Search the region
23382 stories
MSTAHIKI MEYA AKITAKA KIWANDA CHA A-ONE KUACHA KUTIRIRISHA MAJI TAKA KWA WANANCHI
MSTAHIKI Meya Manispaa ya Kibaha Dkt Nicas Mawazo amekielekeza kiwanda cha A-One kilichopo Kata ya Visiga kuacha kutirirsha majitaka kwenye maeneo ya makazi ya watu ambapo yanaenda kusababisha athari za kiafya kwa binadamu na viumbe hai na kuwapatia siku 14 kujenga mfumo wa uchakataji maji taka. Kiwanda hicho kinajishughulisha na ununuaji wa chupa za plastiki na kuzichakata kisha Kupata malighafi mpya, ambapo Malighafi hiyo inaweza kutumika kutengeneza bidhaa nyingine za plastiki au kuuzwa kwa viwanda vinavyohitaji malighafi hiyo. Mstahiki Meya Dkt Nicas ametoa maelekezo kwa kiwanda hicho kuwa hawaruhusiwi kutiririsha maji taka bila kibali kutoka kwa Bonde la Wami Ruvu na hata baada ya kupatiwa kibali ni lazima maji hayo yawe yametibiwa ili yasiwe na athari kwa wananchi wa maeneo ya karibu. Dkt Nicas amesema, Manispaa ya Kibaha ipo makini katika kuhakikisha afya za wananchi wake zinakuwa salama, kutiririsha maji haya kwenye mazingira ya wakazi sio salama na hivyo anawapatia siku 14 kuweza kujenga mfumo sahihi wa kuchakata maji taka na wafuatilie kibali ili waruhusiwe kutiririsha maji ambayo tayari washayatibu na hayatakuwa na madhara kwa wananchi. Afisa Mazingira Manispaa ya Kibaha, Byson Mpogoza amesema kiwanda cha A-One wamekuwa wanawapa maelekezo zaidi ya mara mbili ila wamekuwa ni watu wasiofuata maelekezo hayo na Mstahiki Meya ameagiza kiwanda hiki waandikiwe ilani na pia amewapatia wiki mbili za kurekebisha makosa yao kabla ua kuwachukulia hatua zinazostahiki. Mstahiki Meya Dkt Nicas ameendelea na ziara zake za kukagua viwanda ndani ya Manispaa ya Kibaha ambavyo amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo.
Fri, 30 Oct 2026 04:50:26 +0000Marioo amshika mkono Malaika Gray
MSANII wa Bongo Fleva, Omary Mwanga maarufu Marioo, amekuwa wa kwanza kufanya wimbo na mwimbaji na mtunzi Mtanzania, Malaika Gray uliopewa jina la My Fever.
RecentlyMSHIKEMSHIKE 29/10/2026 - AZAMTV
Azam TV
2026-10-30T04:21:55+00:00NBCPL | Walichokizungumza makocha wa Namungo na Polisi Tanzania
#NBCPL Imemalizika na pointi tatu zimebaki kwa Wauaji wa Kusini....! FT: Namungo FC 1-0 Polisi Tanzania LIVE #AzamSports1HD #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi #NamungoFCVSPolisiTanzania #NamungoFC #PolisiTanzania
2026-10-30T04:33:24+00:00Woman found buried in shallow grave in Kajiado,husband arrested
Latest · News
RecentlyCHIBAMBA AZITAKA NCHI ZA ZIWA TANGANYIKA KUONGEZA UFADHILI
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV NCHI nne zinazopakana na Ziwa Tanganyika zimetakiwa kuimarisha ufadhili, udhibiti wa mafuriko na uhifadhi wa samaki ili kulinda ziwa hilo na jamii zinazotegemea rasilimali zake kwa maisha na shughuli za kiuchumi. Mwenyekiti wa kikao cha maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika (LTA), Dkt. Douty Chibamba, ametoa wito huo leo Oktoba 29, 2026, jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa maandalizi ya Mkutano wa 14 wa Kawaida wa Mawaziri wa mamlaka hiyo. Dkt. Chibamba amesema upatikanaji wa fedha za kutosha na za uhakika, pamoja na maamuzi yanayozingatia ushahidi wa kisayansi, ni muhimu katika kutekeleza makubaliano ya kikanda na kufikia malengo yaliyowekwa. Amewataka wajumbe kuandaa mapendekezo mahususi kuhusu mpango kazi na bajeti ya mwaka 2027, akisisitiza kuwa Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Tanzania na Zambia zinapaswa kuhakikisha vipaumbele vyao vinaendana na upatikanaji wa fedha na watumishi wenye sifa stahiki. “Vipaumbele vyetu lazima viambatane na ufadhili wa kutosha na wa uhakika, ikiwemo kutimiza kwa wakati wajibu wa kifedha wa nchi wanachama,” amesema. Akizungumzia udhibiti wa mafuriko, Dkt. Chibamba ametaja pendekezo la kuondoa tope na mchanga katika Mto Luga na kufanya upembuzi yakinifu kuhusu uwezekano wa kujenga bwawa la kudhibiti viwango vya maji katika Ziwa Tanganyika. Amesema mapendekezo hayo yanahitaji tathmini za kina za kisayansi na kiufundi ili kubaini uwezekano wa kuyatekeleza na athari zake kwa jamii, miundombinu na mazingira. Kuhusu uvuvi, amehimiza kufanyika kwa tafiti za kisayansi zitakazobaini hali ya akiba ya samaki na kusaidia kuweka mikakati ya uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali hiyo. Aidha, amewataka wajumbe kuchambua ripoti ya mwaka ya mamlaka hiyo, kubaini mapungufu ya kiutendaji na kupendekeza hatua za kuimarisha uwajibikaji, uratibu na utendaji, huku nchi wanachama zikishughulikia changamoto za uhaba wa fedha na watumishi. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Reuben Kwagilwa, amesema ushirikiano wa Burundi, DRC, Tanzania na Zambia ni muhimu katika kusimamia rasilimali za ziwa na kulinda mazingira kwa manufaa ya jamii zinazozitegemea. Amesema wajumbe wanatarajiwa kuwasilisha mapendekezo kuhusu sera, masuala ya kiufundi, uimarishaji wa taasisi na ufadhili ili yazingatiwe na mawaziri katika mkutano huo. Mkutano huo umewakutanisha maafisa wa serikali, wataalamu na washirika wa maendeleo kutoka nchi hizo nne zinazopakana na Ziwa Tanganyika.
Fri, 30 Oct 2026 04:44:19 +0000Tanzania Grants TPDC Four Oil and Gas Exploration Licences, Takes Over Songosongo Operations
Read the full report from the original source.
RecentlyGermany news: Merz calls for global free trade alliance in Asia
Read the full report from the original source.
RecentlyJuma Jux: Maisha ya kimuziki yalibadilikia hapa...!
Mafanikio makubwa ya Jux kimuziki hasa upande wa kimataifa, yalianza kuonekana mara baada ya kuachia kolabo yake na Diamond Platnumz, Enjoy (2023) ambayo ilitayarishwa na S2kizzy kutokea studio...
RecentlyMan convicted over 6.7 Million fraud using forged KCSE certificate
Latest · News
RecentlyRekodi ngumu inayozisubiri Simba, Yanga CAF
Read the full report from the original source.
RecentlyUS uncovers alleged $200m ghost student fraud linked to Kenyan network
DIPLOMACY · Quick read
RecentlyOburu dismisses calls for written pre-2027 deal with UDA by ‘ODM outsiders’
News · 4 hours ago
RecentlyRussia-Africa agricultural ties key to strengthening food security, says analyst
Latest · AGRICULTURE
RecentlyIKIBIRIRAHO , Israel: Imigambwe itavuga rumwe n’ubutegetsi yagirije Netanyahu kugerageza gutuma ivyavuye mu matora bitemerwa
Imigambwe itavuga rumwe n’ubutegetsi hamwe n’iyihurikiyemwo Abayahudi b’Abarabu yateye ivyatsi Benjamin Netanyahu, inyuma y’uko avuze ko amatora yibwe.
RecentlyNeville warns managers need sacking 'for their own good' as Carrick fights on
Read the full report from the original source.
RecentlyVenezuela: Opposition leader Machado says US backs 2027 election
Read the full report from the original source.
RecentlyKivuli cha Ferguson chaitesa Man United
Read the full report from the original source.
RecentlyCRA recommends Sh457 billion allocation to counties in equitable share
Read the full report from the original source.
RecentlyBayer wins Roundup cancer trial after Supreme Court ruling
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 542 of 1170 · 23382 stories