia upya muundo wa tozo zinazohusiana na pembejeo, baada ya kuelezwa kuwa gharama za mikopo zinapunguza mapato ya wakulima wa tumbaku. Amesema mapitio hayo yafanyike kwa kuangalia tozo moja baada ya nyingine ili kupata ufumbuzi wa mzigo unaowakabili wakulima. Dkt. Mwigulu ametoa maelekezo hayo leo (Jumatano, Novemba 11, 2026), akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Stendi ya Nyamilangano, Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, mkoani Shinyanga. “Niwaelekeze Waziri wa TAMISEMI, Waziri wa Fedha, pamoja na Waziri wa Kilimo, wakae waangalie upya huu muundo wa hizi tozo,” amesema. Maelekezo hayo yamefuatia hoja ya Mbunge wa Ushetu, Emmanuel Peter Cherehani, aliyelalamikia gharama za mikopo katika mfumo wa upatikanaji wa pembejeo za tumbaku. Cherehani amesema msambazaji anapokopa kununua pembejeo anatozwa riba, na chama cha msingi kinapokopa kumlipa msambazaji nacho kinatozwa riba, huku mzigo huo ukimwathiri mkulima. Waziri Mkuu amesema atakaa na mawaziri hao pamoja na wabunge wa maeneo yanayoathiriwa na changamoto hiyo ili kupata ufumbuzi. Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu amemwelekeza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga, Ntuli Mwaikokesye, kuharakisha usanifu wa kina wa barabara iliyotajwa na Mbunge wa Ushetu, ili ukamilike kabla ya maandalizi ya bajeti mpya. Mwaikokesye alipoeleza kuwa usanifu unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi minne, Waziri Mkuu amemtaka kupunguza muda huo ili mradi uwe tayari kuzingatiwa Serikali itakapoanza kupokea miradi mipya ya barabara. “Fanyeni kazi usiku na mchana, tumalize hiyo detailed design,” amesema. Kuhusu umeme, Waziri Mkuu ameielekeza TANESCO kuzingatia hali halisi ya maeneo ya vijijini badala ya kutumia majina ya kiutawala ya miji kuwatoza wananchi gharama kubwa za kuunganishiwa huduma hiyo. Amesema wananchi wa maeneo hayo waunganishiwe umeme kwa shilingi 27,000, bila kutozwa gharama kubwa kwa kigezo cha maeneo yao kuitwa miji kiutawala. Aidha, amepokea ombi la kujengwa kwa chuo cha ufundi stadi Ushetu, akisema Serikali itapanga utekelezaji wake kwa kuzingatia uamuzi wa kila halmashauri kuwa na chuo cha VETA.

Wed, 11 Nov 2026 13:05:12 +0000
Uncategorized · Agence Burundaise de Presse

Améliorer les capacités institutionnelles de l’Etat, un objectif de la vision 2040-2060

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Agence Burundaise de Presse

La jeunesse appelée à promouvoir la paix, la sécurité et la cohésion sociale

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Jamhuri Media

Mataragio, Katibu Mkuu wa Petroli Zambia wajadili mikakati ya ushirikiano sekta ya mafuta

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

Big Bass Christmas Blast 1000 Kukupa Ushindi Wa Hadi Mara 20,000

MSIMU wa sikukuu unapokaribia, burudani inazidi kupamba moto ndani ya Meridianbet kupitia mchezo mpya wa Big Bass Christmas Blast 1000 kutoka Pragmatic Play. Huu si mchezo wa kawaida wa kuvua samaki, bali ni safari maalumu inayochanganya mazingira ya Krismasi, uvuvi wa kusisimua na nafasi ya kupata ushindi mkubwa. Fikiria ukiwa katikati ya milima iliyofunikwa na theluji, maji yaliyoganda kwa baridi na nyumba nzuri zilizopambwa kwa mapambo ya sikukuu. Hapo ndipo safari yako inaanzia, huku kila mzunguko ukikupa sababu nyingine ya kutazamia kitakachofuata. Big Bass Christmas Blast 1000 imekuja na mfumo rahisi lakini wenye msisimko mkubwa. Mchezo huu una reels tano, safu tatu na mistari 10 ya ushindi inayolipa kuanzia kushoto kwenda kulia. Alama mbalimbali zinajumuisha namba na alama za kadi pamoja na vifaa vya uvuvi vilivyovishwa mapambo ya Krismasi. Utakutana na viboksi vya zawadi, viboko vya uvuvi vyenye miundo ya pipi za Krismasi na mapambo mengine yanayoufanya mchezo huu kuwa wa kipekee. Lakini kama ilivyo kwenye mchezo wowote wa ushindani, kinachovutia zaidi ni kile kinachoweza kutokea wakati alama zinazohitajika zinapokutana kwenye reels. Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Kivutio kikubwa zaidi ni Fisherman Wild, ambaye ana jukumu muhimu katika kuongeza msisimko wa mchezo. Alama hii inaweza kuchukua nafasi ya alama nyingine zote isipokuwa Scatter. Pia, alama za fedha zinapojitokeza, Fisherman Wild anaweza kukusanya thamani zake na kuongeza nafasi ya kupata matokeo makubwa. Hapo ndipo mambo yanapokuwa ya kuvutia zaidi, kwani kila Fisherman Wild wa nne anayeonekana katika kipengele cha bonasi anaweza kupata mizunguko ya bure. Mbali na hilo, mchezo huu una mizunguko ya bure inayochochewa na alama za Scatter, hivyo kukupa nafasi ya kuendelea na safari ya burudani bila kuishia kwenye mizunguko ya kawaida. Pia, kuna chaguo la Ante Bet na kununua mizunguko kwa wachezaji wanaotaka kufikia vipengele maalumu kwa haraka zaidi. Kila kipengele kimeongezwa kwa lengo la kuleta ladha tofauti kwenye mchezo huu. Na kinachoufanya Big Bass Christmas Blast 1000 kuwa gumzo zaidi ni uwezo wake wa kutoa ushindi wa juu kabisa wa hadi mara 20,000 ya dau lako. Sasa ni wakati wa kuingia kwenye ulimwengu huu wa uvuvi wa Krismasi kupitia Meridianbet. Je, utaweza kukutana na Fisherman Wild, kufungua mizunguko ya bure na kufurahia kila kinachojificha nyuma ya zawadi hizo za sikukuu? Big Bass Christmas Blast 1000 inakuletea mandhari nzuri, vipengele vya kuvutia na burudani ya kipekee. Tembelea Meridianbet, jisajili na ufurahie safari yako.

Wed, 11 Nov 2026 04:00:00 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

MATUMIZI YA KIDIJITALI YARAHISISHA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA PSSSF

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (wapili kulia), akipokea mkoba wenye machapisho yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa PSSSF, kutoka kwa Meneja wa Mfuko huo Ofisi ya Zanzibar, Bi. Mariam Saleh, alipotembelea Banda la PSSSF kwenye Maonesho yanayofanyika sambamba na Mkutano wa 11 wa Mtandao wa Wasimamizi wa Rasilimaliwatu katika Taasisi za Umma Barani Afrika ( APS-HRMnet) mjini Unguja, Zanzibar Novemba 10, 2026. Meneja Rasilimali Watu Bi. Gloria Mboya kulia, akiwa na Meneja wa Ofisi ya PSSSF Zanzibar, Bi. Mariam Saleh, wakitoa huduma kwa mwanachama katika banda la Maonesho ya Mkutano wa 11 wa APS-HRMnet (11th APS-HRMnet Annual Conference Delegates) unaoendelea Verde Hoteli, Zanzibar. Meneja wa Utawala Bi. Fatma Chondo wa kwanza kulia akiwa na Afisa utekelezaji Bi. Zakia Mohamed, wakitoa huduma kwa wanachama wakati wa Maonesho ya Mkutano wa 11wa Mwaka wa APS-HRMnet (11th APS-HRMnet Annual Conference Delegates) Verde Hotel, Zanzibar. Novemba 10,2026. Makamu wa Kwanza wa Rais, Mhe.Othman Masoud Othman, akimsikiliza Meneja wa Ofisi ya Zanzibar ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bi. Mariam Saleh alipotembelea banda la mfuko huo kwenye Maonesho ya Mkutano wa 11 wa Mwaka wa APS-HRMnet (11th APS-HRMnet Annual Conference Delegates) Hotel Verde, Zanzibar. Novemba 10, 2026. Novemba 10, 2026. Zanzibar Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, ameipongeza PSSSF kwa matumizi ya kidijitali katika kutoa huduma, amesema kwamba imechangia kwa kiasi kikubwa kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama na kuwaondolea usumbufu wa kufika mara kwa mara katika ofisi za Mfuko kufuata huduma. Mhe. Othman ameyasema hayo leo, Novemba 10, 2026, alipotembelea banda la PSSSF katika Maonesho ya Mkutano wa 11 wa Mwaka wa APS-HRMnet (11th APS-HRMnet Annual Conference Delegates) yaliyofanyika Zanzibar. Akizungumza baada ya kupata maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko, Mhe. Othman alisema kuwa matumizi ya mifumo ya kidijitali yameleta urahisi mkubwa kwa wanachama. Mhe. Othman, alimuwakilisha Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kufungua mkutano huo, katika Banda la PSSSF alipokelewa na Meneja wa PSSSF Ofisi ya Zanzibar, Bi. Mariam Saleh aliyemueleza namna Mfuko ulivyoendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa kutumia ambapo sasa huduma zote zinapatikana kidijitali ili kuongeza ufanisi na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama. Aidha, alielezwa kaulimbiu mpya ya Mfuko isemayo 'Tunalipa Jana', inayosisitiza dhamira ya PSSSF ya kuhakikisha wanachama wanapata mafao yao kwa wakati na kwa ufanisi zaidi ikiwemo kuimarisha mifumo ya usimamizi na ufuatiliaji wa michango ili kuwezesha ulipaji wa mafao kwa wakati.

Wed, 11 Nov 2026 12:53:51 +0000
Sports · Azam TV Videos

VIWANJANI | Kocha wa Yanga, Fadlu Davids anachokifanya kwenye kambi inayoendelea Zanzibar na kikosi.

Kocha wa boli, Michael Hyera anachambua kiufundi zaidi akisema anachokifanya sasa ni kutengeneza mfumo na jinsi anavyotaka timu icheze na kwamba.... ".....wasiokuwepo wakirejea waifuate timu inavyocheza na sio timu kuwafuata wao". Kwa upande mwingine Godlisten Muro amesema Yanga imekuwa ikikosa nafasi ya kufuzu robo fainali kutokana na sababu mbalimbali, lakini miongoni mwa sababu kubwa anayoitaja ni mabadiliko ya mara kwa mara ya benchi la ufundi, ambayo yanaathiri mwendelezo wa kazi na utekelezaji wa mipango ya timu.

2026-11-11T12:40:43+00:00
Uncategorized · Agence Burundaise de Presse

Les administratifs et confessions religieuses ont un rôle important dans la prévention de la maladie à virus d’Ebola

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Senate fails to muster 15 lawmakers for second week despite 689 pending matters

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Is UDA-ODM political marriage in distress?

Growing dissent among ODM grassroots leaders is exposing tensions despite assurances from senior officials that the broad-based alliance is intact.

Recently
Uncategorized · Agence Burundaise de Presse

L’UCCD organise une formation de deux jours sur le leadership transformationnel à Butanyerera

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Issa Michuzi

Benki ya Letshego Faidika yaanza kugawa zawadi za kampeni ya Weka Tukuwekee

Mfanyabiashara Peter Mwambo wa jijini Arusha amekuwa mshindi wa kwanza kujishindia pikipiki katika kampeni ya kukuza utamaduni wa kuweka akiba ya Benki ya Letshego Faidika, inayojulikana kama  “Weka. Tukuwekee!” Mwambo amejishindia pikipiki hiyo kupitia mpango wa zawadi za kila mwezi wa kampeni hiyo ya wiki 12, ambayo ilizinduliwa Oktoba 5, 2026, ikiwa na lengo la kuwahamasisha Watanzania kuongeza akiba zao na kutumia huduma rasmi za kibenki. Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hiyo, Meneja wa Tawi la Benki ya  Letshego Faidika la Arusha, Neema Malisa, alisema benki hiyo imefurahi kumpata mshindi wake wa kwanza wa pikipiki tangu kuanza kwa kampeni hiyo. Malisa alimpongeza Mwambo kwa ushindi huo na kuwahimiza wakazi wa Arusha pamoja na mikoa jirani kutumia huduma za benki hiyo kwa kuweka akiba na kupata fursa ya kushiriki katika kampeni zinazoandaliwa na kufaidika nazo. Alisema kampeni ya  ‘Weka. Tukuwekee’ imekusudiwa kufanya uwekaji wa akiba kuwa rahisi, wenye manufaa na unaoweza kumwezesha kila Mtanzania kujenga utamaduni wa kuweka fedha kwa ajili ya mahitaji na mipango yake ya baadaye. Aliongeza kuwa benki hiyo inaendelea kuboresha huduma zake ili kuwafikia wateja wengi zaidi, huku akieleza kuwa akaunti zake za akiba zinawapa wateja fursa ya kuweka fedha na kunufaika na huduma mbalimbali za kibenki. Kwa upande wake, Meneja wa Masoko na Mawasiliano wa Letshego Faidika Bank, Kenneth Misigaro, alisema kampeni hiyo ni sehemu ya dhamira ya benki hiyo ya kuifanya huduma ya kuweka akiba iwe rahisi, yenye thamani na inayopatikana kwa Watanzania wengi zaidi. Misigaro alisema benki inaendelea kupanua njia za uwekaji fedha na kusogeza huduma karibu na wananchi ili kuondoa vikwazo vinavyoweza kuwazuia kutumia huduma rasmi za kifedha. Alisema wateja wanaweza kuweka fedha katika akaunti zao za LetsGo kupitia matawi na vituo vya benki hiyo, mawakala wake pamoja na mitandao ya simu ya M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa na HaloPesa. Pia, wateja wanaweza kuhamisha fedha kutoka benki nyingine kwenda kwenye akaunti zao za Letshego. Benki hiyo imepanua zaidi mtandao wake kwa kuruhusu wateja kuweka fedha kupitia mawakala wa CRDB na matawi ya Tanzania Commercial Bank (TCB), bila gharama za ziada za huduma hiyo. Kampeni hiyo itakayohitimishwa Desemba 27, 2026, inatekelezwa katika kanda tano za benki hiyo nchini ambazo ni Kaskazini, Kati, Kusini, Magharibi na Ziwa. Kupitia kampeni hiyo, wateja wanaoweka fedha katika akaunti za LetsGo wanashindanishwa katika makundi matatu kulingana na kiasi cha amana wanachoweka. Katika kundi la Wathubutu, linalohusisha wateja wanaoweka hadi Sh50,000, mshindi wa kila wiki anapata Sh50,000. Kundi la Wajenzi, lenye amana za kati ya Sh50,000 na Sh500,000, linatoa zawadi ya Sh100,000, huku kundi la Wakubwa, kwa wanaoweka zaidi ya Sh500,000, likiwa na zawadi ya Sh200,000 kwa mshindi wa wiki. Mbali na zawadi hizo za fedha, mteja atakayekuwa ameweka amana kubwa zaidi kila mwezi anajishindia pikipiki mpya, huku mteja atakayekuwa na jumla kubwa zaidi ya amana katika kipindi chote cha kampeni akitarajiwa kupata zawadi kuu ya guta la mizigo. Akizungumzia ushindi wake, Mbwambo alisema hakutarajia kupata zawadi hiyo licha ya kuwa na utaratibu wa kuweka akiba katika benki mbalimbali. Alisema ushindi huo ni wa kipekee kwake kwa kuwa hajawahi kupata zawadi ya aina hiyo kutokana na utaratibu wake wa kuweka akiba. "Ni zawadi kubwa sana kwangu. Nitaiboresha biashara yangu kwa kuitumia pikipiki hii katika shughuli za usafirishaji na kuwafikia wateja wangu. Awali nilikuwa nikitumia pikipiki za kukodi, lakini sasa nitakuwa na yangu mwenyewe," alisema Mwambo. Meneja wa Tawi la Benki ya  Letshego Faidika la Arusha, Neema Malisa (kulia) akikabidhi funguo ya pikipiki kwa mshindi wa kwanza wa kampeni ya Weka Tukuwekee, Peter Mwambo ambaye ni mfanyabiashara wa mkoa wa Arusha.Kampeni hiyo itakayodumu kwa wiki 12, imeanza tangu Oktoba 5 na inatarajiwa kumalizika Desemba 27, 2026, ikiwa inatekelezwa katika kanda tano nchini ambazo ni Kanda, Kati, Kusini, Magharibi, Ziwa na Kaskazini Meneja wa Tawi la Benki ya  Letshego Faidika la Arusha, Neema Malisa (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pikipiki wa droo ya kwanza ya kampeni ya kampeni ya Weka Tukuwekee, Peter Mwambo ambaye ni mfanyabiashara wa mkoa wa Arusha. Wa kwanza kulia ni meneja wa Amana wa Benki ya Letshego Faidika. Neema Soka. Kampeni hiyo itakayodumu kwa wiki 12, imeanza tangu Oktoba 5 na inatarajiwa kumalizika Desemba 27, 2026, ikiwa inatekelezwa katika kanda tano nchini ambazo ni Kanda, Kati, Kusini, Magharibi, Ziwa na Kaskazini. Wafanyakazi wa benki ya Letshego Faidika na wadau wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pikipiki wa droo ya kwanza ya kampeni ya kampeni ya Weka Tukuwekee, Peter Mwambo (wa saba kutoka kulia) mara baada ya zoezi la kumkabishi zawadi yake ya kuwa mshindi wa kwanza wa kampeni ya Weka Tukuwekee. Kampeni hiyo itakayodumu kwa wiki 12, imeanza tangu Oktoba 5 na inatarajiwa kumalizika Desemba 27, 2026, ikiwa inatekelezwa katika kanda tano nchini ambazo ni Kanda, Kati, Kusini, Magharibi, Ziwa na Kaskazini.

Wed, 11 Nov 2026 09:30:00 +0000
Uncategorized · The Star Kenya

Court: Refugee work permit restrictions unlawful

High Court rules that the restrictions amount to indirect discrimination and undermine their right to human dignity

Recently
Uncategorized · Agence Burundaise de Presse

Validation des cinquième et sixième rapports sur les droits économiques, sociaux et culturels

Read the full report from the original source.

Recently

Page 246 of 1139 · 22775 stories