Unganishwa

Search the region

22395 stories

Business · Issa Michuzi

CHINA YAIPA TANZANIA KIPAUMBELE CHA KWANZA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI

-Yasema Itashirikiana na Tanzania Kufikia Malengo ya Dira ya 2050 -Dkt.Kiruswa Aeleza Fursa ya Ujenzi wa Kiwanda cha Betri za Magari ya Umeme Nchini Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia Taasisi yake ya National Development and Reform Commission (NDRC), pamoja na Kampuni ya Vast Rock International Investment Co. Ltd inayojihusisha na uwekezaji katika Sekta ya Madini, zimeitaja Tanzania kuwa eneo la kipaumbele la kimkakati kwa uwekezaji wa madini barani Afrika, ikieleza utayari wake wa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuendeleza sekta hiyo na kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Kauli hiyo imetolewa Novemba 24, 2026, kwenye kikao kati ya Wizara ya Madini na ujumbe kutoka China  kilicholenga kujadili maeneo ya ushirikiano na fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini. Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni siku mbili tu baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini (TMIC 2026), uliowakutanisha wadau zaidi ya 1,700 kutoka ndani na nje ya nchi. Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa NDRC, Dkt. Jing Qin, amesema ujumbe huo umefika nchini kwa lengo la kupata taarifa za kina zitakazowezesha kuanzishwa kwa ushirikiano wa kibiashara katika kuendeleza miradi mbalimbali ya madini nchini. Ameeleza kuwa uamuzi wa kuipa Tanzania kipaumbele umechangiwa na uhusiano wa muda mrefu na wa kihistoria kati ya Tanzania na China, pamoja na mazingira mazuri ya uwekezaji yanayowezeshwa na Sera madhubuti za Serikali katika Sekta ya Madini. Dkt. Jing amesisitiza kuwa katika kuchagua miradi ya kuwekeza, kampuni za China huzingatia uimara wa sera, uendelevu wa miradi na uwepo wa manufaa ya pande zote, huku manufaa kwa jamii zinazozunguka miradi hiyo yakiwa miongoni mwa vipaumbele muhimu. Aidha, amesema China iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza Sekta ya Madini ili iweze kuchangia ipasavyo na kutimiza malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kujenga uchumi wa Dola za Marekani trilioni moja, akibainisha kuwa wanafahamu kwamba  sekta hii ina nafasi kubwa katika kufanikisha azma hiyo. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Vast Rock amesema kampuni hiyo itaendelea kuhamasisha kampuni za China zilizowekeza nchini kushiriki kikamilifu katika kuboresha ustawi na maendeleo ya jamii katika maeneo mbalimbali wanakotekeleza miradi yao hapa nchini. Naye, Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, ameeleza kuhusu fursa ya uwekezaji katika ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata madini ya metali na madini mengine katika eneo lililotengwa la Buzwagi Economic Zone. Aidha, Dr. Kiruswa amesisitiza kuwa eneo hilo lina umuhimu wa kimkakati kwa Serikali kwani linalenga kuweka miundombinu ya uchakataji wa madini na viwanda vya uongezaji thamani madini nchini. Katika hatua nyingine, Dkt. Kiruswa ameeleza pia fursa ya uwekezaji katika ujenzi wa kiwanda cha betri za magari ya umeme nchini, akisisitiza umuhimu wa kuongeza thamani ya madini ndani ya nchi na kuimarisha mnyororo wa thamani wa madini, hatua itakayochochea uanzishaji wa viwanda na ukuaji wa uchumi. Pia amezitaja fursa nyingine zilizopo katika Sekta ya Madini kuwa ni pamoja na shughuli za utafiti wa madini, uongezaji thamani wa madini ndani ya nchi pamoja na utekelezaji wa miradi ya ubia kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Dkt. Kiruswa amewahakikishia wawekezaji kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa uwekezaji, huku akisisitiza kuwa utajiri wa rasilimali madini uliopo nchini unatoa fursa pana za uwekezaji na ushirikiano wa kibiashara.

Tue, 24 Nov 2026 11:55:29 +0000
Uncategorized · The Star Kenya

IEBC: Why we might not livestream 2027 polls

IEBC chair says nationwide live broadcasts would require cameras, technical staff and extensive logistical preparations ahead of the August 2027 polls

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

IEBC explain why it might not livestream 2027 polls

IEBC chair says nationwide live broadcasts would require cameras, technical staff and extensive logistical preparations ahead of the August 2027 polls

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Kenya to bar importation of pre-2020 vehicles from January 2027

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Agence Burundaise de Presse

Nathan Ntahondi élu président du Conseil national de la communication

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Ankole Times

Disbelief As Comedian Amooti Omubalanguzi Is Spotted Travelling On A Boda Boda Days After Receiving Brand New Car From Mickey Seems 2 Funny’s Fundraiser

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · BBC Afrique

Avion disparu en RDC : accident ou appareil abattu par les rebelles ? Ce que l'on sait

L’armée congolaise a perdu le contact avec un avion-cargo dans l’est de la RDC, tandis que le groupe rebelle FRN affirme l’avoir abattu.

Recently
Uncategorized · KBC

Kenya, Oman commit to stronger ties during golden jubilee celebration

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Agence Burundaise de Presse

Vers une uniformisation de la loi sur les régimes matrimoniaux et les successions

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KBC

DPP urges court to uphold 20-year jail term for former Venezuelan Embassy official, Kenyan in Ambassador’s murder

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Agence Burundaise de Presse

Un inventaire national répertorie et classifie 205 sites touristiques

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · BBC Rwanda

Igitero ku bwato bw'Uburusiya muri Libya coba kivuga iki ku ntambara yo muri Ukraine?

Igitero ca Ukraine ku bwato bw’intambara bw’Uburusiya ku kivuko co muri Libya congereje ubukana bw’iyi ntambara, nk’uko vyanditswe na Frank Gardner.

Recently
Uncategorized · The Citizen

Tanzania eyes tourism boost after CNN ranks Serengeti Africa’s top destination

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Agence Burundaise de Presse

Les agriculteurs de Cibitoke appelés à combiner la fumure organique et engrais chimiques pour améliorer la production agricole

Read the full report from the original source.

Recently
Entertainment · The Star Kenya

Iranian authorities flog singer who performed without hijab

Parastoo Ahmadi, three musicians and a producer were each given 74 lashes in the city of Qom, a member of their defence team told the BBC.

Recently
National · HabariLeo

Serikali yaonya madereva wasiofuata sheria

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Standard

Meru lawyers welcome new courts but ask for more

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Security tightened after 10 killed in Isiolo-Garissa clashes

Among the key resolutions is an intensive, intelligence-led operation by Inspector General of Police Douglas Kanja to recover illegal firearms

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Five women killed every hour by family members or partners — UN report

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Authority gives large water users until April 2027 to install smart meters

The requirement targets licensed water users as the regulator seeks more accurate data on resource allocation, use and discharge.

Recently

Page 27 of 1120 · 22395 stories