Unganishwa

Search the region

23267 stories

Uncategorized · Isango Star

NOTICE OF RESTORATION OF A COMPANY IN THE REGISTER OF COMPANIES

Tue, 27 Oct 2026 17:29:58 +0200
Uncategorized · The Star Kenya

Raila Jr, Arati meet Nairobi ODM aspirants

Raila Junior has recently stepped up his political engagements in ODM as he prepares to contest the Kibra parliamentary seat.

Recently
Uncategorized · BBC Rwanda

RD Congo : 'Ni ikimenyetso c'uko atigeze akunda igihugu', Tshisekedi kuri Kabila na FRN

Ni bwo bwa mbere umutegetsi wa RD Congo agize ico ashikiriza ku mugaragaro kw'ishingwa ry'umuhari FRN na Joseph Kabila awurongoye.

Recently
Uncategorized · Chimpreports

UPDF Major Who Posed as General Charged in Shs13bn Gold Fraud

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Chimpreports

US Hosts Congo, Rwanda Military Planners in Germany to Finalise FDLR Neutralisation Plan

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Issa Michuzi

NAESA KUSHIRIKIANA NA WATAALAMU WA KILIMO KUBORESHA HUDUMA ZA UGANI KILIMANJARO

MOSHI. MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, ameitaka Taasisi ya Wakala wa Taifa wa Huduma za Ugani (NAESA) kushirikiana kwa karibu na maafisa kilimo wa mkoa huo ili kuongeza tija katika sekta za kilimo na ufugaji, hususan katika utoaji wa elimu na ushauri wa kitaalamu kwa wakulima kupitia maafisa ugani. Babu ameyasema hayo alipokutana na wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo waliotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa lengo la kuitambulisha NAESA ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuboresha usimamizi na utendaji wa huduma za ugani nchini. Ameeleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuimarisha huduma za ugani na kuhakikisha kuwa wakulima na wafugaji wanatumia mbinu bora za uzalishaji, hatua itakayochangia kukuza uchumi wa wananchi na maendeleo ya sekta ya kilimo nchini. Akizungumza wakati wa utambulisho huo, Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka NAESA, Felix Mrisho, ameeleza kuwa miongoni mwa majukumu ya taasisi hiyo ni kuratibu na kusimamia huduma za ugani katika sekta ya kilimo pamoja na kuanzisha na kusimamia miundombinu ya teknolojia za kilimo. Alifafanua kuwa kitaifa NAESA itashirikiana na Ofisi za Wakuu wa mkoa, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na wadau wengine wa sekta ya kilimo katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli za ugani. Hata hivyo ushirikiano huo unalenga kuboresha upatikanaji na kuongeza ufanisi wa huduma za ugani kwa wakulima, ili kuwawezesha kupata utaalamu na mbinu bora za kilimo zitakazochochea uzalishaji na tija katika sekta hiyo.

Tue, 27 Oct 2026 15:16:31 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

WAZIRI SANGU:MICHANGO YA WANACHAMA PSSSF INALINDWA,INAKUA NA KUREJESHA FAIDA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Ajira na Mahusiano Mhe Deus Sangu, akimpongeza Mkurugenzi wa Fedha Mfuko wa PSSSF Bw. Ally Yakuti, baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.07 ikiwa ni Gawio kutokana na uwekezaji wa Mfuko kwenye Mradi wa Rock City Mall ya jijini Mwanza. Hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma Oktoba 27, 2026. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Ajira na Mahusiano Mhe Deus Sangu, akizungumza wakati wa hafla hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mwanza City Company Limited, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSSSF Bw Fortunatus Magambo (kulia) akisalimiana na viongozi wa jiji la Mwanza wakati wa hafla ya kukabidhi Gawio kwa wabia wa Rock City Mall jijini Dodoma Oktoba 27, 2026 Dodoma, Oktoba 27, 2026 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF kwenye mradi wa Rock City Mall jijini mwanza ni ishara kwamba michango ya wanachama inalindwa, inakua na kurejesha faida kwa Taifa. Mhe. Sangu ameyasema hayo jijini Dodoma Oktoba 27, 2026 wakati Kampuni ya Mwanza Rock City Ltd ambayo ndiyo inasimamia mradi huo ikitoa gawio la jumla ya Shilingi 1.18 bilioni kwa wabia wake watatu ambao ni; PSSSF ambayo imepokea Shilingi 1.07 bilioni; Halmashauri ya Jiji la Mwanza imepokea Shilingi 71.3 milioni na Manispaa ya Ilemela imepokea Shilingi 47.56 milioni. PSSSF ambayo ni taasisi iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), ndiye mwekezaji mkuu katika mradi huo. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wakiwemo Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Constatine Sima, Mstaiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mhe. Sarah Ng’wani, na Mstaiki Meya wa Halmashauri ya Ilemela, Mhe Renatus Mulunga pamoja na Waheshimiwa Madiwani. “Ninapenda kutoa pongezi za dhati kwa Bodi na Menejimenti ya Mifuko yetu ya Hifadhi ya Jamii, hususan PSSSF, kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuhakikisha michango ya wanachama inalindwa, inakua na kurejesha faida kwa Taifa. Leo hatupokei gawio tu, tunapokea uthibitisho kuwa mfumo wetu wa hifadhi ya jamii uko imara, unakua na unalipa.” Alisema Mhe. Sangu. Mhe. Waziri Sangu alisema, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaogozwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050. Dira hiyo inatuambia kuwa Tanzania tunayoitaka ni ya uchumi imara, wa viwanda, usio na umaskini, na wenye ajira zenye staha kwa kila Mtanzania. “ Hivyo, jitihada hizi zinaonekana kwa wabia wote wa mradi huu wa Rock City Mall ambao ni PSSSF, Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Halmashauri ya Ilemela kwa usimamizi mzuri wa mradi ambao pia umezalisha ajira. Bila usimamizi wenu pengine leo tusingekuwa hapa kushuhudia tukio hili kubwa kwa wabia hawa. Hongereni sana….!” Alisema. Nawapongeza PSSSF kwa uwekezaji huu wenye tija kwa taifa letu, kwani nimeelezwa mpaka sasa asilimia 98 ya jengo lina wapangaji. Pamoja na kupendezesha jiji letu la Mwanza, mradi huu unanufaisha watu zaidi ya 1000 kupitia ajira za kudumu na za muda, kwa kufanya hivyo mnaunga mkono juhudi za Serikali kwa kuzalisha ajira kwa vijana wetu, alisema Mhe. Sangu. Aidha Mhe. Sangu ametoa wito kwa PSSSF na taasisi nyingine zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) kuhakikisha wanafuata miongozo ya uwekezaji inayotolewa na Benki Kuu ya Tanzania pamoja na sera za uwekezaji za taasisi husika ili kuweza kufanya uwekezaji wenye tija kama huu ambao leo tunashuhudia ukitoa gawio kwa wabia wake. “Lengo la kuwekeza ni kulinda thamani ya michango ya Wanachama ili wanapokuja kustaafu waweze kulipwa mafao ambayo ni zaidi ya michango yao waliyokuwa wanachangia katika Mfuko, hivyo, kutokana na mafanikio ya mradi huu tunaamini sehemu hii ya gawiwo itachangia katika kuwafanya wanachama wa PSSSF KULIPWA JANA.” Alisisitiza. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSSSF, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mwanza Rock City Company Limited, Bw. Fortunatus Magambo, amelinganisha tukio hilo na siku ya mavuno. “Hakika ile mbegu tuliyopanda, ilimea vyema na hatimaye leo tunavuna tulichopanda, hakika leo ni siku muhimu sana.” Alisema Bw. Magambo. Bw. Magambo alisema, Rock City Mall ina mchango kwa jamii na maendeleo ya Jiji la Mwanza kwa kuwa kituo cha huduma mbalimbali, ambapo faida zake ni pamoja na; Kurahisisha upatikanaji wa huduma, inakusanya huduma mbalimbali katika eneo moja, zikiwemo maduka, huduma za benki na migahawa mbalimbali. “Hii huwasaidia wananchi kuokoa muda na kurahisisha shughuli zao, Rock City Mall inatoa nafasi za biashara na ajira, inatoa maeneo ya kufanyia biashara na kuchangia fursa za ajira kupitia maduka, migahawa na huduma nyingine zinazopatikana hapo. Aidha, Bw. Magambo alisema, PSSSF inawekeza ili kulinda thamani ya michango ya Wanachama ili wanapokuja kustaafu waweze kupata mafao zaidi ya michango yao waliyokuwa wanachangia katika Mfuko. “ Uwekezaji wa Mfuko unaongozwa na Mwongozo wa Uwekezaji kutoka Benki Kuu ya Tanzania pamoja na Sera ya Uwekezaji ya Mfuko. Sehemu kubwa ya uwekezaji upo katika dhamana za serikali, hisa za kampuni na amana za mabenki na si kwenye majengo kama wengi wanavyodhani.” Alisisitiza.

Tue, 27 Oct 2026 15:12:39 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

KABUDI: MAJENGO 37 YA WIZARA NA TAASISI MTUMBA KUZINDULIWA OKTOBA 30.

Na Janeth Raphael - MichuziTv Serikali inatarajia kuzindua rasmi majengo 37 ya wizara na taasisi za Serikali pamoja na kilomita 57.1 za barabara za lami katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, Oktoba 30, 2026, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha utendaji wa Serikali na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Profesa Palamagamba Kabudi, amesema majengo yatakayozinduliwa yanajumuisha majengo 24 ya wizara na 13 ya taasisi za Serikali. Ameeleza kuwa ujenzi wa barabara hizo za lami umegharimu Shilingi Bilioni 110.5. Profesa Kabudi amesema kukusanywa kwa wizara na taasisi za Serikali katika eneo moja kutarahisisha uratibu wa shughuli za Serikali, kuboresha mawasiliano baina ya taasisi na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi. Hatua hiyo pia inalenga kupunguza changamoto zinazotokana na ofisi za Serikali kutawanyika katika maeneo mbalimbali. Ameeleza kuwa majengo hayo ni sehemu ya awamu ya pili ya mradi wa Mji wa Serikali Mtumba, unaohusisha pia majengo mengine 35 ya taasisi mbalimbali yaliyokamilika nje ya eneo la Mji wa Serikali, yakiwemo yaliyopo Chang’ombe na Njedengwa. Kwa mujibu wa Profesa Kabudi, uwekezaji huo unaendelea kuimarisha hadhi ya Dodoma kama Makao Makuu ya nchi na kitovu cha shughuli za Serikali, huku ukifungua fursa mbalimbali za kiuchumi kwa wananchi na sekta binafsi. Amewahimiza wafanyabiashara na wawekezaji kutumia fursa zinazotokana na ukuaji wa jiji la Dodoma, hususan katika sekta za usafirishaji, malazi, biashara na huduma za kitaalamu. Amesema kukamilika kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato kunatarajiwa kuongeza zaidi fursa hizo kadiri idadi ya watu wanaotembelea jiji hilo itakavyoongezeka. Aidha, amewataka watumishi wa umma watakaofanya kazi katika Mji wa Serikali Mtumba kutumia miundombinu hiyo kwa ufanisi na kuzingatia misingi ya uwajibikaji, uadilifu, nidhamu na uzalendo ili kuhakikisha wananchi wananufaika na uwekezaji uliofanywa na Serikali. Katika hatua nyingine, Profesa Kabudi amewaalika wananchi, hususan wakazi wa Dodoma, kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo. Amesema shamrashamra za kuelekea uzinduzi zitahusisha upigaji fataki usiku wa kuamkia Oktoba 30, 2026. Amesisitiza kuwa mradi huo unaakisi dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuendeleza miundombinu ya kisasa na kuimarisha utoaji wa huduma za umma nchini.

Tue, 27 Oct 2026 15:14:54 +0000
Uncategorized · The Star Kenya

‘Small wheelbarrow’: Nyoro caught in political storm

His defection to PPK has triggered a bitter feud with Rigathi Gachagua’s allies, even as William Ruto’s inner circle raises questions on his moves

Recently
Sports · Mwanaspoti

Kishindo cha Mourinho El Clásico

KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho, ameendelea kuonyesha makali yake katika pambano la watani wa jadi, El Clásico, baada ya kuiongoza timu hiyo kuichapa Barcelona mabao 2-1 katika mchezo mkali...

Recently
Entertainment · Mwanaspoti

Haya ndo maisha ya G Nako nje ya muziki

Read the full report from the original source.

Recently
Sports · Mwanaspoti

Kane aandika historia upya Ballon d’Or

MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich na nahodha wa England, Harry Kane, ametwaa tuzo ya Ballon d’Or na kuandika historia kwa kuwa Mwingereza wa kwanza kushinda tuzo hiyo ya mchezaji bora wa dunia ndani...

Recently
Uncategorized · BBC Afrique

Comment la Russie renforce ses partenariats et étend son influence en Afrique

Le renforcement des relations entre la Russie et les gouvernements militaires du Mali, du Burkina Faso et du Niger sera au cœur du troisième Sommet Russie-Afrique, qui se tiendra à Moscou les 28 et 29 octobre 2026.

Recently
Uncategorized · Daily News

PM flies to Moscow for Oct 28’s Russia-Africa Summit

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

Businesses smell fortunes in newly signed Swiss-Tanzania Chamber of Commerce deal

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Human rights victims get until November 14 to file claims

All claims received by the deadline, including those that have already been submitted, will undergo verification and authentication

Recently
Uncategorized · Jamhuri Media

TBS Yakutana na wadau kujadili Viwango vya Petroli

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Israel election: Turnout at record levels at halfway stage

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · SoftPower News

Uganda’s TVET: From Skills Training to Meaningful Livelihood

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Pastor tells court murdered university student’s phone was found in church offerings

Read the full report from the original source.

Recently

Page 594 of 1164 · 23267 stories