Unganishwa

Search the region

22831 stories

Uncategorized · The Star Kenya

Special prosecutors lined up to tackle hate speech

Igonga said the team would handle election-related offences before, during and after the polls, as the country enters the electioneering period.

Recently
Uncategorized · The Standard

Why President Ruto shouldn't put his hopes on Oburu's Linda Ground

A year since Railas death, the ODM map has shrunk and some of the leaders sounding loyal to Ruto are transactional, chasing appointments, tenders or harambees.

Tue, 10 Nov 2026 17:07:10 +0300
Uncategorized · Citizen Digital

Lopez double earns Liga leaders Barca win at Atletico

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Standard

Why President shouldn't put his hopes on Oburu's Linda Ground

A year since Railas death, the ODM map has shrunk and some of the leaders sounding loyal to Ruto are transactional, chasing appointments, tenders or harambees.

Tue, 10 Nov 2026 17:07:10 +0300
Uncategorized · Daily News

Tanzanian Mufti to grace the East African Maulid celebrations in Tang this Friday

DAR ES SALAAM: TANZANIA’S Mufti, Dr Aboubakari Zubeir Bin Ali, is expected to be the guest of honour at the…

Recently
Uncategorized · Daily News

anzania cherishes JICA’s 60-year cooperation in advancing its socio-economic projects

DAR ES SALAAM: TANZANIA has recognised and appreciated the contribution of the Government of Japan, through the Japan International Cooperation…

Recently
Uncategorized · UN News Burundi

COP31 opens in Antalya: Can climate promises finally deliver results?

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

TRAMEPRO YAIOMBA SERIKALI KUIMARISHA TIBA ASILIA, YATAKA KUJIFUNZA KUTOKA INDIA

Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania (TRAMEPRO) limeiomba Serikali kuimarisha mfumo wa Tiba Asilia na Tiba Mbadala nchini kwa kuwekeza katika elimu, tafiti za kisayansi, udhibiti wa ubora wa dawa, uhifadhi wa mimea tiba na uwekezaji katika sekta hiyo. Katika waraka wa mapendekezo ya kimkakati uliotolewa Novemba 2026, TRAMEPRO imependekeza Tanzania kujifunza kutoka Jamhuri ya India, ambayo imepiga hatua katika kurasimisha na kuendeleza mifumo ya tiba za jadi kupitia Wizara maalumu ya AYUSH. Shirika hilo limeeleza kuwa Tanzania ina utajiri mkubwa wa mimea tiba na maarifa ya jadi yaliyorithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine, lakini bado kuna changamoto zinazohitaji kushughulikiwa ili sekta hiyo iweze kuchangia kikamilifu katika afya ya jamii na uchumi wa taifa. Miongoni mwa changamoto zilizobainishwa ni upungufu wa tafiti za kisayansi, mifumo ya mafunzo na viwango vya kitaaluma, vifaa vya kupima ubora wa bidhaa, pamoja na uharibifu wa mazingira unaosababisha kupungua kwa baadhi ya mimea tiba. TRAMEPRO imependekeza pia kuimarishwa kwa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa kuongeza rasilimali watu, fedha, vifaa na mifumo ya kidijitali ili liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Aidha, shirika hilo limetaka kuanzishwa kwa mfumo wa mafunzo ya kitaaluma utakaowawezesha wataalamu wa tiba asili kupata elimu ya kisasa kuhusu usalama wa wagonjwa, matumizi sahihi ya dawa, maadili ya taaluma na umuhimu wa kuwapeleka wagonjwa kwenye huduma za kisasa pale inapohitajika. Katika eneo la utafiti, TRAMEPRO imependekeza kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), vyuo vikuu, taasisi za afya na wataalamu wa tiba asili ili kuchunguza kisayansi mimea tiba, viambato vyake, usalama na ufanisi wake. Kwa upande wa uchumi, shirika hilo limehimiza Serikali kuweka mazingira rafiki kwa uwekezaji katika viwanda vya kuchakata mimea tiba, maabara za kupima ubora, uzalishaji wa bidhaa zenye viwango na upanuzi wa masoko ya ndani na nje ya nchi. Katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, TRAMEPRO imependekeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kuanzisha mazungumzo rasmi na Wizara ya AYUSH ya India ili kuwezesha kubadilishana uzoefu, mafunzo, teknolojia, tafiti za pamoja na fursa za uwekezaji. Waraka huo pia unapendekeza utekelezaji wa mpango wa miaka mitano kuanzia 2027 hadi 2031, utakaoanza na tathmini ya mfumo uliopo, kuimarisha taasisi na mifumo ya udhibiti, kuendeleza tafiti na uzalishaji, kukuza uwekezaji na hatimaye kufanya tathmini ya matokeo. TRAMEPRO imeiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya kupokea na kutathmini mapendekezo hayo, kuitisha mkutano wa kitaifa wa wadau wa Tiba Asilia na Tiba Mbadala, pamoja na kuimarisha utekelezaji wa Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala, Sura ya 244. Akieleza msimamo wa shirika hilo, Katibu Mkuu wa TRAMEPRO, Boniventura F. Mwalongo, amesema maendeleo ya sekta hiyo yanapaswa kujengwa kwa ushirikiano wa Serikali, wataalamu, taasisi za utafiti, vyuo vikuu na sekta binafsi. Amesisitiza kuwa lengo la mapendekezo hayo si kuiga mfumo wa India, bali kujifunza kutokana na uzoefu wake na kujenga mfumo wa Tanzania unaozingatia mazingira, rasilimali na mahitaji ya nchi. Kauli mbiu ya waraka huo ni: “Tuisimamie Tiba Asili kwa Maarifa, Tuiendeleze kwa Sayansi, Tuilinde kwa Sheria na Tuikuze kwa Uchumi.”

Tue, 10 Nov 2026 14:22:21 +0000
Sports · Mwanaspoti

Kaizer Chiefs yawinda beki Azam FC

Soma zaidi hapa

Recently
Sports · Mwanaspoti

Chama aibua jambo jipya Bongo

Soma zaidi hapa

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

Kili Trust, TACAIDS, taasisi zakutana kufanya tathmini ya fedha za Kili Challenge dhidi ya mapambano ya Ukimwi

Meneja wa Masuala ya Uendelevu  wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita ( GGML) Bw. Gilbert Mworia akizungumza  wakati wa mkutano wa kufanya tathmini ya fedha za GGM Kili Challenge  against HIV & AIDS uliojumuisha taasisi zilizopata fedha hizo kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi. Bi Neema Julius kutoka Taasisi ya Konga la Waviu Arusha akiwasilisha namna taasisi hiyo ilivyonufaika na  mgao wa fedha zilizotolewa  na kampeni ya GGM Kili Challenge Against HIV & AIDS  wakati wa tathmini ya kikao kinachoendelea Moshi, mkoani Kilimanjaro Wadau wakifatilia mada Na Mwandishi Wetu MOSHI, KILIMANJARO – GGM Kilimanjaro Challenge Against HIV & AIDS Trust kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imeanza kufuatilia utekelezaji wa miradi ya taasisi/mashirika zilizopokea fedha kupitia kampeni hiyo kwa msimu wa mwaka 2025/26 ili kutathmini mafanikio, changamoto na matokeo ya uwekezaji huo katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI nchini. Ufuatiliaji huo unafanyika kupitia semina ya siku mbili katika Hoteli ya Weruweru, jijini Moshi, mkoani Kilimanjaro, itakayofuatiwa na ziara ya siku tatu katika maeneo mbalimbali yanakotekelezwa miradi ya taasisi/mashirika hayo. Akizungumza katika semina hiyo, Mwenyekiti wa Timu ya Ufundi, ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa TACAIDS, Bw. Nyangusi Laiser, alisema rasilimali zinazopatikana kupitia kampeni hiyo ni muhimu katika kuimarisha mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI nchini. Alisema licha ya hatua zilizopigwa katika kupunguza maambukizi, ugonjwa huo bado ni changamoto, huku vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 wakiwa miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari kubwa ya maambukizi. Aliongeza kuwa wanawake ndio kundi lilioathiriwa zaidi, likiwakilisha asilimia 80 ya maambukizi yote nchini, yanayohusisha watu 1,548,000, kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2023. “Wote tunafahamu kuwa rasilimali fedha kutoka kwa mashirika ya kimataifa zilizokuwa zikitumika kusaidia mapambano dhidi ya UKIMWI barani Afrika zimepungua. Hivyo, kampeni hii inayosimamiwa na GGML kwa zaidi ya miaka 24 ni muhimu katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kutokomeza ugonjwa huu nchini,” alisema Bw. Laiser. Katika uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji, taasisi zilizopokea fedha kupitia kampeni hiyo zilieleza kuwa ufadhili huo umekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya watu wanaoishi na VVU na UKIMWI. Aliisema fedha hizo zimewezesha kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa ajili ya kuongeza kipato, kutoa elimu kuhusu kujikinga na maambukizi mapya, kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI (ARV) na kurahisisha upatikanaji wa huduma katika vituo vya tiba na matunzo (CTC). Akielezea mafanikio ya mradi wao, Afisa wa Kikundi cha Jali Afya Yako, Epuka Maambukizi Mapya, Fuata Ushauri na Nasaha (KIJAEFA), Bw. Roymen Siria, alisema taasisi hiyo kupitia kampeni hiyo ya mwaka 2025/26 ilipokea mgao wa Sh milioni 30 ambazo zimewekezwa katika mradi wa uzalishaji wa unga wa lishe kwa ajili ya kuimarisha afya ya jamii na kuongeza kipato cha wanufaika. “Tumewekeza katika ununuzi wa vifaa mbalimbali na kuanzisha uzalishaji wa unga wa lishe kama njia ya kujiongezea kipato na wakati huohuo kuchangia kuboresha afya ya jamii,” alisema Bw. Siria. Alisema kwa sasa wanaendelea na mchakato wa kusajili bidhaa zao katika taasisi mbalimbali za Serikali, ikiwemo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), ili ziweze kukidhi vigezo vinavyohitajika na kuingia katika masoko ya kitaifa na kimataifa. Aliongeza kuwa ukosefu wa kipato ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili watu wanaoishi na VVU, hivyo mradi huo unalenga kuwapatia fursa za kiuchumi zitakazowasaidia kujitegemea na kuboresha maisha yao. Kwa upande wake, Bi. Neema Julius kutoka taasisi ya Konga la Waviu Arusha, ambayo pia ni mnufaika wa fedha hizo, alisema taasisi yao imejikita katika kutoa elimu kuhusu VVU na UKIMWI, kuhamasisha upimaji wa afya katika kaya na kuwaunganisha watu wanaobainika kuwa na maambukizi na huduma stahiki za matibabu. “Taasisi yetu inajikita zaidi katika kutoa elimu kuhusu VVU na UKIMWI, kufanya upimaji wa afya katika kaya na kutoa rufaa kwa watu wanaobainika kuwa na maambukizi ili waweze kupata huduma sahihi katika vituo vya afya,” alisema Bi. Julius. Alisema ufadhili huo umeongeza uwezo wa watoa huduma wa taasisi hiyo kuwafikia wananchi wengi zaidi na kutoa elimu inayolenga kupunguza maambukizi mapya na athari za VVU na UKIMWI katika jamii. Akizungumzia mchango wa kampeni hiyo, Meneja wa Kili Trust, Bw. Stephen Mhando, alisema fedha zinazotolewa kwa taasisi hizo zinatokana na kampeni ya kuchangisha fedha kupitia kampeni ya kupanda mlima Kilimanjaro inayofanyika kila mwaka kwa njia ya miguu na baiskeli. Alisema kampeni hiyo inalenga kukusanya rasilimali fedha kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa afua mbalimbali za mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali. “Tumeendesha kampeni hii kwa zaidi ya miaka 24 sasa, huku ushirikiano wetu na TACAIDS ukiwa umeanza mwaka 2014. Lengo letu ni kuhakikisha ndoto ya kuwa na Tanzania isiyo na maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vinavyotokana na Ukimwi inatimia,” alisema Bw. Mhando. Alisema licha ya mafanikio yaliyopatikana kutokana na michango ya taasisi na mashirika mbalimbali, bado kuna haja ya wadau kuendelea kushirikiana kwa kuwa maambukizi ya VVU bado yapo nchini. “Ni muhimu wadau wote tuendelee kushikana mikono na kuimarisha juhudi hizi ili kuifanya Tanzania kuwa salama dhidi ya VVU na UKIMWI,” alisisitiza. Naye Mkurugenzi wa Masuala ya Uendelevu wa GGML, Bw. Gilbert Mworia, alisema upatikanaji wa rasilimali fedha ni nguzo muhimu katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, akizitaka taasisi, mashirika na vikundi vinavyotekeleza afua mbalimbali kuanzisha miradi ya kiuchumi itakayoviwezesha kupata fedha dhidi ya mapambano hayo. Alisema hatua hiyo itasaidia taasisi hizo kuendelea kutoa huduma kwa jamii hata pale ufadhili kutoka nje unapopungua au kukosekana. “Tunawashauri kutumia fursa ya uwezeshaji unaotokana na kampeni ya GGM Kili Challenge kuanzisha miradi ya kiuchumi itakayowapatia rasilimali fedha, ili muweze kuendelea kuhudumia jamii katika maeneo yenu hata kama ufadhili kutoka nje utapungua au kukatika,” alisema Bw. Mworia. Akifafanua kuhusu madhumuni ya semina na ziara hiyo, Afisa Utawala wa kampeni ya Kili Challenge, Bi. Njile Mabula, alisema kukutana na taasisi wanazozisaidia pamoja na kutembelea maeneo yao ya utekelezaji ni utaratibu wa kila mwaka unaolenga kutathmini maendeleo ya miradi hiyo. Alisema ziara hizo pia hutoa fursa ya kubaini mafanikio, changamoto na maeneo yanayohitaji maboresho ili kuhakikisha fedha zinazotolewa zinatumika ipasavyo na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Tue, 10 Nov 2026 14:19:19 +0000
Uncategorized · Daily News

TAZARA suspends all train services between Makambako and Mbeya until Dec 1

DAR ES SALAAM: THE Tanzania-Zambia Railway Authority (TAZARA) has suspended passenger and cargo train services between Mbeya and Makambako until…

Recently
Health · The Nile Post

Doctors Warn Couples Against Untreated Infections at PLU Medical Camp

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Jamhuri Media

Serikali yaipongeza TIA kwa kongamano la biashara

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · HabariLeo

RUWASA yataka wadau kutumia mpango wa WASH

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Daily News

EAC Ministers use the 49th SCTIFI meeting to advance regional trade, investment, economic ties

DAR ES SALAAM: THE East African Community (EAC) has officially commenced the 49th Meeting of the Sectoral Council of Ministers…

Recently
Uncategorized · Business Daily

KPLC inflated, irregularly awarded Sh228m thermal power contracts

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

RAMEPRO YAADHIMISHA REMEMBRANCE DAY 2026, YATOA WITO WA AMANI NA HESHIMA KWA UHAI

Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania (TRAMEPRO) limeungana na jumuiya ya kimataifa kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya mashujaa na wahanga wa Vita Vikuu vya Kwanza na vya Pili vya Dunia, maarufu kama Remembrance Day, kwa kutoa wito wa kuheshimu uhai, kudumisha amani na kuhifadhi historia ya binadamu. Katika taarifa iliyotolewa Novemba 8, 2026, jijini Dar es Salaam, TRAMEPRO imetambua umuhimu wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Makaburi ya Mashujaa wa Vita vya Jumuiya ya Madola (Commonwealth War Cemetery), yaliyohudhuriwa na Balozi wa India nchini Tanzania, Bishwadip Dey, Mshauri wa Masuala ya Ulinzi, Commodore Agyapal Singh, maafisa wa Ubalozi wa India pamoja na wanajumuiya wa India wanaoishi nchini. Shirika hilo limeipongeza Serikali ya India kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kwa kuendeleza utamaduni wa kuwakumbuka na kuwaenzi watu waliopoteza maisha yao katika vita, likieleza kuwa uwekaji wa mashada ya maua na sala ni ishara ya heshima, mshikamano na kuthamini historia ya binadamu. TRAMEPRO imeeleza kuwa maadhimisho hayo yanatokana na historia ya kusitishwa kwa mapigano ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Novemba 11, 1918, kupitia makubaliano ya Armistice, ambapo baadaye Novemba 11 ikawa siku ya kuwakumbuka wahanga wa vita mbalimbali duniani. Aidha, shirika hilo limeeleza kuwa Jumapili ya pili ya Novemba huadhimishwa kama Remembrance Sunday katika utamaduni wa Jumuiya ya Madola, ambapo mwaka huu imeangukia Novemba 8, 2026. Katika kuhusisha historia hiyo na Tanzania, TRAMEPRO imekumbusha nafasi ya Tanganyika katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, wakati eneo hilo lilipokuwa likijulikana kama Afrika Mashariki ya Kijerumani, ambapo mapigano yalihusisha majeshi ya Ujerumani na Washirika, wakiwemo wanajeshi kutoka India na mataifa mengine. Pia, shirika hilo limehimiza kutambuliwa kwa mchango na athari za vita kwa Waafrika, wakiwemo askari wa King’s African Rifles na wananchi walioguswa na mapigano hayo. Katika hatua nyingine, TRAMEPRO imepanua wito huo wa kumbukumbu kwa kuwakumbuka pia wataalamu wa Tiba Asili na wahifadhi wa maarifa ya jadi waliotangulia mbele ya haki, ikieleza kuwa mchango wao katika kuhudumia jamii, kuhifadhi maarifa na kutumia rasilimali za asili unapaswa kuenziwa. Limesisitiza kuwa heshima kwa wataalamu hao inapaswa kuonekana kupitia juhudi za kuendeleza utafiti, elimu, usalama wa wagonjwa, maadili ya kitaaluma na uhifadhi wa mazingira. Katika wito wake kwa Serikali za dunia, taasisi za dini na jamii, TRAMEPRO imehimiza matumizi ya diplomasia na mazungumzo katika kutatua migogoro, kulindwa kwa maisha ya raia na kuimarishwa kwa ushirikiano wa kimataifa katika kudumisha amani na haki za binadamu. Viongozi wa dini wametakiwa kuendelea kuhubiri upendo, msamaha, uvumilivu na mshikamano, huku vijana wakihimizwa kujifunza historia ili kuelewa athari za vita na umuhimu wa kujenga dunia yenye amani. Kwa upande wa wataalamu wa afya na Tiba Asili, shirika hilo limewataka kuweka usalama wa wagonjwa mbele, kuendeleza tafiti na kuhifadhi maarifa ya jadi kwa kuzingatia maadili na haki za jamii. Akihitimisha ujumbe huo, Katibu Mkuu wa TRAMEPRO, Boniventura F. Mwalongo, amesisitiza kuwa kumbukumbu ya mashujaa na wahanga wa vita inapaswa kuwa fundisho kwa dunia kuhusu umuhimu wa kulinda maisha, kuheshimu utu na kujenga mshikamano. Amesema amani si kutokuwepo kwa vita pekee, bali pia ni uwepo wa haki, usalama, afya bora, upendo na mazingira salama kwa kila mwanadamu. TRAMEPRO imehitimisha kwa ujumbe wake wa kimataifa “Lest We Forget” (Hatutasahau), huku ikisisitiza kuwa amani ni wajibu wa kila mmoja katika kujenga dunia bora kwa vizazi vijav

Mon, 09 Nov 2026 14:02:00 +0000
Uncategorized · BBC Afrique

Envie de grignoter avant d'aller au lit ? Voici pourquoi et comment y remédier

Il existe des raisons biologiques qui peuvent vous inciter à consommer des sucreries avant de vous coucher, mais vous pouvez changer cette habitude.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Omtatah flags legal loopholes exposing public funds to abuse

The Busia senator identifies borrowing, offshore spending and special-purpose funds operating outside ordinary parliamentary budgetary controls.

Recently

Page 271 of 1142 · 22831 stories