Unganishwa

Search the region

23375 stories

Uncategorized · Daily News

Dr Magembe warn against excessive consumption of salt,sugar and fat

DODOMA: THE Permanent Secretary of the Ministry of Health, Dr Grace Magembe has urged citizens to reduce the consumption of…

Recently
National · Issa Michuzi

POLISI MORO YAWASHIKILIA WATATU KWA TUHUMA ZA KUMTOROSHA MWANAFUNZI

Farida Mangube, Morogoro Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kumtorosha mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Sokoine Memorial, katika eneo la Wami Sokoine, wilayani Mvomero, huku likiendelea na msako wa kubaini mahali alipopelekwa. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Andrew Kantimbo, Tukio hilo limetokea Oktoba 26, 2026, majira ya saa 9:00 alasiri, wakati mwanafunzi huyo akitoka shuleni na wenzake katika eneo la Wami Sokoine, Kata ya Dakawa. Imedaiwa mwanafunzi huyo alichukuliwa kwa nguvu na kupelekwa kwa kutumia pikipiki kabla ya watu waliokuwa naye kutokomea kusikojulikana. Wanaoshikiliwa na Polisi ni Kandolo Rosingo Kibasisi (56), mkazi wa Sokoine Shule, Michael Jackson Shabala (32), mkazi wa Victoria Ngale, pamoja na Hagiro (41), ambao wote wanatajwa kuwa wafugaji na wakazi wa Sokoine Shule. Kamanda huyo wa Polisi amesema Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini alipo mwanafunzi huyo na kuhakikisha wote waliohusika wanachukuliwa hatua za kisheria. Katika taarifa hiyo, Polisi wameeleza kuwa tukio hilo linahusishwa na mila potofu zinazodaiwa kuwepo katika baadhi ya maeneo ya jamii ya Kimasai, zinazohusisha kumchukua binti kwa nguvu anapokataa kuolewa kwa hiari, kisha familia kukutana na kujadiliana kuhusu mahari. Kutokana na hali hiyo, Kamanda Kantimbo amewataka wananchi kuachana na mila zinazohatarisha usalama na haki za watoto, huku akisisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kusimamia malezi na elimu ya watoto wao. Aidha akawasihi wananchi na jamii kwa ujumla kuhakikisha watoto, hususan wanafunzi wa kike, wanalindwa na kupewa mazingira salama ya kuendelea na masomo ili waweze kutimiza malengo yao na kuchangia maendeleo ya Taifa.

Fri, 30 Oct 2026 12:15:41 +0000
Uncategorized · The Standard

Police step up security ahead of ODM's Jacaranda rally tomorrow

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Chimpreports

Court Upholds Ssenyonyi’s Election Victory, Orders EC to Pay Costs Over Nomination Errors

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Chimpreports

Police Arrest 300 Suspects in Crackdown on Criminal Gangs in Kampala

Read the full report from the original source.

Recently
National · Capital FM

Items stolen from Man Utd Munich air disaster memorial

Latest · English Premier League

Recently
National · Daily News

Tanzania’s new government city in Mtumba officially begins operations

DODOMA: TANZANIA has officially inaugurated office buildings housing government ministries and institutions, together with paved road infrastructure at the Government…

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Sub-Saharan Africa’s Growing Cities Offer Path to Millions of New Jobs

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Ronaldo closes in on 1,000th goal with hat-trick

Latest · football

Recently
Uncategorized · HabariLeo

TRA yawekeza mil 37/- elimu ya kodi Tosamaganga

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

WAZIRI MKUU ATAKA UBALOZI URUSI UPANUE MASOKO YA BIDHAA ZA TANZANIA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi waendelee kuitangaza vyema nchi na kuongeza juhudi za kutafuta fursa za masoko kwa bidhaa za Tanzania nchini humo. Ameyasena hayo leo Oktoba 30, 2026, wakati akizungumza na watumishi wa Ubalozi huo ulioko jijini Moscow na kuwapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuiwakilisha vema Tanzania nchini humo. Sambamba na hayo, Mheshimiwa Dkt Mwigulu amebainisha kuwa hivi sasa nchi imekuwa na uzalishaji wa mazao wa ziada unaohitaji masoko ya uhakika. “Bado tunahitaji masoko ya bidhaa zetu. Tumekuwa na uzalishaji wa mazao wa ziada nchini, hivyo tumieni fursa hii kutengeneza masoko katika miji mingine kwa maana nchi hii ni kubwa sana. Kadhalika, endeleeni kufuatilia fursa zilizopo katika sekta ya elimu, jambo ambalo pia limejitokeza kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi,” amesema. Aidha, Waziri Mkuu amewataka watumishi hao wafuatilie na kusimamia utekelezaji wa maagizo yote yaliyotokana na ziara ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, nchini Urusi, iliyofanyika Juni, mwaka huu. Awali, Dkt. Mwigulu alitembelea duka la AZBUKA VKUSA linalouza bidhaa kutoka Tanzania, jijini Moscow.

Fri, 30 Oct 2026 12:01:48 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

MADIWANI SIMANJIRO WATAKA MIRERANI NA ORK ZIWEZESHWE VIKAO

Na Mwandishi wetu, Simanjiro MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Mkoani Manyara, wamemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, kuwezesha miji midogo ya Mirerani na Orkesumet ili wafanye vikao. Madiwani hao wamepitisha azimio hilo kwenye kikao chao kilichofanyika makao makuu ya Wilaya hiyo mji mdogo wa Orkesumet. Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii, Albert Msole amesema miji midogo ya Mirerani na Orkesumet inapaswa kuwezeshwa ili wajumbe wake waweze kukutana kujadili na kupitisha maendeleo yao. "Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri awezeshe mamlaka ya miji midogo ya Orkesumet na Mirerani ili ziweze kujiendesha na kufanya vikao kwa mujibu wa sheria," amesema. Pia, baraza hilo la madiwani limemuagiza Mkurugenzi aweke kwenye bajeti mpango wa kujenga ofisi na nyumba za watumishi wa ngazi ya vijiji na kata. Amesema Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya afuatilie wawekezaji mbalimbali Wilayani ili kuwezesha Halmashauri kupata fedha kutokana na michango ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) iliyopo kwa mujibu wa sheria. "Pia Mkurugenzi mtendaji aweke kwenye bajeti ijayo ujenzi wa zahanati kwenye vijiji ambavyo hazina zahanati," amesema Msole. Amesema Mkurugenzi mtendaji aweke mkakati wa kuondoa tatizo la upungufu wa madarasa na madawati katika shule ya msingi na sekondari. "Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri aendelee kuagiza watendaji wa kata na vijiji watunge sheria ndogo zinazowataka wazazi kuchangia chakula cha mchana cha wanafunzi na rasimu ya sheria hiyo ipitishwe kwenye mikutano mikuu ya vijiji, zoezi hilo liwe limekamilika mwishoni mwa mwezi Novemba 2026," amesema. Amesema Mkurugenzi mtendaji awaagize watendaji wa Kata na Vijiji kuendelea kuweka mikakati ya kujenga miundombinu mbalimbali kwa kuzingatia upungufu ikiwa pamoja na ujenzi wa shule mpya kwenye Kata na Vijiji vyenye uhitaji wa shule za sekondari ili kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza Januari 2028. Ameeleza kwamba pia, Mkurugenzi mtendaji anapaswa kuweka mikakati ya kukamilisha ujenzi wa maabara za shule za sekondari ambao ujenzi wake ulianza muda mrefu na hazijakamilika.

Fri, 30 Oct 2026 11:59:49 +0000
Uncategorized · Capital FM

Kenya Railways targets car dealers with new SGR freight service

Business · 4 hours ago

Recently
Uncategorized · Capital FM

First casualty retrieved from Eastleigh building collapse

Latest · NATIONAL NEWS

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Kiambu woman, granddaughter found dead at home

According to police officers, the case came to light after a neighbour reportedly heard screams and responded to the disturbance

Recently
Uncategorized · Jamhuri Media

Tanzania yapokea uenyekiti Baraza la Mawaziri la Mamlaka ya Ziwa Tanganyika

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Omollo asks MPs to support recruitment of 5,000 cops

Omollo said the government needed more officers to strengthen security operations and ensure Kenyans had access to adequate protection

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

RITA KIBAHA YAONYA DHIDI YA KUGHUSHI VYETI, YAWAASA WANANCHI KUFUATA TARATIBU

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha WANANCHI zaidi ya 200 wamejitokeza kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), zikiwemo za usajili na upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa, katika mabanda ya maonyesho ya Kampeni ya Samia Legal Aid, Maili Moja, Kibaha. Huduma hizo zinatolewa katika siku ya pili ya utekelezaji wa kampeni hiyo ya awamu ya pili, iliyoanza Oktoba 28 na inatarajiwa kuhitimishwa Novemba 7, 2026, ikiwa na jumla ya siku 10 za utoaji huduma mbalimbali za kisheria kwa wananchi. Msajili Mwandamizi wa RITA Wilaya ya Kibaha, George Chuwa, alisema wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kusajili matukio muhimu ya kijamii na kisheria, ikiwemo vizazi, vifo, ndoa na talaka na huduma za udhamini na ufilisi. Alieleza wananchi wanapaswa kuhakikisha watoto wanasajiliwa mara wanapozaliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa, huku akisisitiza umuhimu wa kusajili vifo kwa kuwa nyaraka hizo ni muhimu katika kulinda haki za kisheria. Chuwa alieleza kuwa kupitia huduma hizo za karibu, majina ya waombaji huingizwa kwenye mfumo na kuchakatwa kwa haraka, huku vyeti vilivyokamilika vikikabidhiwa kwa wahusika ili kuhakikisha vinawafikia walengwa kwa wakati. Hata hivyo, aliwataka wananchi kufuata taratibu halali za kupata vyeti na kuepuka kughushi nyaraka au kutumia njia zisizo halali, akisisitiza kuwa vitendo hivyo ni kosa la jinai. Pia aliwahimiza wananchi kujenga tabia ya kuandika wosia mapema na kusajili bodi za udhamini ili kupunguza migogoro ya kifamilia na mali. Kwa upande wao, baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma hizo, akiwemo Linda Samwel, mkazi wa Tangini, na Jonathan Isack, wameishukuru kampeni hiyo kwa kusogeza huduma karibu na kurahisisha upatikanaji wa huduma ambazo awali zilihitaji kusafiri umbali mrefu na kutumia muda zaidi.

Fri, 30 Oct 2026 11:43:00 +0000
Uncategorized · The Standard

Standard Group appoints Dr Naim Bilal Yaseen as new Group CEO

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Russia offers 70 additional scholarships to Kenyan students

Latest · DIPLOMACY

Recently

Page 530 of 1169 · 23375 stories