Search the region
22991 stories
NMB YAPATA DOLA MILIONI 30 CHINA KUINUA BIASHARA NDOGO NA ZA KATI.
Benki ya NMB imepata mkopo wa dola za Marekani milioni 30 kutoka Benki ya Maendeleo ya China (CDB) kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa mitaji kwa biashara ndogo na za kati nchini Tanzania. Makubaliano hayo yametiwa saini katika Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam, yakilenga kuchochea ukuaji wa biashara na kuimarisha ushirikiano wa kifedha kati ya Tanzania na China. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, amesema fedha hizo zitaongeza uwezo wa benki kufadhili wafanyabiashara wanaohitaji mitaji ya kupanua shughuli zao. Amesema upatikanaji wa fedha ni muhimu katika kukuza biashara, kuongeza uzalishaji na kuchochea ajira nchini. Zaipuna amesema ushirikiano huo pia utaimarisha huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara na China. Kupitia mfumo wa CIPS, NMB inatoa huduma za malipo kwa sarafu ya China (RMB), akaunti za biashara na ufadhili wa biashara za kimataifa, huku ikiunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na wazalishaji wa China kupitia maonesho ya Canton Fair. Makubaliano hayo yanafikiwa wakati NMB ikiwa imetambuliwa na jarida la Global Finance kuwa Benki Bora kwa Biashara Ndogo na za Kati Tanzania mwaka 2026. Mkopo huo unatarajiwa kuongeza fursa za mitaji kwa wajasiriamali, kuimarisha biashara kati ya Tanzania na China na kuunga mkono utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Thu, 05 Nov 2026 12:04:35 +0000Ubufaransa: Abakozi, abanyeshuri n’izindi nzego bigabije imihanda mu myigaragambyo ikomeye
Abakozi bo mu nzego za Leta n’iz’abikorera, abanyeshuri, urubyiruko n’abageze mu zabukuru bitabiriye imyigaragambyo yabereye mu Bufaransa ku wa 5 Ugushyingo (11) 2026, basaba kongererwa imishahara, kugabanya izamuka ry’ibiciro no kurengera serivisi rusange. Ni mu gihe inzego z’umutekano zari zoherejwe hirya no hino mu gihugu.
Thu, 05 Nov 2026 13:54:31 +0200Kalonzo revives Raila’s Canaan dream during Migori tour
Latest · Politics
RecentlyPerceived socioecomic impacts of corruption
According to the findings, corruption significantly exacerbates poverty and lowers living standards (14.5%) while driving up the overall cost of living (14%)
RecentlyBill seeks to protect independence of official statistics
Read the full report from the original source.
RecentlyKenGen in High Court to stop Sh2.3bn tax on dividend
Read the full report from the original source.
RecentlyABDI AWATAKA VIONGOZI WA CCM RUKWA KULINDA UMOJA NA MSHIKAMANO
Na Jane Mwakyoma, Rukwa NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Abdi Mahamoud Abdi, amewataka viongozi wa chama hicho mkoani Rukwa kulinda na kuendeleza umoja na mshikamano uliopo ndani na nje ya chama ili kuhakikisha unadumu na kurithishwa kwa vizazi vijavyo. Abdi alimeyasema hayo Novemba 5, 2026, alipomwakilisha Mlezi wa CCM Mkoa wa Rukwa, Jamal Kassim Ali, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa kilicholenga kusimamia vikao vya tathmini ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kupitia utekelezaji wa majukumu ya chama na Serikali pamoja na kujadili mapendekezo ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Alisema umoja na mshikamano ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa, hivyo viongozi wa chama na Serikali wanapaswa kuudumisha kupitia utendaji wao wa kila siku. Aidha, aliwashukuru viongozi hao kwa kuendelea kudumisha mshikamano na kuwataka kuulinda Muungano ulioasisiwa na viongozi waasisi wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume. "Kama wasingekuwa viongozi wetu hawa wawili, Mwalimu Nyerere na Rais Karume, nchi hizi mbili zisingekuwa na Muungano huu wala umoja huu. Muungano wa ASP na TANU ndiyo uliofanya CCM kuwa hapa. Nataka kuwaambia kuwa mshikamano ndiyo msingi wetu, hasa kwa nchi yetu," alisema Abdi Alisisitiza kuwa viongozi hao wanapaswa kujiandaa na uchaguzi ndani ya chama kwa kuhakikisha unafanyika kwa amani, utulivu na demokrasia, huku wakiepuka vitendo vinavyoweza kuvuruga umoja uliojengwa ndani ya CCM. "Nataka kuona mshikamano huu mlionionyesha hapa hata baada ya uchaguzi nione ukiendelezwa," alisisitiza. Awali, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, Silafu Maufi, akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu huyo, alisema kikao hicho kililenga kujadili tathmini ya kazi za chama na Serikali pamoja na mapendekezo ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Aliwataka wajumbe wa kikao hicho kujadili na kutathmini ajenda zilizowasilishwa kwa kuzingatia maslahi ya maendeleo ya taifa. Maufi aliongeza kuwa siasa zinapotumika vizuri huwa chachu ya kujenga uchumi na kuleta maendeleo, hivyo viongozi wanapaswa kuzitumia kwa manufaa ya nchi. "Siasa ni uchumi na siasa ni maendeleo, na ndani ya maendeleo kuna siasa," alisema Maufi.
Thu, 05 Nov 2026 11:52:11 +0000Tanzania moves to establish DTI College to advance digital technology profession
DAR ES SALAAM: TANZANIA is set to establish a Digital Technology Institute (DTI) in Dodoma at a cost of more…
RecentlyVijana waomba ushiriki ngazi za maamuzi
Read the full report from the original source.
RecentlyRonaldo announces retirement from Portugal
Latest · Football
RecentlyYas pledges continued support for Zanzibar health camps
ZANZIBAR: Yas Tanzania has pledged continued support for health camps organised by the Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), helping more…
RecentlyMTN Uganda’s nine months of 2026: the good, the cautious and the worrying
Read the full report from the original source.
RecentlyVIWANDA VYA NDANI KUWA CHACHU YA AJIRA NA UCHUMI JUMUISHI-TEMDO.
Kuimarika kwa uzalishaji wa bidhaa nchini kunatarajiwa kuwa miongoni mwa nguzo muhimu za kukuza uchumi jumuishi, kupanua fursa za ajira na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na nje ya nchi, kupitia utekelezaji wa sera mpya ya Maendeleo Endelevu ya viwanda na sera ujasiriamali Ndogo na za kati ya mwaka 2003 Toleo la mwaka 2025. Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) Eng. Profesa Frederick C. Kahimba, amesema sera hizo zimeweka msingi wa kuimarisha uwezo wa viwanda vya ndani kuchakata malighafi zinazopatikana nchini na kuzibadilisha kuwa bidhaa zenye thamani hatua itakayosaidia kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa taifa. Akizungumza mara baada ya hafla ya uzinduzi wa sera hizo, Kahimba amesema maendeleo ya viwanda yana nafasi kubwa katika kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira, akitoa mfano wa viwanda vikubwa vya nguo ambavyo vina uwezo wa kuajiri maelfu ya Watanzania na kuchochea shughuli nyingine za kiuchumi. Amesema kuongeza uzalishaji wa bidhaa zinazotengenezwa nchini kutasaidia kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje, kulinda ajira za ndani na kupunguza matumizi ya fedha za kigeni, huku uzalishaji wa ziada ukifungua fursa za kuuza bidhaa za Tanzania katika masoko ya kimataifa. Akifafanua mchango wa taasisi anayoiwakilisha katika kukuza sekta hiyo, Kahimba amesema ina majukumu ya kufanya tafiti za teknolojia za viwandani, kutoa huduma za kihandisi kwa viwanda, kuandaa mafunzo ya kitaalamu na kubuni teknolojia zinazoongeza thamani ya mazao na bidhaa mbalimbali. Ameeleza kuwa teknolojia hizo zinahusisha sekta za kilimo, mifugo, madini na afya, kwa lengo la kuongeza tija na kujenga uwezo wa kutumia rasilimali zilizopo nchini kuzalisha bidhaa zenye thamani zaidi. Aidha, amewahimiza Watanzania kuunga mkono bidhaa zinazozalishwa nchini kwa kuzitumia na kuziamini, akisisitiza kuwa mafanikio ya sera hizo yanahitaji ushirikiano wa Serikali, sekta binafsi, wajasiriamali na wananchi katika kujenga viwanda imara vitakavyopanua ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi. Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) inabuni na kutengeneza mashine mbalimbali za kusaidia uzalishaji na kuongeza thamani ya malighafi, miongoni mwa mashine hizo ni za kukamua mafuta ya alizeti, kusindika matunda, kupukuchua mahindi, kusindika maziwa na asali, kutengeneza chakula cha mifugo na kuchakata ngozi, pia hutengeneza vifaa tiba kama vitanda vya wagonjwa, kwa lengo la kupunguza gharama za uzalishaji na kukuza viwanda vya ndani.
Thu, 05 Nov 2026 11:32:58 +0000MoH warns against misuse of cetirizine for vaginal wellness
Read the full report from the original source.
RecentlyTFS YAIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA KWA WATUMISHI WAKE.
Naibu Kamishna na Mkurugenzi wa Mipango na Masoko wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Salehe Beleko, amesema kutoa elimu kwa watumishi wa Wakala huo kuhusu madhara ya rushwa, hatua za kukabiliana nayo, sambamba na kuimarisha maadili, uwajibikaji na uadilifu katika utendaji kazi, utaongeza uelewa na kuimarisha uwezo wa watumishi katika kupambana na vitendo vya rushwa. Akizungumza katika semina ya maadili na mapambano dhidi ya rushwa kwa watumishi wa TFS jijini Dodoma, Beleko amesema pamoja na elimu inayotolewa lakini bado mapambano dhidi ya rushwa yanahitaji kuendelea kuimarishwa kupitia mafunzo na usimamizi wa utekelezaji wa miongozo iliyopo, ameeleza kuwa TFS ina utaratibu wa kuchukua hatua kali kwa watumishi watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa. Aidha, amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kupata huduma kwa kufuata taratibu zilizowekwa na Serikali bila kulazimishwa kutoa fedha au rushwa ya aina yoyote, huku watumishi wakitakiwa kutoa taarifa sahihi kuhusu upatikanaji wa huduma na muda wa kuzitoa. Kwa upande wake, Askari Daraja la Pili Jesicka Michael, amesema elimu ya kuzuia na kupambana na rushwa inapaswa kuendelea kutolewa kwa jamii ili kuwajengea wananchi uelewa na kuwahamasisha kutoshiriki vitendo hivyo, akisisitiza kuwa rushwa ni adui wa haki. Naye Askari Mhifadhi Daraja la Pili wa TFS, Godfrey Raphael Mbazo, amesema mafunzo hayo yamemwongezea uelewa kuhusu maana ya rushwa, madhara yake na namna ya kukabiliana nayo, jambo litakalomsaidia kutekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria bila upendeleo wala kushawishiwa na rushwa, amewataka watumishi wa umma kuzingatia sheria na viapo vyao vya kazi, kufanya kazi kwa uadilifu na kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya rushwa. Semina hiyo iliyoanza Novemba 2 na kufungwa rasmi Novemba 3, 2026, ni sehemu ya juhudi za TFS kuimarisha maadili, uwajibikaji na mifumo ya kuzuia na kupambana na rushwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya uhifadhi wa misitu nchini.
Thu, 05 Nov 2026 11:28:57 +0000UN peacekeeping chief warns of ‘security vacuum’ as Blue Helmets leave Lebanon and Western Sahara
Read the full report from the original source.
RecentlyBugema University Set to Hold 32nd Graduation Weekend Under Theme “Running the Race with Endurance
Read the full report from the original source.
RecentlyRESCUE ME YOUR EXCELLENCY! Desperate Elderly Mother Cries Out to Museveni as Rogue RDC Son Drives Her Out of Family House
Read the full report from the original source.
RecentlyKinatwa Sacco faces inquiry into debts, assets and management
Corporate · Quick read
RecentlyBENKI YA CRDB, BENKI YA MAENDELEO YA CHINA KUCHOCHEA UTEKELEZAJI WA MIRADI MIKUBWA YA KIMKAKATI NA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050
Benki ya CRDB imesaini makubaliano ya kimkakati ya ushirikiano na Benki ya Maendeleo ya China (China Development Bank – CDB), yanayofungua fursa za ufadhili wa miradi mikubwa ya kimkakati, uwekezaji na maendeleo ya sekta muhimu za uchumi, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Ushirikiano huo pia unalenga kuimarisha biashara kati ya Tanzania na China, ambayo thamani yake inatarajiwa kuvuka Shilingi trilioni 31 mwaka 2026. Makubaliano hayo yanafungua fursa za ufadhili katika sekta za nishati, madini, viwanda, biashara ndogo na za kati, pamoja na miradi ya maendeleo endelevu. Miongoni mwa miradi inayotazamwa kunufaika na fursa za ushirikiano huo ni ujenzi wa Kituo cha Kuhifadhi na Kuchakata Taarifa (Data Centre) Zanzibar na mradi wa kufufua na kuboresha Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA). Hafla ya utiaji saini iliyofanyika katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa benki hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Prof. Neema Mori, ambaye ameeleza kuwa ushirikiano huo ni hatua muhimu katika kuimarisha nafasi ya Benki ya CRDB kama mshirika wa kimkakati katika maendeleo ya Taifa, hususan katika kuvutia mitaji ya kimataifa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa itakayochochea mageuzi ya kiuchumi. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Nsekela, amesema ushirikiano huo unafungua ukurasa mpya wa fursa za uwekezaji kwa kuunganisha mitaji ya kimataifa na mahitaji ya maendeleo nchini, huku ukitarajiwa kuchochea ukuaji wa viwanda, kuongeza ajira, kuimarisha miundombinu na kukuza ushindani wa Tanzania katika biashara za kikanda na kimataifa, na kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Naye Rais wa Benki ya Maendeleo ya China, Huang Zhiqiang, ameeleza kuwa ushirikiano huo unaimarisha uhusiano wa kifedha na kiuchumi kati ya Tanzania na China, huku ukifungua fursa za kuendeleza miradi yenye tija na uwekezaji wa muda mrefu utakaonufaisha wafanyabiashara na wananchi wa nchi zote mbili.
Thu, 05 Nov 2026 11:23:59 +0000Page 374 of 1150 · 22991 stories