Unganishwa

Search the region

22809 stories

National · Issa Michuzi

TAKUKURU GEITA YAREJESHA ZAIDI YA MILIONI 242

Na Nasra Ismail,Geita Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita imefanikiwa kusaidia kurejesha jumla ya Shilingi 242,957,748.52 katika kipindi cha Aprili hadi Septemba 2026, kupitia ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, chambizo za mifumo, uchunguzi na mashtaka. Taarifa hiyo imetolewa leo na makamu Mkuu wa TAKUKURU (M) Geita, Alex Mpemba, katika taarifa kwa umma kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo. Katika ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kiasi cha Shilingi 24,658,549.52 zimerejeshwa kutokana na ufuatiliaji wa miradi 38 yenye thamani ya Shilingi 61,526,803,015.26 katika sekta za Elimu, Afya, Barabara, Utawala, Maji na Miradi ya Maendeleo ya Jamii. Kati ya miradi hiyo, miradi 32 imebainika kuwa na mapungufu madogo ambapo ushauri umetolewa kurekebisha mapungufu hayo, huku miradi 6 ikiwa na kasoro kubwa ambapo hatua za haraka zilichukuliwa. Baadhi ya hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kudhibiti malipo ya Shilingi 2,400,000 yasilipe kwa Mzabuni baada ya kuwasilisha madawati 30 yaliyokuwa yametengenezwa kwa mbao mbichi katika ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Butambala iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe. Pia, kudhibiti malipo ya Shilingi 3,310,000.00 ikiwa ni sehemu ya malipo ya ufundi na vifaa katika mradi wa ujenzi wa nyumba ya Mtumishi “2 in 1” katika Zahanati ya Nyarubanga, na kuwasilisha kiasi cha Shilingi 6,874,216.19 kwenye akaunti ya Kamishina wa Kodi za Ndani ambacho kilikuwa hakijawasilishwa katika Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya TANESCO Wilaya ya Bukombe. TAKUKURU Mkoa wa Geita imefanya chambizo 10 za mifumo ikiwemo uchambuzi wa mfumo wa makadirio na makusanyo ya mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Katika chambizo hizo ziliwekwa maazimio manne ambayo utekelezaji wake katika mwaka 2025/2026 umewezesha kiasi cha Shilingi 14,037,955 kukusanywa. Katika kutoa elimu kwa umma, TAKUKURU imefanya semina 32 uimarishaji wa Klabu 148, mikutano ya hadhara 38, maonyesho 05 na utoaji wa habari 09. Hatua hiyo imelenga kuongeza uelewa wa jamii na kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa. Kiasi cha Shilingi 198,161,244.00 kimerejeshwa Serikalini kutokana na uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mapato ya ndani (Own Source) zilizokusanywa kupitia mashine za POS na kupitia mfumo wa kielektroniki wa LGRICS. Fedha hizo ni pamoja na kiasi cha Shilingi 174,782,610.00 kilichodhibitiwa katika akaunti za Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Shilingi 23,378,634.00 kilichorejeshwa katika akaunti za Halmashauri ya Wilaya ya Chato na Mbogwe, pamoja na kiasi cha Shilingi 6,100,000 kilirejeshwa katika akaunti ya mfuko wa maendeleo ya jamii baada ya fidia ya ardhi kwa eneo ambalo alimilikishwa kabla ya eneo hilo kutwaliwa na mgodi wa Buckreef katika Kijiji cha Mnekezi. Aidha, jumla ya malalamiko 72 yalipokelewa. Kati ya hayo, malalamiko 57 yalikuwa yahusuyo rushwa, na malalamiko 15 yahusuyo makosa yasiyo ya rushwa. Malalamiko yasiyohusu rushwa yalishughulikiwa kwa kupewa ushauri, huku yale yaliyohusu rushwa yakipelekwa kwa uchunguzi, na mengine yakirudishwa kwenye taasisi za mamlaka husika kwa ufanyiwaji kazi. Kesi 28 ziliamuliwa ambapo Jamhuri ilishinda kesi zote 28. Katika kipindi hiki kesi 37 mpya ziliunguliwa Mahakamani. Katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2026, TAKUKURU imejipanga kuongeza kiwango cha kufuatilia matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuimarisha kiwango cha kuelimisha umma katika makundi tofauti ili kuongeza uelewa wa mapambano dhidi ya rushwa kwa wananchi, pamoja na uboreshaji wa Programu ya TAKUKURU RAFIKI.

Wed, 11 Nov 2026 06:17:49 +0000
Uncategorized · Azam TV Videos

MSHIKEMSHIKE - AZAM TV 10/11/2026

Azam TV

2026-11-11T05:43:34+00:00
Uncategorized · The Citizen

Tanzania turns to value addition to unlock $220 billion export ambition

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Mwananchi

Mapya yaibuka kutekwa kwa Mwaipaya, shahidi asema...

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

'True great' Kane set to break England appearance record

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Farmers urged to embrace bee pollination to increase crop yields

Nyuki Marathon to be held in Nairobi on February 7, 2027, to raise awareness about the role of bees in pollination, food security and biodiversity conservation.

Recently
Uncategorized · Daily News

TANAPA revenue triples to 534bn/-

DAR ES SALAAM: TANZANIA National Parks Authority (TANAPA) has more than tripled its revenue over the past five years, with…

Recently
Uncategorized · Mwananchi

Operesheni ya helmeti Zanzibar, nia njema, utekelezaji wenye maswali

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Citizen

Government seeks wider gains from exceptional teachers’ novelty

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Standard

Joho summoned by Senate over Lake Nakuru fish

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Ankole Times

From An Orphan To Billionaire! Inside The Secret Life And Wealth Of Patrick Bitature

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Observer Uganda

Forensic experts summoned in case of journalist who claimed Janet Museveni was dead

The Law Development Centre Grade One Magistrate’s court has issued witness summons to the investigating officer and forensic experts in the case against journalist and…

Recently
Uncategorized · Daily News

TZ pushes for climate justice

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Vendors using chemicals to delay, hasten fruit ripening

Scientists say chemicals raise health concerns because exposure can affect the liver, nervous system and reproductive health

Recently
Sports · Mwanaspoti

Kisa Yanga MC Alger yabadili gia angani

Soma zaidi hapa

Recently
Uncategorized · The Citizen

Tanapa moves to attract investment, new tourism markets

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KBC

US House blocks bid to impeach Defence Secretary Pete Hegseth

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Citizen

Justice and democracy dominate Alute Lissu’s funeral

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

The world's biggest economies in 2026

IMF data ranks the world's largest economies by nominal Gross Domestic Product (GDP), measured in current US dollars.

Recently
Uncategorized · The Citizen

Stakeholders propose lasting solution to roadside trading

Read the full report from the original source.

Recently

Page 258 of 1141 · 22809 stories