Search the region
22965 stories
Govt, PPP projects open doors to jobs and economic growth
DAR ES SALAAM: TANZANIA is banking on investment, infrastructure development and private-sector expansion to turn the ambitions of Dira 2050…
RecentlyREA YAAHIDI KUENDELEA KUSIMAMIA FEDHA ZA MIRADI KULETA MATOKEO YALIKUSUDIWA
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuimarisha ushirikiano na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha fedha zinazotolewa na Wabia wa Maendeleo zinatumika kutekeleza miradi ya nishati yenye tija kwa wananchi, sambamba na kufanikisha malengo ya Serikali katika kuboresha huduma za kijamii na kukuza uchumi wa wananchi. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Said, wakati wa ziara ya Wabia wa Maendeleo katika Sekta ya Nishati walipotembelea kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na REA katika Visiwa vya Chole, Juani na Jibondo mkoani Pwani. Mhandisi Said amesema REA imekuwa na utaratibu wa kufanya vikao hivyo mara mbili kwa mwaka, kikiwemo kikao cha kupanga utekelezaji wa miradi kwa mwaka wa fedha husika na kingine cha kukagua maendeleo ya miradi iliyokubaliwa kwa pamoja, hatua inayowapa wadau wa maendeleo fursa ya kuona matumizi ya fedha zao na matokeo yaliyopatikana kwa wananchi. Amesema ziara hiyo imewawezesha wadau kujionea utekelezaji wa mradi mkubwa na wa kipekee wa kusambaza umeme visiwani kwa kutumia nyaya zinazolazwa chini ya bahari, maarufu kama ‘Submarine Cables’, ambao unatarajiwa kuhudumia takribani vitongoji 11 katika visiwa hivyo, ikiwemo vitongoji sita vya Jibondo, ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Novemba, 2026. Ameongeza kuwa mradi huo ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya umeme, huku akieleza kuwa wadau wa maendeleo wamefurahishwa na maendeleo ya mradi pamoja na ushuhuda wa wananchi kuhusu manufaa ya nishati hiyo katika shughuli za kijamii na kiuchumi. Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Styden Rwebangila, amewataka wananchi wanaonufaika na miradi ya umeme kushiriki kikamilifu katika kulinda miundombinu ya nishati, zikiwemo mashine umba (transfoma) na nguzo, ili kuepusha vitendo vya wizi na uharibifu vinavyoweza kusababisha kukatika kwa huduma kwa muda mrefu. Rwebangila amesema miradi hiyo ni mali ya wananchi, hivyo ni wajibu wa jamii kushirikiana na viongozi wa serikali za vijiji katika kuhakikisha miundombinu inalindwa ili Serikali iweze kuendelea kuwafikia wananchi wengine ambao bado hawajapata huduma ya umeme. Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu, amesema REA imetoa shilingi bilioni 6.8 kwa ajili ya kufanikisha mradi wa kupeleka umeme katika maeneo hayo ya visiwani. Amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kutumia fursa ya kupatikana kwa umeme kujiandaa kuunganisha huduma hiyo katika nyumba na shughuli zao za uzalishaji, ili kunufaika na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali. Akizungumza kwa niaba ya Wabia wa Maendeleo katika Sekta ya Nishati, Mtaalamu Mwandamizi wa nishati kutoka Benki ya Dunia, Dkt. Rhonda Jordan, amesema wadau wa maendeleo wamefurahishwa na namna wananchi wa Jibondo walivyojiandaa kupokea huduma ya umeme, akieleza kuwa upatikanaji wa nishati hiyo utafungua fursa za kuboresha huduma za afya, kuongeza shughuli za uzalishaji na kukuza uchumi wa eneo hilo. Akizungumzia manufaa ya mradi huo, mkazi wa kisiwa cha Jibondo, Faki Hatibu, amesema upatikanaji wa umeme utachochea kuanzishwa kwa viwanda vidogo vya kuchakata mwani na kuongeza thamani ya mazao ya bahari, ambayo kwa sasa yanachakatwa kwa kutumia teknolojia za kienyeji. Aidha, mkazi mwingine wa Jibondo, Rehema Ngoma, ambaye ni fundi cherehani, amesema upatikanaji wa umeme utarahisisha shughuli zake za ushonaji kwa kutumia mashine za kisasa zinazotumia umeme. Amesema umeme utasaidia kuongeza ufanisi wa kazi, kupunguza gharama za usafiri na kuongeza kipato cha wanawake wanaojishughulisha na shughuli za ujasiriamali katika kisiwa hicho.
Fri, 06 Nov 2026 06:55:12 +0000Hatima ya Lissu leo, hukumu yaanza kusomwa
Soma hapa...
RecentlyKenya: Abagore bashyira umuti wa cetirizine mu gitsina baraburirwa
Abagore bamaze gushyira ibyo binini mu gitsina barasabwa guhita babihagarika, kandi bakagana kwa muganga kugira ngo basuzumwe igihe bibaye ngombwa.
RecentlyAlcaraz into Paris Masters quarters after Berrettini withdraws
Read the full report from the original source.
Recently'We curse them' CJ Koome condemns goon financiers
"The last time I checked, it's a crime against the Rome Statute and against humanity. People get charged with organised crime in International Criminal Court"
RecentlyWhy safe sporting infrastructure is everyone’s responsibility
TANZANIA: BILLIONS of money are being invested in modern sports facilities, providing world-class arenas where athletes perform and supporters unite.…
RecentlyM-Pesa na huduma za intaneti zachochea ukuaji wa biashara ya Vodacom Tanzania katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/27.
Vodacom Tanzania Plc imetoa ripoti yake ya nusu mwaka kwa mwaka wa fedha 2027 ikionesha ongezeko la mapato yatokanayo na huduma kwa asilimia 20.8 hadi Sh trilioni 1.067 huku faida baada ya kodi ikipanda kwa asilimia 182.7 hadi Sh bilioni 117.8. Ukuaji huo katika kipindi cha miezi sita kilichoishia Septemba 30, 2026, umechangiwa na huduma za M-Pesa na data za simu, ambazo mapato yake yameongezeka kwa asilimia 26.2 na 24.6 mtawalia. Idadi ya wateja wa kampuni hiyo imeongezeka kwa asilimia 17 na kufikia milioni 29.2, huku watumiaji wa huduma za data na M-Pesa wakiongezeka kwa asilimia 13.9 na 14.1 mtawalia. Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc Philip Besiimire, alisema matokeo hayo yanaakisi kuongezeka kwa wateja na matumizi ya huduma za kampuni, pamoja na uwekezaji unaoendelea katika mtandao na teknolojia. Aidha katika kipindi hicho, kampuni iliwekeza Sh bilioni 246 kuimarisha miundombinu na kupanua upatikanaji wa huduma za kidijitali na kifedha. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni hiyo, Hilda Bujiku, alisema matokeo hayo yanaonesha uimara wa kifedha wa kampuni, unaotokana na ukuaji wa mapato na faida, pamoja na kuongezeka kwa fedha zinazotokana na shughuli za biashara. Hali hiyo inaiwezesha kampuni kuendelea kugharamia uwekezaji wake katika miundombinu ya mtandao na teknolojia. Soma zaidi: https://vodacom.co.tz/assets/uploads/Vodacom_Tanzania_interim_condensed_consolidated_financial_results_2026_4286e52015.pdf?_gl=1*6qlh5p*_gcl_au*MTA3NzYyMTYwMS4xNzkwODU3NjY1
Fri, 06 Nov 2026 02:30:00 +0000TANZANIA YAFAFANUA MASUALA YA HAKI ZA JAMII NA ARDHI KATIKA BARAZA LA HAKI ZA BINADAMU LA UN
GENEVA, Uswisi: Tanzania imefafanua kuwa mfumo wake wa kisheria hautambui jamii za asili, watu wa asili na ardhi za mababu, ikisisitiza kuwa wananchi wote ni raia wenye haki sawa bila kujali kabila, asili, mila, dini, rangi au hali zao za kijamii. Ufafanuzi huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo, aliyewasilisha hotuba kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu (Universal Periodic Review – UPR) yanayofanyika katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Geneva, Uswisi, Novemba 5, 2026. Katika hotuba hiyo, Profesa Malebo amesema Tanzania ina zaidi ya makabila 120 yanayounda jamii yenye utajiri wa lugha, mila, tamaduni na historia mbalimbali. Amebainisha kuwa jamii za Tanzania zinawakilisha familia kuu nne za lugha za Afrika ambazo ni Khoisan, Cushitic, Bantu na Nilotic, zikiwa na historia tofauti za uhamaji na mwingiliano wa kijamii uliochangia kuunda jamii za sasa. Akifafanua kuhusu utambuzi wa jamii za asili (Indigenous Peoples) na ardhi za mababu (Ancestral Land), amesema Katiba na sheria za ndani za Tanzania hazitambui kundi maalumu la kisheria la watu wa asili wala aina tofauti ya ardhi inayotambulika kisheria kama ardhi za mababu. Amesisitiza kuwa msimamo wa Serikali ni kwamba wananchi wote ni raia wenye haki sawa, bila kujali kabila, asili, mila, dini, rangi au hali zao za kijamii. Katika hotuba hiyo, ameeleza pia muktadha wa kihistoria kuhusu uhamaji wa jamii mbalimbali nchini, ikiwemo Wamasai, na mwingiliano wao na makundi mengine katika maeneo mbalimbali ya Tanzania. Kwa mujibu wa maelezo yaliyowasilishwa, uhamaji wa kihistoria wa Wamasai kuelekea kusini ulihusisha mwingiliano na migogoro kuhusu matumizi ya ardhi na maeneo ya malisho kati ya jamii mbalimbali. Ametaja pia makundi ya Khoisan, Cushitic na Bantu, pamoja na jamii za Wadatoga, akieleza kuwa historia ya makazi na mwingiliano wa jamii hizo ni sehemu ya muktadha wa mijadala kuhusu haki na madai ya ardhi. Kuhusu changamoto zinazohusishwa na masuala hayo, Profesa Malebo amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuzishughulikia kwa kuzingatia misingi ya utawala wa sheria, heshima kwa haki za binadamu na utawala bora, huku ikilinda utu, maisha na mila za wananchi. Katika sehemu nyingine ya hotuba hiyo, ameeleza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi sambamba na kulinda haki za binadamu. Ametaja uhuru wa kujieleza, uhuru wa kutembea na haki ya kukusanyika kwa amani kuwa miongoni mwa haki zinazopaswa kuheshimiwa kwa mujibu wa Katiba na mikataba ya kimataifa na kikanda ambayo Tanzania imeridhia. Aidha, Tanzania imesisitiza umuhimu wa Baraza la Haki za Binadamu kuzingatia misingi ya ulimwengu wote, kutokuwa na upendeleo, usawa na kutobagua katika kushughulikia masuala ya haki za binadamu. Ushiriki wa Profesa Malebo katika ujumbe wa Tanzania unaonesha nafasi ya Tume ya Taifa ya UNESCO katika mijadala ya kimataifa inayohusisha maeneo ya kazi za UNESCO, yakiwemo utamaduni, lugha, urithi wa jamii, mawasiliano na upatikanaji wa taarifa. Kupitia ushiriki huo, Tume inaendelea kushiriki katika mijadala inayolenga kuendeleza uelewa kuhusu umuhimu wa kuhifadhi urithi wa kitamaduni, kuthamini utofauti wa jamii na kukuza heshima kwa haki na utu wa binadamu. Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu (UPR) ni utaratibu wa Umoja wa Mataifa unaofanyika chini ya Baraza la Haki za Binadamu, ambapo nchi wanachama huwasilisha taarifa kuhusu hatua walizochukua katika kukuza na kulinda haki za binadamu, hupokea mapendekezo kutoka kwa nchi nyingine na kueleza hatua wanazokusudia kuchukua katika kuimarisha utekelezaji wa haki hizo.
Fri, 06 Nov 2026 06:44:40 +0000Rigathi Gachagua mourns the passing of elder sister Eunice Nyangari
Read the full report from the original source.
RecentlyGovt pushes modern printing plant to unlock C’s growth potential
DAR ES SALAAM: AS President Dr Samia Suluhu Hassan marks one year since she was sworn in for her current…
RecentlyTanzania targets funding to drive green transition
Country to push for accessible climate finance, adaptation support, technology transfer and climate justice at Antalya conference DAR ES SALAAM:…
RecentlyIndustrial drive hinges on skilled workforce: Experts
Read the full report from the original source.
RecentlyPolice tighten security in Tanzania’s commercial capital ahead of Lissu verdict
Read the full report from the original source.
RecentlyIG Kanja assures Moyale residents of security as thousands flee into Kenya
Read the full report from the original source.
RecentlySoggy affair: Nairobians brave heavy morning rains
Commuters and traffic officers navigated wet roads as Nairobi faced a morning downpour amid above-average rain forecasts.
RecentlyUS judge temporarily blocks Trump's arch project after panel approval
Read the full report from the original source.
RecentlyMtumba model inspires DRC development plans
DODOMA: THE Democratic Republic of Congo (DRC) is looking to Tanzania’s experience in developing the Mtumba Government City as a…
RecentlyNaming traditions delay newborn registration
GEITA: CULTURAL practices surrounding the selection of children’s names are delaying the immediate registration of newborns in health facilities in…
RecentlyBunge approves new sugar industry deal
DODOMA: TANZANIA is set to expand value addition in its sugar industry after National Assembly approved a resolution to ratify…
RecentlyPage 358 of 1149 · 22965 stories