Unganishwa

Search the region

23312 stories

Business · Issa Michuzi

SELF MICROFINANCE FUND KUPANUA HUDUMA ZA MIKOPO NAFUU

Afisa  Mtendaji Mkuu wa Self Microfinance  Fund Santiel Yona akizungumza na wahariri kuhusiana na mafanikio na Mikakati ya Taasisi hiyo huduma za  Mikopo ya Kifedha  Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia  Positive Cooker Atukuzwe Nkya akuzungumza kuhusiana na wanavyoshirikiana na Self Microfinance Fund kutoa kutoa mikopo ya nishati Safi ya Kupikia. Afisa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma katika Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Alex Malanga akizungumza kuhusiana na Ofisi hiyo ilivyojipanga katika Taasisi zilizochini ya Msajili kutoa taarifa za maandeleo Mwakilishi wa Mwenyekiti wa TEF ,Bakari Kimwanga akizungumza kuhusiana na umuhimu wa taarifa kwa wananchi kuhusiana na huduma za kifedha za Mikopo zinazotolewa na Self Microfinance Fund ,jijini Dar es Salaam. Baadhi ya matukio katika picha Katika mkutano uliohusisha wahariri na Self Microfinance Fund Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam MFUKO wa Self Microfinance Fund umeeleza kuwa umejipanga kupanua wigo wa huduma za mikopo nafuu kwa wananchi, hususan wakulima, wafugaji na wajasiriamali, ili kuwawezesha kukuza shughuli zao za kiuchumi na kuchangia maendeleo ya taifa. Hatua hiyo inalenga kutimiza malengo ya kuanzishwa kwa mfuko huo, ikiwamo kuwapa wananchi fursa ya kupata huduma za kifedha na kuondoa dhana kwamba Watanzania hawakopesheki kutokana na changamoto za urejeshaji wa mikopo katika taasisi za kifedha. Hayo yameelezwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa mfuko huo, Santiel Yona, wakati wa kikao kazi kati ya taasisi hiyo, Ofisi ya Msajili wa Hazina na wahariri wa vyombo vya habari, jijini Dar es Salaam, kilicholenga kueleza mafanikio yaliyopatikana. Yona alisema katika mwaka wa fedha 2024/2025, mfuko huo umechangia upatikanaji wa ajira 262,624, huku ukiendelea kutoa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wajasiriamali. Alisema mfuko huo una uwezo wa kutoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 54, hivyo kuwataka Watanzania kutumia fursa hiyo kuendeleza shughuli zao za uzalishaji na biashara. Akizungumzia urejeshaji wa mikopo, Yona alisema kiwango cha urejeshaji kimefikia asilimia 95, hali inayoonesha mwenendo mzuri katika usimamizi wa mikopo inayotolewa na taasisi hiyo. Alisema mfuko umeweka mikakati ya kuendelea kuimarisha urejeshaji wa mikopo kwa kufanya tathmini ya uwezo wa wakopaji, kuchunguza sababu zinazowafanya baadhi yao kushindwa kulipa kwa wakati na kuweka utaratibu wa kuwasaidia kurejesha mikopo yao. Alifafanua kuwa hatua hizo ni pamoja na kuingia mikataba mipya pale inapohitajika na kuwaongezea wakopaji muda wa kurejesha mikopo kulingana na taratibu zilizowekwa. “Aliyekopa ni lazima arejeshe fedha alizokopa. Tunaweza kumuongezea muda wa kulipa hadi miaka miwili, kuingia naye mkataba mpya na kujua sababu zilizomfanya ashindwe kurejesha mkopo wake kwa wakati,” alisema Yona. Kwa upande wake, Manongi alisema katika kipindi cha miaka mitatu, Self Microfinance Fund imefanikiwa kufungua matawi 12 yanayotoa huduma katika kanda mbalimbali nchini, hatua inayolenga kusogeza huduma za kifedha karibu na wananchi. Alisema mafanikio mengine ni pamoja na kutoa gawio la Sh milioni 490.9 na kupata faida ya Sh bilioni 3.19 baada ya kodi. Aidha, alisema mfuko huo unashiriki katika juhudi za kukuza matumizi ya nishati safi kupitia mradi wa mikopo ya majiko yanayotumia umeme kwa ufanisi, kwa kushirikiana na kampuni ya Positive Cooker. Aliongeza kuwa mfuko huo pia unatoa mikopo kwa ajili ya ununuzi wa bajaji na pikipiki, zinazoweza kutumiwa na wajasiriamali wadogo katika kuendesha na kupanua shughuli zao za kiuchumi. Katika hatua nyingine, Afisa Mtendaji Mkuu alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mchango wake katika kuwezesha mafanikio ya Self Microfinance Fund.

Wed, 28 Oct 2026 12:45:55 +0000
Uncategorized · Daily News

Dr Bashiru pushes for livestock keepers’ direct benefits from subsidised pasture seeds

MPWAPWA: THE Minister for Livestock and Fisheries, Dr Bashiru Kakurwa has stressed the importance of livestock keepers to directly benefit…

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Rescuers detect signs of life in Eastleigh building

National Disaster Management Director Duncan Onyango said specialised acoustic life detectors had picked up signs of life during the ongoing operation

Recently
Uncategorized · Daily News

Makonda envisions Tanzania to host Miss World pageant if ongoing talks succeed

DODOMA: THE Minister for Information, Culture, Arts and Sports, Paul Makonda, has said that Tanzania can host the Miss World…

Recently
Uncategorized · Daily News

Tanzania tasked to use its growing oil and gas industry in creating jobs

DODOMA: TANZANIA has been urged to strengthen local participation in the oil and gas sector by equipping young people with…

Recently
Uncategorized · Daily News

Tanzania issues oil and gas exploration licences for Mnazi Bay, Songo Songo, Eyasi Wembere, Lindi-Mtwara blocks

DAR ES SALAAM: THE Energy Minister Dr Juma Homera has signed four oil and gas exploration licences for the Mnazi…

Recently
Uncategorized · Daily News

Tanzania lifts the lid on issuance of 4 gas exploration licences to TPDC

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda Inspirer

Low salaries and staff shortages put pressure on Rwanda’s nurses and midwives

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Chimpreports

Mbale, China’s Guiyang City Sign Deal to Boost Coffee Exports

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Chimpreports

Police, NWSC Agree to Vacate Busega–Mpigi Expressway Route Before Compensation

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Let us not make politics a matter of life and death - DP

DP argued that political disagreements should not turn into personal hostility, urging leaders to conduct their engagements in a manner that promotes unity

Recently
Uncategorized · SoftPower News

UCAA, Uganda Airlines Rally Girls to Pursue Aviation Careers

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

MPANGO WA MIAKA MITANO NGORONGORO NI DIRA YA KULINDA UHAI WA HIFADHI: JENERALI MABEYO

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Jenerali Mstaafu Venance Mabeyo, ameipongeza mamlaka hiyo kwa kuandaa Mpango Mkakati wa Shirika (CSP) wa miaka mitano na Mpango wa Muda Mrefu (LTTP) wa miaka 25 unaozingatia uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii. Mabeyo ametoa pongezi hizo jijini Arusha wakati wa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kinachojadili utekelezaji wa shughuli za mamlaka hiyo kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027, kuanzia Julai hadi Septemba. Amesisitiza kuwa uhifadhi wa ikolojia ya Hifadhi ya Ngorongoro na Pori la Akiba la Pololeti unapaswa kupewa kipaumbele na kulindwa kwa nguvu zote kutokana na mchango wake katika kuimarisha uhifadhi, kulinda ajira za Watanzania na kuongeza mapato ya Serikali kupitia utalii. Ameeleza kuwa mapato yanayotokana na utalii huchangia kuboresha huduma za jamii na kuchochea maendeleo ya taifa. Kwa upande wake, Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA, Abdul-Razaq Badru, amesema mipango hiyo imezingatia nyaraka na miongozo mbalimbali ya Serikali, ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025–2050 na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2025–2030.

Wed, 28 Oct 2026 13:00:09 +0000
Sports · Azam TV Videos

CAF DRAW | Alichokisema Makamu wa Rais wa Yanga SC, Arafat Haji baada ya droo

CAF DRAW | ''Huwezi kuwa bora kama hujakutana na wenzako mnaolingana viwango'' Makamu wa Rais wa Yanga SC, Arafat Haji amesema timu hiyo ina uzoefu na baadhi ya wapinzani waliopangwa nao katika hatua ya makundi, huku akisisitiza kuwa watajipanga kuhakikisha wanafanya vizuri. Aidha, amewahimiza mashabiki kuendelea kuisapoti timu yao katika safari hiyo ya mashindano. Mambo yako LIVE #AzamSport1HD.

2026-10-28T12:51:32+00:00
Uncategorized · Agence Burundaise de Presse

La première dame burundaise attendue à Dakar

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

Bolt Send Yakua Zaidi ya Mara Sita Katika Usafirishaji wa Bidhaa Tanzania

Bolt Send imeongezeka kwa zaidi ya mara sita katika shughuli za usafirishaji wa bidhaa nchini Tanzania tangu ilipozinduliwa Agosti 2024, hali inayoonesha kuongezeka kwa kasi kwa mahitaji ya huduma za haraka na rahisi za kusafirisha bidhaa ndani ya miji bila wateja au wafanyabiashara kulazimika kufanya safari wenyewe. Huduma hiyo, ambayo sasa inapatikana katika miji minne nchini Tanzania, imekua kwa takribani mara 6.6 kutoka ilipozinduliwa hadi Aprili 2026, huku shughuli zake zikiongezeka kwa asilimia 46.4 kati ya Januari na Julai 2026. Kwa sasa, Tanzania ina kiwango cha matumizi ya Bolt Send kilicho juu kwa asilimia 22.5 ikilinganishwa na Ghana. Ukuaji huo unaonesha mabadiliko ya tabia za watumiaji mijini, ambapo watu wanazidi kutarajia nyaraka, manunuzi, vifurushi na bidhaa mbalimbali kufikishwa kwa urahisi sawa na jinsi wanavyopata huduma za usafiri wa abiria. Kwa wafanyabiashara, hususan wafanyabiashara wadogo ambao hawana magari au mfumo wao wa usafirishaji, huduma hii inawapa fursa ya kuwafikia wateja bila kulazimika kuwekeza katika miundombinu yao wenyewe ya usafirishaji. Dar es Salaam inaendelea kuwa soko kuu la Bolt Send nchini, ikichangia asilimia 98.2 ya shughuli zote za huduma hiyo Tanzania. Shughuli za usafirishaji jijini humo zimekua kwa mara 6.4 tangu huduma hiyo ilipozinduliwa hadi kufikia kiwango chake cha juu miezi 20 baadaye. Ukuaji pia unaongezeka nje ya Dar es Salaam. Dodoma imerekodi ongezeko la mara 11 la safari za usafirishaji ndani ya miezi 13 tangu huduma hiyo kuzinduliwa, huku Mwanza, ambako Bolt Send ilizinduliwa Mei 2026, ikifikia takribani mara nane ya kiwango chake cha awali ndani ya miezi miwili. Arusha nayo inaendelea kurekodi ukuaji wa mwezi hadi mwezi. Takwimu hizo zinaonesha kuwa mahitaji ya huduma rahisi za usafirishaji hayapo Dar es Salaam pekee, bali yanaanza kuwa sehemu ya shughuli za kila siku za biashara katika miji mingine nchini. Ubora wa huduma umeendelea kuwa wa kiwango cha juu sambamba na ukuaji huo, huku wasafirishaji wakipata wastani wa alama 4.88 kati ya 5 kutoka kwa wateja. Kwa wastani, safari moja ya Bolt Send hufikia umbali wa takribani kilomita 7.7. “Si lazima mtu aache kazi, afunge biashara au avuke jiji kwa ajili tu ya kupeleka bidhaa moja,” alisema Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu Mwandamizi wa Bolt Afrika Mashariki. “Ukuaji tunaouona unaonesha fursa iliyopo kwa teknolojia kuondoa changamoto ndogo za usafirishaji na kuwapa wateja na wafanyabiashara nafasi ya kutumia muda wao katika shughuli zenye tija zaidi,” aliongeza. Bolt sasa inajiandaa kupanua huduma ya Send hadi Morogoro kabla ya mwisho wa mwaka 2026. Fursa inaendelea kuwa wazi zaidi: kadri miji ya Tanzania inavyokua na biashara kuhitaji huduma za haraka zaidi, huduma rahisi za usafirishaji wa hatua ya mwisho zinaweza kuwa kiungo muhimu zaidi kati ya wateja, wauzaji na wafanyabiashara.

Wed, 28 Oct 2026 05:30:00 +0000
Uncategorized · BBC Afrique

Ce que l'on sait jusqu'à présent sur le tragique accident ferroviaire en Espagne

Plus de 500 passagers se trouvaient à bord des trains lorsque l'incident s'est produit dans la province de Tolède, au sud de Madrid.

Recently
Uncategorized · Agence Burundaise de Presse

La lutte contre la corruption, une affaire de tous

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · UBC

Janet Museveni Urges Collective Effort to Equip Young Ugandans With Life Skills

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

MABEYO AIPONGEZA NCAA KWA MIPANGO YA UHIFADHI YA MIAKA 25

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Jenerali Mstaafu Venance Mabeyo, ameipongeza mamlaka hiyo kwa kuandaa Mpango Mkakati wa Shirika (CSP) wa miaka mitano na Mpango wa Muda Mrefu (LTTP) wa miaka 25 unaozingatia uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii. Mabeyo ametoa pongezi hizo jijini Arusha wakati wa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kinachojadili utekelezaji wa shughuli za mamlaka hiyo kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027, kuanzia Julai hadi Septemba. Amesisitiza kuwa uhifadhi wa ikolojia ya Hifadhi ya Ngorongoro na Pori la Akiba la Pololeti unapaswa kupewa kipaumbele na kulindwa kwa nguvu zote kutokana na mchango wake katika kuimarisha uhifadhi, kulinda ajira za Watanzania na kuongeza mapato ya Serikali kupitia utalii. Ameeleza kuwa mapato yanayotokana na utalii huchangia kuboresha huduma za jamii na kuchochea maendeleo ya taifa. Kwa upande wake, Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA, Abdul-Razaq Badru, amesema mipango hiyo imezingatia nyaraka na miongozo mbalimbali ya Serikali, ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025–2050 na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2025–2030.

Wed, 28 Oct 2026 12:50:54 +0000

Page 575 of 1166 · 23312 stories