Search the region
22504 stories
Search for missing Aberdare hiker enters second week
The Kenya Wildlife Service (KWS) has deployed a helicopter and drones to support the search.
RecentlyTanzania, Kenya, Zambia expand access to oral health services at primary care level
JAPAN: TANZANIA Kenya and Zambia are bringing affordable oral health care closer to people. In Tanzania, government investment has raised…
RecentlyBoT, IMF assess risks to safeguard stability
DAR ES SALAAM: THE Bank of Tanzania (BoT) and the International Monetary Fund (IMF) are assessing financial sector oversight and…
RecentlyTANAPA promotes conservation, tourism under Vision 2050
TANZANIA: STANDING as tourist magnets in both Tanzania and Africa, Tanzania national parks have been a strong source of tourism…
RecentlyTanzania eyes vaccine self-sufficiency by 2030 amid new agreements
Read the full report from the original source.
RecentlyBush hails Kiambaa Ladies' performance on Kenya Cup debut
Read the full report from the original source.
RecentlyNungwi inferno leaves Zanzibar counting major tourism losses
Read the full report from the original source.
RecentlyWhy local businesses must rethink cloud trust
TANZANIA: ON 12 November this year, Microsoft Outlook and a wide range of Microsoft 365 services went down in one…
RecentlyKenya, DRC agree on return of ambassadors after diplomatic tensions
The two countries agreed to prioritise diplomatic channels and restore ambassadorial relations following talks in the Republic of the Congo.
RecentlyBALOZI OMAR ATOA WITO WA KUREJESHA MAADILI MEMA KATIKA JAMII
Na. Peter Haule, WF, Dar es Salaam Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ametoa wito kwa Watanzania kushirikiana katika kurejesha na kuimarisha maadili mema katika jamii, akisisitiza kuwa jukumu la kujenga jamii yenye maadili si la Serikali pekee, bali linawahusu wazazi, walezi, walimu, viongozi wa dini na kila mwanajamii. Mhe. Omar ameyasema hayo wakati wa hafla ya ugawaji wa zawadi kwa washiriki na washindi wa mashindano ya Sira ya Mtume Muhammad (SAW) yaliyoandaliwa kupitia Kampeni ya Rudisha Maadili kwa Jamii na Uzinduzi wa Huduma ya Daktari wangu kupitia Mfuko wa Bima ya Mufti, iliyofanyika katika Msikiti wa BAKWATA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Amesema suala la maadili ni jambo la msingi katika maendeleo ya jamii na linapaswa kuanzia katika familia, kuendelezwa shuleni, katika nyumba za ibada na maeneo mbalimbali ya kijamii. “Hapo awali malezi ya watoto yalikuwa jukumu la pamoja la wazazi na jamii nzima, huku walimu na viongozi wa dini wakichangia katika kuwajenga watoto katika misingi ya heshima, nidhamu na uwajibikaji, kwa sasa kuna changamoto katika mfumo wa malezi, hali inayohitaji jamii kutafakari upya wajibu wake na kuchukua hatua za pamoja kurejesha utamaduni wa kulea watoto katika misingi ya maadili mema”, amesema Mhe. Balozi Omar. Aidha, ametoa pongezi kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuendelea kusisitiza umuhimu wa maadili katika jamii. Akizungumzia mashindano ya Sira ya Mtume Muhammad (SAW), Mhe. Omar amesema mashindano hayo yamekuwa sehemu ya kutoa elimu kwa washiriki kuhusu maisha na mafundisho ya Mtume, huku akisisitiza kuwa lengo la elimu hiyo halipaswi kuishia katika kushiriki mashindano au kupata zawadi. Amesema washindi waliopata zawadi wanastahili pongezi, lakini kwa maana pana, kila aliyeshiriki na kupata elimu kupitia mashindano hayo ni mshindi, kwa sababu mafanikio makubwa yatakuwa pale elimu hiyo itakapotumika katika maisha halisi. Vilevile Mhe. Balozi Omar ametoa shukrani kwa waandaaji wa kampeni hiyo, washiriki na wadau wote waliofanikisha mashindano hayo, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano katika kurejesha na kudumisha maadili mema kwa maendeleo ya jamii ya Watanzania. Kwa upande wake Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zubeir, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, taasisi za dini na jamii katika kuimarisha maadili na kuchochea maendeleo ya Watanzania. Amesema ujenzi wa jamii yenye maadili mema unahitaji kila upande kutekeleza wajibu wake kwa kushirikiana, huku akibainisha kuwa maendeleo ya nchi yanapaswa kuzingatia maeneo muhimu ya elimu, uchumi, afya na ustawi wa jamii. Sheikh Dkt. Zubeir ameeleza kuwa Serikali na wadau wengine wanapaswa kuendelea kuweka mazingira yatakayowezesha wananchi kupata elimu na huduma muhimu, pamoja na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo. Naye Meneja Mahusiano wa Taasisi ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Bi. Khadija Maulid, akizungumzia suala la Bima kwa wote, ametoa wito kwa Watanzania kushirikiana na kuunga mkono Mfuko wa Bima ya Mufti katika kuhamasisha upatikanaji wa huduma za bima ya afya, hususan kwa wananchi wenye uhitaji. Amesema ushirikiano kati ya taasisi mbalimbali ni muhimu katika kuhakikisha Watanzania wanapata fursa ya kupata huduma za matibabu bila kukabiliwa na changamoto kubwa za kifedha pale wanapougua. Awali Mtoto Rehema Suleiman Kizenza aliyeibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya Sira ya Mtume Muhammad (S.A.W), baada ya kuonesha umahiri na uelewa mkubwa kuhusu maisha, mwenendo na mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W), alisema somo la Sira ya Mtume lina umuhimu mkubwa katika maisha ya kila siku, hususan kwa watoto na wanafunzi, kwa kuwa linawafundisha maadili mema. Alisema kujifunza Sira ya Mtume kunamsaidia yeye na wanafunzi wenzake kuwa waaminifu, wakweli, wenye huruma, wanyenyekevu na wenye kuzingatia adabu katika maisha yao ya kila siku. Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiagana na Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zubeir baada ya hafla ya ugawaji wa zawadi kwa washiriki na washindi wa mashindano ya Sira ya Mtume Muhammad (SAW) na Uzinduzi wa Huduma ya Daktari wangu kupitia Mfuko wa Bima ya Mufti, iliyofanyika katika Msikiti wa BAKWATA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akitoa zawadi kwa Ikram Khalfan Kanuti ambaye ni miongoni mwa washindi wa mashindano ya Sira ya Mtume Muhammad (SAW) iliyofanyika katika Msikiti wa BAKWATA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akitoa wito wa kurejesha maadili mema wakati wa hafla ya ya ugawaji wa zawadi kwa washiriki na washindi wa mashindano ya Sira ya Mtume Muhammad (SAW) na Uzinduzi wa Huduma ya Daktari wangu kupitia Mfuko wa Bima ya Mufti, iliyofanyika katika Msikiti wa BAKWATA, Kinondoni, jijini Dar es Salaama. Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zubeir, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, taasisi za dini na jamii katika kuimarisha maadili na kuchochea maendeleo ya Watanzania. Baadhi ya washiriki wa hafla ya ugawaji wa zawadi kwa washindi wa mashindano ya Sira ya Mtume Muhammad (SAW) na Uzinduzi wa Huduma ya Daktari wangu kupitia Mfuko wa Bima ya Mufti, wakifuatilia mambo mbalimbali, katika Msikiti wa BAKWATA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Dar es Salaam)
Mon, 23 Nov 2026 06:48:44 +0000If floods strike tonight: Is the emergency response system ready?
DAR ES SALAAM: AS anticipated heavy rains continue to raise concerns about flooding in different parts of the country, a…
RecentlyPOLISI IRINGA WAPONGEZWA KWA KUREJESHA NIDHAMU, KUPUNGUZA UHALIFU NA KUBORESHA VITENDEAKAZI
NA DENIS MLOWE, IRINGA. MJUMBE wa Kamati Ndogo ya uhamasishaji vijana michezo utamaduni Sanaa wazazi Ccm Taifa Joseph Mgongolwa kutoka Mkoa wa Iringa amempongeza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, kwa juhudi za kuimarisha usalama, kuboresha vitendea kazi vya jeshi la polisi, kurejesha nidhamu kwa askari na kupunguza matukio ya uhalifu mkoani humo. Akizungumza na wanahabari mkoa wa Iringa Joseph Mgongolwa amesema wameona mabadiliko katika utendaji wa Jeshi la Polisi, akitaja ujenzi na uboreshaji wa vituo vya polisi, ukarabati wa magari yaliyokuwa yameharibika pamoja na kuhakikisha vituo vinakuwa na vitendea kazi vinavyorahisisha shughuli za ulinzi na usalama. Mgongolwa amesema hatua hizo zimechangia kurejesha heshima ya jeshi hilo kwa wananchi, huku akieleza kuwa usimamizi wa Kamanda Bukumbi umeongeza nidhamu kwa askari na kuimarisha utendaji wa kazi zao. Amesema wananchi wanapaswa kuendelea kuwa na imani na Jeshi la Polisi na kutoa ushirikiano katika kufichua vitendo vya uhalifu, akieleza kuwa usalama wa jamii unategemea pia ushirikiano wa wananchi na vyombo vya dola. Mgongolwa ameeleza kuwa kampeni ya “Ongea na Kamanda” imekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha mawasiliano kati ya polisi na wananchi, kwa kuwa kamanda amekuwa akitembelea maeneo mbalimbali na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi, hatua ambayo amesema imeongeza uelewa, uwazi na uaminifu katika ushirikiano wa pande hizo mbili. Aidha, amesema kupitia kampeni hiyo na mikakati mingine ya kiusalama, matukio ya mauaji, ubakaji na uhalifu mwingine yamepungua kwa kiwango kikubwa, akidai baadhi ya matukio hayo yamepungua kwa takribani asilimia 90. Katika pongezi hizo, Mgongolwa pia ameishukuru Serikali na uongozi wa Jeshi la Polisi kwa kuendelea kusimamia maboresho ya kiutendaji, huku akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, kwa ushirikiano wake katika masuala ya usalama na maendeleo ya mkoa. Amesema Mkuu wa Mkoa Kheri James amekuwa akifanya kazi kwa karibu na vyombo vya usalama kutokana na nafasi yake ya kuongoza Kamati ya Usalama ya Mkoa, akieleza kuwa uongozi wake umechangia kuimarisha usimamizi wa masuala ya usalama. Katika hatua nyingine, Mgongolwa ametoa ombi kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) kumwangalia SACP Bukumbi kwa uwezekano wa kuongezewa muda wa utumishi endapo atakuwa karibu na kustaafu, akieleza kuwa wanaamini kuendelea kwa uongozi wake kutasaidia kudumisha mafanikio yaliyopatikana katika kuimarisha usalama wa Iringa. Amesema ombi hilo linatokana na mabadiliko yaliyofanywa na kamanda huyo katika kuboresha utendaji wa jeshi, kuimarisha nidhamu, kufufua magari ya polisi na kuongeza ushirikiano kati ya wananchi na polisi. Kwa upande wake, Maximilian Lugenge amesisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu kwa vyombo vya usalama na kushiriki kikamilifu katika polisi jamii, akieleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuzuia uhalifu na kujenga jamii yenye amani.
Mon, 23 Nov 2026 06:42:53 +0000Research funding shortfalls threaten $1 trillion economy goal
Read the full report from the original source.
RecentlySamia set to launch Africa maternal health plan
Read the full report from the original source.
RecentlyCop dies after falling and sustaining head injuries
The officer had a known history of epilepsy and sustained a head injury following the fall, police said adding the incident remained under investigation.
RecentlyTanzania’s road to prosperity runs through jobs
TANZANIA: TANZANIA is entering a crucial stage in its economic development, with increasing emphasis on ensuring that economic growth translates…
RecentlyMWIGULU AKEMEA UZEMBE ,KUFANYA KAZI KWA MAZOEA, AAGIZA WANAOKIUKA MAELEKEZO WAWAJIBISHWE
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani WAZIRI Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka rekodi katika kuimarisha sekta ya afya nchini kwa kujenga zahanati 2,700, vituo vya afya 600, hospitali za wilaya 119 pamoja na kutoa magari ya huduma za afya kwa kila mkoa. Aidha, katika sekta ya elimu, amesema Serikali imejenga shule za msingi 2,700 na shule za sekondari 1,300, huku kila mkoa ukiwa na shule za wasichana, pamoja na kujenga shule 29 za ufundi na shule 100 za amali. Akizungumza Novemba 21, 2026, wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Pwani, Dkt. Mwigulu amesema Rais Samia ameonyesha dhamira na jitihada kubwa katika uwajibikaji na kuboresha huduma kwa wananchi, hivyo viongozi na watendaji wanapaswa kutekeleza maelekezo ya Serikali kwa uaminifu bila kufifisha juhudi hizo. “Serikali imejenga hospitali, vituo vya afya, imeweka dawa, unakuta watu wanazuiliwa miili ya marehemu wao, hospitali zinazuia miili ya marehemu, ziache mambo hayo,” amesema. Vilevile, amekemea tabia ya baadhi ya hospitali kuwatoza ndugu wa wagonjwa wa dharura fedha za mafuta ya magari ya wagonjwa (ambulance), pamoja na kuwaamuru wanawake wajawazito wanaofika kujifungua kuleta vifaa kama ndoo na beseni, akisisitiza kuwa vitendo hivyo havipaswi kuendelea. Dkt. Mwigulu amewaonya watendaji wazembe wanaojificha nyuma ya viongozi na watendaji wengine wanaowajibika, akitaka kila mmoja kutekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria, taratibu na maelekezo ya Serikali, huku akisisitiza wanaokiuka wafukuzwe kazi ili iwe fundisho kwa wengine.
Sun, 22 Nov 2026 06:37:00 +000024 civilians killed in fresh South Sudan violence
Read the full report from the original source.
RecentlyMan with Alzheimer's found alive after 11 days in Brazilian Amazon
Read the full report from the original source.
RecentlyRuto and Tshisekedi hold talks to resolve Kenya-DRC standoff, restore diplomatic relations
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 61 of 1126 · 22504 stories