Unganishwa

Search the region

23013 stories

Uncategorized · The Citizen

Mwigulu urges Tanzanians to prioritise locally made goods

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

M-Pesa, Ethiopia operations push Safaricom half-year profit to Sh58.2bn

Latest · Business

Recently
Uncategorized · Daily News

Kilindo answers VP’s call, backs UDSM Outsiders

DODOMA: UDSM Outsiders have become the first basketball team to announce sponsorship ahead of the 2026 National Basketball League (NBL),…

Recently
Uncategorized · Daily News

NSC opens applications for TPBRC leadership positions

DAR ES SALAAM: THE National Sports Council of Tanzania (NSC) has opened applications for leadership positions at the Tanzania Professional…

Recently
Business · Issa Michuzi

WANUFAIKA WA TUINUKE PAMOJA WANUFAIKA NA FURSA ZA KUKUZA BIASHARA

Mratibu wa Mradi wa Tuinuke Pamoja kutoka Shirika la Aga Khan Foundation, Magreth Lushakuzi, amewahimiza wajasiriamali na vikundi vya wanufaika wa mradi huo katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Dodoma, kutumia maonesho ya biashara yanayofanyika katika maeneo mbalimbali nchini kama fursa ya kutafuta masoko, kujifunza teknolojia mpya na kupanua shughuli zao za biashara. Akizungumza Novemba 4, 2026, jijini Dodoma, amesema ushiriki wa vikundi hivyo katika Maonesho ya Bidhaa za Viwanda na Biashara umeviwezesha kukutana na wajasiriamali wengine, viongozi wa Serikali na kampuni zinazotengeneza mashine na vifaa vya uzalishaji, hivyo kupata maarifa na fursa za kuboresha bidhaa na kuongeza uwezo wa uzalishaji. Amesema kupitia Mradi wa Tuinuke Pamoja unaofadhiliwa na Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania, Aga Khan Foundation inalenga kuwawezesha wanawake kiuchumi katika ngazi ya jamii kupitia kuwajengea uwezo na kuimarisha shughuli zao za kiuchumi, huku akiwataka wanufaika kutumia elimu na mitandao waliyoipata kukuza biashara zao na kujenga ujasiriamali endelevu. Kwa upande wake, mnufaika wa Mradi wa Tuinuke Pamoja na mwakilishi wa Kikundi cha Kondoa Women Group mkoani Dodoma, Haruna Makunga, amesema ushiriki wao katika maonesho hayo umewapa fursa ya kutangaza bidhaa zao, kujifunza mbinu za kuboresha uzalishaji na kufahamu taratibu za usajili na viwango vya ubora ili kuongeza ushindani na kupanua wigo wa biashara zao. Naye mnufaika wa mradi huo kutoka Kikundi cha JUWACHA kilichopo Chamwino Ikulu, amesema mafunzo waliyopata kupitia mradi huo yamewawezesha kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, ikiwemo kujifunza uzalishaji wa mafuta ya mimea. Ameishukuru Serikali kwa kuwapa wakulima wadogo fursa ya kuonesha bidhaa zao na kujifunza kutoka kwa wajasiriamali wengine. Aidha, Halima Salim Fundi, mwanakikundi wa Tujikomboe Makamaka Women Group, ameishukuru Aga Khan Foundation kwa kuwawezesha kushiriki maonesho hayo, akisema yamewapa fursa ya kujifunza mbinu mpya za kukuza biashara na kuboresha bidhaa zao ili ziweze kushindana katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Maonesho hayo yamefanyika sambamba na uzinduzi wa Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda ya Mwaka 2025 na Sera ya Maendeleo ya Wajasiriamali Ndogo na wa Kati ya Mwaka 2003 (Toleo la Mwaka 2025), ambazo zimezinduliwa rasmi Novemba 4, 2026, jijini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba. Sera hizo zinalenga kuimarisha uzalishaji, kuongeza thamani ya malighafi za ndani, kuboresha upatikanaji wa mitaji na masoko pamoja na kukuza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Thu, 05 Nov 2026 07:21:02 +0000
Uncategorized · The Star Kenya

Kiswahili Lugha, Insha on schedule as KCSE enters day 4

Candidates will sit two Kiswahili papers as examination authorities maintain heightened surveillance to guard against malpractices.

Recently
Uncategorized · Daily News

Arajiga selected for CAF elite referees’ seminar

DAR ES SALAAM: TANZANIAN referee Ahmed Arajiga has been selected by the Confederation of African Football (CAF) to attend a…

Recently
Uncategorized · Daily News

Food security demands more than bumper harvests

ARUSHA: TANZANIA is strengthening efforts to achieve sustainable food security through improved seed varieties, agricultural innovation, stronger extension services and…

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

PSSSF YAKABIDHI MIRADI YA MAJI SHULE MBILI DODOMA

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Ally Akida (Wapili kushoto), Meneja wa Mfuko wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw. Lulyalya Sayi (Wanne kushoto), na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kimaghai A, Bi. Eudia Medaa (Watano kushoto) na baadhi ya viongozi wa wilaya na walimu wa shule hiyo, wakiungana kuzindua, mradi wa maji uliofadhiliwa na Mfuko wa PSSSF katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika shuleni hapo Novemba 4, 2026. Meneja wa Mfuko wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw. Lulyaya Sayi (Aliyesimama) akizungumza katika hafla ya kukabidhi mradi wa kisima Cha maji katika Shule ya Sekondari Kimaghai A, Wilayani Mpwapwa jijini Dodoma Novemba 4, 2026. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Bw, Ally Akida (Aliyesimama) akizungumza katika hafla ya kukabidhi mradi wa kisima Cha maji uliofadhiliwa na Mfuko wa PSSSF katika Shule ya Sekondari Kimaghai A, jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika Novemba 4, 2026. Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw, Lulyaya Sayi, Kaimu Afisa Elimu wa Halmashauri ya mji Dodoma Bw, Yasin Mponda, Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru wakishuhudia uwepo wa maji kwa uhakika baada ya kukamilika kwa mradi huo katika Shule ya Msingi Uhuru. Picha ya pamoja ikionyesha Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw. Lulyaya Sayi, Kaimu Afisa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Dodoma, Bw. Yassin Mponda, Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru, Bi. Agatha Mosha, pamoja na watumishi, wazazi, na wanafunzi waliohudhuria katika uzinduzi wa mradi wa maji katika Shule ya Msingi Uhuru. Kaimu Afsa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Dodoma, Bw, Yasin Mponda akizungumza katika hafla ya kukabidhi mradi mradi wa kisima Cha maji katika Shule ya Msingi Uhuru, Dodoma. Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw, Lulyaya Sayi akizungumza katika hafla ya kukabidhi mradi wa kisima Cha maji katika Shule ya Msingi Uhuru. *Miradi Kunifaisha zaidi ya Watu 1000 *Wanafunzi Waanzisha Bustani Kuboresha Lishe Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umekabidhi miradi miwili ya visima vya maji vyenye thamani ya Shilingi milioni 55 katika Shule ya Sekondari Kimaghai, Mpwapwa, na Shule ya Msingi Uhuru, jijini Dodoma, inayotarajiwa kunufaisha zaidi ya watu 1,000. Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa Kimaghai A, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Ally Akida, aliishukuru PSSSF kwa kutatua changamoto ya muda mrefu ya maji, akieleza kuwa mradi huo utanufaisha zaidi ya watu 600. Naye Kaimu Afisa Elimu wa Jiji la Dodoma, Bw. Yasin Mponda, aliipongeza PSSSF kwa kukubali ombi la Shule ya Msingi Uhuru, akieleza kuwa Mfuko umeifanya shule hiyo kujiona inathaminiwa. Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru, Bi. Agatha Mosha, aliishukuru PSSSF kwa mradi huo ambao umewezesha kuanzishwa kwa kilimo cha mbogamboga kwa ajili ya kuboresha lishe ya wanafunzi na unatarajiwa kunufaisha zaidi ya watu 500. Makabidhiano ya miradi hiyo yalifanyika tarehe 3 na 4 Novemba 2026, yakiongozwa na Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw. Lulyaya Sayi, aliyewataka wanafunzi, walimu na wananchi kutunza visima na miundombinu yake ili iendelee kutoa huduma kwa muda mrefu.

Thu, 05 Nov 2026 07:13:08 +0000
Business · Issa Michuzi

WMA: VIPIMO SAHIHI NI MSINGI WA MAFANIKIO YA SERA ZA VIWANDA NA UJASIRIAMALI

Na. WMA - DODOMA, Wakala wa Vipimo (WMA) imesema matumizi ya vipimo sahihi ni msingi muhimu wa kuimarisha uzalishaji viwandani, kulinda haki za wafanyabiashara na walaji, na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na nje. Kauli hiyo imetolewa wakati wa uzinduzi wa Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda ya Mwaka 2025 na Sera ya Maendeleo ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati ya Mwaka 2003 (Toleo la 2025), uliofanywa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC), jijini Dodoma. Akizungumza katika tukio hilo, Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Bw. Alban Kihulla, amesema vipimo sahihi vinajenga uaminifu katika biashara kwa kuhakikisha wanunuzi wanapata kiasi cha bidhaa kinacholingana na thamani ya fedha wanazolipa. Amesema WMA inatekeleza jukumu hilo kwa kukagua bidhaa zilizofungashwa zinazozalishwa nchini pamoja na zinazoagizwa kutoka nje ya nchi kupitia bandari na vituo vya mipakani, ili kuhakikisha kuwa uzito au ujazo ulioainishwa kwenye vifungashio unalingana na kiasi halisi cha bidhaa kilichomo. “Mnunuzi wa ndani au wa nje ya nchi anapochukua bidhaa yenye nembo ya Made in Tanzania, anatakiwa kupata kile hasa kilichoandikwa kwenye kifungashio. Hiyo ndiyo kazi yetu, na ndiyo sababu tunaziona sera hizi kama fursa ya kuimarisha imani kwa bidhaa za Kitanzania,” amesema Bw. Kihulla. Ameeleza kuwa WMA pia hushirikiana na taasisi na mashirika ya vipimo ya kikanda na kimataifa katika kuimarisha ulinganifu wa vipimo na kusaidia kupunguza vikwazo vya biashara vinavyohusiana na vipimo. Akizungumzia biashara ya mazao, amesema WMA inaendelea kuhakiki mizani inayotumika katika vituo vya ununuzi na viwanda vya usindikaji ili kuhakikisha wakulima wanapimiwa kwa usahihi na kulipwa kulingana na uzito halisi wa mazao yao. “Mkulima anapouza korosho, kahawa au pamba, mizani inayotumika lazima iwe sahihi ili alipwe kwa uzito halisi wa mazao yake. Tunaendelea kuhakiki mizani katika vituo vya ununuzi na viwanda vya usindikaji, na kupambana na ufungashaji wa lumbesa unaomnyima mkulima haki yake,” amesema. Kwa upande wa wajasiriamali wadogo na wa kati, amesema matumizi ya vipimo sahihi huwasaidia kufungasha bidhaa kwa kiasi kilichoainishwa, kudhibiti upotevu na kujenga uaminifu kwa wateja. Amesema WMA inaendelea kutoa elimu kupitia njia mbalimbali, zikiwemo redio na televisheni, ili kuwawezesha wajasiriamali na wafanyabiashara kuelewa na kuzingatia matakwa ya vipimo katika shughuli zao. Wakala pia hutumia klabu za vipimo mashuleni kujenga uelewa wa matumizi ya vipimo sahihi tangu umri mdogo. Aidha, amesema ukuaji wa viwanda na uwekezaji unaongeza mahitaji ya huduma za vipimo, ikiwemo uhakiki wa mizani, mita za umeme na mita za gesi asilia, pamoja na idhini za miundo ya vipimo vinavyokusudiwa kutumika katika shughuli zinazodhibitiwa kisheria. Ameongeza kuwa WMA inaendelea kuboresha mifumo ya kidijitali ili kurahisisha upatikanaji wa huduma, sambamba na kuimarisha ukaguzi wa bidhaa zinazozalishwa nchini na zinazoagizwa kutoka nje, pamoja na uhakiki wa vipimo vinavyotumika viwandani na katika biashara. “Tunawaomba wananchi wahakikishe mizani na vipimo wanavyotumia vina alama ya uhakiki ya WMA, na watoe taarifa pale wanapoona kipimo kisicho sahihi. Kipimo sahihi ni haki ya kila mwananchi,” amesisitiza. WMA ni miongoni mwa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara zilizoshiriki maonesho na kongamano lililoambatana na uzinduzi huo. Wananchi na wafanyabiashara waliotembelea banda la Wakala walipata elimu kuhusu matumizi ya vipimo sahihi na huduma zinazotolewa na WMA. Sera hizo zinalenga kuimarisha maendeleo ya viwanda na ujasiriamali kwa kuongeza uzalishaji, thamani ya malighafi za ndani, fursa za ajira na upatikanaji wa mitaji na masoko kwa wajasiriamali, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Thu, 05 Nov 2026 07:15:52 +0000
Uncategorized · Daily News

Who dares wins: LPG, the next frontier for Africa’s downstream

AT the IEA’s first Summit on Clean Cooking in Africa in Paris in May 2024, Akinwumi Adesina, then African Development…

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

What the Democrats' midterms win means for the US economy and Trump

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KBC

Vaginal tightening: Pharmacists warn against cetirizine misuse amid high demand

PSK also noted reports of increased demand, price rises and stock shortages in some outlets

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Recruitment agency director charged with swindling Ksh.20M from UK job seekers

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Antonelli back to work as Mercedes chase title double

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Trans Nzoia county leads in TFGBV cases as most perpetrated on Facebook

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Man arrested for impersonating cops on Jogoo Rd

When confronted, he introduced himself as a sergeant attached to the General Service Unit (GSU) Training School

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

CHOGM 2026 opens with drive to unlock prosperity for Commonwealth’s 2.7 billion people

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Types of press freedom violations recorded

The report, covering July to September 2026, lists 34 cases of assault, followed by five threats

Recently
National · Issa Michuzi

JESHI LA POLISI ULANGA LAENDELEA KUIMARISHA UHUSIANO, WANANCHI KITUTI WAITIKA KUPITIA KAMPENI YA 'ONGEA NA KAMANDA'

Jeshi la Polisi Wilaya ya Ulanga limeendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati yake na wananchi kupitia programu ya “Ongea na Kamanda” iliyofanyika katika Kijiji cha Kituti, Kata ya Ruaha, wilayani Ulanga, Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kujenga jamii yenye uelewa wa mambo ya amani na usalama pamoja na kuzuia vitendo vya uhalifu. Akitoa Elimu hiyo, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ulanga, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Deogratius Challe, alieleza maana na malengo ya kampeni hiyo, akisisitiza umuhimu wa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kudumisha usalama na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa wakati ili hatua sitahiki ziwezekuchukuliwa kwa wakati. Katika programu hiyo, wananchi walipatiwa elimu mbalimbali kuhusu utii wa sheria bila shuruti, usalama migodini, utunzaji wa fedha, ukatili wa kijinsia, utunzaji wa eneo la tukio la uhalifu, utoaji wa taarifa za uhalifu. Aidha Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Polisi Wilaya akatumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi wanaomiliki silaha kinyume na utaratibu kusalimisha silaha hizo katika vituo vya Polisi na ofisi za serikali za vijiji huku akiwakumbusha na tahadhari dhidi ya mvua za El Niño. Licha ya ananchi walilipongeza Jeshi la Polisi kwa juhudi zake za kuimarisha usalama na kudumisha amani katika jamii wananchi hao, wameliomba Jeshi hilo kuendelea kutoa elimu ili kuwajengea uelewa Juu ya mambo ya kiusalama. Kwa ujumla, programu ya “Ongea na Kamanda” imeendelea kuwa jukwaa muhimu la mawasiliano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi, likichochea ushirikiano katika kuzuia uhalifu, kutatua changamoto za kiusalama na kujenga jamii yenye amani, utulivu na usalama.

Thu, 05 Nov 2026 07:00:49 +0000

Page 383 of 1151 · 23013 stories