Unganishwa

Search the region

23170 stories

Uncategorized · Rwanda News Agency

PM Nsengiyumva attends installation of new Primate of the Anglican Church of Rwanda

Read the full report from the original source.

Recently
Sports · Azam TV Videos

Magoli | Geita Gold FC 1-1 Fountain Gate FC | NBC Premier League 25/10/2026

Geita Gold FC imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Fountain Gate FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa kwenye Dimba la Bukombe, mkoani Geita. Waliotangulia ni Fountain kwa penati ya MacDonald Chukwunonye Obasi, kabla ya Geita kusawazisha kupitia kwa Yusuph Mhilu. Haya ni magoli..

2026-10-25T19:22:14+00:00
Uncategorized · Capital FM

Muturi calls for binding livestreaming rules ahead of 2027 polls

News · Quick read

Recently
Uncategorized · Capital FM

CS Mutua Appoints Atwoli to National Board for Social Protection

Latest · NATIONAL NEWS

Recently
National · Rwanda News Agency

Rwandan Peacekeepers in CAR provide free medical services to 143 residents of Bangui

Read the full report from the original source.

Recently
National · Citizen Digital

Approval lapses...blame games: How 18-storey Eastleigh building came tumbling down

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Issa Michuzi

PWANI YAWEKA MIKAKATI KUDHIBITI MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani MKUU wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, wametaka maeneo maalumu ya kilimo na ufugaji kutengwa na kusimamiwa ipasavyo ili kudhibiti migogoro kati ya wakulima na wafugaji. Nyongo ametoa agizo hilo kwa viongozi wa wilaya, akiwataka kuhakikisha maeneo ya malisho ya mifugo yanatengwa ili kupunguza migogoro inayojirudia kati ya makundi hayo. Amesema tayari ametoa tamko la kutenga maeneo maalumu ya malisho, akisisitiza kuwa hataki kuona mauaji yanayotokana na migogoro hiyo. “Nimeshatoa tamko la kutenga maeneo hayo kuondoa magomvi hayo na katika mkoa wangu sitaki kuona mauaji ya wakulima na wafugaji,” alisema Nyongo, akibainisha kuwa ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kuhakikisha hali hiyo inadhibitiwa. Aidha, amewataka wakulima na wafugaji kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutumia kamati za usuluhishi kutatua changamoto zao kwa mujibu wa sheria. Pia, amewataka wakulima na wafugaji kuzingatia taratibu zinazokubalika katika matumizi ya ardhi, huku akisisitiza umuhimu wa wafugaji kuepuka kuingiza mifugo katika mashamba ya watu na kuharibu mazao. Kwa upande wake, Kikwete amewataka viongozi wa vijiji, Serikali na vyombo vinavyohusika kusimamia matumizi ya ardhi na kudhibiti uingizaji holela wa mifugo katika mashamba ya wakulima. Amesema migogoro hiyo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na ushindani wa matumizi ya ardhi, maji na malisho, pamoja na uhamaji wa wafugaji wanaotafuta rasilimali hizo. Kutokana na hali hiyo, amependekeza kutengwa kwa maeneo maalumu ya kilimo na ufugaji, kusimamiwa kwa njia za kupitisha mifugo na kusajiliwa kwa wakulima na wafugaji ili kurahisisha usimamizi wa shughuli zao. Kikwete pia amesisitiza umuhimu wa kuimarisha vikao vya ujirani mwema vitakavyowapa wakulima na wafugaji nafasi ya kujadili na kutatua changamoto zao kwa pamoja kabla hazijazua migogoro mikubwa. Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga, amesema Serikali imekuwa ikifanya operesheni za kukabiliana na migogoro ya ardhi, ikiwemo inayohusisha wakulima na wafugaji. Amesema jitihada hizo zinaambatana na kuhamasisha umoja, amani na kuheshimiana, kwa kuzingatia maeneo na shughuli za kiuchumi za kila kundi. Kwa upande wake, mfugaji wa Chalinze, Seleman Hassan, ameishukuru Serikali kwa kutoa elimu kwa wafugaji, akisema wataendelea kushirikiana na wakulima ili kuondoa kero zinazojitokeza na kudumisha amani katika maeneo wanayoishi. Migogoro ya wakulima na wafugaji imeendelea kuwa changamoto katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani, yakiwemo Chalinze, Bagamoyo, Rufiji, Kisarawe, Kibaha Vijijini na Kibiti.

Sun, 25 Oct 2026 19:13:09 +0000
National · Rwanda News Agency

India and Rwanda celebrate ITEC Day 2026 in Kigali

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Issa Michuzi

TANZANITE YENYE THAMANI YA SH3.23 BILIONI YAZALISHWA MIRERANI

Na Mwandishi Wetu, Mirerani KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeelezwa kuwa jumla ya gramu 274,634.32 za madini ya Tanzanite, zenye thamani ya Sh3.23 bilioni, zimezalishwa katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2026. Takwimu hizo zimetolewa na Ofisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Mirerani (RMO), George Kaseza, mbele ya kamati hiyo ilipotembelea maeneo ya uchimbaji wa madini ya Tanzanite kwa lengo la kujifunza na kutathmini shughuli za uchimbaji, biashara na uongezaji thamani wa madini hayo. Kaseza amesema uzalishaji huo ni wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027, huku akieleza kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha usalama na usimamizi wa shughuli za uchimbaji ndani ya Ukuta wa Mirerani. Amesema hatua hizo zinajumuisha ujenzi wa ukuta uliokamilika Aprili 2018, kuanzishwa kwa Soko la Madini la Mirerani mwaka 2021, pamoja na uwekaji wa kamera 310 za CCTV na taa 573 za usalama. Aidha, amesema mwaka 2026 Serikali iliagiza kofia ngumu 12 zenye kamera kwa ajili ya wadhibiti wa shughuli za uchimbaji chini ya migodi. Akizungumzia biashara ya Tanzanite, Kaseza amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026, mnada wa wafanyabiashara wadogo uliofanyika Mei 15, 2026, ulihusisha uuzaji wa gramu 2,809.31 za madini hayo, zilizoripotiwa kuwa na thamani ya Sh271.270 bilioni. Amesema mnada wa wafanyabiashara wakubwa uliofanyika Mei 21, 2026, uliwezesha kuuzwa kwa gramu 10,174.92 za Tanzanite, zenye thamani iliyoripotiwa kuwa Sh721.750 bilioni. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Subira Mgalu, amesema ziara hiyo imelenga kujifunza na kutathmini shughuli za uchimbaji, biashara na uongezaji thamani wa madini zinazofanyika ndani ya Ukuta wa Mirerani. Akitoa maoni ya wadau wa sekta hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara (MAREMA), Elisha Mnyawi, ameiomba Serikali kuruhusu lango la kuingia na kutoka ndani ya ukuta wa madini ya Tanzanite kufanya kazi saa 24. Mnyawi amesema kwa sasa, ifikapo saa 12 jioni, wachimbaji hawaruhusiwi kuingiza zana za kazi, hali ambayo amesema inahitaji kuangaliwa ili kurahisisha shughuli za uchimbaji. Naye Mwenyekiti wa MAREMA Tawi la Mirerani, Samwel Rugemalila, ameishukuru Serikali kwa hatua mbalimbali inazoendelea kuchukua kuboresha sekta ya madini. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Madini ndani ya Ukuta wa Mirerani, Magreth Nelson, ameishukuru Serikali kwa kurejesha minada ya madini, akisema hatua hiyo imewawezesha wafanyabiashara kuuza madini yao kwa uwazi na katika mazingira ya ushindani wa bei. Hata hivyo, mjumbe wa chama cha wafanyabiashara wa madini, Victor Kunyara, ameiomba kamati hiyo kuangalia uwezekano wa kuweka kanuni zitakazowataka wachimbaji kutenga asilimia 10 ya uzalishaji wao na kuwauzia wafanyabiashara wa ndani. Amesema hatua hiyo itasaidia wafanyabiashara kupata madini kwa ajili ya biashara zao na kuongeza uwezekano wa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria.

Sun, 25 Oct 2026 19:09:49 +0000
Sports · Rwanda News Agency

Rwandan peacekeepers serving under UNMISS crowned champions in UN Day sports tournament

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

KAMATI YA LAAC YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA IRINGA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Ado Shaibu, imeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, huku ikisisitiza kukamilishwa kwa miradi hiyo kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vya ubora. Leo, Oktoba 24,2026, Kamati hiyo imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ya kimkakati, ikiwemo ujenzi wa barabara ya Mtwivila machinjio ya kisasa Ngelewala na Soko la kihesa kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wake. Akizungumza baada ya ukaguzi, Mhe. Ado Shaibu amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji na kutoa maelekezo kwa Halmashauri kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na inakidhi viwango vinavyotakiwa. Ziara hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James; Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mhe. Benjamin Sitta, Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Doris Kalasa; Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Bi. Zaina Mlawa; Mstahiki Meya wa Manispaa, Mhe. Ibrahim Ngwada; Katibu Tawala Wilaya, Ndg. Bernard Urassa, Wajumbe wa Kamati ya LAAC, pamoja na wakuu wa idara na vitengo wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa na wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Sun, 25 Oct 2026 19:01:22 +0000
Business · Issa Michuzi

KAMATI YA UCHUMI, AFYA NA ELIMU YAPONGEZA MAENDELEO YA UJENZI KITUO CHA AFYA WAMBI

Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu ya Halmashauri ya Mji Mafinga ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri,Kaimu Mkurugenzi pamoja na Wakuu wa Idara wa Halmashauri imefanya Ziara katika Kata ya Wambi na kupongeza Maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Wambi. Akiwasilisha ripoti ya Ujenzi wa Kituo hicho cha Afya, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Ndugu Eusebius Ngatunga amesema wamepokea Fedha za Ujenzi Kutoka Serikali kuu Tsh.Milioni Mia Tatu na hatua ya ujenzi inakaribia kukamilika kwa wakati ili kuwawezesha Wakazi wa Kata ya Wambi kupata huduma ya Afya. Akizungumza katika Ziara hiyo Diwani wa Kata ya Wambi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi,Afya na Elimu Mhe.Frank Kalinga amesema anampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwatengea Fedha za Mradi kwa sababu ujenzi ukikamilika utasaidia kutatua changamoto za Afya kwa Wananchi wa Kata ya Wambi. Naye kiongozi wa Ziara hiyo ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe.Regnant Kivinge amepongeza jitihada za Wananchi na kamati ya Ujenzi kwa ushirikiano na amewasihi waendelee kusimamia Mradi huo kwa weledi ili waweze kufikia Malengo. Aidha,Diwani wa Viti Maalumu wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe.Dainess Msolwa amewapongeza Wananchi wa Kata ya Wambi kwa kutenga muda wao kusaidia shughuli za ujenzi pamoja na kushirikiana vyema na kamati ya Ujenzi kwa lengo la kukamilisha Jengo kwa wakati. Sambamba na hayo,Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Peter Ngussa amepongeza jitihada za ujenzi pia amewasisitiza kamati ya ujenzi ifikapo January 2027 ujenzi wa Kituo hicho uwe umekamilika ili huduma za awali za Afya zianze kutolewa kwa Wananchi wa Kata ya Wambi.

Sun, 25 Oct 2026 19:02:09 +0000
World · DW Rwanda

Low voter turnout in Bulgaria triggers presidential run-off

Read the full report from the original source.

Recently
National · KT Press

Government Wants Churches More Involved in Families

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

HOMERA ATANGAZA MAPINDUZI YA UMEME VITONGOJINI, AIPONGEZA REA KWA UTEKELEZAJI

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Homera, amepongeza juhudi za Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy, katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, huku akitangaza kuongezwa kwa kasi ya operesheni ya kuwasha umeme katika kila kitongoji nchini. Waziri Homera amesema operesheni hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuhakikisha huduma ya umeme inawafikia wananchi katika maeneo yote nchini, sambamba na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, hususan katika maeneo ya vijijini. Akizungumza wakati akiwasha umeme Kitongoji cha Lindi B, Wilaya ya Namtumbo, na Kitongoji cha Nakanyonyo, Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, amesema Wakuu wa Mikoa wataendelea kushiriki katika kuwasha umeme kwenye miradi iliyokamilika ili kuhakikisha wananchi wanaanza kunufaika na huduma hiyo kwa wakati. Ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza kasi ya matumizi ya miundombinu ya umeme iliyokamilika, huku Serikali ikiendelea kutekeleza miradi mipya katika vitongoji ambavyo bado havijafikiwa na huduma hiyo. Akizungumzia hali ya upatikanaji wa umeme mkoani Ruvuma, Waziri Homera amesema mkoa huo una jumla ya vitongoji 3,691, ambapo vitongoji 2,235 tayari vimefikiwa na umeme, sawa na takribani asilimia 61 ya vitongoji vyote. Amesema Serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 224.7 katika miradi mbalimbali ya umeme inayotekelezwa na REA mkoani humo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupanua wigo wa upatikanaji wa nishati hiyo kwa wananchi. Kwa mujibu wa Waziri Homera, vitongoji 799 vipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya kuviunganishia umeme, huku vitongoji 657 vikiwa bado havijafikiwa na huduma hiyo na havipo katika miradi inayoendelea kutekelezwa. Amefafanua kuwa kukamilika kwa miradi inayoendelea kutasaidia kuongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme katika vitongoji vya Mkoa wa Ruvuma kutoka asilimia 61 ya sasa hadi takribani asilimia 82. Amesema ongezeko hilo linatarajiwa kufungua fursa zaidi za shughuli za kiuchumi, ikiwemo biashara, uzalishaji mali na utoaji wa huduma za kijamii, hivyo kuboresha maisha ya wananchi wa maeneo ya vijijini. Aidha, Waziri Homera amewataka wananchi kuendelea kuiombea Wizara ya Nishati ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha azma ya kufikisha umeme kila kitongoji inafikiwa. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy, amesema kasi ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini imeendelea kuongezeka na kwamba Wakala hautarudi nyuma katika kutimiza dhamira ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na huduma ya umeme. Mhandisi Saidy amesisitiza kuwa Wakala utaendelea kuongeza juhudi za kusogeza huduma ya umeme katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa, sambamba na kufungua fursa mpya za kiuchumi, kuongeza uzalishaji na kuboresha ustawi wa wananchi wa vijijini.

Sun, 25 Oct 2026 18:57:13 +0000
Sports · Capital FM

End of the road for Tusker in Caf Confederations after tame draw with Singida

Latest · Kenyan Premier League

Recently
National · Issa Michuzi

TANZANIA YATAKA HATUA ZA DHATI KULINDA ZIWA TANGANYIKA

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv TANZANIA imetoa wito kwa nchi wanachama zinazopakana na Ziwa Tanganyika kutekeleza kwa vitendo makubaliano ya kikanda ya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira, mabadiliko ya tabianchi na shinikizo la matumizi ya rasilimali zinazotishia mfumo wa ikolojia wa ziwa hilo. Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Dk. Richard Muyungi, leo Oktoba 25, 2026, wakati akifungua Mkutano wa 15 wa Kawaida wa Kamati ya Usimamizi ya Mamlaka ya Ziwa Tanganyika unaofanyika Dar es Salaam. Dk. Muyungi amesema kulinda ziwa hilo kunahitaji ushirikiano wa kikanda, ufuatiliaji madhubuti wa mazingira na uwajibikaji ili kuhakikisha maazimio yanayofikiwa yanatekelezwa kwa vitendo. Amesema mkutano huo unajadili mpango kazi na bajeti ya mamlaka hiyo kwa mwaka 2026 pamoja na utekelezaji wa maazimio ya mawaziri yaliyopitishwa mjini Livingstone, Zambia. Ameonya kuwa kuharibika kwa mazingira ya ziwa hilo kunatishia maisha na kipato cha mamilioni ya watu wanaotegemea rasilimali zake, hivyo Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia zinapaswa kuratibu mikakati ya kulinda ziwa hilo. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika, Dk. Emma Liwenga, amesema mamlaka hiyo inaendelea kuboresha Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa mwaka 2012 na kuandaa ripoti ya kina ya bonde la ziwa hilo kwa msaada wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Mfuko wa Dunia wa Mazingira (GEF). Amesema mipango mingine ni pamoja na tathmini ya hali ya samaki katika ziwa lote inayoungwa mkono na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), pamoja na miradi ya uhifadhi wa bayoanuwai na usalama wa maji. Mwenyekiti wa mkutano huo, Richard Mlungu, amesema Ziwa Tanganyika ni rasilimali muhimu kwa nchi wanachama kutokana na mchango wake katika upatikanaji wa maji, uvuvi, bayoanuwai na shughuli za kiuchumi. Hata hivyo, amesema ziwa hilo linakabiliwa na changamoto zinazoongezeka, zikiwemo uvuvi usio endelevu, uchafuzi wa mazingira, uharibifu wa makazi ya viumbe hai, mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la watu. Amesema mkutano huo pia unajadili ripoti ya mwaka ya Mamlaka ya Ziwa Tanganyika (LTA), mpango kazi na bajeti ya mwaka 2027, huku akizitaka nchi wanachama kuongeza ushirikiano na rasilimali za kifedha kwa ajili ya kulinda ziwa hilo. Naye Mkurugenzi wa Mazingira na Mjumbe wa Kamati, Kemilembe Mutasa, amesema Ziwa Tanganyika si mpaka wa kijiografia unaotenganisha nchi wanachama, bali ni rasilimali inayozileta pamoja kutokana na mchango wake katika maisha ya wananchi, usalama wa chakula na maendeleo ya kiuchumi. Amesema maamuzi na ushauri wa Kamati ya Usimamizi kwa Baraza la Mawaziri la mamlaka hiyo ni muhimu katika kuhakikisha linatekeleza wajibu wake kwa ufanisi na kusimamia rasilimali za ziwa hilo kwa uendelevu.

Sun, 25 Oct 2026 18:54:09 +0000
National · Issa Michuzi

DKT. KIJAJI: HAKUNA KULALA, MIRADI YA UTALII IKAMILIKE KWA WAKATI NA VIWANGO

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, ameitaka Menejimenti ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kuhakikisha miradi ya kuboresha miundombinu ya utalii inakamilika kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa. Amesema uboreshaji wa miundombinu katika vivutio vya utalii vya Maporomoko ya Maji ya Endoro na Mapango ya Tembo ni sehemu ya jitihada za kufanikisha azma ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kufikisha idadi ya watalii milioni nane ifikapo mwaka 2030. Dkt. Kijaji ameyasema hayo wakati akikagua maendeleo ya miradi hiyo, ambapo alieleza kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wake, akisisitiza kuwa fedha za miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Utalii (TDL) zinapatikana na hivyo hakuna sababu ya kuchelewesha utekelezaji wake. Amesema hadi sasa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imetengewa Sh bilioni 10 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa barabara, huku akibainisha kuwa wakandarasi wanaendelea kulipwa kulingana na hatua za utekelezaji wa kazi. Aidha, amesema Sh bilioni 1.67 zimetengwa kwa ajili ya kuboresha vivutio vya utalii vya Endoro na Ngoitoktok vilivyopo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro. Miradi hiyo imefikia asilimia 68 ya utekelezaji na inatarajiwa kukamilika Desemba 2026. Msimamizi wa miradi hiyo, SACC Mariam Kobelo, amesema mradi wa Endoro unahusisha ujenzi wa majengo ya ofisi, geti, njia za kutembelea kwa miguu zenye urefu wa mita 2,200, njia za mbao (boardwalk), alama za maelekezo, vyoo pamoja na maeneo ya wageni kupumzikia. Ameongeza kuwa mradi wa Ngoitoktok unalenga kuboresha mazingira ya eneo la mapumziko ya wageni kwa kuongeza miundombinu itakayowawezesha watalii kukaa na kupumzika kwa urahisi. Kwa upande wake, Kamishna wa Uhifadhi wa Ngorongoro, Abdul-Razaq Badru, amesema ujenzi wa barabara ya tabaka gumu kutoka Loduare hadi Geti la Seneto, yenye urefu wa kilomita 29.5, unaendelea vizuri. Amesema mradi huo unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili kwa gharama ya Sh bilioni 80.36 umefikia asilimia nane ya utekelezaji, huku juhudi zikiendelea kuimarisha usimamizi na kuongeza kasi ya kazi ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati.

Sun, 25 Oct 2026 18:47:47 +0000
National · Issa Michuzi

MSIGWA AFUNGUKA BILIONI 730 ZA EL NIÑO, ASEMA SI BAJETI MPYA YA SERIKALI

Na Janeth Raphael -MichuziTv Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amefafanua kuwa makadirio ya Shilingi Bilioni 730 yaliyotajwa katika Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kujiandaa na Kukabiliana na Madhara ya El Niño kwa mwaka wa fedha 2026/2027 si bajeti mpya ya Serikali, bali ni jumla ya makadirio ya rasilimali zinazohitajika kutoka taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali kwa ajili ya kutekeleza shughuli za kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Oktoba 25, 2026, Msigwa amesema mpango huo umeandaliwa kufuatia utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ulioonesha uwezekano wa kutokea kwa El Niño yenye nguvu na kusababisha madhara yakiwemo mafuriko, maporomoko ya ardhi na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama. Amesema maandalizi ya mpango huo yaliratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikisha Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa, mashirika ya kitaifa na kimataifa, taasisi zisizo za kiserikali pamoja na sekta binafsi. Amefafanua kuwa taasisi hizo zitatekeleza majukumu yake kwa kutumia rasilimali na bajeti zilizoidhinishwa kwa mwaka wa fedha 2026/2027, huku kipaumbele kikitolewa kwa shughuli za kulinda maisha na mali za wananchi. Kwa mujibu wa Msigwa, shughuli zilizopangwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara, madaraja na mitaro, kuimarisha huduma za afya, elimu, maji na umeme, kuhifadhi akiba ya chakula, kununua vifaa vya uokoaji, kuandaa maghala ya misaada ya kibinadamu na makazi ya muda kwa wananchi watakaolazimika kuhama maeneo hatarishi. Serikali pia itaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na majanga. Katika hatua nyingine, Msigwa amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoanzishwa, akieleza kuwa utekelezaji wake unaendelea katika hatua tofauti kulingana na upatikanaji wa rasilimali. Amesema pamoja na dhamira ya kukamilisha miradi yote, Serikali haiwezi kutekeleza mahitaji yote kwa wakati mmoja, hivyo baadhi ya miradi hutekelezwa kwa awamu ili kuzingatia vipaumbele vya maendeleo na majukumu mengine ya kitaifa. Akizungumzia maendeleo yaliyofikiwa, Msigwa amesema idadi ya watu nchini imeongezeka kutoka milioni 12.3 mwaka 1967 hadi takribani milioni 70 mwaka 2026, huku umaskini wa mahitaji ya msingi ukipungua kutoka asilimia 38.6 mwaka 1991/92 hadi asilimia 25.1 mwaka 2025. Aidha, ametoa wito kwa wananchi kufuatilia taarifa rasmi za tahadhari zinazotolewa na TMA na mamlaka husika, huku akizitaka pia taasisi za habari kuzingatia weledi, maadili na misingi ya uandishi wa habari katika kuripoti masuala ya umma.

Sun, 25 Oct 2026 18:42:40 +0000
Sports · Capital FM

Carrick future under major threat – can he survive?

Latest · English Premier League

Recently

Page 632 of 1159 · 23170 stories