Search the region
23057 stories
WAZIRI MKUU DRC AVUTIWA NA MAENDELEO YA TANZANIA, ASISITIZA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI NA USALAMA
Na Janeth Raphael - MichuziTv Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Judith Suminwa Tuluka, amepongeza ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na nchi yake, huku akiishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na DRC katika masuala ya usalama na maendeleo ya kiuchumi. Akizungumza Novemba 4, 2026, baada ya kutembelea Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma, Tuluka amesema Tanzania na DRC zina uhusiano wa kihistoria unaotokana na undugu na ujirani mwema, hivyo ni muhimu kwa mataifa hayo kuendelea kuimarisha mshikamano na ushirikiano katika maeneo yenye maslahi ya pamoja. Ameeleza kuwa ushirikiano huo una mchango mkubwa katika kulinda usalama wa nchi hizo na kuchochea maendeleo ya kiuchumi, ikiwemo kuboresha miji na mazingira ya maisha ya wananchi. Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi wa DRC, John Banza Lunda, amesema amevutiwa na hatua kubwa ambazo Tanzania imepiga katika sekta ya miundombinu, akibainisha kuwa ziara yake imemwezesha kujionea uwekezaji uliofanywa na Serikali katika miundombinu ya usafiri na majengo ya umma. Amesema safari yake kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma imempa nafasi ya kushuhudia maendeleo ya miundombinu, ikiwemo majengo ya Bunge na Mji wa Serikali wa Mtumba, ambayo ni sehemu ya uwekezaji unaochochea ukuaji wa uchumi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Aidha, Banza Lunda amesema DRC inaendelea na mikakati ya kuimarisha miundombinu yake ili kukuza shughuli za kiuchumi na kijamii, huku akieleza kuwa nchi hiyo inatekeleza mradi wa ujenzi na uendelezaji wa bandari katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, inayotarajiwa kuanza kufanya kazi Machi 2027. Amesema bandari hiyo itarahisisha usafirishaji wa bidhaa na kukuza biashara katika maeneo yanayozunguka ziwa hilo. Ameongeza kuwa anatarajia kutumia Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kurejea Dar es Salaam ili kujionea zaidi uwekezaji wa Tanzania katika sekta ya usafiri wa reli, huku akiishukuru Serikali ya Tanzania na Rais Samia kwa ukarimu na mapokezi mazuri waliyoyapata. Naye Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, amesema Tanzania imefurahi kupokea ujumbe wa DRC katika ziara hiyo ya kindugu na kirafiki, ambayo inalenga kuendeleza uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya mataifa hayo mawili. Amesema uhusiano wa Tanzania na DRC umejengwa katika misingi ya historia ya pamoja, undugu na ujirani mwema, hivyo ziara hiyo ni fursa muhimu ya kuendeleza urafiki na kuimarisha ushirikiano uliopo. Kairuki ameongeza kuwa Tanzania inathamini uhusiano wake na DRC na itaendelea kuweka mazingira mazuri yatakayowezesha mataifa hayo kushirikiana katika sekta mbalimbali. Amesisitiza kuwa ziara za viongozi na ujumbe wa mataifa hayo zina umuhimu mkubwa katika kuimarisha mshikamano, kufungua fursa mpya za ushirikiano na kuhakikisha wananchi wa pande zote mbili wananufaika na mahusiano hayo, hususan katika maeneo ya maendeleo ya kiuchumi, miundombinu na ustawi wa jamii.
Wed, 04 Nov 2026 16:49:53 +0000High Court outlaws corporal punishment in schools
Read the full report from the original source.
RecentlyGishubi : arrestations politiques ou affaire sécuritaire ?
Read the full report from the original source.
RecentlyFarouk Ibrahim is learning to build what people actually need
Read the full report from the original source.
RecentlyTenerife, Andorra matches postponed after De Miguel tragedy
Read the full report from the original source.
RecentlyCA targets network blackspots ahead of 2027 polls
The move is aimed at ensuring the IEBC has reliable internet connectivity to transmit results and help officials locate polling centres across the country
RecentlyWorld Bank says Kenya overpaid Sh117bn for Mombasa-Naivasha SGR
Read the full report from the original source.
RecentlyBABA LEVO AIPONGEZA SERIKALI KWA VIWANJA, ATAKA HOJA ZA CAG ZIFANYIWE KAZI
Na Janeth Raphael - MichuziTv Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mhe. Clayton Revocatus Chipando, maarufu kama Baba Levo, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuboresha na kujenga viwanja vya kisasa vya michezo nchini. Akichangia hoja bungeni, Baba Levo amesema uwekezaji unaofanywa na Serikali katika miundombinu ya michezo ni hatua muhimu itakayoiwezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano mbalimbali ya kimataifa. Amesema viwanja hivyo vitakuwa na mchango mkubwa katika maandalizi na kufanikisha mashindano yanayotarajiwa kufanyika nchini mwaka 2027, sambamba na matukio mengine makubwa ya michezo yatakayofuata. Mbunge huyo amesema ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya michezo unaonesha dhamira ya Serikali ya kuikuza sekta hiyo na kuweka mazingira bora kwa wanamichezo kushiriki na kufanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa. Katika mchango wake, Baba Levo pia amesisitiza umuhimu wa wabunge kujadili kwa kina hoja na mapendekezo yanayotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Amesema mjadala wa hoja hizo utawasaidia wananchi kufahamu namna wawakilishi wao wanavyosimamia matumizi ya fedha za umma, pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yanayotolewa katika taarifa za ukaguzi. Baba Levo ameongeza kuwa wabunge wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha hoja zinazobainishwa na CAG zinapatiwa ufumbuzi na hatua stahiki zinachukuliwa, ili kuimarisha uwajibikaji na kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa ufanisi na kwa manufaa ya wananchi.
Wed, 04 Nov 2026 16:43:22 +0000MATIKO AIBUA HOJA YA BILIONI 13.88 ZA MIKOPO YA ASILIMIA 10% ZISIZOWAFIKIA WALENGWA
Na Janeth Raphael – MichuziTv Bungeni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Esther Matiko, amehoji hatima ya Shilingi Bilioni 13.88 zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri, akitaka Serikali kueleza fedha hizo zilipoelekezwa baada ya kubainika kuwa hazikuwafikia walengwa waliokusudiwa. Matiko ameeleza kuwa fedha hizo zilipaswa kuwanufaisha makundi maalumu ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kupitia mfumo wa mikopo inayotolewa na Halmashauri, lakini ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeibua hoja kuhusu kutofikishwa kwa fedha hizo kwa walengwa. Akichangia hoja bungeni jijini Dodoma leo, Novemba 4, 2026, Matiko amesema hali hiyo inahitaji maelezo ya kina kutoka Serikalini, kwa kuwa fedha hizo zilitengwa kwa lengo maalumu la kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuwasaidia kuanzisha au kuendeleza shughuli za uzalishaji mali. Amesisitiza kuwa sheria inayosimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa inaelekeza Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya makundi hayo, hivyo ni muhimu kuhakikisha matakwa ya sheria yanafuatwa na fedha zinawafikia walengwa bila kugeuzwa matumizi mengine. Katika kauli yake, Matiko amekosoa utaratibu wa kuelekeza fedha hizo kwenye matumizi mengine kupitia mabadiliko ya bajeti (reallocation), akisisitiza kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya makundi maalumu hazipaswi kuhamishiwa kwenye shughuli zisizokuwa na uhusiano na madhumuni yake. Amesema Serikali inapaswa kuweka wazi sababu zilizosababisha Shilingi Bilioni 13.88 kutowafikia wanufaika, pamoja na kuchukua hatua kuhakikisha fedha za mikopo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kuwafikia vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Hoja ya Matiko inalenga kuimarisha uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za umma, hususan mikopo ya asilimia 10 inayotarajiwa kuwa chachu ya kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuongeza fursa za kujiajiri kupitia shughuli mbalimbali za maendeleo.
Wed, 04 Nov 2026 16:45:24 +0000Comment le riz peut aider à construire les maisons du futur
La balle de riz est un résidu agricole particulièrement problématique pour l'environnement ; elle est toutefois désormais transformée en un matériau de construction solide et résistant.
RecentlyLes habitants de Bugarama saluent les actions de la Coopérative « Twijukire Uburimyi n’Ubworozi vyo soko ry’iterambere »
Read the full report from the original source.
RecentlyHelium Health secures $2.5 million Google grant to tackle maternal deaths with AI
Read the full report from the original source.
RecentlyA new dawn? Kenya launch ambitious strategy to revolutionise women’s football
Latest · Sports
RecentlyDKT. MWIGULU AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA DRC
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemkorasi ya Kongo (DRC), Judith Suminwa Tuluka na wamejadiliana njia mbalimbali za kuimarisha uchumi baina ya nchi hizo mbili. Katika mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma leo (Jumatano, Novemba 04, 2026), Dkt, Mwigulu amesema Tanzania na DRC zina fursa ya kukuza ushirikiano wa kiuchumi katika nyanja mbalimbali ikiwemo madini, usafirishaji na uchukuzi, chakula na utoaji wa huduma za afya. “Bado kuna fursa kubwa ya kukuza ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa yetu mawili. Kama ujuavyo, Tanzania na DRC ni mataifa yaliyobarikiwa kuwa na utajiri mkubwa, ikiwemo madini, ardhi yenye rutuba, misitu, maziwa na mito.” Akielezea uwepo wa fursa za kibiashara, Waziri Mkuu Mwigulu amesema nchi hizo bado zinaweza kuongeza kiwango cha sasa cha biashara ikiwa watahamasisha sekta binafsi kutumia fursa zinazotolewa na mifumo ya kikanda na ya bara. “Tanzania na DRC tuna nafasi chanya nyingi za kufanya biashara zaidi. Tutawatuma mawaziri wa sekta zinazohusika ili waendelee kukutana na kukamilisha hayo masuala,” amesema. Dkt. Mwigulu amesema DRC ni mtumiaji namba moja wa Bandari ya Dar es Salaam, ikiwa na mchango wa asilimia 48 ya shehena yote ya mizigo ya nchi zisizo na bandari na akatumia fursa hiyo kumpongeza Waziri Mkuu wa DRC kwa kutenga muda na kutembelea bandari hiyo. “Nimefurahi kwenye ziara hii umepata fursa ya kutembelea Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu ya Kwala, ambako tumetoa eneo kubwa kwa DRC. Kipekee nitumie fursa hii kuipongeza Serikali ya DRC kwa uamuzi wake wa kujenga barabara kutoka Lubumbashi kuja Kalemie. Hatua hii itafungua fursa za kibiashara kwa upande wa Tanzania,” amesema. Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa DRC, Judith Suminwa Tuluka aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa misaada yote iliyoipatia nchi hiyo ikiwemo ya kijeshi, kutunza wakimbizi na vyakula na vifaa tiba wakati nchi hiyo ilipopata maafa. “Tunaishukuru na Serikali ya Tanzania na hasa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye kupitia vikao mbalimbali vya kikanda na kimataifa alipambana na kuisaidia Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo iweze kubaki na amani,” alisema na kuongeza: “Hatuwezi kuisahau Tanzania kwa kuwapokea na kuwapa hifadhi wakimbizi zaidi ya 90,000 wakati nchi yetu ilipokuwa inapambana na Rwanda. Tunaishukuru sana Tanznaia kwa mshikamano huo.” Akielezea mafanikio ya nchi hiyo, alisema wamefanya mageuzi ya kiuchumi kupitia programu mbalimbali za ndani na nje. “Tumefanya mageuzi katika mfumo wetu wa kifedha na tukafanikiwa kujenga imani yetu kwenye medani za kimataifa. Faranga imepanda thamni ikilinganishwa na dola ya Marekani. Wakati naingia ofisini Juni 2024, dola moja ya Marekani ilikuwa sawa na Faranga 3,000 lakini hivi sasa dola moja ni sawa na Faranga 2,250.” Alisema kutokana na hali hiyo, nchi yao imefanikiwa mikopo ya Dola za Marekani milioni moja na imeanza kujiondoa kwenye orodha ya nchi zenye madeni chechefu. “DRC kwa sasa ina imani chanya katika ngazi ya kimataifa,” alisisitiza.
Wed, 04 Nov 2026 16:40:15 +0000TAKUKURU YAOKOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 106 KATIKA STESHENI YA SGR MOROGORO
NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 106.08 zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya ununuzi na usafirishaji wa maji kwa magari maalumu (bowser) katika Stesheni ya Reli ya Kisasa ya Jakaya Kikwete kwa mwaka mmoja. Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Mwandamizi wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro Casius Kiaro, amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya taasisi hiyo kubaini changamoto ya upatikanaji wa maji katika kituo hicho kupitia ufuatiliaji wa huduma za kijamii. Amesema ufuatiliaji huo ulihusisha Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) pamoja na uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kwa lengo la kutafuta suluhisho la kudumu la changamoto hiyo. Ameeleza kuwa kabla ya hatua hiyo, Stesheni ya SGR ya Jakaya Kikwete haikuwa na huduma ya uhakika ya maji, hali iliyolazimu kituo hicho kununua na kusafirisha maji kwa kutumia magari maalumu kwa ajili ya matumizi ya kawaida pamoja na huduma za mabehewa ya treni. Kwa mujibu wa Kiaro, gharama za ununuzi na usafirishaji wa maji zilifikia zaidi ya shilingi milioni mbili kwa wiki, sawa na shilingi milioni 8.84 kwa mwezi na jumla ya shilingi milioni 106.08 kwa mwaka. “Kupitia ushirikiano huo, huduma ya maji safi na salama imeanza kupatikana kwa uhakika katika kituo hicho kuanzia mwezi Agosti 2026, hatua iliyopunguza utegemezi wa ununuzi wa maji kwa kutumia magari,” amesema Kiaro. Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Stesheni ya Jakaya Kikwete, Salvatory Kimaro, amekiri kuwa changamoto ya upatikanaji wa maji ilikuwa ya muda mrefu, lakini imekwisha baada ya TAKUKURU kufuatilia suala hilo na kuwakutanisha na MORUWASA ili kupata suluhisho. Kimaro amesema kwa sasa kituo hicho kinapata maji saa 24, ingawa bado kuna uhitaji wa kuboresha miundombinu ya kuhifadhi maji ili kuwa na akiba ya kutosha kwa matumizi ya kituo hicho. “Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TRC, napenda kuishukuru sana TAKUKURU kwa hatua hii. Tulikuwa tunapata shida kubwa ya maji na kutumia gharama nyingi kununua na kusafirisha maji kwa ajili ya matumizi ya kituo,” amesema Kimaro. Naye Meneja wa Kanda Namba Moja wa MORUWASA, Mhandisi Gidion Chahe, amesema pamoja na kutatua changamoto hiyo, mamlaka hiyo inaendelea na mikakati ya kuboresha miundombinu ya maji ili kuhakikisha kituo hicho kinapata huduma ya uhakika kulingana na ongezeko la matumizi ya maji linalotokana na kuongezeka kwa idadi ya abiria. Amesema maboresho hayo ni muhimu ili kuhakikisha huduma ya maji inaendelea kupatikana kwa uhakika hata kadri shughuli za usafiri wa reli zinavyoendelea kukua. Hata hivyo, TAKUKURU imeeleza itaendelea kufanya ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali pamoja na wadau wa maendeleo zinatumika ipasavyo na miradi inayotekelezwa inazingatia thamani halisi ya fedha.
Wed, 04 Nov 2026 16:35:07 +0000Les enfants errants, une menace pour les commerçantes de Ndagala à Kabezi
Read the full report from the original source.
RecentlyKiambu officer found dead near duty station with two gunshot wounds
NATIONAL NEWS · 5 hours ago
RecentlyOver 200 Kilimani boda boda riders trained on road safety and emergency response
NATIONAL NEWS · 5 hours ago
RecentlyKMPDU issues 21-day strike ultimatum to 17 counties over doctors’ salaries
Latest · Capital Health
RecentlyKyaggwe Clinches First Masaza Cup Crown as Centenary Bank Strengthens Sports Development Partnership
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 398 of 1153 · 23057 stories