Unganishwa

Search the region

22951 stories

Uncategorized · Chimpreports

UFZEPA Pushes for VAT Reforms to Boost Free Zone Competitiveness

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Observer Uganda

Austria, UNICEF commit Shs 15bn to ease West Nile’s water crisis

In parts of West Nile, 71 pupils share a single school latrine, nearly twice Uganda’s recommended standard of 40. At the same time, one in…

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Kalonzo seeks Nyanza support, promises to fulfill Raila's vision

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Sinner to replace coach Cahill with Magnus Norman at year's end

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Tesla to 'wind down' production of flop Cybertruck

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Watchdog Uganda

BIG BOOST FOR HEALTH SECTOR: Uganda secures $25M Pandemic Fund grant as Minister Baryomunsi, Dr Kyobe get top Africa CDC roles

KAMPALA — Vice President Maj. (Rtd) Jessica Alupo has announced a major financial boost for Uganda’s healthcare system after the country secured a $25 million (approx. UGX 92 billion) grant…

Recently
National · Watchdog Uganda

Minister Babalanda Warns Busoga Leaders Against Corruption and Political Interference in NUSAF IV Implementation

BUSOGA – The Minister for the Presidency and Member of Parliament for Budiope West Constituency, Hon. Babirye Milly Babalanda, cautioned political, administrative and technical leaders in Busoga against corruption, polit

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Human speech follows the same patterns as birdsong — new research

Songbirds first evolved about 50 million years ago, long before the first lines of humans split from the other great apes.

Recently
Uncategorized · Business Daily

Quickmart IPO oversubscribed by Sh3.4bn

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Kenyan products showcased as China hosts Africa trade exhibition

Displays at the 2026 China-Africa Trade Commodity Exhibition include coffee, tea, wine, handicrafts, jewellery, skincare products and shea butter.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

KUHARIBU NOTI FAINI YA SH. 500,000 KWA KILA NOTI AU JELA MWAKA MMOJA

Kitendo cha kuchana, kuchoma au kuharibu noti za fedha kwa makusudi kinaweza kumwingiza mtu Katika mkono wa Sheria huku adhabu yake ikitajwa kuwa faini ya Shilingi 500,000 kwa kila noti au kifungo cha mwaka mmoja jela, kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu. Masharti hayo yanatajwa katika Kifungu cha 332A cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16, kinachohusu uharibifu wa noti na sarafu zinazotambulika kisheria kuwa fedha halali. Akifafanua Sheria hiyo Afisa wa Benki Kuu , Kurugenzi ya Sarafu, Bw. Shadrack Mapunda katika semina ya waandishi wa habari Jijini  Dar es salaam amesema sheria hiyo inalenga kuhakikisha fedha zinazotumika nchini zinalindwa dhidi ya vitendo vya uharibifu vinavyofanywa bila kufuata taratibu zilizowekwa. Amesisitiza kuwa ulinzi wa fedha ni sehemu muhimu ya kuimarisha uaminifu katika mfumo wa fedha na kuhakikisha noti zinaendelea kutumika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi. Sambamba na hilo, sheria imeweka pia masharti dhidi ya vitendo vya kughushi fedha na nyaraka mbalimbali. Kifungu cha 338 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kinatajwa kuweka adhabu kali kwa makosa ya kughushi, ikiwemo kifungo cha maisha jela kwa mujibu wa masharti husika. Aidha, mahakama inaweza kuamuru mali au nyaraka zinazohusishwa na uhalifu huo kutaifishwa kwa mujibu wa sheria. \Hatua hiyo inasisitiza umuhimu wa wananchi kuheshimu fedha za taifa na kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha uhalali na uaminifu wa mfumo wa fedha nchini.

Fri, 06 Nov 2026 16:59:58 +0000
National · Issa Michuzi

TAKUKURU RUVUMA YAREJESHA MILIONI 44 ZA MIRADI TUNDURU NA NAMTUMBO

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imefanikiwa kurejesha Zaidi ya shilingi milioni 44.1 fedha za miradi katika Halmashauri za wilaya ya Tunduru na Namtumbo. Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda akizungumzia utendaji kazi wa Taasisi hiyo katika kipindi cha kuanzia Aprili hadi Septemba 2026,amesema TAKUKURU imefanikiwa kurejesha kiasi hicho cha fedha kupitia ufutiliaji matumizi ya fedha za mradi wa ujenzi wa shule mpya ya msingi Majimaji wilayani Tunduru na mradi wa ujenzi wa vyumba sita vya madarasa katika shule ya msingi Mageuzi wilaya ya Namtumbo. Mwenda amebainisha kuwa TAKUKURU wilaya ya Tunduru ilifanya uokoaji wa fedha Zaidi ya shilingi milioni 38.8 kiasi ambacho kilikuwa kimelipwa kwenda kwa Mzabuni Njowele Invstiment LTD aliyekabidhi mabati 227 ambayo yalikuwa chini ya kiwango. Amesema baada ya ufuatiliaji uliofanywa na TAKUKURU kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tunduru pamoja na wasimamizi wa mradi na kuwekeana maazimio,mabati 227 yasiyo na ubora yaliondolewa na kuletwa mapya 227 yenye ubora unaotakiwa. Amesema katika wilaya ya Namtumbo TAKUKURU ilifanya uokoaji wa fedha kiasi cha shilingi milioni 5.1 ambacho kilitakiwa kulipwa kwa mzabuni Bryce General Supply aliyewasilisha matofali yaliyokuwa chini ya kiwango. Amesema baada ya ufuatiliaji wa TAKUKURU kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Namtumbo matofali yasiyokuwa na ubora yaliondolewa na kuletwa matofali mapya yenye ubora unaotakiwa. Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma amesema TAKUKURU katika kipindi hicho ilifanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo 31 yenye thamani ya shilingi bilioni 5.7 katika sekta za Utawala,miundombinu,afya na Elimu ili kuhakikisha thamani ya fedha inapatikana na utekelezaji wa miradi unalingana na fedha zilizotumika. Hata hivyo amesema kati ya miradi 31 iliyotekelezwa,TAKUKURU imetoa mapendekezo ya kurekebisha mapungufu kwenye miradi 12 yenye thamani ya shilingi bilioni 2.2. Akizungumzia uchunguzi wa mashitaka,Mwenda amesema TAKUKURU ilipokea malalamiko 118 kati ya hayo,malalamiko 85 yalihusu rushwa na 33 hayakuhusu rushwa na kwamba malalamiko yote yanayohusu rushwa uchunguzi umeanzishwa na upo katika hatua mbalimbali. Ameyataja matarajio ya TAKUKURU katika kipindi cha Oktoba-Desemba 2026 kuwa ni pamoja na kuendelea kuelimisha na kuwashirikisha wananchi na wadau mbalimbali kwenye mapambano dhidi ya rushwa ili jamii ibadili mtazamo na kuichukia rushwa.

Fri, 06 Nov 2026 17:01:10 +0000
Business · Issa Michuzi

KAHAMA YAKARIBISHA UWEKEZAJI, YATAJA FURSA ZA KIUCHUMI NA USHIRIKIANO NA TASAC

MKUU wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Dkt. Francis Mlacha, amesema Wilaya ya Kahama ina fursa nyingi za uwekezaji na iko tayari kushirikiana na wadau mbalimbali, ikiwemo Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), katika kuimarisha uchumi na kukuza sekta ya viwanda. Akizungumza leo, tarehe 6 Novemba, 2026, alipokutana na Bodi ya Wakurugenzi ya TASAC, amesema Kahama imejipanga kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo kupitia uwekezaji katika sekta mbalimbali, hususan viwanda, ili kuongeza uzalishaji, ajira na biashara. Amesema Wilaya hiyo ina maeneo yenye fursa kubwa za uwekezaji, yakiwemo Buzwagi, Nyashimbi na Chapurwa, pamoja na rasilimali za madini na kilimo zinazoweza kuchochea maendeleo ya viwanda. Aidha, amesema Kahama ina nafasi ya kimkakati kijiografia inayoiwezesha kufikia masoko ya nchi tano jirani ambazo ni Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Uganda, Rwanda na Burundi, hivyo kuwa na fursa pana za biashara na uwekezaji. Amesisitiza kuwa Serikali ya Wilaya iko tayari kupokea mapendekezo ya wadau yatakayosaidia kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuondoa changamoto za kiuchumi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TASAC, Nahodha Mussa Mandia, amesema ufanisi wa shughuli za bandari na sekta ya usafirishaji unahitaji ushirikiano na uratibu mzuri kati ya Serikali na wadau wa biashara. Amesema ziara ya Bodi imelenga kujionea utendaji wa shughuli za bandari, kubaini changamoto za wadau na kutafuta suluhisho la kuboresha huduma, kurahisisha biashara na kuvutia uwekezaji. Katika ziara hiyo, Bodi ya Wakurugenzi ya TASAC ilitembelea eneo la GALCO Inland Container Depot (ICD) Isaka, kujionea miundombinu na shughuli za bandari kavu zinazosaidia kurahisisha usafirishaji wa mizigo na kukuza biashara.

Fri, 06 Nov 2026 16:55:31 +0000
Uncategorized · The Citizen

Tanzania urged to probe election-related abuses

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

Mkuranga residents set to benefit from Mafia electricity project

DAR ES SALAAM: Residents of Mkuranga District in Coast Region are expected to benefit from the construction of a 33-kilovolt…

Recently
Health · Issa Michuzi

GHARAMA ZA MATIBABU ZASUKUMA FAMILIA KUUZA MALI, BIMA YA AFYA YAONEKANA SULUHISHO

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv GHARAMA za matibabu ya magonjwa makubwa zinaweza kuzilazimisha familia kutumia akiba, kuuza mali na kutegemea michango ya ndugu na marafiki, hali inayodhihirisha umuhimu wa Bima ya Afya katika kulinda ustawi wa familia na uchumi wa wananchi. Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR), Sabato Kosuri, amevitaka vyombo vya habari kuongeza elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa Bima ya Afya na manufaa yake katika kupunguza mzigo wa gharama za matibabu. Kosuri amesema huduma za afya si suala la matibabu pekee, bali pia ni sehemu muhimu ya kulinda ustawi wa familia na uchumi wake, akibainisha kuwa ugonjwa unaohitaji matibabu ya gharama kubwa unaweza kuathiri hali ya kifedha ya familia ambayo haina maandalizi ya kukabiliana na changamoto hiyo. Akizungumza katika mkutano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na wahariri wa vyombo vya habari ulioandaliwa na OTR, Novemba 6, 2026, jijini Dar es Salaam, amesema mifumo ya Bima ya Afya inasaidia kugawana hatari za gharama za matibabu na kupunguza mzigo unaoweza kuzikabili familia. “Hali hii inaibua maswali muhimu kuhusu mustakabali wa familia ambazo hazina ndugu, marafiki au uwezo wa kifedha wa kuwasaidia zinapokabiliwa na magonjwa yanayohitaji matibabu ya gharama kubwa. “Hapa ndipo umuhimu wa NHIF na mifumo ya Bima ya Afya unapopaswa kuonekana, kwa kuwa inasaidia kugawana hatari zinazotokana na gharama za matibabu na kupunguza mzigo kwa familia moja moja,” amesema Kosuri. Amesema NHIF ina jukumu muhimu katika kulinda rasilimali watu na jamii kwa ujumla kwa kusaidia wananchi kupata huduma za afya zinazowawezesha kuendelea kushiriki katika shughuli za uzalishaji na kuchangia ujenzi wa uchumi imara. Ameongeza kuwa maendeleo ya taifa hayapaswi kupimwa kwa kuzingatia mitaji na miradi pekee, bali pia ustawi wa wananchi, akisisitiza kuwa jamii yenye afya njema ni msingi muhimu wa maendeleo endelevu. Aidha, amevitaka vyombo vya habari kutumia nafasi yake kuelimisha umma kwa kutoa taarifa sahihi kuhusu huduma zinazotolewa na NHIF, haki na wajibu wa wanachama pamoja na namna ya kunufaika na huduma hizo. Amesema ushirikiano kati ya taasisi za afya na vyombo vya habari, hususan wahariri na waandishi wa habari, unaweza kuongeza uelewa na hamasa ya wananchi kujiunga na mifumo ya Bima ya Afya na kufanya maamuzi sahihi kuhusu ulinzi wa afya zao na familia zao. Mkutano huo ni sehemu ya juhudi za OTR kuimarisha uwazi, utawala bora na uwajibikaji katika taasisi na mashirika ya umma kupitia majadiliano ya moja kwa moja na wahariri wa vyombo vya habari.

Fri, 06 Nov 2026 16:45:45 +0000
Uncategorized · DW Rwanda

Data center protesters break into Microsoft site in Amsterdam

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Jamhuri Media

Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kwenda Kisiwa cha Mafia kunufaisha wananchi wa Mkuranga.

Read the full report from the original source.

Recently
Health · Issa Michuzi

NHIF YATAJA MAFANIKIO YA MIAKA 25, MUDA WA KULIPA MADAI WAPUNGUA HADI SIKU 50

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeongeza ufanisi katika ulipaji wa madai ya vituo vya kutolea huduma za afya, ambapo muda wa wastani wa malipo umepungua kutoka siku 120 hadi siku 50, ikiwa ni miongoni mwa mafanikio ya miaka 25 ya Mfuko huo. Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Irene Isaka, amesema hayo leo Novemba 6, 2026 jijini Dat ea Salaam, wakati wa mkutano na wahariri wa vyombo vya habari ulioratibiwa na ofisi ya msajili wa hazina, akieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na kuboresha usimamizi wa rasilimali na kudhibiti matumizi. Amesema katika kipindi hicho, mapato ya Mfuko yameongezeka kwa asilimia 10.3, huku matumizi yakipungua kwa asilimia 10. Aidha, uwiano wa matumizi ya matibabu ukilinganishwa na mapato umeshuka kutoka asilimia 87 hadi asilimia 71. Dkt. Isaka amesema idadi ya wanachama wakuu imeongezeka kwa asilimia 17 na wategemezi kwa asilimia 6.2, huku mtandao wa vituo vya kutolea huduma za afya vinavyoshirikiana na NHIF ukifikia zaidi ya vituo 10,300. Katika kuadhimisha miaka 25, NHIF imepanga maonesho ya siku saba katika viwanja vya Kinangari, Dodoma, kuanzia Novemba 23 hadi 29, 2026, pamoja na mbio za marathon zinazotarajiwa kushirikisha zaidi ya watu 10,000. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, ameipongeza NHIF kwa kutambua mchango wa wanahabari katika kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa bima ya afya. Balile amesema nafasi 100 za bima ya afya zilizotolewa kwa wanahabari ni fursa muhimu, akishauri ziwanufaishe zaidi waandishi na wahariri walio kazini ambao hawana bima. Ameeleza kuwa TEF itashirikiana na NHIF kuweka utaratibu wa kuwapata wanahabari hao. Naye Mratibu wa Elimu kuhusu Bima ya Afya kwa Wote kutoka Wizara ya Afya, Said Makora, amesema Serikali inaendelea kuongeza watumishi wa afya kujiandaa na mahitaji yatakayoongezeka wakati wa utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote. Amesema kati ya ajira 5,000 zilizotolewa katika sekta ya afya, watumishi 808 wamepelekwa katika ngazi ya huduma za afya ya msingi, zikiwemo hospitali na vituo vya afya. Hata hivyo, amesema bado kuna upungufu wa watumishi, huku Serikali ikiendelea na mikakati ya kuongeza wataalamu katika kada muhimu, ikiwemo huduma za mama na mtoto pamoja na matibabu ya saratani.

Fri, 06 Nov 2026 16:39:41 +0000
Uncategorized · The Observer Uganda

Man who defrauded NBS journalist of Shs 55 in a bogus land deal convicted

Buganda Road Chief Magistrate’s court has convicted Moses Mugalya on three counts of forgery, uttering false documents, and defrauding an NBS TV journalist of Shs…

Recently

Page 342 of 1148 · 22951 stories