Unganishwa

Search the region

23144 stories

Uncategorized · The Star Kenya

Mbadi: How PAYE changes will affect workers

Mbadi said the economy had begun showing signs of recovery and that some of the gains should now benefit lower-income salaried workers

Recently
Business · Issa Michuzi

TAWEN YOUTH YAZINDULIWA DAR, VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam VIJANA nchini wametakiwa kutumia fursa zinazopatikana katika sekta za elimu, fedha, uwekezaji, biashara na utamaduni, huku wakitumia teknolojia ya kisasa kujiletea maendeleo na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa. Wito huo umetolewa na Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wafanyabiashara Wanawake Afrika Mashariki (EAWiBP), Janice Benson Kimaro, wakati wa uzinduzi wa TAWEN Youth Dar es Salaam, tawi la vijana la Mtandao wa Uwezeshaji Wanawake Tanzania (TAWEN), uliofanyika jijini Dar es Salaam. Janice amesema uzinduzi huo unaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 inayosisitiza upatikanaji wa fursa sawa kwa wote, akibainisha kuwa vijana wanapaswa kuwa washiriki hai wa maendeleo kupitia ubunifu, uongozi na utekelezaji wa shughuli za maendeleo. “Tunaposema fursa sawa kwa vijana wetu, tunamaanisha kujenga mazingira ambayo kila kijana anapata nafasi ya kujifunza, kukuza kipaji chake, kuanzisha biashara na kupata ujuzi,” amesema. Amewataka vijana kutambua na kuendeleza vipaji vyao badala ya kutegemea elimu ya darasani pekee, huku akiwahimiza kujifunza Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ili kufahamu fursa zilizopo na namna ya kuzitumia. Aidha, amesema ukuaji wa teknolojia, ikiwemo Akili Unde (AI), umefungua fursa nyingi kwa vijana, hivyo wanapaswa kutumia ujuzi wao wa teknolojia kupata taarifa sahihi, kutafuta fursa na kuunganishwa na watu na taasisi zinazoweza kuwasaidia kufikia malengo yao. “Vijana mko vizuri sana katika mambo ya teknolojia. Tumieni elimu hiyo kutazama maudhui muhimu na kutambua mitandao inayowaunganisha na fursa. TAWEN Youth itoe semina kwa vijana ili kuwaonesha fursa muhimu zilizopo,” amesema. Amesisitiza kuwa uzinduzi wa TAWEN Youth unapaswa kuwa mwanzo wa utekelezaji wa mipango yenye matokeo yanayopimika, badala ya kuishia katika kuandika malengo bila kuyafanyia kazi. Amesema ni muhimu kwa viongozi wa jukwaa hilo kuweka utaratibu wa kutathmini utekelezaji wa mipango yao baada ya muda maalumu ili kubaini mafanikio na maeneo yanayohitaji maboresho. Kuhusu soko la Afrika Mashariki na Soko Huru la Afrika, Janice amewataka vijana kujifunza kwa kina kuhusu fursa za masoko hayo ili waweze kuzitumia kukuza biashara, uwekezaji na shughuli nyingine za kiuchumi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAWEN Taifa, Balozi Amina Salum Ally, amesema TAWEN Youth itakuwa jukwaa muhimu la kuendeleza falsafa ya vijana na kuwahamasisha kujitolea kushiriki katika shughuli za maendeleo ya taifa. Naye Mwenyekiti wa TAWEN Youth Dar es Salaam, Tarik Ninga, amesema jukwaa hilo limeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha vijana katika uongozi, stadi za maisha na ujasiriamali. Amesema pia litawaunganisha vijana na fursa za elimu, ajira, uwekezaji, masoko na mitandao ya kibiashara, huku likihamasisha ubunifu katika matumizi ya teknolojia kama nyenzo ya maendeleo na upatikanaji wa ajira. Malengo mengine ya jukwaa hilo ni kuimarisha ushiriki wa vijana katika uhifadhi wa mazingira na matumizi ya nishati jadidifu, kukuza mchango wao katika utafiti, pamoja na kuandaa mijadala, midahalo na mafunzo ya mara kwa mara. Ninga amesema TAWEN Youth pia inalenga kuwaunganisha vijana na taasisi zinazoweza kuwapatia fursa, mitaji na ushauri utakaowawezesha kutekeleza mawazo yao na kujenga msingi imara wa kujitegemea kiuchumi.

Sun, 25 Oct 2026 08:28:15 +0000
Uncategorized · The Standard

20 people killed, scores injured in Kanga head-on collision

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Fugitive Murder Suspect Arrested in Tanzania After Two-Year Manhunt

Latest · NATIONAL NEWS

Recently
Business · Jamhuri Media

Serikali yapiga marufuku shughuli za kilimo ndani ya Hifadhi ya Makame

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Ruto Praises Kalonzo for Recognising Govt Development Record in Ukambani

NATIONAL NEWS · Quick read

Recently
Business · Issa Michuzi

KASESELA AWAHIMIZA WANAWAKE MVOMERO KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Richard Atufigwege Kasesela, amewahimiza wanawake wilayani humo kutumia hekima, ujuzi na fursa mbalimbali za kiuchumi kujikwamua kimaisha, akisisitiza kuwa mwanamke imara ni msingi wa familia imara na jamii yenye maendeleo. Kasesela ameyasema hayo wakati akizungumza katika Kongamano la Wanawake la Wilaya ya Mvomero lililobeba kaulimbiu isemayo “Hekima ya Mwanamke ni Nguvu ya Jamii, Mwanamke Imara Jamii Imara,” ambapo amesisitiza umuhimu wa kutambua na kuthamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya familia na taifa. Amesema wanawake wana nafasi kubwa katika kilimo, biashara, ujasiriamali, malezi na uongozi, hivyo amewahimiza kuanzisha biashara kulingana na uwezo wao, kujiunga na vikundi vya kuweka na kukopa, pamoja na kutumia fursa za mikopo na programu za uwezeshaji zinazotolewa na Serikali na taasisi za fedha. Aidha, amesisitiza umuhimu wa wanawake kuwekeza katika elimu, mafunzo ya ujasiriamali, usimamizi wa fedha na matumizi ya teknolojia ili kuongeza thamani ya bidhaa zao, kupanua masoko na kukuza kipato. Katika hatua nyingine, Kasesela ameitaka jamii kushirikiana kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanawake, zikiwemo unyanyasaji wa kijinsia na vikwazo vya upatikanaji wa mitaji na elimu, huku akiwahimiza wanaume kuwaunga mkono wanawake katika shughuli za maendeleo na kushiriki majukumu ya kifamilia. Amesisitiza kuwa Serikali na wadau wa maendeleo wanapaswa kuendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayowawezesha wanawake kupata elimu, huduma bora za afya, rasilimali za uzalishaji na fursa za kiuchumi, pamoja na kushiriki katika nafasi za uongozi na maamuzi yanayohusu maendeleo ya jamii.

Sun, 25 Oct 2026 08:19:29 +0000
Uncategorized · The Citizen

Tanzanian university students make sci-fi movie about alien invasion

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

KWS kills elephant linked to fatal attack in Kitui, carcass to be incinerated

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Kalonzo Tells Ruto: ‘I Am Your Rival’ After President Names Him Main Political Competitor

NATIONAL NEWS · Quick read

Recently
Sports · Capital FM

Why are Liverpool struggling for Premier League goals?

Latest · English Premier League

Recently
Uncategorized · Jamhuri Media

Afrika ‘iwekeze’ katika teknolojia ya nyuklia kwa maendeleo endelevu

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

SERIKALI YATOA MAELEKEZO SABA KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI CHEMBA, KITETO

Na.Mwandishi Wetu SERIKALI imetoa maelekezo saba yanayolenga kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro wa ardhi unaohusisha Wilaya za Chemba na Kiteto, ikiwemo kusitisha shughuli za kilimo ndani ya Hifadhi ya Wanyamapori Makame na kutenga ekari 1,200 katika Kijiji cha Ngamboro kwa ajili ya wakulima watakaostahili kupatiwa maeneo mbadala. Maelekezo hayo yametolewa Oktoba 24, 2026, katika Kijiji cha Ndaleta, Wilaya ya Kiteto, Mkoa wa Manyara, na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo, baada ya Serikali kukamilisha uchunguzi wa mgogoro huo na kuchambua maoni ya pande mbalimbali zilizohusika. Amesema maamuzi hayo yanalenga kuhakikisha ardhi inatumika kwa kuzingatia sheria, mipaka ya kiutawala na mipango ya matumizi ya ardhi. Dkt. Akwilapo amesema mpaka wa kiutawala kati ya Halmashauri za Wilaya za Chemba na Kiteto haujawahi kubadilishwa kama ilivyodaiwa, hivyo wananchi na viongozi wanapaswa kuutambua na kuuheshimu. "Wananchi waliopewa maeneo ya kilimo ndani ya Hifadhi ya Wanyamapori Makame wanapaswa kusitisha shughuli zao, huku wale watakaostahili wakitambuliwa na kupangiwa maeneo mbadala katika ekari 1,200 zilizotengwa na Kijiji cha Ngamboro. "amesema Dkt. Akwilapo Aidha, amesema maeneo yaliyotengwa katika mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji vya Makame, Irkisibor, Ndedo na Katikati yataendelea kutumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa, huku vijiji vinavyohusika vikielekezwa kuhuisha mipango yao ya matumizi ya ardhi na kuweka alama zinazoonekana wazi katika mipaka ya hifadhi ili kuzuia uvamizi na migogoro ya baadaye. Waziri huyo pia amewataka viongozi wa vijiji kuhakikisha hawagawi ardhi nje ya mamlaka yao, akibainisha kuwa maeneo yanayodaiwa kugawiwa na vijiji vya Ndaleta na Mwitikia, maeneo ya Katikati na Ngamboro yalihusisha mamlaka ambazo hazikuwa na uwezo wa kisheria wa kuyagawa, hususan maeneo yaliyo nje ya mipaka ya vijiji au yaliyotengwa kwa ajili ya uhifadhi. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamad Hassan Chande, amewataka wananchi kupokea maamuzi ya Serikali kwa utulivu, kuheshimu maelekezo yaliyotolewa na kuendeleza ushirikiano ili kurejesha shughuli za maendeleo na kudumisha amani. Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa maeneo husika katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi. Naye Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martin Shigela, amesisitiza umuhimu wa kusimamia matumizi sahihi ya ardhi na kuhakikisha ugawaji wa maeneo unazingatia mipaka na matumizi yaliyokubaliwa. Amesema serikali itatoa maelekezo na mwongozo kwa halmashauri ili kuzuia kujirudia kwa makosa yanayohusiana na ugawaji wa ardhi, hususan maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za wananchi. Shingela amewataka watendaji wa kata, wakuu wa wilaya, wakuu wa idara na viongozi wengine wa serikali kuhakikisha wanakomesha vitendo vya baadhi ya viongozi wa vijiji kutumia madaraka yao vibaya kwa kugawa maeneo ya malisho kwa ajili ya kilimo au maeneo ya kilimo kwa ajili ya malisho. Aidha ameonya kuwa watendaji wa serikali watakaokiuka maelekezo yaliyotolewa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu zinazotumika. Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza umuhimu wa kuwatambua wananchi wanaopaswa kuhama kutoka maeneo yaliyopangwa kwa matumizi mengine na kuwahamishia katika eneo la hekta 1,200 lililotengwa kwa ajili yao. Amesema zoezi hilo linapaswa kufanyika kwa kuzingatia misingi ya haki na usalama, bila upendeleo katika ugawaji wa ardhi. Ameeleza kuwa hakuna sababu ya mtu mmoja kupewa eneo kubwa huku wengine wakibaki na maeneo madogo yasiyolingana na mahitaji yao. "Timu ya wataalamu ikiongozwa na Kamishna wa Ardhi itashirikiana na Mkuu wa Wilaya, kamati ya usalama na Mkurugenzi wa Halmashauri kutambua ukubwa wa eneo lililotengwa pamoja na kuandaa orodha ya wananchi wote wanaopaswa kuhamishwa. Amesema hatua hiyo itasaidia kuhakikisha ardhi inagawiwa kwa usawa na wananchi wote wanaostahili wanapata maeneo yao kwa kuzingatia haki."amesema Mhe.Shingela Vilevile, amewataka wananchi kuwa wavumilivu na kutoa ushirikiano kwa serikali ili zoezi hilo likamilike kwa haraka kabla ya kuanza kwa msimu wa mvua, hatua itakayowawezesha kupata maeneo ya kuzalisha. Amesema wananchi wenye mahitaji mengine ya kiserikali wanapaswa kufuata njia rasmi kupitia kwa watendaji wa kata na vijiji, Mkuu wa Wilaya, madiwani, Mkurugenzi wa Halmashauri na mbunge ili kupata suluhisho la kudumu kwa changamoto zinazowakabili.

Sun, 25 Oct 2026 08:06:47 +0000
Health · Issa Michuzi

UGANDA YAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS SAMIA YA KUIMARISHA AFYA YA UZAZI, YAPAMBANA NA MALARIA.

Serikali ya Uganda imepongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ni Kinara wa Umoja wa Afrika (AU) wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, katika kuongoza juhudi za kuimarisha afyaya uzazi na ustawi wa wanawake, watoto na vijana barani Afrika na kupambana na magonjwa ikiwemo Malaria. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi wa Afya wa Uganda, Mhe. Anifa Bangirana, alipokutana na ujumbe wa Serikali ya Tanzania jijini Kampala,  kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria. Waziri Bangirana amesema mapambano dhidi ya Malaria ni muhimu katika kuimarisha afya ya uzazi, kwa kuwa ugonjwa huo huathiri wanawake wajawazito na watoto hivyo kuongeza hatari ya vifo au athari zinazoweza kuzuilika. Amesema kuwa Uganda inalenga kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030 kupitia Mkakati wa Kitaifa na Mpango wa Kutokomeza Malaria Busoga (Busoga Malaria Eradication Programme-BMEP), unaohusisha Serikali, wadau na jamii katika kutekeleza afua za kinga, upimaji na matibabu. Taarifa ya utafiti wa viashiria vya Malaria nchini Uganda ya mwaka 2024/25 inaonesha kuwa matumizi ya kinga dhidi ya Malaria kwa wanawake wajawazito yameimarika, ambapo asilimia 73 walipata angalau dozi tatu za dawa za kinga, ikilinganishwa na asilimia 41 mwaka 2018/19. Hata hivyo, maambukizi ya Malaria kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 59 imeongezeka kutoka 10% mwaka 2018/19 hadi 13% mwaka 2024/25, hali inayoonesha umuhimu wa kuimarisha juhudi za mapambano dhidi ya ugonjwa huo. Kwa upande wake, Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania, Dkt. Sunday Dominico, Naibu Mkuu wa Sekretarieti ya Kinara wa Umoja wa Afrika - Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, ameeleza kuwa Rais Samia amekuja na lengo la Sifuri tatu kuelekea kuimarisha afya ya Mama na Mtoto ifikapo mwaka 2030. “Rais Samia amelenga hadi ifikapo mwaka 2030 Bara la Afrika tuwe na Sifuri ya kujifungulia nyumbani, Sifuri ya vifo vya mama na mtoto vinavyoweza kuzuilika, na Sifuri ya watoto wasiokuwa na chanjo” amefafanua Dkt. Sunday na kusisitizakuwa kuwa mapambano dhidi ya Malaria ni sehemu muhimu ya kufanikisha shabaha hizo na kulinda Afya ya Mama na Mtoto. Akiongoza mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria katika Mkoa wa Busoga, Dkt. Specioza Wandira Kazibwe, Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke wa Uganda (Mstaafu) na Mshauri Mwandamizi wa Rais wa Uganda kuhusu Idadi ya Watu na Afya amesema utafiti wa awali (pilot study) uliofanyika katika eneo la Busoga umeonesha mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya Malaria. “Takwimu zinaonesha kupungua kwa msongamano wa mbu aina ya ‘Anopheles’ kwa asilimia 88.7, kiwango cha maambukizi mapya ya Malaria yaliyobainika katika vituo vya kutolea huduma za afya yameshuka kutoka 90% hadi 10%” amebainisha Dkt. Kazibwe na kuikaribisha Tanzania pamoja na wadau wengine kufika Busoga kujifunza namna walivyofanikisha programu hiyo. Katika ziara hiyo, ujumbe wa Tanzania, ukiongozana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Meja Jenerali Marco Gaguti, umetembelea Kata mbalimbali katika Wilaya ya Iganga, Mkoa wa Busoga, kujifunza namna jamii inavyoshiriki katika utekelezaji wa Mpango wa BMEP katika kuimarisha afua za kinga na kudhibiti maambukizi ya Malaria.

Sun, 25 Oct 2026 08:07:21 +0000
Business · Issa Michuzi

PROF. SHEMDOE AKAGUA MIRADI YA BILIONI 26 MPANDA, AWATAKA WATUMISHI KUTOA HUDUMA BORA ZINAZOAKISI UWEKEZAJI HUO

Na OWM–TAMISEMI, Mpanda - Katavi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amekagua miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 26 katika Manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi, na kuwataka watumishi wa umma kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ili uwekezaji huo uwe na manufaa kwa wananchi na tija kwa Taifa. Prof. Shemdoe ametoa wito huo Oktoba 24, 2026, katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda, wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua miradi ya maendeleo na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma katika manispaa hiyo. Katika ziara hiyo, Prof. Shemdoe alikagua miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 26 ikiwemo ujenzi wa shule ya kwanza ya sekondari ya wavulana Katavi Boys, ujenzi wa barabara za lami za mjini kupitia Mradi wa TACTIC, madaraja mawili pamoja na ujenzi wa Jengo la Watoto Wachanga katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda. Baada ya kukagua Jengo la Watoto Wachanga, Prof. Shemdoe amewataka watumishi wa hospitali hiyo kuendelea kuwahudumia wagonjwa kwa weledi na uzalendo ili uwekezaji uliofanywa uendane na ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi. “Niendelee kuwaomba watumishi wote, na si wa hapa hospitalini pekee, tuendelee kuwasikiliza na kuwahudumia wananchi kwa lugha nzuri. Kumpa mtu tabasamu kwa kumhudumia vizuri ni baraka kwako, lakini akiondoka akiwa ananung’unika, huwezi kupata baraka,” amesisitiza Prof. Shemdoe. Aidha, Prof. Shemdoe amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji wa shilingi bilioni 26 katika miundombinu ya elimu, barabara na afya ya msingi katika Manispaa ya Mpanda, akieleza kuwa uwekezaji huo umeboresha huduma za elimu, usafiri na usafirishaji, pamoja na matibabu kwa wakazi wa Mpanda. Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mhe. Charles Philipo, akitoa neno la shukrani kwa Prof. Shemdoe alipotembelea Shule ya Sekondari ya Katavi Boys, amemshukuru Mhe. Rais kwa kumteua Prof. Shemdoe na kumpongeza Prof. Shemdoe kwa utendaji kazi wake mzuri, huku akimwomba aridhie bweni mojawapo shuleni hapo lipewe jina lake, ombi ambalo Prof. Shemdoe aliliridhia. Miradi hiyo yenye thamani ya bilioni 26 aliyoikagua Prof. Shemdoe ni sehemu ya kiasi cha shilingi Trilioni 1.4 ambacho Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani aliridhia kilektwe Mkoani Katavi kwa ajili ya miradi maendeleo, Trilioni 1.4 ni takwimu zilizotolewa Oktoba 13, 2026 na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko kwa Makamu wa Rais Mhe. Deogratius Ndejembi alipowasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Sun, 25 Oct 2026 08:10:14 +0000
Uncategorized · The Standard

The price of compassion: Pauline Kawira turns painful nursing ordeal into a book

Read the full report from the original source.

Recently
Sports · Capital FM

When is Premier League ‘sacking season’ – and who should be worried?

Latest · English Premier League

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Two siblings killed in explosive blast in Garissa

The minors aged 15 and 16 were playing with the explosive while they were herding cattle in Bura when it exploded, killing them.

Recently
Uncategorized · BBC Rwanda

'Aka ni ko karyo ka nyuma ko kumuzibira': Obama yateye ivyatsi Trump mu kwiyamamariza Abademokarate

Obama yavuze ko aya matora ari yo "mahirwe yacu meza ya nyuma yo kugerageza guhagarika ubupfu bumwe bumwe buranga iyi ntwaro."

Recently
Uncategorized · PML Daily

Austria commits Ugx15bn to fight gender-based violence in Northern Uganda

KAMPALA — More than 12,000 reported domestic violence cases and persistent gaps in access to specialised care for rape survivors are among the challenges a new €3.2 million (about shs15.45 billion)...

Recently

Page 641 of 1158 · 23144 stories