Search the region
23275 stories
Ikibazo cy'abahinzi bahawe imashini itogosa ibitunguru kandi baguze iyumisha kiri mu rukiko - Minagri
Read the full report from the original source.
RecentlyRuto directs CS Joho to open Magadi mining industry to new investors
Read the full report from the original source.
RecentlyEbola: 20 contacts released from quarantine in Kenya, amid vaccine ‘hope’ in DR Congo
Read the full report from the original source.
RecentlyFour in five domestic workers lack formal job protections, UN finds
Read the full report from the original source.
RecentlyRevealed: Where stolen water meters in Dodoma end up
Read the full report from the original source.
RecentlyKenya becomes regional abduction hub
Kenya has long been a beacon of hope for those fleeing conflict and repression in the Great Lakes region and the Horn of Africa. That beacon is now dead.
Wed, 28 Oct 2026 00:00:00 +0300Uburusiya bwahishuye uko ibihugu bya Afurika byanze kubutera umugongo nubwo byotswaga igitutu
Umuvugizi wa Minisiteri y’ububanyi n’amahanga y’Uburusiya, Maria Zakharova, yatangaje ko ibihugu bya Afurika byakomeje gushikama mu mibanire yabyo n’u Burusiya, nubwo byotswaga igitutu gikomeye n’ibihugu by’u Burengerazuba byo kubutandukaho.
Tue, 27 Oct 2026 18:49:06 +0200Dar bridges African, Russian women in nuclear
Read the full report from the original source.
RecentlyUnconfirmed Reports Claim Museveni Endorsed Muhoozi at NRM CEC Meeting in Entebbe
ENTEBBE | Unconfirmed reports circulating on Tuesday claim President Yoweri Museveni endorsed his son, Chief of Defence Forces Gen. Muhoozi Kainerugaba, during a Central Executive Committee (CEC) meeting of the…
RecentlyLOCAL GOVERNMENT: I am implementing Museveni’s Anti- Corruption Directive’- Kumumanya
The Permanent Secretary explains the Ministry of Local Government’s role in accountability, decentralisation and improving service delivery. By Brian Mugenyi When President Yoweri Museveni appointed Benjamin Kumumanya am
RecentlyWorld News in Brief: ‘No safe place in Ukraine’, IAEA calls for Iran nuclear inspections, Kenya hosts thousands of Ethiopians fleeing clashes
Read the full report from the original source.
RecentlyIsrael election: Anti-Netanyahu bloc ahead, but no majority
Read the full report from the original source.
RecentlyIsrael election: Anti-Netanyahu bloc ahead, but no majority
Read the full report from the original source.
RecentlyMCHENGERWA AWATAKA WAFAMASIA KUZINGATIA MAADILI, UBORA WA DAWA
Na Mwandishi Wetu, Arusha WAZIRI wa Afya, Mohammed Mchengerwa, amewataka wafamasia na wataalamu wa dawa nchini kuzingatia maadili ya taaluma na kuhakikisha viwanda vya dawa vinavyojengwa nchini vinazalisha dawa salama na zenye ubora unaokidhi viwango vinavyotakiwa. Mchengerwa ameyasema hayo leo, Oktoba 27, 2026, jijini Arusha, wakati akifungua Kongamano la 27 la Chama cha Wateknolojia Dawa Tanzania (TAPHATA), akisisitiza kuwa kuimarisha uzalishaji wa dawa nchini kutapunguza utegemezi wa bidhaa hizo kutoka nje, kuongeza ajira na kukuza uchumi wa taifa. Amesema Serikali inalenga kuhakikisha Tanzania inazalisha asilimia 70 ya mahitaji yake ya dawa ifikapo mwaka 2030, hatua inayohitaji ushirikiano kati ya Serikali, wawekezaji, taasisi za udhibiti na wataalamu wa dawa. Amesisitiza kuwa wataalamu hao hawapaswi kushawishiwa na maslahi binafsi yanayoweza kuhatarisha ubora na usalama wa dawa, akibainisha kuwa jukumu lao kuu ni kulinda afya za Watanzania. Ameongeza kuwa kukua kwa viwanda vya dawa kutafungua fursa za ajira katika maeneo mbalimbali, yakiwemo uzalishaji, utafiti, uhakiki wa ubora, usajili wa bidhaa na usimamizi wa ugavi wa dawa. Kwa upande wake, Rais wa TAPHATA, Thabiti Milandu, amesema kongamano hilo ni fursa kwa wataalamu kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto za sekta na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuboresha taaluma, usalama wa dawa na upatikanaji wa huduma bora za afya. Milandu amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya wataalamu, taasisi za Serikali, vyuo vya mafunzo, sekta binafsi na wadau wa maendeleo ili kukuza viwanda vya ndani na kuhakikisha vinakidhi mahitaji ya soko. Aidha, ameeleza kuwa kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza fursa za mafunzo endelevu kutawajengea uwezo wataalamu wa dawa kushiriki kikamilifu katika uzalishaji na matumizi ya teknolojia za kisasa, huku kukipanua wigo wa ajira katika sekta ya umma na binafsi. Naye Mfamasia wa Viwanda kutoka Wizara ya Afya, Felista Rugarabamu, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ujuzi wa wataalamu wa Kitanzania katika uzalishaji wa dawa, utafiti na matumizi ya teknolojia za kisasa. Amesema uwekezaji katika mafunzo, utafiti na uhamishaji wa teknolojia utasaidia kuongeza uwezo wa viwanda vya ndani, kupunguza changamoto ya upatikanaji wa wataalamu wenye ujuzi maalumu na kuimarisha uzalishaji wa dawa zinazokidhi viwango vya ubora na usalama. Ameongeza kuwa ushirikiano endelevu kati ya Serikali, wataalamu wa dawa na sekta binafsi ni muhimu katika kujenga tasnia imara itakayokidhi mahitaji ya ndani na kupanua fursa za soko la kikanda. Waziri wa Afya,Mohammed Mchengerwa akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wadhamini wa Kongamano la 27 la Chama cha Wateknolojia Dawa Tanzania (TAPHATA) jijini Arusha. Wajumbe wa Kongamano la 27 la Chama cha Wateknolojia Dawa Tanzania (TAPHATA) jijini Arusha. Waziri wa Afya,Mohammed Mchengerwa akifungua Kongamano la 27 la Chama cha Wateknolojia Dawa Tanzania (TAPHATA) jijini Arusha. Mfamasia wa Viwanda kutoka Wizara ya Afya, Felista Rugarabamu akiwasilisha mada wakati wa kongamano hilo jijini Arusha. Wajumbe wa Kongamano la 27 la Chama cha Wateknolojia Dawa Tanzania (TAPHATA) jijini Arusha.
Tue, 27 Oct 2026 20:19:00 +0000Tayebwa Proposes Reconciliation Committee to Address Political Tensions
Read the full report from the original source.
RecentlyNATCOM KUIMARISHA UHIFADHI WA URITHI PEMBA KUPITIA UTAFITI NA ELIMU
Pemba, Zanzibar | 24 Oktoba 2026 Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (NATCOM) imeeleza dhamira ya kuimarisha uhifadhi wa urithi wa Pemba kupitia utafiti na uwekaji kumbukumbu za maarifa ya tiba asili, pamoja na kuandaa mwongozo wa kuongoza Vilabu vya Urithi (Heritage Clubs) mashuleni. Dhamira hiyo ilielezwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (NATCOM), Profesa Hamisi Masanja Malebo, alipokuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Urithi Pemba yaliyofanyika tarehe 24 Oktoba 2026. Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Uhifadhi wa Urithi Pemba (Pemba Heritage Conservation Society – PHCS) chini ya kaulimbiu “Urithi Wetu – Hatma Yetu.” Akizungumza katika maadhimisho hayo, Profesa Malebo alisema urithi wa Pemba ni sehemu muhimu ya utambulisho wa jamii, unaojumuisha maeneo ya kihistoria, utamaduni, lugha, maarifa ya jadi na mazingira asilia. Alibainisha kuwa kuutunza kunahitaji juhudi zinazoratibiwa na taasisi, jamii na wadau mbalimbali. NATCOM KUUNGA MKONO UTAFITI WA TIBA ASILI Profesa Malebo alisisitiza umuhimu wa kutafiti na kuweka kumbukumbu za maarifa ya tiba asili ya Pemba, ambayo yamerithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Alisema kumbukumbu rasmi zitasaidia kuhifadhi maarifa hayo na kupunguza hatari ya kupotea kwake. “Ni lazima tufanye utafiti wa kina na wa haraka ili kuorodhesha na kuweka kumbukumbu rasmi za tiba asili zote walizotumia mababu zetu hapa Pemba,” alisema Profesa Malebo. Alieleza kuwa NATCOM itashirikiana na Wizara ya Afya pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHIR), kama ilivyotajwa katika hotuba yake, katika juhudi za kufanya utafiti na kuhifadhi maarifa hayo. Utafiti huo unapaswa kuzingatia taratibu husika, usalama na ubora pale maarifa hayo yanapohusishwa na matumizi ya afya. Katika risala yake, PHCS iliomba kufanyika kwa tafiti kuhusu mimea ya asili iliyotumiwa na wazee kutibu maradhi mbalimbali, pamoja na maeneo ya kihistoria ya Pemba. Ombi hilo linaonyesha nafasi ya ushirikiano kati ya taasisi za uhifadhi na wadau wa utafiti katika kutambua na kuweka kumbukumbu za maarifa ya jadi. VILABU VYA URITHI KUIMARISHA ELIMU MASHULENI Katika eneo la elimu, Profesa Malebo alisema NATCOM itashirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuandaa mwongozo rasmi wa kuanzisha na kuendesha Vilabu vya Urithi mashuleni. Alieleza kuwa shule ni mazingira muhimu ya kuwajengea watoto na vijana uelewa kuhusu historia na utamaduni wa maeneo yao. Kupitia vilabu hivyo, wanafunzi wanatarajiwa kujifunza kuhusu maeneo ya kihistoria, mila, desturi na rasilimali asilia, na kushiriki katika shughuli za kuhamasisha utunzaji wake. Kwa mujibu wa risala ya PHCS, mpango huo unatarajiwa kuhusisha ziara za kielimu katika maeneo ya kihistoria, mashindano na shughuli nyingine za kuwasaidia wanafunzi kuongeza maarifa kuhusu Pemba. Jumuiya hiyo pia iliomba Profesa Malebo kuwa mlezi wa Vilabu vya Urithi Pemba; ombi hilo liliwasilishwa katika risala wakati wa maadhimisho. URITHI WA PEMBA NA FURSA ZA MAENDELEO Profesa Malebo alitaja Ras Mkumbuu, Jambangome, Ngome ya Mkamandume iliyopo Pujini na Msitu wa Ngezi kuwa miongoni mwa maeneo yenye umuhimu wa kihistoria na kimazingira yanayopaswa kutambuliwa na kutunzwa. Alieleza kuwa urithi wa Pemba unajumuisha pia lugha ya Kiswahili, sanaa za kitamaduni, mila na maarifa ya jadi yanayobeba historia na utambulisho wa jamii. Alisisitiza kuwa utalii wa kiutamaduni na kiikolojia unaweza kutoa fursa za kiuchumi kwa wananchi, iwapo utaendelezwa kwa kuzingatia ulinzi wa maeneo, ushirikishwaji wa jamii na sheria husika. PHCS ilieleza kuwa mojawapo ya malengo yake ni kuelimisha jamii kuhusu utunzaji wa maeneo ya kihistoria na kuhamasisha wananchi kutambua fursa za utalii katika maeneo yao. Jumuiya hiyo pia iliripoti kuwa mazungumzo ya awali na wadau yameanza kuhusu mradi wa Tanga–Pemba unaohusu urithi wa baharini. UTUNZAJI WA MAZINGIRA NI SEHEMU YA URITHI Profesa Malebo alihimiza wananchi kupanda na kutunza miti ya kivuli, matunda na dawa, akieleza kuwa utunzaji wa mazingira ni sehemu ya kulinda urithi wa asili na kusaidia ustawi wa jamii. Pia alizipongeza Serikali, PHCS na wadau wengine kwa juhudi za upandaji wa mikoko katika maeneo ya Tinga Tinga na Tibirinzi, Chake Chake. Mikoko huchangia kulinda makazi ya viumbe wa baharini na mazingira ya pwani, na ina umuhimu kwa jamii zinazotegemea rasilimali hizo. Katika risala yake, PHCS ilieleza kuwa tangu kusajiliwa tarehe 8 Machi 2021, imefanya shughuli zikiwemo upandaji wa mikoko, usafi wa maeneo ya kihistoria, vipindi vya elimu kupitia redio na televisheni, na uhamasishaji wa uhifadhi mashuleni na katika jamii. Hata hivyo, jumuiya hiyo ilitaja uhaba wa fedha na vitendea kazi kuwa miongoni mwa changamoto zake. USHIRIKIANO KWA MANUFAA YA VIZAZI VIJAVYO Maadhimisho hayo yaliwakutanisha wawakilishi wa taasisi za Serikali, asasi za kiraia, walimu, waandishi wa habari na wanafunzi kutoka skuli sita za Pemba. Katika hotuba yake, Profesa Malebo alihimiza jamii na vijana kujifunza historia ya maeneo yao na kushiriki katika kulinda maeneo ya kale. Alisisitiza pia umuhimu wa taasisi za Serikali, mamlaka za uhifadhi, sekta binafsi na wadau wengine kushirikiana katika juhudi hizo. Maadhimisho hayo yameweka msisitizo katika kuunganisha utafiti, elimu, utunzaji wa mazingira na ushiriki wa jamii katika kulinda urithi wa kihistoria, kiutamaduni na asili wa Pemba. Kupitia juhudi zake na ushirikiano na wadau, NATCOM inaendelea kuhamasisha uelewa kuhusu maeneo ya kazi ya UNESCO nchini na mchango wake katika maendeleo endelevu. Kaulimbiu “Urithi Wetu – Hatma Yetu” inasisitiza kuwa kulinda historia, utamaduni, mazingira na maarifa ya jadi ni wajibu wa pamoja, unaohitaji juhudi endelevu ili urithi wa Pemba uweze kuthaminiwa na kurithishwa kwa vizazi vijavyo.
Tue, 27 Oct 2026 20:15:58 +0000MKURUGENZI MKUU TBS ATAJA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA SERIKALI AWAMU YA SITA
-Aelezea jinsi shirika lilivyotumia mabilioni ya fedha kusogeza huduma karibu na wananchi -Asema TBS ina jumla ya maabara 14 na zote zimeweza kupata ithibati za umahiri Na Said Mwishehe,Michuzi TV KATIKA kipindi cha Serikali ya awamu ya Sita (2021-2026), chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan Shirika la Viwango Tanzania( TBS) limekuwa mafanikio makubwa katika utekelezaji wa majukumu yake. Mafanikio hayo yanaendana na kutimiza azma ya Shirika katika masuala mbalimbali yakiwemo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali iliwa na lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi. Hayo yamesemwa leo Oktoba 27,2026 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS) Dkt. Ashura Katunzi alipokuwa akizungumza kwenye kikao kazi kilichohusisha Wahariri wa vyombo vya habari nchini.Kikao kazi hicho kimeratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ikiwa ni muendelezo wa mashirika ya umma na taasisi kutoa taarifa za mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita. Akifafanua zaidi Dk.Katunzi amesema TBS inaendelea na hatua za mwisho za ukamilishaji na makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa maabara na ofisi katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma, au kwa jina jingine mradi wa Viwango House – Dodoma wenye thamani ya TZS 24.7 Bilioni. Pia Shirika linaendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa ofisi na maabara katika Kanda ya Ziwa eneo la Kiseke Wilaya ya Ilemela – Mwanza unaojulikana kama Viwango House- Mwanza ambao unakadiriwa kugharimu Sh.bilioni 12.1 Bilioni huku pia likiwa hatua za awali za maandalizi za mradi wa ujenzi wa ofisi na maabara Jijini Arusha. Pia amesema kwa upande wa Dodoma, maabara zilizojengwa zinahudumia pia mikoa ya karibu na Dodoma hususani Singida na Tabora. Aidha, maabara za Mwanza zinatarajiwa kuhudumia mikoa sita, ambayo ni Mwanza, Kagera, Mara, Geita, Shinyanga na Simiyu. Amefafanua hatua hiyo ya ujenzi wa ofisi na maabara itasaidia kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa majibu ya vipimo vya sampuli. Wakati huo huo amesema Serikali kupitia TBS imetumia zaidi ya Sh.bilioni 9.8 bilioni kwa ajili ya kuimarisha ofisi tisa za kanda. Pia amesema ili kuwezesha Biashara, Shirika lina Kamati za Kitaalam (Technical Commitees) za Uandaaji Viwango 117 katika sekta ya chakula, kemikali, uhandisi mitambo, uhandisi umeme, uhandisi ujenzi, nguo na ngozi, madini na mitambo ya uchimbaji madini, mazingira na taaluma mtambuka (general tecniques). “Katika mchakato wa kuandaa viwango Kamati hizo zinashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo vyuo vikuu, taasisi za utafiti, wafanyabiashara, wazalishaji, vyama vya walaji, vyama na bodi za wataalam, taasisi za udhibiti na watunga sera.” Pia amesema Shirika limefanikiwa kuandaa viwango 3901 vya sekta mbalimbali kwa kuzingatia mahitaji ya soko ambavyo vinasaidia wafanyabiashara, wajasiriamali na watoa huduma kuzalisha bidhaa bora zenye kukidhi matakwa ya viwango, hivyo kuwawezesha kufanya biashara ndani na nje ya nchi, hatua ambayo italeta tija na kuchochea ukuaji wa uchumi. Aidha, jumla ya vyeti na leseni za ubora 3,940 vimetolewakwa wazalishaji, miongoni mwao wakiwemo wajasiriamali wadogo 1,683. Serikali kupitia TBS imekuwa ikitenga zaidi ya TZS milioni 300 kila mwaka kwa madhumuni ya kuhudumia wajasiriamali wadogo bila ya malipo yoyote. “Leseni hizi zimesaidia wazalishaji kuzalisha bidhaa bora, ikiwa ni pamoja na bidhaa zao kuweza kuaminika sokoni na pia kufanya biashara nje ya mipaka ya Tanzania, hivyo kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa Taifa. “Shirika limeendelea na huduma za usajili wa bidhaa za chakula na vipodozi pamoja na maeneo ya uzalishaji, uuzaji, usambazaji na uhifadhi wa chakula na vipodozi kwa lengo la kuhakiki ubora na usalama wa maeneo hayo ili kuendelea kulinda afya za walaji ambapo jumla ya bidhaa 9,731 zilisajiliwa na maeneo 80,836 yalisajiliwa.” Ameongeza katika kuimarisha ukaguzi wa bidhaa zinazoingia nchini kutoka nchi za nje, TBS huhakiki ubora wa bidhaa na magari yaliyotumika kabla ya kusafirishwa kuja nchini ambapo katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita jumla ya shehena za bidhaa 183,186 zilikaguliwa kabla ya kuingia nchini kupitia mfumo wa Pre-Shipment to Conformity (PVoC). “Shehena za bidhaa 426,842 zilikaguliwa baada ya kufika nchini kupitia mfumo wa Destination Inspection (DI).Jumla ya magari 249,386 yalikaguliwa. Bidhaa hizo zinakaguliwa kwa lengo la kuiepusha Tanzania kuwa jalala la bidhaa duni pamoja na kulinda afya, usalama na mazingira ya watumiaji. Kuhusu kuongeza ufanisi wa maabara amesema TBS ina jumla ya maabara 14 na zote zimeweza kupata ithibati za umahiri, ambapo maabara hizo zimehakikiwa na kupatiwa vyeti vya ithibati ya umahiri wa kimataifa. “Hatua hiyo inamaanisha kuwa majibu ya sampuli kutoka katika maabara hizo yanaaminika na kukubalika popote duniani na hivyo kurahisisha biashara ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu.Katika kipindi hicho TBS imeweza kupima sampuli zaidi ya 188,952 na kufanyia ugezi vifaa 54,396ambapo suala hili litasaidia kuhakikisha katika soko kunakuwa na bidhaa zenye ubora.” Pia, maabara hizo zina mashine za kisasa (state-of -art-equipment) zinazopelekea kupata majibu kwa wakati na sahihi, Serikali imeweza kutumia kiasi kisichopungua Sh.12.9 bilioni kuhakikisha mashine hizi zinapatikana. “Kuna mashine za kipekee ikiwemo ya hydrostatic pressure test ya kupima mabomba ya maji na yenye uwezo wa kupima mabomba yenye kipenyo cha milimita 12 sawa na inch 0.5 hadi milimita 800 sawa na inchi 32. Mashine hiyo ina uwezo pia wa kupima sampuli 120 kwa wakati mmojana kati ya nchi 54 za Barani Afrika inapatikana katika nchi tano tu ikiwemo Tanzania.
Tue, 27 Oct 2026 20:07:49 +0000EL NINO IWEPO AU ISIWEPO, UHIFADHI NA UTALII USILALE – MABULA
Na Mwandishi Wetu, Ngorongoro NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Nkoba Mabula, ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kuboresha miundombinu ya barabara, maji, umeme na mawasiliano, pamoja na kuimarisha vitendea kazi na kutoa elimu kwa watumishi na wadau ili kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño zinazotarajiwa. Akiwa katika ukaguzi wa miundombinu ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mabula ameelekeza kasi ya maboresho iongezwe katika maeneo hatarishi, maandalizi ya mitambo na huduma za afya, pamoja na kutolewa kwa mafunzo ya vitendo kwa timu za uokoaji zinazojumuisha maafisa na askari wa uhifadhi. “Kama El Niño itakuja, itukute tumejiandaa. Mitambo, magari ya huduma, mafuta na vipuri viwepo wakati wote ili kuhakikisha usalama wa watalii, wananchi na rasilimali za wanyamapori na malikale zilizopo,” amesema Mabula. Ameongeza kuwa ni muhimu kuweka alama katika maeneo hatarishi ili kuongeza tahadhari kwa watumiaji wa barabara na maeneo mengine yanayoweza kuathiriwa na mvua hizo. Akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa Ngorongoro, SACC Gloria Bideberi, amesema mamlaka hiyo imeendelea kutoa elimu kuhusu namna ya kukabiliana na athari za mvua hizo kwa makundi mbalimbali. Amesema hadi sasa elimu imetolewa kwa watumishi 200, viongozi wa vijiji na kata 275, wanafunzi zaidi ya 1,550 na wananchi 4,965 katika kata 10 zilizopo ndani ya hifadhi. Aidha, amesema maeneo 80 ya huduma za malazi yamehusishwa katika maandalizi hayo, huku magari ya huduma za dharura na vifaa tiba vikiandaliwa kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza. Kwa upande wake, Mratibu wa Shughuli za Miundombinu, Mhandisi Shaban Felician, amesema mitambo zaidi ya 11 imeandaliwa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara, pamoja na uokoaji wa magari ya wageni yanayoweza kukwama kutokana na mvua. Amesema mamlaka hiyo pia inaendelea kuhakikisha mtandao wa barabara wenye urefu wa zaidi ya kilomita 600 ndani ya hifadhi unabaki kupitika katika msimu wote wa mvua, ili kuwezesha shughuli za uhifadhi na utalii kuendelea bila kukwama.
Tue, 27 Oct 2026 20:11:02 +0000President William Ruto leaves the country for Russia
Read the full report from the original source.
RecentlyPresident Ruto heads to Moscow for Russia-Africa Forum
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 589 of 1164 · 23275 stories