Search the region
23208 stories
DKT. MWIGULU AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM KIGOMA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Jumatatu, Novemba 2, 2026, ameongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma. Dkt. Mwigulu, ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Kigoma, ameongoza kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi za CCM za mkoa huo.
Mon, 02 Nov 2026 19:44:09 +0000Simba SC 3-2 Namungo FC | Highlights | NBC Premier League 02/11/2026
Ilikuwa ni funga nikufunge, Simba ikitangulia, kisha kutokea nyuma na kushinda mechi dhidi ya Namungo FC, mchezo ukipigwa kwenye Dimba la Uhuru Dar es Salaam. Anicet Oura amefunga mawili huku lingine likifungwa na Rushine de Reuck kwa penati wakati magoli mawili ya Namungo yakitoka kwa Raymond Lulendi.
2026-11-02T19:27:45+00:00MSHIKEMSHIKE - AZAM TV 02/11/2026
Azam TV
2026-11-02T19:33:55+00:00DC NKURLU ATOA TUMAINI LA AJIRA KWA WAHITIMU WA JESHI LA AKIBA VIWANDANI NA MAKAMPUNI YA ULINZI
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha MKUU wa Wilaya ya Kibaha, Fadhil Emmanuel Nkurlu, amewahakikishia vijana 83 waliohitimu mafunzo ya awali ya Jeshi la Akiba kuwa wilaya itawasiliana na makampuni ya ulinzi na viwanda ili kuwapa kipaumbele katika ajira na kupunguza makali ya ukosefu wa ajira. Nkurlu ametoa ahadi hiyo wakati akifunga mafunzo ya awali ya Jeshi la Akiba kundi namba 19 mwaka 2026, yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Miembesaba, Kibaha mkoani Pwani, Novemba 2, mwaka huu. Amewataka wahitimu hao kuwa wazalendo, waadilifu na tayari kulitumikia taifa, akisisitiza kuwa mafunzo waliyopata yanapaswa kuwa chachu ya kulinda amani na usalama wa raia pamoja na mali zao, badala ya kutumika kuwatisha wananchi. "Mafunzo mliyopata yasiwe vitisho mitaani, msiende kutoa mkwala mitaani, nendeni mkawe mabalozi mitaani katika masuala ya amani na usalama kwa raia na mali zao," amesema Nkurlu. Aidha, amewaasa vijana hao kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vinavyokiuka maadili, huku akiwataka kutumia mafunzo hayo kwa manufaa ya jamii. Kwa upande wake, Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya , Lt col Katumbi Chinguku amesema mafunzo hayo yalianza Julai mwaka huu, ambapo yalifunguliwa Julai 6 yakiwa na vijana 97. Chinguku amesema vijana 83 wamehitimu mafunzo hayo, huku 14 wakiacha kutokana na sababu mbalimbali. Wahitimu hao wameiomba serikali kuwasaidia kupata ajira ili waweze kujikimu kimaisha, wakieleza kuwa kurejea uraiani bila fursa za ajira kutawaacha katika hali ya kuhangaika.
Mon, 02 Nov 2026 19:38:18 +0000Trump Moves to Expel Rwanda, South Africa from AGOA Programme
Read the full report from the original source.
RecentlyDC Nkurlu atoa tumaini la ajira kwa wahitimu wa Jeshi la Akiba viwandani na makampuni ya ulinzi
Read the full report from the original source.
RecentlyBODI YA WAKURUGENZI TASAC YATEMBELEA MIUNDOMBINU YA BANDARI NA BANDARI KAVU DAR ES SALAAM
BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), leo tarehe 2 Novemba, 2026, imefanya ziara ya kutembelea Bandari ya Dar es Salaam na baadhi ya bandari kavu jijini humo kwa lengo la kujionea miundombinu iliyopo, maendeleo ya uwekezaji na namna inavyosaidia kuongeza ufanisi wa huduma za kibandari. Ziara hiyo imefanyika katika kipindi ambacho uboreshaji wa miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam, ukiwemo uwekezaji uliofanywa na Kampuni ya DP World, umechangia kupunguza msongamano wa mizigo na magari bandarini na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma. Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TASAC, Nahodha Mussa Mandia, amesema ziara hiyo imewapa Wajumbe wa Bodi fursa ya kujionea miundombinu iliyopo na kuelewa namna inavyosaidia kurahisisha shughuli za kibandari. Amesema kuwa ufanisi wa bandari unategemea uwepo wa miundombinu bora inayowezesha upokeaji, uhifadhi na uondoshaji wa mizigo kwa wakati, hivyo kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika miundombinu na mifumo ya usafirishaji. Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya DP World, Bw. Elitunu Mallamia, amesema kampuni hiyo imeendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za bandari kupitia uwekezaji na maboresho mbalimbali ya miundombinu na mifumo ya uendeshaji. Naye Mkurugenzi Mkuu na Mmiliki wa Kampuni ya Bravo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji, hatua inayochochea ushiriki wa sekta binafsi katika mnyororo mzima wa uwekezaji na utoaji wa huduma za kibandari nchini. Ziara hiyo imeshirikisha viongozi na watendaji kutoka TASAC, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na wadau kutoka Kampuni ya DP World, Kampuni ya TEAGTL, African ICD na Bravo.
Mon, 02 Nov 2026 19:26:02 +0000Kibabii University student arrested in suspected KCSE exam cheating syndicate
Read the full report from the original source.
RecentlyTenerife player in intensive care with injury
Latest · football
RecentlyTASAC YAHIMIZA SEKTA BINAFSI KUWEKEZA USAFIRISHAJI
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Nahodha Mussa Mandia, ametoa wito kwa sekta binafsi kuendelea kuwekeza katika shughuli za usafirishaji na uhifadhi wa shehena kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya huduma hizo, kufuatia ukuaji wa shehena katika Bandari ya Dar es Salaam. Mandia ametoa wito huo wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi ya TASAC iliyotembelea Bandari Kavu za Bravoo na Mainland Logistics jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kujionea shughuli za uwekezaji na utoaji wa huduma katika sekta ya usafirishaji. Amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kushiriki katika uwekezaji, hivyo kuwataka Watanzania kutumia fursa zilizopo kuwekeza katika sekta hiyo. Ameeleza kuwa Bandari ya Dar es Salaam inapokea shehena kubwa zinazohitaji kuondolewa bandarini na kuhifadhiwa katika maeneo maalumu kabla ya kusafirishwa kwenda kwa watumiaji, hali inayoongeza umuhimu wa uwepo wa kampuni zinazotoa huduma za bandari kavu. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Bravoo, Anjelina Ngalula, amesema Serikali ya Awamu ya Sita imefungua milango kwa wazawa kuwekeza katika sekta ya usafirishaji kupitia reli kuondosha Shehena Bandarini na barabara. Amesema usikivu wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sekta binafsi umechangia kuwepo kwa mazingira rafiki ya uwekezaji, ikiwamo fursa ya wadau kujadili changamoto zinazokabili shughuli zao na kuzitafutia ufumbuzi. Aidha, amewahimiza Watanzania wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya usafirishaji na uhifadhi wa shehena kutembelea Kampuni ya Bravoo ili kujifunza namna shughuli hizo zinavyofanyika na kutumia fursa zilizopo. Amesema uwekezaji zaidi katika eneo hilo utasaidia kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania.
Mon, 02 Nov 2026 19:19:17 +0000Trump asks Supreme Court to block 20,000 California midterm ballots
Read the full report from the original source.
RecentlyStarlink eases Libra School’s internet connectivity woes
Libra International School located in Zirobwe, Luweero district, has turned to Starlink satellite technology to overcome persistent internet connectivity challenges that had hindered digital learning,…
RecentlyPresident Chapo: We consider relations with other countries of South–South Cooperation extremely important
Read the full report from the original source.
RecentlyTanzania Yaalika Uwekezaji wa Kilimo Kutoka Algeria
Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare Matinyi, amezialika kampuni za Algeria za teknolojia ya kilimo, ufugaji na usindikaji wa mazao ya chakula kuja nchini kuona fursa zilizopo za biashara na uwekezaji. Akizungumza na vyombo vya habari vya Algeria kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers, Balozi Matinyi alisema Serikali ya Tanzania imeweka mkazo kwenye uboreshaji wa sekta ya kilimo na uongezaji thamani wa mazao ya kilimo na kwamba utaalam na uzoefu wa kampuni za Algeria unahitajika Tanzania. Akielezea maendeleo ya ushirikiano baina ya Tanzania na Algeria kwa mwezi Oktoba, Balozi Matinyi alisema Ubalozi ulialikwa kwenye maonesho ya kilimo na pia kufanya ziara kwenye viwanda vya kusindika bidhaa za kilimo na ufugaji na kutumia fursa hiyo kuzialika kampuni mbalimbali za Algeria kuja nchini. Balozi Matinyi alisema kwamba mbali ya juhudi katika sekta ya kilimo, Serikali ya Tanzania inatekeleza pia miradi ya ujenzi wa mji mkuu wa Dodoma, inapanua sekta ya dawa na nishati, inafufua viwanda na inaimarisha miundombinu ya uzalishaji na usafirishaji ili kukidhi mahitaji ya kitaifa na kikanda. “Kufanya biashara na kuwekeza Tanzania kutaimarisha ushirikiano wa kiuchumi uliopo baina ya nchi zetu mbili rafiki na kuchochea ukuaji wa biashara barani Afrika,” alidokeza Balozi Matinyi mbele ya vyombo hivyo vya habari. Awali Balozi Matinyi alimshukuru Waziri wa Biashara ya Nje na Uhamasishaji wa Mauzo ya Nje, Mhe. Kamel Rezig, kwa kumwalika kwenye Maonyesho ya Biashara ya Chakula na Kilimo yaliyoandaliwa na wizara hiyo na kufanyika mjini Blida tarehe 17 Oktoba, 2026 huku yakivutia washiriki zaidi ya 100. Balozi Matinyi alitaarifu kuwa katika maonesho ya Blida na mengine ya jijini Annaba na Constantine, Ubalozi ulizielezea fursa zilizopo Tanzania na kuzikaribisha kampuni nyingi zikiwemo za usindikaji nyama na mazao ya kilimo, teknolojia ya ufugaji, uzalishaji chakula cha mifugo na mbolea, umwagiliaji na ufungashaji wa bidhaa za chakula. “Mbali ya Blida tulipata fursa ya kuongea na kampuni kadhaa tarehe 13 jijini Annaba kwenye maonesho ya Agri Tech Expo na tarehe 28 jijini Constantine kwenye maonesho ya Agrest Expo na zote tumezialika zije Tanzania kuona fursa zilizopo na namna ya kushirikiana na Watanzania,” alisema Balozi Matinyi. Balozi Matinyi aliongeza, “Tulifanya pia ziara mjini Blida tarehe 21 Oktoba kuona teknolojia ya juu ya usindikaji nyama ya kuku kwenye kiwanda cha Groupe Bellat na pia kushuhudia teknolojia ya usindikaji nyanya na pilipili kwenye kiwanda cha Groupe Amour na tumewakaribisha waje kuona fursa zilizopo Tanzania”. Aidha, Balozi Matinyi pia alikuwa mgeni wa heshima kwenye maonesho ya sekta ya ujenzi jijini Constantine mnamo tarehe 14 Oktoba na siku iliyofuatia Ubalozi ulifanya ziara kwenye kiwanda cha dawa za tiba cha Physiopharm ili kukivutia kije kuwekeza nchini. Kampuni ya TANOIL ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) nayo ilituma ujumbe wake uliongozwa na Kaimu Maneja Mkuu, James Sanawa, kuhudhuria Maonesho na Mkutano wa Nishati na Haidrojeni wa Afrika Kaskazini na Mediterania, uliofanyika kuanzia tarehe 5 hadi 7 Oktoba jijini Oran, Algeria. TANOIL ambayo husambaza bidhaa za gesi na petroli nchini, ilipata fursa ya kujadiliana namna ya kushirikiana kiufundi na kampuni mbalimbali likiwemo Shirika la Algeria la Gesi na Mafuta (Sonatrach) na kampuni yake tanzu ya usambazaji ya Naftal. Ukiwa jijini Oran, Ubalozi pia ulifanya ziara tarehe 6 Oktoba kwenye kiwanda cha Tapidor kinachotengeneza mazulia ya nyuzi zitokanazo na kemikali za petroli kwa lengo la kukivutia kuanzisha biashara nchini Tanzania na kulenga soko kubwa zaidi ya kikanda. Kadhalika, Mamlaka ya Taifa ya Bidhaa za Dawa ya Algeria (ANPP) ikiambatana na kampuni ya serikali ya dawa ya Saidal Group na baadaye kampuni binafsi ya dawa ya Frater Razes nazo zilifanya ziara nchini Tanzania ili kuanzisha ushirikiano wa kiufundi, kibiashara na kiuwekezaji katika sekta ya afya.
Mon, 02 Nov 2026 19:12:15 +0000Perezida Kagame yagaragaje imyumvire ikwiye guhinduka ku ishoramari muri Commonwealth
Read the full report from the original source.
RecentlyRetired UPDF General Peter Elwelu Arrested in Soroti as Military Announces Prosecution
Read the full report from the original source.
RecentlyBrief: How Nairobi-Nakuru jams are set to end
These are the stories making the headlines in your free copy of the Tuesday Star; get in from a vendor near you, countrywide
RecentlyMilioni 6 Za Expanse Reel Warriors Zawasubiri Mashujaa Wa Sloti
MASHABIKI wa michezo ya kasino mtandaoni wana sababu nyingine ya kuongeza msisimko kupitia Meridianbet, baada ya mashindano ya Expanse Reel Warriors kuanza rasmi Oktoba 27, 2026. Huu ni wakati wa kuingia kwenye ulimwengu wa michezo ya sloti, kujaribu bahati yako na kushindania sehemu ya zawadi nono za jumla ya TZS 6,000,000. Mashindano haya yanawaleta pamoja wachezaji wanaopenda msisimko wa kila raundi, huku nafasi ya kupanda kwenye orodha ya washindani bora ikiongeza ladha ya ushindani. Kupitia Expanse Reel Warriors, Meridianbet inakupa fursa ya kushiriki mashindano yanayojumuisha michezo 15 tofauti ya sloti kutoka Expanse Studios. Kila mchezo una upekee wake, na wachezaji wanaweza kuchagua michezo wanayoipenda huku wakifuatilia nafasi zao kwenye msimamo. Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jisajili leo kwa kutembelea tovuti ya MERIDIANBET au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Miongoni mwa michezo inayopatikana kwenye mashindano haya ni Pia Premium, Wild White Whale, Meridian Scatter Whale, Wild Icy Fruits, God of Coins na Zombie Apocalypse, pamoja na mingine mingi. Kila jina linakualika kugundua mazingira tofauti ya burudani ya sloti kupitia jukwaa la Meridianbet. Ukiwa na michezo 15 ya kuchagua na zawadi 20 zinazotarajiwa kutolewa, mashindano haya yanaweka burudani na ushindani katika safari moja ya kidijitali. Mashindano haya yalianza Oktoba 27 na yataendelea hadi Novemba 8, 2026, hivyo bado kuna muda wa kushiriki kabla ya pazia kufungwa. Kiwango cha chini cha dau ni TZS 1,000 kwa kila mzunguko, na wachezaji wanapaswa kuelewa namna ya kushiriki, kukusanya pointi na kupanda kwenye msimamo. Kwa hiyo, ikiwa unapenda michezo ya sloti na unatafuta burudani yenye ushindani, Expanse Reel Warriors kupitia Meridianbet inakupa nafasi ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha zawadi za milioni 6. Chagua mchezo unaoupenda kati ya michezo 15 inayoshiriki, cheza na ufuatilie msimamo hadi mwisho wa mashindano, Novemba 8.
Mon, 02 Nov 2026 07:03:00 +0000Muturi faults Gachagua’s tactics in opposition, cautions against 2027 coalition fragmentation
DP leader accuses the former Deputy President of promoting divisive political tactics and calls for a united national movement ahead of the 2027 polls.
RecentlyCAR officers and other ranks complete basic special operations force training in Rwanda
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 457 of 1161 · 23208 stories