Search the region
22837 stories
NMB Yawakutanisha wadau wa korosho Mtwara, CBT yaahidi malighafi kwa viwanda
NA MWANDISHI WETU BODI ya Korosho Tanzania (CBT) imewahakikishia wawekezaji wanaojenga viwanda vya kubangua korosho nchini kuwa watapata malighafi za kutosha kuendesha shughuli zao, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza uwezo wa viwanda vya kubangua korosho nchini ifikapo mwaka 2030. Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Francis Alfred, amesema bodi itahakikisha wawekezaji wanaotumia fedha nyingi kujenga viwanda hawajikuti wakishindwa kuviendesha kutokana na uhaba wa korosho ghafi. Alfred ametoa kauli hiyo Novemba 7, 2026, mkoani Mtwara, wakati wa kikao cha wadau wa korosho kilichoandaliwa na Benki ya NMB, kikihusisha wabanguaji, wanunuzi na wafanyabiashara kujadili fursa za ufadhili zinazolenga kutatua changamoto katika mnyororo wa thamani wa zao hilo. Amepongeza hatua ya NMB kuwakutanisha wadau hao, akisema ushirikiano kati ya taasisi za fedha na wafanyabiashara wa korosho ni muhimu katika kuongeza uzalishaji na kufanikisha azma ya nchi ya kupanua uwezo wa viwanda vya kubangua korosho ifikapo mwaka 2030. Aidha, amezihimiza taasisi nyingine za fedha kuwa karibu na wadau wa sekta hiyo ili kutambua mahitaji yao na kutoa masuluhisho yanayochochea ukuaji wa biashara. Alfred pia amezitaka benki kuhakikisha malipo ya wakulima yanafanyika kwa wakati ili kuwawezesha kutimiza mahitaji yao ya kifedha na kujiandaa kwa shughuli zinazofuata za uzalishaji. Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Biashara ya Kilimo kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Christopher Mwalugenge, amesema benki hiyo imejipanga kusaidia biashara za korosho katika msimu wa 2026/2027 kupitia masuluhisho mbalimbali ya kifedha. Amesema huduma hizo zinalenga kuwawezesha wanunuzi wa korosho kupitia minada na masoko ya awali kupata mitaji ya kununua mazao kwa wakati na kwa kiwango kinachohitajika, huku wabanguaji wakipata fedha za kununua malighafi za kuendesha viwanda vyao. Mwalugenge amesema NMB pia inatoa masuluhisho ya kifedha yanayokidhi mahitaji ya wasafirishaji wa korosho nje ya nchi, ili kuwawezesha kufanya manunuzi kwa wakati na kutekeleza mikataba yao ya biashara katika masoko ya kimataifa. Ameongeza kuwa benki hiyo imeimarisha huduma zake za malipo na miamala ili kurahisisha shughuli za biashara katika hatua mbalimbali za mnyororo wa thamani wa korosho. Kikao hicho kinatarajiwa kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za fedha na wadau wa korosho, hususan katika kuongeza upatikanaji wa mitaji, kuchochea ubanguaji wa korosho nchini na kuhakikisha wakulima wanalipwa kwa wakati.
Tue, 10 Nov 2026 12:02:18 +0000ROOM TO READ, TET WASAINI KUSHIRIKIANA KUBORESHA ELIMU
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Room to Read Tanzania, Bi. Joan Ndaambuyo Minja (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba (kulia) wakisaini hati ya makubaliano kupanua ushirikiano eneo la uimarishaji wa stadi za kusoma na kuandika kwa watoto, pamoja na kukuza stadi za maisha na usawa wa kijinsia kwa vijana, hususan wasichana, hafla iliyofanyika ofisi za TET jijini Dar es Salam. Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Room to Read Tanzania, Bi. Joan Ndaambuyo Minja (kushoto) akibadilishana nyaraka na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba (kulia) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kupanua ushirikiano eneo la uimarishaji wa stadi za kusoma na kuandika kwa watoto, pamoja na kukuza stadi za maisha na usawa wa kijinsia kwa vijana, hususan wasichana, hafla iliyofanyika ofisi za TET jijini Dar es Salam. Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Room to Read Tanzania, Bi. Joan Ndaambuyo Minja na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba (kulia) wakionesha hati za makubaliano mara baada ya kuzisaini kwenye ofisi za TET jijini Dar es Salam. SHIRIKA la Room to Read, limeingia makubaliano na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), ikiwa ni sehemu ya kuendeleza, kuimarisha na kupanua ushirikiano eneo la uimarishaji wa stadi za kusoma na kuandika kwa watoto, pamoja na kukuza stadi za maisha na usawa wa kijinsia kwa vijana, hususan wasichana. Akizungumza katiha hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkazi wa Room to Read, Bi. Joan Ndaambuyo Minja alisema wanatambua na kuthamini dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora, jumuishi na yenye kumjengea maarifa, stadi na uwezo wa kushiriki katika maendeleo ya Taifa, hivyo lina kila sababu ya kuunga mkono juhudi hizo. Alisema shirika hilo li nauchukulia ushirikiano na Serikali kuwa ni sehemu ya kutekeleza vipaumbele vya kitaifa katika sekta ya elimu, badala ya kuwa utekelezaji wa programu za Room to Read moja kwa moja. “… Leo ni siku muhimu katika historia ya ushirikiano kati ya Taasisi ya Elimu Tanzania na Shirika la Room to Read Tanzania. Utiaji saini wa Hati hii ya Makubaliano unaweka msingi rasmi wa kuendeleza, kuimarisha na kupanua ushirikiano wetu katika maeneo mawili muhimu: uimarishaji wa stadi za kusoma na kuandika kwa watoto, pamoja na kukuza stadi za maisha na usawa wa kijinsia kwa vijana, hususan wasichana,” alisema, Bi. Minja. Alibainisha kuwa makubaliano waliosaini yan aendana na mwelekeo wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, Toleo la 2023, inayosisitiza umuhimu wa elimu yenye ubora, usawa wa fursa, ujumuishi na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika kuendeleza elimu nchini. Aliongeza kuwa Sera inatambua kuwa jukumu la kuboresha elimu si la Serikali pekee. Linahitaji ushirikiano wa karibu kati ya Serikali, taasisi zake, sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, wadau wa maendeleo, wazazi na jamii kwa ujumla. “…ushirikiano huu unaendana na matarajio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kujenga Taifa lenye watu wenye maarifa, ujuzi, ubunifu na uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii. Dira hii inatukumbusha umuhimu wa kuwekeza katika rasilimali watu kuanzia hatua za awali za ujifunzaji, kuimarisha elimu yenye ubora na kuhakikisha kuwa wanawake na wanaume, wasichana na wavulana wanapata fursa sawa za kujifunza, kuendeleza vipaji vyao na kushiriki katika maendeleo ya Taifa,” amesisitiza, Bi. Joan Minja. Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Room to Read Tanzania, Bi. Joan Ndaambuyo Minja (kulia) akizungumza kwenye hafla ya kusaini hati ya makubaliano kupanua ushirikiano eneo la uimarishaji wa stadi za kusoma na kuandika kwa watoto, pamoja na kukuza stadi za maisha na usawa wa kijinsia kwa vijana, hususan wasichana, naTaasisi ya Elimu Tanzania (TET). Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Room to Read Tanzania, Bi. Joan Ndaambuyo Minja (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba (kulia) wakisaini hati ya makubaliano kupanua ushirikiano eneo la uimarishaji wa stadi za kusoma na kuandika kwa watoto, pamoja na kukuza stadi za maisha na usawa wa kijinsia kwa vijana, hususan wasichana, hafla iliyofanyika ofisi za TET jijini Dar es Salam. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba akizungumza katika hafla hiyo, alisema miongoni mwa malengo makuu ya Hati ya Makubaliano waliosaini ni Kushirikiana katika uandaaji, kupitia na kuhuisha vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili viendane na viwango vya Mitaala ya Taifa, kwa kuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023, na Mwongozo wa Kitaifa wa Mitaala ya ElimuMsingi, kwa lengo la kuimarisha ubora na ufanisi wa ujifunzaji wa stadi za msingi. Alisema mengine muhimu waliokubaliana na katika ushirikiano huo ni, kuimarisha umahiri wa walimu kupitia mifumo ya mafunzo ya ualimu kabla ya kuanza kazi na mafunzo endelevu kwa walimu walio kazini, kwa kuandaa na kutekeleza mafunzo kwa kuzingatia Mkakati wa Taifa wa Maendeleo na Usimamizi wa Walimu pamoja na vipaumbele vya kitaifa vya kuimarisha umahiri wa walimu na kuboresha ufundishaji na ujifunzaji darasani. Aidha alibainisha na Pia tumekubaliana; k uwezesha upatikanaji wa elimu bora kwa usawa na bila ubaguzi, kwa kuzingatia mahitaji ya kijinsia, kwa mujibu wa Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Jinsia pamoja na vipaumbele vya elimu jumuishi vilivyoainishwa. Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Room to Read Tanzania, Bi. Joan Ndaambuyo Minja (kushoto) akibadilishana nyaraka na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba (kulia) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kupanua ushirikiano eneo la uimarishaji wa stadi za kusoma na kuandika kwa watoto, pamoja na kukuza stadi za maisha na usawa wa kijinsia kwa vijana, hususan wasichana, hafla iliyofanyika ofisi za TET jijini Dar es Salam. Picha ya pamoja.
Tue, 10 Nov 2026 12:04:14 +0000Bulgaria: People killed in massive highway pileup
Read the full report from the original source.
RecentlyDuale unveils plan for health data intelligence centre
“We must move away from fragmented health information systems and duplication. Data must be translated into better planning, resource allocation..."
RecentlyIndia: Sonia Gandhi's memoir 'Belonging: A Journey of Love' released
Read the full report from the original source.
RecentlyTanzania to host 2027 EAC Jua Kali Exhibitions
KIGALI: TANZANIA has been selected to host the 27th East African Community (EAC) Small and Medium Enterprises (SMEs) Trade Fair,…
RecentlyIndia: Sonia Gandhi's memoir on the Gandhi-Nehru family released
Read the full report from the original source.
RecentlyKNH performs two groundbreaking Nerve Reconstruction Surgeries
A four-year-old boy and a 43-year-old man who lost their hand and arm, respectively, underwent nerve reconstruction surgeries.
RecentlyVIWANJANI | Yanga SC kinara timu zilizotengeneza nafasi nyingi za mashuti yaliyolenga lango NBC PL.
Yanga ndio kinara wa kupiga mashuti yaliyolenga lango kwenye ligi kuu msimu huu hadi kufikia sasa, akifuatiwa na Simba, Azam FC na JKT Tanzania. Hizi hapa takwimu kamili kutoka Viwanjani ambapo Godlisten Muro anachambua kwa hisabati akionesha jinsi ambavyo timu zote za ligi kuu zina udhaifu katika matumizi ya nafasi. Muro anasema Simba na Yanga wana unafuu katika matumizi ya nafasi licha ya kwamba "...hawajafikia hata nusu ya kubadilisha nafasi zao kuwa mabao". Yanga imepiga jumla mashuti 71 yaliyolenga lango, na Simba mashuti 69, lakini wote wamefunga magoli 23 pekee....
2026-11-10T11:39:22+00:00Ubunifu wafungua soko jipya la bidhaa za mkonge
Read the full report from the original source.
RecentlyGovernment seeks to turn refugee-hosting areas into economic hubs
Interior CS Kipchumba Murkomen says humanitarian assistance must be complemented by sustainable development initiatives that benefit both refugees and host communities.
RecentlyFINCA loan boosts mother’s ambition to grow business and educate her son
LIRA - At just 29, Robinah Omolo is determined to build a successful business in Lira City while securing a brighter future for her nine-year-old son. Her journey into entrepreneurship began...
RecentlyMaj Gen Oscar Munanura Takes Over As Chief Of Defence Intelligence And Security
Read the full report from the original source.
RecentlyMaj Gen Munanura Takes Over Military Intelligence
Read the full report from the original source.
RecentlyRuto’s Gusii gamble: Can development edge out Matiang’i?
Ruto is banking on development projects and political alliances to win over Gusii voters, but Matiang’i’s presidential bid threatens his 2027 ambitions.
RecentlyTanzania, Italy agree to bolster their Mattei Plan ties in agriculture, health, energy
DAR ES SALAAM: TANZANIA has reaffirmed its commitment to strengthening and expanding economic cooperation with Italy, with a focus on…
RecentlyUK Seeks to Put Rwanda Climate Finance Partnership on COP31 Agenda
Read the full report from the original source.
RecentlyAfrica largest crypto economies(Shbn)
South Africa tops the continent with a massive Sh5.10 trillion (Sh5,107.43 billion) in crypto volume
RecentlyGwajima asisitiza ushiriki wanawake sekta ya majini
Read the full report from the original source.
RecentlyAn acacia-inspired landmark takes shape at Bomas
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 274 of 1142 · 22837 stories