Unganishwa

Search the region

22818 stories

Uncategorized · HabariLeo

Tanzania mwenyeji maonesho ya Jua Kali 2027

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

What Tanzania’s 604.6bn/- school investment means for education

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Malaysia's Najib Razak moves to house arrest over 1MDB scandal

Read the full report from the original source.

Recently
Entertainment · The Ankole Times

Scandal: Chameleone Exposed! Consultant Hired To Set Up Leone TV Dismisses Singer’s Claims, Reveals Shocking Details

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Abigael Chepkirui wins silver at Dakar Games to lift Kenya’s medal tally to six

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Chanzo

Hotuba ya Lissu Siku Aliyohukumiwa Kifungo, Na Mikakati Iliyokuwa Ikiendelea Nyuma ya Pazia

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

KATIBU WA BUNGE AWAPA VIJANA SOMO LA DEMOKRASIA NA UONGOZI

Na Janeth Raphael - MichuziTv KATIBU wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraka Leonard, amewataka Wabunge wa Bunge la Vijana 2026 kuzingatia misingi ya demokrasia, haki, nidhamu na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yao, huku wakiheshimu tofauti za kimtazamo na kuzingatia Kanuni pamoja na taratibu za Kibunge. Leonard ametoa wito huo leo, Novemba 10, 2026, jijini Dodoma, wakati akifungua rasmi Bunge la Vijana 2026, lililoanza Novemba 9 na linatarajiwa kuhitimishwa Novemba 13, 2026. Amesema Bunge la Vijana ni jukwaa muhimu katika kuwaandaa vijana kuwa viongozi bora wa sasa na baadaye, kwa kuwajengea uwezo na uelewa kuhusu misingi ya demokrasia, uongozi, uwakilishi, uwajibikaji na taratibu mbalimbali za Kibunge. Ameeleza kuwa katika kipindi cha siku tano za mafunzo, washiriki wanapata ujuzi katika maeneo mbalimbali, yakiwemo historia ya Bunge, uendeshaji wa shughuli za Kibunge, mchakato wa kutunga na kupitisha sheria pamoja na Kanuni za Bunge la Vijana. Aidha, amesema vijana hao tayari wameshiriki katika uchaguzi wa viongozi wa Bunge hilo, wakiwemo Spika, Naibu Spika na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, sambamba na uteuzi wa Katibu wa Bunge na Makatibu Mezani watakaosaidia kuratibu shughuli za chombo hicho. Kwa mujibu wa Leonard, washiriki pia wamepata uzoefu wa vitendo kupitia mchakato wa kuthibitisha jina la Waziri Mkuu na uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hatua inayowajengea uelewa mpana kuhusu mifumo ya kidemokrasia na taratibu za kiuongozi. Akizungumzia wajibu wa viongozi waliochaguliwa, Leonard amewataka kuongoza kwa haki, usawa na busara, huku wakihakikisha kila Mbunge anapata nafasi ya kutoa maoni na kushiriki katika mijadala bila upendeleo. Amewapongeza vijana wote waliopata nafasi za uongozi, huku akiwahimiza wale ambao hawakuchaguliwa kuendelea kushiriki kikamilifu katika mijadala kwa kutoa hoja, kujenga hoja mbadala na kuchangia mawazo yatakayosaidia kuleta tija. “Uongozi si kushika nafasi pekee, bali ni kuwa na dhamira, uwezo na utayari wa kuleta mabadiliko. Bunge imara halijengwi na viongozi pekee, bali kwa ushiriki na michango ya kila Mbunge,” amesema Leonard. Amesisitiza kuwa vijana wanapaswa kulitumia Bunge hilo kama jukwaa la kuibua na kujadili changamoto zinazowakabili wenzao, zikiwemo elimu, ajira, ujasiriamali, teknolojia, afya, mazingira, ushiriki katika maamuzi na fursa za kiuchumi. Leonard amesema haitoshi kubainisha changamoto pekee, bali vijana wanapaswa kuchambua chanzo cha changamoto hizo na kuibua mapendekezo ya suluhisho yanayotekelezeka kwa manufaa ya vijana na Taifa kwa ujumla. Katika hotuba yake, Katibu wa Bunge amesisitiza mambo manne muhimu yatakayokuwa msingi wa mafanikio ya Bunge la Vijana 2026, ambayo ni nidhamu na uzingatiaji wa Kanuni za Bunge, uwezo wa kujenga hoja na kujadiliana kwa weledi, uwajibikaji katika kuwakilisha vijana, pamoja na uadilifu, uzalendo na dhamira ya kulitumikia Taifa. Amesema nidhamu ni nguzo muhimu ya kuhakikisha mijadala inafanyika katika mazingira ya heshima, utulivu na uvumilivu, akibainisha kuwa tofauti za kimawazo hazipaswi kuwa chanzo cha uhasama, bali ziwe fursa ya kupanua uelewa na kupata suluhisho bora zaidi. Pia amewataka Wabunge wa Bunge la Vijana kujenga hoja kwa kuzingatia ukweli, ushahidi, mantiki na maslahi ya umma, akisisitiza kuwa uwezo wa kiongozi haupimwi kwa wingi wa maneno anayozungumza, bali kwa uwezo wake wa kusikiliza, kuchambua na kujibu hoja za wengine kwa busara. Akizungumzia maadhimisho ya miaka 100 ya Bunge la Tanzania, Leonard amesema vijana hao watapata fursa ya kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria unaohusu Maadhimisho ya Miaka 100 ya Bunge la Tanzania, hatua aliyoieleza kuwa ni fursa ya kipekee kwao kushiriki katika tukio muhimu la kihistoria la Taasisi hiyo. Amesema mwaka 2026 ni wa kihistoria kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambalo linaadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Kutunga Sheria la Tanganyika, lililojulikana kwa jina la The Legislative Council of Tanganyika Territory, mwaka 1926. Kwa upande wake, Spika wa Bunge la Vijana 2026, Anna Mrema, amewataka vijana kutambua wajibu wao katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii na Taifa kwa kuanza kuchukua hatua sasa, badala ya kusubiri fursa za uongozi hapo baadaye au kuendelea kuwalaumu viongozi kwa changamoto zinazowakabili wananchi. Mrema pia amesisitiza umuhimu wa vijana kuzingatia nidhamu, uadilifu na heshima, akieleza kuwa uongozi ni dhamana ya kuwahudumia watu na si nafasi ya kujinufaisha binafsi. Ameongeza kuwa vijana walioshiriki katika Bunge hilo wanapaswa kuwa mabalozi wa mabadiliko chanya watakaporejea katika vyuo na jamii zao, kwa kusambaza maarifa waliyoyapata na kuhamasisha vijana wengine kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo. Bunge la Vijana 2026 linaendelea jijini Dodoma chini ya dhamira ya kuwajengea vijana uzoefu wa vitendo kuhusu uongozi, demokrasia na uwakilishi, huku likiwaandaa kushiriki kwa ufanisi zaidi katika maendeleo ya jamii na Taifa.

Tue, 10 Nov 2026 20:27:17 +0000
Health · Issa Michuzi

BABU TALE AGHARIMIA HUDUMA ZA MATIBABU YA KIBINGWA BURE KWA WANANCHI MOROGORO

Na FARIDA MANGUBE, MOROGORO Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale maarufu Babu Tale, amegaramia huduma za matibabu ya kibingwa bure kwa wananchi kupitia kambi maalumu ya afya inayoendelea katika Tarafa ya Ngerengere. Kambi hiyo ya siku 10, iliyoanza Novemba 10 hadi 20, 2026, imeandaliwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), ikilenga kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi. Akizungumza wakati wa uzinduzi uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Queen Sendiga, Babu Tale amesema wananchi watapata vipimo, matibabu na dawa bila malipo, ili kuhakikisha hakuna anayekosa huduma kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Huduma zinazotolewa ni pamoja na uchunguzi wa moyo kwa teknolojia za ECHO na ECG, ushauri wa madaktari bingwa pamoja na matibabu kulingana na mahitaji ya wagonjwa. Aidha, Babu Tale ametangaza mpango wa kutoa bima za afya bure kwa kaya maskini 150 ndani ya jimbo hilo, hatua inayolenga kuwasaidia wananchi wenye kipato duni kupata huduma za afya. Kambi hiyo inatarajiwa kunufaisha wakazi wa Ngerengere na maeneo jirani kwa kuwawezesha kupata huduma za kibingwa ambazo awali zilikuwa changamoto kutokana na gharama na umbali wa vituo vya matibabu.

Tue, 10 Nov 2026 20:24:04 +0000
Uncategorized · UBC

Uganda Railways begins cement transportation for Hima Cement

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · HabariLeo

MABADILIKO YA BOOST: Bil 604/- zajenga shule mpya 676 nchi nzima

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Issa Michuzi

AGITF YAWEKA WAZI FURSA ZA MIKOPO KWA WAKULIMA WA MATUNDA NA MBOGAMBOGA.

Mfuko wa Udhamini wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) umewahimiza wakulima wa mazao ya matunda na mbogamboga, hususan vijana na wanawake, kutumia fursa za mikopo yenye riba nafuu inayotolewa na mfuko huo ili kuimarisha uzalishaji, kuongeza thamani ya mazao na kupanua masoko ya bidhaa za kilimo. Akizungumza Novemba 10, 2026, jijini Arusha katika Maonesho ya Kilimo cha Mbogamboga, Matunda na Maua (Hortilogistical Africa 2026), Kaimu Meneja Uendeshaji wa AGTIF, Jane Hebron, amesema mfuko huo unatoa mikopo ya moja kwa moja kwa wakulima binafsi, vikundi na vyama vya ushirika, pamoja na kuwawezesha kupata mikopo kupitia taasisi za fedha kwa utaratibu wa kuwapa hati ya dhamana ili waweze kukopesheka na kulindwa kama dhamana zao hazitoshelezi ili waweze kunufaika na kilimo. Amesema kupitia programu ya Jenga kesho Iliyobora (BBT), mfuko huo unatoa mikopo kwa vijana wa kiume wenye umri wa miaka 18 hadi 40 na wanawake wenye umri wa miaka 18 hadi 65 kwa riba ya asilimia 4.5 kwa mwaka, huku muda wa marejesho ukiwa kati ya mwaka mmoja hadi mitatu kulingana na aina ya mradi, mikopo hiyo inalenga kugharamia mahitaji mbalimbali ikiwemo uchimbaji wa visima, miundombinu ya umwagiliaji, greenhouses, vitalu nyumba, ununuzi wa mbegu na pembejeo pamoja na mitaji ya kuendesha shughuli za kilimo. Amesema pia mfuko huo unatoa mikopo kwa ajili ya ununuzi wa mashine za kuchakata mazao ili kuongeza thamani na kuwawezesha wakulima kuzalisha bidhaa zinazokidhi vigezo vya masoko ya ndani na nje ya nchi, ameeleza kuwa ushiriki wao katika maonesho hayo ni fursa ya kukutana na wakulima wa horticulture, kuwapatia elimu kuhusu huduma za kifedha na kuwaelekeza namna ya kupata mitaji ya kuendeleza shughuli zao. Ameongeza kuwa wakulima wanaweza kuomba mikopo hiyo kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Taasis hiyo kwa kuchagua mfumo wa e-Kilimo na kufuata maelekezo ya maombi, amewahimiza wakulima na wadau wa kilimo kutembelea banda la AGITF katika maonesho hayo ili kupata elimu zaidi kuhusu mikopo na fursa za kukuza biashara zao za kilimo. Akizungumza Anjelina Silyvester Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Elite Brand kutoka Iringa amesema kupitia programu ya BBT wamefanikiwa kupata mkopo kutoka AGITF wenye  riba nafuu uliowawezesha kuongeza mashine kiwandani, kupunguza muda wa uzalishaji na kuongeza uwezo wa kuingiza bidhaa zao sokoni, na kukuza biashara zao. Kwa upande wake, Kamal Haji Simba, mkulima kutoka Paje, Zanzibar, ambaye alitembelea banda la AGITF, amesema amejifunza kuhusu fursa za mikopo yenye riba nafuu inayotolewa na mfuko huo kwa vijana na wanawake, huku akiwashauri vijana kuchangamkia fursa hiyo ili kupata mitaji ya kuwekeza katika kilimo na kujikwamua kiuchumi.

Tue, 10 Nov 2026 20:16:34 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

MAKAMU WA RAIS ATOA MAAGIZO UKAMILISHAJI WA BARABARA YA AMANI MAKORO – RUANDA

MBINGA, RUVUMA Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameonesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya Amani Makoro - Ruanda yenye urefu wa kilomita 35, wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma, baada ya mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 60.5 kuchelewa kwa miaka miwili na miezi 10. Akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo katika eneo la Amani Makoro, wilayani Mbinga, Makamu wa Rais amebaini kuwa ni kilomita 10.5 pekee zilizojengwa kati ya kilomita 35 zilizopangwa, licha ya mkataba wa awali wa ujenzi kuwa wa miezi 18. Kutokana na hali hiyo, Makamu wa Rais ameiagiza Wizara ya Ujenzi kuandaa mpango kazi na mkakati madhubuti wa kuhakikisha mradi huo unakamilika, huku akisisitiza umuhimu wa kubaini na kushughulikia sababu zinazokwamisha utekelezaji wake. Ameelekeza kuwa iwapo ucheleweshaji unasababishwa na mkandarasi, hatua stahiki zichukuliwe kwa kuzingatia sheria na taratibu za manunuzi ya umma. Aidha, iwapo changamoto inatokana na upatikanaji wa fedha, Serikali itafute ufumbuzi wa kuhakikisha fedha zinazohitajika zinapatikana ili kukamilisha mradi huo Akizungumza na wananchi wa Amani - Makoro, wakati wa ziara hiyo, Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha unakamilika na kuanza kutoa manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi. Amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutakuwa kichocheo muhimu cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Wilaya ya Mbinga na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla, hususan katika kurahisisha shughuli za uzalishaji, biashara na usafirishaji. Ameongeza kuwa barabara hiyo ina umuhimu wa kimkakati katika kuimarisha miundombinu inayohudumia shughuli za uwekezaji, ikiwemo miradi ya uchimbaji wa makaa ya mawe inayotekelezwa wilayani Mbinga. Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais amesisitiza kuwa dhamira ya Serikali ni kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwa kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na fedha za umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Amesema Serikali itaendelea kuweka mbele maslahi ya wananchi, huku ikiimarisha usimamizi na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuzuia upotevu wa fedha na kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana katika miradi inayotekelezwa. Akizungumzia changamoto ya bei ya mahindi, Makamu wa Rais amewahakikishia wananchi kuwa Serikali inaendelea kushughulikia suala hilo ili kulinda maslahi ya wakulima na kuimarisha sekta ya kilimo. Amewataka wananchi kuendelea kujikita katika uzalishaji wa mazao, hususan mahindi, na kuongeza kiwango cha uzalishaji katika msimu ujao wa kilimo. Amesema Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa bei ya mahindi na kuchukua hatua za kuhakikisha changamoto na makosa yaliyojitokeza katika upangaji wa bei hayajirudii. Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini, Mhe. Judith Kapinga, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa uwekezaji mkubwa katika miradi ya maendeleo mkoani Ruvuma, hususan katika Jimbo la Mbinga Vijijini. Amesema uwekezaji huo una mchango mkubwa katika kuboresha huduma za kijamii, kuimarisha miundombinu na kufungua fursa mpya za kiuchumi kwa wananchi. Hata hivyo, amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha miradi inayoendelea kutekelezwa inakamilika kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika na uwekezaji huo. Aidha, ameiomba Serikali kuharakisha utekelezaji wa miradi mingine muhimu katika jimbo hilo, ikiwemo miradi ya maji, ili kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu na kuboresha maisha ya wananchi. Kukamilika kwa barabara ya Amani Makoro - Ruanda kunatarajiwa kuimarisha shughuli za kiuchumi, kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa pamoja na kuchochea uwekezaji katika Wilaya ya Mbinga na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.

Tue, 10 Nov 2026 20:07:36 +0000
Health · Issa Michuzi

MAJERUHI WA AJALI YA BASI LA MAOKOTO WANAENDELEA VIZURI, SERIKALI YATOA UHAKIKA WA MATIBABU

NA DENIS MLOWE, IRINGA MKUU wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amesema majeruhi wa ajali ya basi la Maokoto iliyotokea katika eneo la Masumbo, barabara kuu ya Iringa–Mbeya, wanaendelea vizuri na huduma za matibabu huku Serikali ikiahidi kuendelea kuhakikisha wanapata matibabu hadi watakapopona. Kheri ameyasema hayo baada ya kuwatembelea majeruhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ya Mkoa, ambapo alipata nafasi ya kujionea hali zao na maendeleo ya matibabu wanayoendelea kupatiwa na kuwapatia fedha za matunda na kujikimu wakati wakiendelea na matibabu. Amesema mkoa umepata pigo kubwa kutokana na ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu na wengine kujeruhiwa, huku akieleza kuwa juhudi za kuokoa maisha ya majeruhi na kuhakikisha wanapata huduma stahiki zinaendelea. Amesema hali za majeruhi waliolazwa hospitalini hapo zinaendelea vizuri, jambo linaloonesha kuwa huduma zinazotolewa na wataalamu wa afya zinasaidia kurejesha afya zao ili waweze kurejea katika majukumu yao ya kila siku. “Serikali imedhamiria kuhakikisha wagonjwa wote ambao bado wanaendelea na matibabu wanapata huduma zinazostahili hadi watakapopona na kurejea katika shughuli zao za kawaida,” amesema Kheri. Aidha, amewapongeza madaktari, wauguzi, manesi na wasimamizi wa sekta ya afya mkoani humo kwa namna walivyojipanga kuwapokea na kuwahudumia majeruhi tangu walipopata taarifa za ajali hiyo. Amesema hakuna mgonjwa aliyepoteza maisha kutokana na uzembe wa wahudumu wa afya, akieleza kuwa majeruhi wote waliopokelewa wameendelea kupatiwa huduma kwa wakati na kwa kuzingatia mahitaji yao ya kiafya. Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kufuatilia hali za majeruhi hadi watakapopata nafuu, huku wale watakaoruhusiwa kurejea nyumbani wakiendelea kufuatiliwa kuhakikisha wanaimarika kiafya. Pia amewataka madaktari na wahudumu wengine wa afya kuendelea kushirikiana na familia za majeruhi kwa kutoa taarifa za maendeleo ya matibabu katika kila hatua ili ndugu waweze kufahamu kinachoendelea katika vituo vya afya vinavyowahudumia wapendwa wao. Katika hatua nyingine, Kheri ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo, akieleza kuwa ni msiba mkubwa ambao utachukua muda kusahaulika. Amesema viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wataungana na familia zilizofikwa na msiba huo katika kipindi hiki cha maombolezo na shughuli za mazishi, huku akiwataka wananchi kuendelea kuonesha mshikamano na kuwafariji waliofiwa. Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Scholastica Malangalila, ambaye ni kaimu nafasi ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, amesema hospitali hiyo ilipokea majeruhi watano wa ajali hiyo, wakiwemo mwanaume mmoja na wanawake wanne. Amesema tangu walipopokelewa, hospitali ilijipanga kutoa huduma kulingana na mahitaji ya kila mgonjwa na kwamba hadi wakati akizungumza, majeruhi wote watano walikuwa wakiendelea vizuri. Ameeleza kuwa kwa mujibu wa tathmini ya madaktari, wanatarajia majeruhi hao kurejea katika hali zao za kawaida baada ya siku tatu, iwapo maendeleo ya matibabu yataendelea kuwa mazuri. Kuhusu miili ya watu waliofariki katika ajali hiyo, Malangalila amesema hospitali imeendelea kutoa huduma kwa ndugu waliofika kuitambua na kuchukua miili ya wapendwa wao, huku akibainisha kuwa zoezi hilo lilikuwa likiendelea bila changamoto yoyote.

Tue, 10 Nov 2026 20:10:26 +0000
Uncategorized · DW Rwanda

US soldier arrested in UK on Russian espionage allegations

Read the full report from the original source.

Recently
National · UN News Burundi

Security Council LIVE: South Sudan’s first elections loom amid rising violence

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Tob Cohen amended will three times to exclude Sarah Wairimu, court told

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

UK court overturns Trinidad and Tobago law criminalizing gay sex

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

FIFA presidential hopeful Vega in it to win it

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Lawyers threaten nationwide strike until advocate Abshir Abdi is found

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Standard

Kenya to open missions in Azerbaijan and Congo, closes Bern Embassy

Read the full report from the original source.

Recently

Page 264 of 1141 · 22818 stories