Search the region
22945 stories
ALMES INTERNATION SCHOOL DODOMA YASISITIZA MATUMIZI SAHIHI YA TEKNOLOJIA KWA WATOTO
Na.Mwandishi Wetu – DODOMA ALMES International School ya Dodoma imesisitiza umuhimu wa elimu bora, malezi yenye maadili na ushirikiano wa karibu kati ya shule na wazazi katika kumwandaa mtoto kuwa kiongozi bora wa baadaye, mwenye uwezo wa kukabiliana na changamoto za kijamii na kiuchumi. Msisitizo huo umetolewa wakati wa mahafali ya nne ya shule hiyo yaliyofanyika, jijini Dodoma, yakihusisha wanafunzi wa Pre-Unit na Grade Seven, ambao wamehitimu hatua mbalimbali za elimu na kuelekea katika hatua nyingine za masomo. Mmiliki wa Almes International School, Weja Ng’olo, amesema shule hiyo imeendelea kuwekeza katika elimu na malezi bora, kwa kuzingatia maadili, kumfundisha mtoto kumkumbuka Mungu, usafi na kuwa na mazingira bora ya kujifunzia, akibainisha kuwa elimu inapaswa kwenda sambamba na maandalizi ya maisha. Amesema shule hiyo inaendelea kujipanga kwa kuhakikisha inaboresha huduma zake mara kwa mara, huku ikiongeza programu za ziada zinazolenga kukuza vipaji, ujuzi na uwezo wa wanafunzi katika maeneo mbalimbali. “Tunawashukuru sana wazazi kwa kutuamini na kutuletea watoto wao. Wazazi ni mabalozi wetu wakubwa, kwa sababu mzazi anapomweleza mzazi mwingine kuhusu huduma anazoziona kwa mtoto wake, hiyo ndiyo njia nzuri ya kuitangaza shule,” amesema Ng’olo. Aidha amesema shule hiyo inaendelea kuboresha miundombinu, kuongeza huduma za elimu na kuimarisha programu za malezi ili kuwapatia wanafunzi elimu bora inayokidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye. Ng’olo amesema shule binafsi zina nafasi kubwa katika kusaidia Serikali kutoa elimu bora kwa wananchi, huku akieleza kuwa uwekezaji wa ndani katika sekta hiyo unaweza kuongeza fursa za elimu na kuwawezesha watoto wa Tanzania kushindana katika soko la elimu na ajira ndani ya Afrika Mashariki na maeneo mengine. Hata hivyo amesema kuwa Almes ina mpango wa kuimarisha elimu ya vitendo na shughuli za ziada, ikiwamo michezo, ushonaji, muziki, kukare na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), huku ikiendelea kuboresha maabara ya kompyuta na kuangalia namna ya kujumuisha teknolojia ya akili bandia (AI) katika mafunzo. Katika hatua nyingine, amesema shule hiyo imeanzisha programu maalumu ya kuwahudumia watoto wakati wa likizo, inayolenga kuwasaidia wazazi wanaokuwa na majukumu ya kikazi huku watoto wao wakiendelea kujifunza na kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo ya kimwili, kiakili na kijamii. Amesema programu hiyo itaanza Novemba 16 hadi Desemba 16, ambapo watoto watashiriki mazoezi ya jumla, michezo ya soka, kikapu, voliboli na tenisi, pamoja na shughuli za kompyuta, muziki, kukare na nyinginezo. Ada ya programu hiyo ni Sh200,000 kwa mwezi kwa wanafunzi wa Almes na Sh250,000 kwa watoto kutoka shule nyingine. Ng’olo amesema programu hiyo inawalenga watoto wote bila kujali shule wanazosoma, akibainisha kuwa ni fursa ya kuwapatia malezi bora, ulinzi na mazingira ya kujifunza wakati wa likizo, badala ya kukaa nyumbani bila shughuli za kuwaendeleza. Hata hivyo, amesema shule binafsi zinazoanza kukua hukutana na changamoto mbalimbali za uendeshaji, ikiwamo kodi na michango ya taasisi mbalimbali, ambazo wakati mwingine huongeza gharama na kuwa mzigo kwa shule zenye idadi ndogo ya wanafunzi. Ameishauri Serikali kuangalia mazingira ya shule changa ili kuziwezesha kukua na kuendelea kutoa huduma bora za elimu. Kwa upande wake, Mkuu wa Shule hiyo, Christine Mwima, amewataka wazazi kuongeza ushiriki wao katika maendeleo ya elimu ya watoto kwa kufuatilia masomo, kazi za nyumbani (homework) na maendeleo yao kwa ujumla, badala ya kuliachia jukumu hilo walimu pekee. Amesema ushirikiano wa wazazi na walimu ni muhimu katika kujenga msingi imara wa elimu na maadili. Mwima pia amesisitiza umuhimu wa wazazi kufuatilia matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watoto wao, kuhakikisha wanaitumia kwa manufaa ya kujifunza na kujenga ujuzi, huku akibainisha kuwa malezi bora ni jukumu la pamoja kati ya familia na shule kwa kuwa watoto wa sasa ndio viongozi wa baadaye. Naye Margreth Fabian, mzazi wa Amaris Charles, mwanafunzi wa shule hiyo, amesema ushirikiano kati ya wazazi na Almes International School umechangia kuleta mabadiliko chanya kwa watoto, hususan katika maendeleo ya masomo, uwezo wa kujieleza na mwenendo wa kitabia. Amesema wazazi wanapaswa kuendelea kufuatilia matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watoto na kuwaelekeza kuitumia katika shughuli zenye tija, ikiwamo kujifunza na kufanya kazi za shule.
Sat, 07 Nov 2026 15:18:22 +0000Rwandan peacekeepers promotes community health and nutrition through clean-up campaign and kitchen garden initiative in Malakal
Read the full report from the original source.
RecentlyUne tempête détruit 53 maisons et sept salles de classe à Kirehe
Read the full report from the original source.
RecentlyMakerere Honours Mastercard Foundation for Supporting Students with Disabilities
Read the full report from the original source.
RecentlyShabana edge Mombasa United in five-goal thriller at Mbaraki
Read the full report from the original source.
RecentlyMudavadi to Western: What 30%? You never voted for us
“You don't vote for us and then you say, 'give us'. Wacheni mchezo. That is the problem that we have in this Western region,” he said.
RecentlyRwanda National Police steps up efforts to prevent and combat fire outbreaks
Read the full report from the original source.
RecentlyGitega : le pavage des routes pèse lourd sur les ménages
Read the full report from the original source.
RecentlyItaly Funds Shs58bn Project to Strengthen Maternal, Child and Cancer Healthcare in Northern Uganda
Read the full report from the original source.
RecentlySon of Iran's shah receives 'Freedom Prize' in Frankfurt
Read the full report from the original source.
RecentlyKCCA says 114 children rescued from Kampala streets
Read the full report from the original source.
RecentlyThe young Somali woman changing how the world sees Mogadishu
Sucdi Abdul Fattah Abdul Khader is among a growing number of local guides taking visitors beyond the headlines to explore Mogadishu's beauty spots
RecentlyOusted FKF members break silence after dismissal
Shikanda, a former Kenyan international, said their ouster was illegal, claiming that the genuine delegates were locked out.
Sat, 07 Nov 2026 17:24:12 +0300Umunyamakuru Marie Jeanne Umutoni yatunguwe no guhamagarwa nk’indashyikirwa akigera ahatangirwaga ibihembo
Read the full report from the original source.
RecentlyWendi Launches Weekly Rewards Campaign to Boost Digital Transactions
Read the full report from the original source.
RecentlyMuseveni Urges Cultural Leaders to Preserve Indigenous Knowledge
Read the full report from the original source.
RecentlyKyabazinga, Inhebantu Welcome Third Son, Prince Nadiope Ezra Josiah
Read the full report from the original source.
RecentlyItaly's Meloni blames pro-Russian hackers for cyberattack on minister
Read the full report from the original source.
Recently2026 FiRe Awards: Pearl Bank Wins Gold as Stanbic, NSSF Crowned Titans
Read the full report from the original source.
RecentlyMudavadi to Luhya nation: Don't follow Sifuna blindly
Mudavadi questioned Linda Mwananchi's electoral strength, arguing that its leadership and lack of nationwide structures undermine Sifuna's presidential ambition
RecentlyPage 329 of 1148 · 22945 stories