Search the region
23139 stories
SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUPAA, SERIKALI YAONGEZA UWEKEZAJI
Na Janeth Raphael -MichuziTv Serikali imeongeza kasi ya uwekezaji katika sekta ya sayansi, teknolojia na ubunifu kwa kuimarisha miundombinu na kuweka mazingira bora ya utafiti na uvumbuzi, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukuza maarifa na teknolojia kwa ajili ya maendeleo ya taifa. Hatua hiyo imejidhihirisha kupitia uwekaji wa jiwe la msingi la jengo jipya la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) jijini Dodoma, mradi unaolenga kuimarisha uwezo wa taasisi hiyo katika kutekeleza majukumu yake ya kusimamia na kukuza maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini. Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema Serikali imeipa sekta ya sayansi, teknolojia na ubunifu kipaumbele kwa kutambua mchango wake katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Amesema dhamira ya Serikali katika kuimarisha sekta hiyo inaonekana kupitia uwekezaji wa fedha za maendeleo, ujenzi wa shule maalumu za sekondari za wasichana zinazosisitiza masomo ya sayansi katika mikoa mbalimbali, pamoja na kupanua fursa za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo hayo. Profesa Mkenda amesema Serikali pia imeimarisha mpango wa Samia Scholarship STEM unaolenga kuwawezesha wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi kidato cha sita kuendelea na elimu ya juu katika fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) ndani ya nchi. Aidha, amesema wigo wa ufadhili umeongezwa kupitia mpango wa Samia Scholarship Extended, unaotoa fursa kwa Watanzania kusoma katika maeneo ya kimkakati yanayohitajika katika maendeleo ya taifa, yakiwemo sayansi ya nyuklia, sayansi ya takwimu (Data Science) na akili unde (Artificial Intelligence). Akifafanua umuhimu wa kuwekeza katika sayansi ya nyuklia, Waziri huyo amesema teknolojia hiyo ina matumizi mengi yanayogusa sekta mbalimbali, ikiwemo afya, kilimo na mazingira, hivyo kuna umuhimu wa kuandaa wataalamu wenye ujuzi katika eneo hilo. Amesisitiza kuwa dhana ya sayansi ya nyuklia haipaswi kuhusishwa na silaha pekee, bali pia kutambua mchango wake katika kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi kupitia matumizi yake katika sekta mbalimbali. “Sayansi ya nyuklia siyo mabomu pekee. Kuna afya, kuna kilimo, kuna mazingira na masuala mengine chungu nzima ambayo yanahitaji wataalamu,” amesema Profesa Mkenda. Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wanafunzi, wahadhiri na watafiti kupata fursa na nyenzo zinazohitajika katika kufanya tafiti zenye tija, kukuza ubunifu na kuzalisha maarifa yatakayochangia maendeleo ya teknolojia nchini. Ujenzi wa jengo la COSTECH ni sehemu ya juhudi za Serikali kuimarisha miundombinu ya taasisi zinazohusika na maendeleo ya sayansi na teknolojia, sambamba na kuwekeza katika rasilimali watu ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kufanya tafiti, kuvumbua teknolojia na kutumia maarifa katika kutatua changamoto za maendeleo.
Tue, 03 Nov 2026 18:56:52 +0000MKURUGENZI SIDO ATEMBELEA BANDA LA WANUFAIKA MRADI WA TUINUKE PAMOJA DODOMA.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), CPA Ahmed Kitara, amewataka wajasiriamali wanufaika wa mradi wa tuinuke pamoja kuendelea kuboresha bidhaa zao kwa kuzingatia ubora, vifungashio na mahitaji ya soko ili kuongeza ushindani na kupata fursa katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Ameyasema hayo Novemba 3, 2026 jijini Dodoma, mara baada ya kutembelea banda la wanufaika wa Mradi wa Tuinuke Pamoja unaotekelezwa na Shirika la Aga Khan Foundation katika Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma kwa ufadhili wa Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania, katika Maonesho ya Viwanda na Biashara yanayoelekea uzinduzi wa Sera ya Maendeleo ya Viwanda na Sera ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati ya mwaka 2003, Toleo la mwaka 2025, utakaofanyika Novemba 4, 2026. Amesema bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali waliopatiwa mafunzo na SIDO zimeonesha kukidhi viwango na kuwa na uwezo wa kushindana katika masoko mbalimbali, akibainisha kuwa baadhi ya bidhaa hizo zimezalishwa na vijana, hususan wanawake, aidha, amewashauri wajasiriamali kujisajili na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kupata uthibitisho wa ubora na nembo ya Made in Tanzania itakayoongeza ushindani wa bidhaa zao katika masoko ya nje. Amesema SIDO iko tayari kuwawezesha wajasiriamali kupitia maeneo manne ambayo ni mafunzo ya ujasiriamali na uzalishaji, teknolojia rahisi za uzalishaji, huduma za mitaji pamoja na upatikanaji wa maeneo ya kufanyia kazi. Amewahimiza vijana na wajasiriamali kutumia fursa hizo kuanzisha biashara na kuzalisha bidhaa zenye ubora zinazokidhi mahitaji ya masoko ya ndani na nje ya nchi. Akizungumza Mnufaika wa mradi wa Tuinuke Pamoja, Keto khalfan kutoka Kata ya Chang'ombe Wilaya ya Dodoma, amesema maelekezo waliyopewa kuhusu ubora, ufungashaji na usajili wa bidhaa itawasaidia kuboresha bidhaa zao na kupanua masoko, ambapo kwa sasa bidhaa zao zinauzwa zaidi ndani ya mkoa na mikoa jirani huku akieleza kuwa SIDO imekuwa msaada kwao kupitia mafunzo ya ujasiriamali, uzalishaji, usimamizi wa fedha, ufungashaji wa bidhaa. Kwa upande wake, Haruna Makunda, mnufaika wa mradi huo kutoka kikundi cha Kondoa Women Group, Wilaya ya Kondoa, amesema ushiriki wao katika Maonesho ya Viwanda na Biashara umewawezesha kupata elimu kuhusu umuhimu wa kusajili biashara kupitia BRELA na kupata uthibitisho wa ubora kutoka TBS ili bidhaa zao ziweze kuingia katika masoko mapana zaidi ikiwemo ya kimataifa, pia kuboresha vifungashio na ubora wa bidhaa ili kukidhi mahitaji ya soko la kisasa, huku akieleza kuwa maelekezo waliyopata kutoka SIDO yatawasaidia kuendeleza biashara zao. Mjasiriamali kutoka kikundi cha Girls Power, Esther Kakurwa Wilaya ya Chamwino, amelipongeza Shirika la Aga Khan Foundation kupitia Mradi wa Tuinuke Pamoja, kwa kushirikisha wajasiriamali katika maonesho hayo akisema fursa hiyo imewasaidia kujitangaza, kujifunza na kupata uelewa wa namna ya kukuza biashara zao, huku akiwahimiza wajasiriamali wengine kuendelea kushiriki maonesho ili kupanua fursa za kibiashara.
Tue, 03 Nov 2026 18:58:54 +0000RIB identifie onze suspects dans un vol de câbles électriques valant 20 millions Frw
Read the full report from the original source.
RecentlyKenya pregnancy-related mortality falls to 287 deaths per 100,000 live births – KNBS
Capital Health · 4 hours ago
RecentlyOkowa heads into second ballot after falling short in UN Security Council vote
News · 4 hours ago
RecentlySierra Leone withdraws ICJ candidate, backs Kenya’s Phoebe Okowa
Latest · News
RecentlyBULAYA: TAKUKURU ISIWE KICHAKA CHA KUWALINDA WEZI WA FEDHA ZA UMMA
Na Janeth Raphael - MichuziTv Bungeni Mbunge wa Bunda Mjini, Mhe. Esther Bulaya, amewataka viongozi na maofisa masuuli katika halmashauri kuacha tabia ya kuwalinda watumishi wanaotuhumiwa kwa wizi na ubadhirifu wa fedha za umma, akisisitiza kuwa vitendo hivyo vinakwamisha uwajibikaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini. Bulaya amesema baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwatetea watumishi wanaotuhumiwa kuiba fedha za umma, wakiwemo wahasibu wanaodaiwa kuchukua mapato ya vituo vya afya, kwa hoja kwamba mashauri yao yako katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), huku watumishi hao wakiendelea na majukumu yao kama kawaida. Amesisitiza kuwa uwepo wa mashauri katika TAKUKURU haupaswi kutumiwa kama kisingizio cha kuwakinga watumishi wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu dhidi ya hatua za kinidhamu na kisheria zinazostahili kuchukuliwa kwa mujibu wa taratibu zilizopo. Aidha, Bulaya ameeleza kuwa Bunge pamoja na kamati zake hazitavumilia uzembe, ubadhirifu wala vitendo vya wizi vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wachache, ambao wanarudisha nyuma juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi maendeleo. Amesisitiza pia umuhimu wa kuhakikisha fedha zote za umma zilizoibwa au ambazo hazijakusanywa zinarejeshwa haraka serikalini ili ziweze kutumika katika kukamilisha miradi ya maendeleo na kuboresha huduma muhimu kwa wananchi kote nchini. Ameonya kuwa ni muhimu kwa kila kiongozi na mtumishi wa umma kutimiza wajibu wake kwa uadilifu, kulinda rasilimali za taifa na kuhakikisha kila fedha inayokusanywa inatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
Tue, 03 Nov 2026 18:54:27 +0000King Charles calls slave trade a 'shameful chapter'
There has been calls from some for the UK to make a formal apology for its historic role in slave trade ahead of the Commonwealth Heads of Government Meeting.
RecentlyVidéo — Le Ballon d'Or pour Harry Kane, un boost pour la Bundesliga
Read the full report from the original source.
RecentlyVidéo — Le Beach Wrestling, une nouvelle discipline aux JOJ de Dakar
Read the full report from the original source.
RecentlyVidéo — Cameroun-Russie : où sont passés leurs proches ?
Read the full report from the original source.
RecentlyVidéo — Des girafes en acier en plein coeur de Douala
Read the full report from the original source.
RecentlyLaissez-vous inspirer !
Read the full report from the original source.
RecentlyExpensive power, taxes among hurdles facing Kenya's manufacturing sector
Read the full report from the original source.
RecentlyCCTV captures abduction of Nairobi lawyer Abshir Abdi along Muchai Road
Read the full report from the original source.
RecentlyLSK condemns abduction of lawyer Abshir Abdi, demands immediate release and probe
Read the full report from the original source.
RecentlySakaja defends switch to ODM from UDA, insists broad-based Gov't ties remain intact
Read the full report from the original source.
RecentlyNairobi court declines to fast-track petition challenging use of public funds in Bayern Munich vs Ajax match
Read the full report from the original source.
RecentlyEACC welcomes sentencing of Waititu, co-accused in Ksh.117M money laundering case
Read the full report from the original source.
RecentlyUzuri wa Kigoma na yaliyomo, mechi ya Mashujaa vs Pamba Jiji ikifunguliwa (NBC PL 02/11/2026)
#NBCPL Karibu Kigoma ya mawese na migebuka… Karibu Kigoma yenye zao la ngazi na michikichi… Karibu Kigoma ushuhudie pishi tamu la dagaa waleeeeee…… Karibu Kigoma upate burudani ya soka kwenye dimba la Lake Tanganyika… . Hii ndio Kigoma kama ilivyosimuliwa na ‘Super Stars wa Zamani’, Issa Suleiman, wakati akifungua matangazo ya mechi kati ya wenyeji Mashujaa FC vs Pamba Jiji SC.. Hii ilikuwa ni “vita ya maziwa mawili” kwa mujibu wa Issa Suleiman…. Je, unayajua maziwa yenyewe.. FT: Mashujaa FC 1-0 Pamba Jiji Burudani hii umeipata LIVE #AzamSports1HD #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi #MashujaaFC #PambaJijiFC #MashujaaPambajiji
2026-11-03T18:21:43+00:00Page 428 of 1157 · 23139 stories