Search the region
23236 stories
Why a Good MSc and PhD Thesis Is Automatic Employment: The Cases of Dr Paul Mwambu and Dr William Ruto
Read the full report from the original source.
RecentlyUWA Considers Fines for Tourists Flouting Gorilla Trekking Rules as IGCP Report Calls for Tougher Enforcement
Read the full report from the original source.
RecentlyVilla drop legal action threat against Carragher
Latest · English Premier League
RecentlyRais Samia akutana na mwalimu wake wakati akisoma Chuo Kikuu cha Mzumbe
Read the full report from the original source.
RecentlySERIKALI YAONGEZA NGUVU KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA WALIMU
Na Janeth Raphael -MichuziTv -Bungeni Serikali imesema itaendelea kuajiri walimu kila mwaka na kujaza nafasi zinazojitokeza kutokana na walimu wanaokoma utumishi, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa walimu katika shule za msingi na sekondari nchini. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange, wakati akijibu swali la Mbunge wa Bukoba Vijijini, Dkt. Jasson Samson Rweikiza, aliyetaka kufahamu ni lini tatizo la upungufu wa walimu katika shule nchini litakoma. Dkt. Dugange amesema Serikali inatambua changamoto ya upungufu wa walimu inayochangiwa na ongezeko la udahili wa wanafunzi kutokana na utekelezaji wa sera ya elimu bila ada, sambamba na kuongezeka kwa idadi ya shule mpya zinazojengwa nchini. Amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali imekuwa ikiendelea kuajiri walimu kila mwaka kulingana na mahitaji yaliyopo. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 hadi 2025/26, jumla ya walimu 64,772 wameajiriwa nchini. Kati ya hao, walimu 15,054 wameajiriwa katika mwaka wa fedha 2025/26 na kupangiwa katika vituo vya kazi, hususan maeneo yenye mahitaji makubwa zaidi ya walimu. Aidha, amesema Serikali inatarajia kuajiri walimu zaidi katika mwaka wa fedha 2026/27, ambao watapangiwa katika maeneo yenye upungufu mkubwa wa walimu. Mbali na kuendelea na ajira mpya, Serikali pia itaendelea kujaza nafasi za walimu wanaokoma utumishi kutokana na sababu mbalimbali, pamoja na kutumia walimu wa kujitolea kwa kuzingatia Mwongozo wa Kujitolea katika Utumishi wa Umma wa mwaka 2026. Hatua hizo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kupunguza upungufu wa walimu na kuhakikisha wanafunzi katika shule za msingi na sekondari wanapata huduma bora za elimu nchini.
Mon, 02 Nov 2026 12:52:32 +0000RAIS SAMIA ATOA MAELEKEZO MAZITO KWA VIONGOZI WAPYA, AHOJI MITAZAMO YA HAKI ZA BINADAMU DUNIANI
Na Janeth Raphael – MichuziTv Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi mbalimbali aliowaapisha Novemba 2, 2026, kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na uwajibikaji, akisisitiza umuhimu wa kufanya kazi zitakazoleta matokeo chanya kwa wananchi na Serikali kwa ujumla. Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi hao, Rais Samia amesema viongozi wanapaswa kuelewa mazingira ya sasa ya dunia, ambako masuala ya haki za binadamu yamekuwa yakitafsiriwa kwa mitazamo tofauti, huku nguvu na ushawishi wa mataifa vikichangia namna yanavyotazamwa na kuhukumiwa. Amesema katika mazingira ya sasa, nchi zinazotekeleza wajibu wa kulinda haki za binadamu zinaweza kujikuta zikishutumiwa kwa ukiukwaji wa haki hizo, wakati nyingine zinazokiuka haki hizo zikipata mtazamo tofauti kutokana na nguvu na ushawishi wake. “Katika dunia ya leo mambo yamekuwa juu chini, mwenye haki ataambiwa si mwenye haki na asiye na haki ataambiwa ana haki. Kuna nchi zinafanya vizuri lakini zitaambiwa zinavunja haki za binadamu, na zinazovunja haki za binadamu zinaonekana hazivunji kwa sababu zina nguvu,” amesema Rais Samia. Kutokana na hali hiyo, amewataka viongozi hao kuwa na utamaduni wa kufuatilia mijadala inayoendelea katika mitandao mbalimbali ya kijamii ili kufahamu taarifa, maoni na tuhuma zinazotolewa kuhusu Serikali, pamoja na mwenendo wa masuala mbalimbali yanayoendelea ndani na nje ya nchi. Aidha, amesisitiza kuwa viongozi hawapaswi kupuuza mijadala inayohusu taasisi na maeneo yao ya kazi, bali wanapaswa kuhakikisha wanatoa ufafanuzi na majibu stahiki kwa hoja zinazowasilishwa, ili wananchi wapate taarifa sahihi na kuepusha upotoshaji. Rais Samia ameeleza kuwa Serikali imekuwa ikikabiliwa kwa muda mrefu na tuhuma zinazohusiana na masuala ya haki za binadamu, akibainisha kuwa suala hilo ni sehemu muhimu ya utawala bora linalohitaji viongozi kuwa makini, wawajibikaji na wenye uwezo wa kueleza hatua zinazochukuliwa na Serikali. Amesisitiza kuwa viongozi hao wanapaswa kuchukulia nafasi walizopewa kama dhamana ya kuwatumikia wananchi, kwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kulinda taswira ya taasisi wanazoziongoza kupitia utendaji wenye matokeo yanayoonekana.
Mon, 02 Nov 2026 12:54:33 +0000NANAUKA: SERIKALI YAFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI KWA VIJANA
Na Janeth Raphael - MichuziTv Serikali imeendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia elimu, mafunzo ya ujuzi, mikopo, ajira na uwekezaji katika sekta za uzalishaji, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kujitegemea na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa na Bara la Afrika. Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Afrika yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Arthur Nanauka, amesema Serikali pia imeweka msisitizo katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kuwekeza katika rasilimali watu kupitia elimu bora na ujuzi unaowawezesha vijana kukabiliana na mahitaji ya soko la ajira na kujiajiri. Amesema Serikali inaendelea kuboresha mitaala kwa mfumo wa umahiri, unaojumuisha masomo ya biashara, TEHAMA na elimu ya fedha, sambamba na kujenga zaidi ya vyuo 60 vya mafunzo ya ufundi stadi. Aidha, zaidi ya Shilingi bilioni tisa zimetengwa mwaka huu kuwezesha vijana kupata mafunzo ya ujuzi, huku Serikali ikitarajia kutoa fursa za ajira kwa vijana 30,000 kupitia taasisi za Serikali na sekta binafsi. Nanauka amesema vijana pia wanashirikishwa katika sekta tisa za vipaumbele vya maendeleo, zikiwemo viwanda, kilimo, utalii, huduma, ubunifu na ujenzi. Ameeleza kuwa Serikali imeendelea kutoa mikopo na mitaji kwa vijana katika kilimo, mifugo, uvuvi na madini, akitolea mfano wa vijana wa Songwe waliowezeshwa kwa Shilingi bilioni 50 katika shughuli za uchimbaji madini, pamoja na vikundi vya vijana wa Mwanza na Manyoni vilivyopata mitaji kwa shughuli za uzalishaji. Kwa upande wao, vijana wa UDOM wameiomba Serikali kuweka utaratibu wa kuwasaidia wanufaika wa mikopo wanaokumbana na changamoto za kiuchumi zinazowazuia kufikia malengo ya miradi na kurejesha mikopo kwa wakati. Mwakilishi wa vijana na mwanafunzi wa UDOM, Raphia Ramadhan Kayaya, amesema maadhimisho hayo yamewapa vijana fursa ya kukutana na viongozi wa Serikali, kueleza changamoto zao na kupata ufafanuzi kuhusu fursa mbalimbali zinazotolewa. Naye Makamu Mkuu wa UDOM, Prof. Lughano Kusiluka, amewataka vijana kuendeleza misingi ya uzalendo na kutumia elimu pamoja na fursa zinazotolewa na Serikali kujenga Taifa. Amesema UDOM ni sehemu ya uwekezaji mkubwa wa Serikali katika elimu na kinatarajia kuwa na zaidi ya wanafunzi 37,000 mwaka huu, jambo linalodhihirisha umuhimu wa kuwaandaa vijana kwa ajili ya mustakabali wa nchi. Maadhimisho ya Siku ya Vijana Afrika, yaliyoanzishwa mwaka 2006 kufuatia kupitishwa kwa Mkataba wa Vijana wa Afrika, yamefanyika mwaka huu chini ya kaulimbiu isemayo, “Afrika Bora Inajengwa na Kijana Mwema, Mzalendo na Mwenye Maadili,” ikisisitiza umuhimu wa vijana kuwa na maadili, uwajibikaji na uzalendo katika kuchochea maendeleo ya Bara la Afrika.
Mon, 02 Nov 2026 12:51:06 +0000MTN Nigeria earns more but keeps less cash
Read the full report from the original source.
RecentlyNine dead in small plane crash near Trump's Florida home
Read the full report from the original source.
RecentlySalome alipongeza Bunge kwa usimamizi mradi wa Julius Nyerere
Read the full report from the original source.
RecentlyCentenary Bank rewards Masaza Cup stars as Kyaggwe beat Gomba
Centenary Bank has rewarded the top performers at this year's Masaza Cup, after Kyaggwe beat Gomba 1-0 in the final at Muteesa II Stadium in Wankulukuku. Mohamed Kasule received UGX 1m...
RecentlyForestry State Department unveils Ksh26B landscape restoration project
Read the full report from the original source.
RecentlyGlobal pedestrian Karl Bushby returns home to UK after 28-year trek
Read the full report from the original source.
RecentlyNSSF charity run seeks UGX 1.5bn to repair public schools
Uganda's National Social Security Fund (NSSF) is aiming to raise about UGX 1.5bn from its annual charity run to renovate around 10 public primary schools. The NSSF Kampala Hills Run will...
RecentlySupermarket freezers in Belgium hit by cyber-attack
It is not clear who is behind the attack, which follows a similar incident last month that affected hundreds of French supermarkets
RecentlyWhy Sakaja has ditched UDA for ODM
Baba, Raila Odinga is the one who told me to join ODM, Sakaja said.
Mon, 02 Nov 2026 15:20:00 +0300Irish business group adopts new identity after 13 years in Kenya
Business · Quick read
RecentlyKenya moves to strengthen cyber defences as attacks surge 114pc
NATIONAL NEWS · 4 hours ago
RecentlyYAS YAKABIDHI VIFAA TIBA HOSPITALI.
KAMPUNI ya YAS Tanzania imekabidhi vifaa Tiba mbali mbali kwa Hospitali ya Wilaya ya Wete Kinyasini, ili kuunga mkono juhudi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto. Akipokea Vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Wete Abdalla Rashid Ali, ameipongeza kampuni hiyo kwa harakati zake za kusaidia huduma mbali mbali za Kijamii. Alisema vifaa hivyo pia vitaweza kuimarisha huduma za mama wajawazito wanaofika hospitali hapo kupata huduma, Pamoja na kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto katika hpspitali hiyo. “Nyinyi sio tu watu wa mawasiliano kumbe muna upande mwengine ambao bado haujajulikana, sasa leo mumekuja kutuonesha mfano kwa kukabidhi baadhi ya hivi vitu ambavyo ni muhimu kwa Hospitali yetu na sehemu ya akina mama wajawazito,”alisema. Alisema Watoto wanapopata huduma nzuri, makuzi mazuri na afya bora, ndio watakaokua watumiaji wakubwa wa mitandao hiyo, huku hospitali ya kinyasini Pemba ikiwa ni ya tatau kwa kutoa huduma bora nchini. Aidh Alisema Vifaa hivyo walivokabidhiwa vitaweza kuongezea malengo yao ya utoaji wa huduma bora kwa jamii, huku akiwataka wafanyakazi wa YAS waliotoa michango yao kutambua kuwa wameekeza katika maisha yao, sambamba na kutambua kuwa Kampuni ya YAS ndio ya kuigwa. Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wafanyakazi kuhakikisha wanavitumia vifaa hivyo kwa malengo yaliokusudiwa, sambamba na kuwa kufanyakazi kwao kwa bidii ni moja ya sadaka muhimu katika maisha yao. Mapema Mkuu wa Kampuni Yas Zanzibar, Mohamed Wakid ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongezwa na Dk.Hussein Ali Mwinyi, katika kuimarisha huduma za afya nchini Pamoja na kuhudumia huduma za kinamama wajawazito nchini. Alisema kupitia kampeni ya Tumaini, kampuni ya Yas imeona ikabidhi vifaa vitakavyoboresha huduma za uzazi kwa akinamama wajawazito wanaofika hospitalini hapo kupata huduma. “Kampeni hii ya Tumaini ni yakipekee, kwani wazo lake limeanzia kwa wafanyakazi wenyewe baada ya kuguswa na changamoto zinazowakabili akinamama wanataka kujifua wanapofika hospitalini,”alisema. Aidha alivitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni Pamoja na Vitanda, viti Mwendo, vitanda vya kujifunguliwa, kanga, mashuka na vitu vyengine mbali mbali. Hata hivyo alisema kamuni hiyo tayari imeshawafikiwa takriba wananchi asilimia 99% wa Zanzibar, kwa kuwapati huduma bora za kimtandao, kwani huduma na namna inavowajibika kwa jamii kila siku. Nao baadhi ya akinamama walikuwepo Hospitalinih apo, wameishukuru kampuni ya Yas Tanzania, kwa misaada yao walioitoa hospitalini hapo. Fatma Juma Hamad ameishukuru Yas kwa kuwapatia msaada walioutoaka, huku wakiyataka makampuni mengine kujitokeza kusaidia huduma mbali mbali kwa hospitali hiyo. Nae Raya Seif Abdalla ameishukuru kampuni hiyo kwa misaada waliowapatia, itaweza kusaidia utoaji wa huduma bora muda wote kwa akinamama wanaofika kupata huduma. MKUU wa Wilaya ya Wete Abdalla Rashid Ali(Katikati)akipokea moja ya vifaa vya kujifungulia mama wajawazito kutoka kwa Mkuu wa Yas Zanzibar Mohamed Waqid na kumkabidhi Daktari dhamana wa Hospitali ya Wilaya ya Wete Dr Fran Swai, vifa hivyo vilivyotolewa na Yas hafla iliyofanyika Kinyasini. MKUU wa Wilaya ya Wete Abdalla Rashid Ali(Katikati), Mkuu wa Yas Zanzibar Mohamed Waqid na i Daktari dhamana wa Hospitali ya Wilaya ya Wete Dr Fran Swai, wakionesha baadhi ya vitu vilivyotolewa na Yas kwa ajili ya kuwakabidhi mama na Watoto waliojifungua katika Hospitali ya Wilaya ya Wete Kinyasini. MKUU wa Wilaya ya Wete Abdalla Rashid Ali(Katikati)akipokea kiti Mwendo kutoka kwa Mkuu wa Yas Zanzibar Mohamed Waqid na kumkabidhi Daktari dhamana wa Hospitali ya Wilaya ya Wete Dr Fran Swai, vifa hivyo vilivyotolewa na Yas hafla iliyofanyika Kinyasini. MKUU wa Yas Zanzibar Mohamed Waqid akimkabidhi mmoja ya wajawazito Zawadi, wakati walipotembelea wodi za mama hao kwa alengo la kukabidhi Zawadi hizo, katika Hospitali ya Wilaya ya Wete Kinyasini.
Mon, 02 Nov 2026 05:00:00 +0000Dokolo Adventists Adopt Monthly Sunday Cleaning in Landmark Deal with Government
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 469 of 1162 · 23236 stories