Search the region
23317 stories
Plus de 5 000 personnes meurent d'Ebola lors de l'épidémie la plus meurtrière qu'ait connue la République démocratique du Congo
Les données gouvernementales montrent que plus de 10 000 personnes ont contracté ce virus rare.
RecentlyU Burusiya bwiyemeje gufasha u Rwanda guteza imbere ibikorwa remezo by’ingufu za Nikeleyeli
Read the full report from the original source.
RecentlyInside Ksh.20 billion deal that ended lecturers strike
Read the full report from the original source.
RecentlyMwamkoa wa wananchi Samia Legal Aid watajwa kuwavutia wananchi Pwani
Read the full report from the original source.
RecentlyRwanda and Russia agree next steps for small nuclear power project
Read the full report from the original source.
RecentlyMhandisi Mashauri Jofrey afunguka fursa Tanzania, Urusi
Read the full report from the original source.
RecentlyMore than 290 arrested in France as some weekend protests turn violent
Read the full report from the original source.
RecentlyAFD sign Rwf 70 million agreement to protect Busaga Natural Forest in Muhanga District
Read the full report from the original source.
RecentlyKampeni ya Mama Samia yawajengea wanafunzi Visiga uwezo wa kupambana na ukatili
Read the full report from the original source.
RecentlyPerezida Kagame yitabiriye itangizwa ry’Imikino Olempike y’Urubyiruko
Read the full report from the original source.
RecentlyINEC YAWAPA NENO MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA KATA YA NONDE
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka Makarani Waongozaji Wapiga Kura katika kata ya Nonde iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya kutekeleza majukumu yao kwa weledi. Hayo yamebainishwa leo Oktoba 31, 2026 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele wakati akizungumza na watendaji hao alipotembelea mafunzo yao ya siku moja ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata ya Nonde unaotarajiwa kufanyika tarehe 04 Novemba,2026. Jaji Mwambegele amewasisitiza washiriki hao kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni ili kuufanya uchaguzi huo kuwa huru na wa haki. Awali kabla ya ufunguzi wa Mafunzo haya, washiriki hao waliapa kiapo cha kutunza siri na kile cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa haki na weledi. Uchaguzi huo utafanyika ikiwa ni miongoni mwa kata kata 11 za Tanzania Bara ambazo ni Lugenge, Halmashauri ya Mji Njombe; Bargish, Halmashauri ya Mji Mbulu; Makole, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza; Mwera, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Oldonyosambu, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro. Nyingine ni Igalula iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Uyui; Shelui, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba; Mvumi, Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa; Nyarero, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Ilolangulu, Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe.
Sat, 31 Oct 2026 18:39:41 +0000Hunger deepens for millions amid conflict, Ebola and climate shocks in DRC
Read the full report from the original source.
Recently'The time is now!' Defiant Kalonzo still confident in 2027 race despite heckling
Read the full report from the original source.
RecentlyGirl swept by floods in Kajiado as hailstones destroy crops in Kericho
Read the full report from the original source.
RecentlyLinda Mwananchi leaders urge opposition to rally behind Sifuna's presidential candidature
Read the full report from the original source.
RecentlyWanawake waonyeshwa njia kutajirika kwa kilimo
Read the full report from the original source.
RecentlyHORTILOGISTICA AFRICA 2026 KUFUNGUA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI WA MAZAO YA HOTIKACHA
TANZANIA inatarajiwa kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji katika sekta ya kilimo cha hotikacha barani Afrika kupitia jukwaa la kimataifa la HortiLogistica Africa 2026, litakalowakutanisha wakulima, wawekezaji, wafanyabiashara, wanunuzi wa kimataifa, wasafirishaji na wadau mbalimbali wa mnyororo wa thamani wa mazao ya mboga, matunda na maua kutoka ndani na nje ya nchi. Jukwaa hilo linatarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 8 hadi 10 mwaka 2026 katika viwanja vya TGT, mkoani Arusha, likiwa na lengo la kuunganisha wazalishaji wa mazao ya hotikacha na masoko ya ndani na kimataifa, pamoja na kuweka mazingira bora ya kuvutia mitaji na teknolojia mpya katika sekta hiyo. HortiLogistica Africa 2026, inayoandaliwa na Asasi Kilele ya Sekta Binafsi inayojishughulisha na kuendeleza na kukuza sekta ya hotikacha nchini (TAHA), kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, inatarajiwa kukutanisha wakulima, wasafirishaji, wanunuzi, teknolojia, vionhozi, wafanyabiashara na wataalamu kutoka zaidi ya nchi 40 duniani. Umuhimu wa jukwaa hilo hauishii katika maonesho pekee, bali linatoa fursa ya kujenga mahusiano ya kibiashara kati ya wakulima na wanunuzi wakubwa wa kimataifa, kupata mikataba ya kuuza mazao nje ya nchi, kuvutia wawekezaji na kubadilishana teknolojia zitakazosaidia kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao. Aidha, jukwaa hilo linatarajiwa kufungua fursa katika maeneo mbalimbali ya mnyororo wa thamani wa hotikacha, yakiwemo uzalishaji wa kisasa, upatikanaji wa mbegu bora, pembejeo, vifaa vya kilimo, teknolojia za umwagiliaji, uhifadhi wa mazao, ufungashaji, usafirishaji na huduma za ugavi wa kimataifa. Katika eneo la biashara ya kimataifa, uwepo wa wanunuzi, wasafirishaji na wawekezaji utatoa nafasi kwa wakulima na kampuni za ndani kupata taarifa za mahitaji ya masoko ya nje, viwango vya ubora vinavyohitajika na namna ya kukidhi masharti ya usafirishaji wa mazao kwenda kwenye masoko mbalimbali duniani. Pamoja na hayo, matumizi ya teknolojia za kisasa za uhifadhi na usafirishaji wa mazao katika mifumo ya cold chain yanatarajiwa kuwa miongoni mwa maeneo muhimu ya majadiliano, hatua inayoweza kusaidia kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvunwa na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika soko la kimataifa. Kwa upande mwingine, jukwaa hilo ni fursa muhimu kwa vijana na wajasiriamali kuingia katika biashara zinazohusiana na hotikacha, ikiwemo huduma za usafirishaji, usindikaji, ufungashaji, uuzaji wa pembejeo, teknolojia za kilimo na huduma za kifedha. Aidha, Serikali imekuwa ikitambua sekta ya hotikacha kama eneo lenye uwezo wa kuchochea uwekezaji, kuongeza mapato ya wakulima, kukuza biashara ya nje na kupanua wigo wa ajira kwa Watanzania. Kupitia HortiLogistica Africa 2026, Tanzania inalenga kutumia nafasi yake ya kimkakati katika ukanda wa Afrika Mashariki na fursa za miundombinu ya usafiri na masoko ili kujenga mazingira yatakayoiwezesha nchi kuwa kitovu cha biashara na usambazaji wa mazao ya hotikacha barani Afrika. Kaulimbiu ya jukwaa hilo ni “Bridging Markets, Cultivating Prosperity”, ikimaanisha kuunganisha masoko na kukuza ustawi kupitia kilimo, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na kuendeleza sekta ya hotikacha. Hivyo, HortiLogistica Africa 2026 inatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kuunganisha uzalishaji na masoko, ambapo mafanikio yake yatapimwa pia kwa uwezo wa kuzalisha mikataba ya biashara, uwekezaji mpya, teknolojia na fursa endelevu kwa wakulima na wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Sat, 31 Oct 2026 18:28:34 +0000TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WABUNGE WANAWAKE UKANDA WA MAZIWA MAKUU
Na Said Mwishehe,Michuzi TV TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wabunge Wanawake kwa mwaka 2026 wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu. Akizungumza leo Oktoba 31,2026 jijini Dar es Salaam Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu amesema mkutano huo muhimu unatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 300 kutoka nchi 12 za Ukanda wa Maziwa Makuu na unatarajia kuanza Novemba 2 mwaka katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere. “Na utawakutanisha viongozi wakuu na wadau mbalimbali ili kujadili masuala yenye maslahi ya pamoja katika kukuza maendeleo, amani, na ushirikiano wa kikanda. Mgeni rasmi katika ufumguzi wa mkutano huo ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. “Viongozi wengine mashuhuri watakaohudhuria hafla ya ufunguzi ni pamoja na Judith Suminwa Tuluka ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambaye ni mgeni maalum; Adao Francisco Correia de Almeida ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Angola naRais wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu; “Wengine ni Amason Jeffah Kingi ambaye ni Spika wa Bunge la Seneti la Kenya, Jacob Oboth – Oboth ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Uganda, Aime Boji Sangara ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zubeir Ali Maulid ambaye ni Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na Malungo Chisangano ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Zambia.” Zungu amesema mkutano huo unafanyika chini ya kauli mbiu isemayo ‘Amani na maendeleo kwa ajili ya Ukanda wa Maziwa Makuu.Lengo lake kuu ni kuimarisha ushirikiano na kuongeza mchango wa wanawake katika maamuzi, Diplomasia ya kibunge, amani, usalama na maendeleo endelevu kwenye Ukanda wa Maziwa makuu. Aidha, Mkutano huo ni fursa muhimu ya kuimarisha mshikamano na ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama, pamoja na kujadili mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazoukabili ukanda wetu. Vilevile, amesema Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano huo kunaleta taswira chanya kwa nchi yetu kuendelea kuaminiwa na mataifa mengine kama nchi yenye amani na inayoendeleza na kutambua misingi ya utawala bora chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Ametoa mwito kwa Watanzania wote kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha wageni wanapokelewa kwa bashasha, upendo, na ukarimu uleule unaoitambulisha nchi yetu duniani. Hiyo ni fursa adhimu ya kuwaonesha utamaduni wetu tajiri, mshikamano wetu thabiti, na uzuri wa kipekee wa Tanzania yetu. “Kila mmoja wetu na awe balozi mwema kwa kuonesha heshima, nidhamu ya hali ya juu, usafi wa mazingira yetu, na moyo wa dhati wa kuwajali wageni wetu. Wewe ukiwa kama Mtanzania simama kama balozi, ili kila mgeni atakayeondoka, aondoke na kumbukumbu nzuri na zisizosahaulika mioyoni mwao kuhusu Tanzania.”
Sat, 31 Oct 2026 18:31:13 +0000Kenya demands immediate review of Saudi Arabia's Ebola travel ban
Read the full report from the original source.
RecentlyRais Dk Mwinyi awakaribisha wawekezaji Korea Kusini kutumia fursa za uwekezaji Zanzibar
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 503 of 1166 · 23317 stories