Unganishwa

Search the region

22984 stories

Uncategorized · Iwacu

Yussuf Ndayishimiye, le roc burundais qui a tenu Nice debout

Il y a des victoires qui se racontent par les buteurs. Et d'autres qui se comprennent en regardant celui qui a empêché l'effondrement. Ce samedi 11 octobre 2026, à l'Allianz Riviera, l'OGC Nice a renversé Strasbourg (2-1). Une victoire arrachée dans la douleur. Et qui porte, en son socle, la griffe d'un Burundais.

Mon, 12 Oct 2026 14:48:23 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

OSHA YAGUSA MAISHA YA WAKAZI WA MKOA WA KILIMANJARO

Mgeni Rasmi wa Bonanza la OSHA la Huduma kwa Jamii (OSHA CSR Bonanza 2026) ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dkt. Christopher Timbuka, akiwahutubia washiriki wa bonanza. Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akitoa salamu za ukaribisho katika Bonanza la OSHA la Huduma kwa Jamii (OSHA CSR Bonanza 2026) lililofanyika Viwanja vya Shule ya Polisi Moshi Oktoba 8, 2026. Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akifuatilia matukio katika Bonanza la OSHA la Huduma kwa Jamii (OSHA CSR Bonanza 2026) lililofanyika Viwanja vya Shule ya Polisi Moshi Oktoba 8, 2026. Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akipanda mti katika Shule ya Sekondari Vudoi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya huduma kwa jamii iliyotekelezwa na Taasisi yake katika Mkoa wa Kilimanjaro Oktoba 7-8, 2026. Baadhi ya maafisa usafirishaji (bodaboda) waliopatiwa mafunzo ya usalama na afya na OSHA katika kampeni ya huduma kwa jamii iliyotekelezwa na OSHA katika Mkoa wa Kilimanjaro Oktoba 7-8, 2026 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa vifaa kinga na Mgeni Rasmi wa tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dkt. Christopher Timbuka. Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mwanga Mpampalika Mfaume na viongozi wengine wa Wilaya ya Mwanga wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Mwanga mara baada ya OSHA kukabidhi msaada wa mashuka 100 katika hospitali hiyo. Na Mwandishi Wetu WAKALA wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umegusa maisha ya wananachi wa Mkoa wa Kilimanjaro kupitia kampeni yake ya huduma kwa jamii ambapo imekabidhi vifaa vya msaada katika mashule, hospitali pamoja na kutoa mafunzo ya usalama na afya kwa wajasiriamali wadogo zaidi ya 500. Makundi yaliyonufaika na kampeni hiyo ni kutoka Wilaya za Mwanga na Moshi Mjini ambapo OSHA imepanda miti 200 ya matunda katika shule mbalimbali za msingi na sekondari ndani ya Wilaya ya Mwanga. Aidha, imekabidhi mashuka 100 katika Hospitali ya Wilaya ya Mwanga, vifaa vya michezo pamoja na kutoa mafunzo ya usalama na afya yaliyofanyika sambamba na kukabidhi vifaa kinga kwa makundi ya wajasiriamali wadogo wenye ulemavu pamoja na maafisa usafirishaji (bodaboda). Akizungumza katika kilele cha kampeni hiyo katika Viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi, Mgeni Rasmi wa Bonanza la OSHA la Huduma kwa Jamii (OSHA CSR Bonanza 2026) ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dkt. Christopher Timbuka, amesema lengo la kampeni hiyo ni kugusa maisha ya makundi yenye mahitaji maalum katika jamii. "Miongoni mwa makundi yaliyonufaika na kampeni hii ni pamoja na Maafisa Usafirishaji (Bodaboda) 200 wa Wilaya ya Mwanga na Moshi, Wanachama 70 kutoka Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA), Shule za Sekondari Mwanga pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Mwanga.” Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, amesema tukio hilo ni utekelezaji wa mkakati wa OSHA wa kurudisha kwa jamii sambamba na utekelezaji wa majukumu yake ya msingi ya kusimamia uzingatiaji wa kanuni bora za usalama na afya katika maeneo ya kazi nchini.“Jukumu letu kubwa ni kuhakikisha maeneo ya kazi yanakuwa na mifumo madhubuti ya kuwalinda wafanyakazi dhidi ya vihatarishi vya ajali, magonjwa na vifo mahali pa kazi. Sambamba na utekelezaji wa majukumu yetu, tumekuwa na desturi ya kuwa na shughuli zinazogusa maisha ya watu katika kipindi ambacho tunashiriki mashindano ya SHIMIWI,” ameeleza Kiongozi Mkuu wa OSHA.Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Mwanga Mpampalika Mfaume pamoja na wanufaika wa kampeni hiyo, wameishukuru Taasisi ya OSHA kwa kubana matumizi yake ili kuwezesha upatikanaji wa mahitaji ya msingi kwa makundi mbalimbali ya jamii. “Nimefurahia mafunzo ya leo kwasababu nimefahamu kazi za OSHA na zaidi nimejifunza kwamba usalama si tu kwa wafanyakazi walioajiriwa bali hata kwetu sisi tuliojiajiri tunatakiwa kuzingatia kanuni bora za usalama na afya kwa ajili ya usalama wetu wenyewe,” ameeleza Bi. Judika Allen Mshiriki wa Mafunzo. Kampeni hiyo ya OSHA ya huduma kwa jamii ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka kama sehemu ya ushiriki wa Taasisi katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara na Wakala za Serikali (SHIMIWI), imehitimishwa kwa Bonanza OSHA la Huduma kwa Jamii (OSHA CSR Bonanza 2026) lililofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi Oktoba 08, 2026.

Mon, 12 Oct 2026 14:37:23 +0000
Uncategorized · Iwacu

Primus Ligue 2026-2027 – Journée 6 : Le trône, le vertige et le gouffre

Il y a des classements qui se lisent. Et il y a ceux qui se ressentent comme un poème d'amour et de cruauté. Au soir de ce 11 octobre 2026, la sixième journée de la Primus Ligue Burundi a rendu son verdict. Et ce verdict a des airs de roman.

Mon, 12 Oct 2026 14:38:52 +0000
Uncategorized · TechCabal East Africa

Millions of Africans have internet coverage but are not online. Here’s why

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Govt turns to podcasts to explain its agenda

Latest · News

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Immigration searches Congresswoman Ilhan's home

The search "is part of an ongoing federal criminal investigation," the spokesperson said

Recently
Uncategorized · Iwacu

Primus Ligue 2026-2027 : La sixième journée, un théâtre d’ivresse et de désillusions

Il y a des journées qui se contentent de faire tourner le ballon. Et il y en a d'autres qui racontent des destins. La sixième levée de la Primus Ligue, étalée sur trois jours, du vendredi 09 au dimanche 11 octobre 2026, aura été de celles-là. Une journée de feu, de fureur et de confirmations, où les certitudes ont vacillé au rythme des crampons sur les pelouses d'Ingoma, de Gatwaro, d'Umuco et d'Urukundo.

Mon, 12 Oct 2026 14:33:46 +0000
Sports · Mwananchi

Yanga njia panda Abuya kurejea dimbani

Kiungo wa Yanga, Duke Abuya, anakabiliwa na uwezekano wa kukaa nje ya uwanja kwa muda usiojulikana baada ya kuthibitishwa kupata jeraha la nyama za paja katika mchezo dhidi ya Simba, uliomalizika...

Recently
Uncategorized · DW Afrique

Gronde après l'accord de Donald Trump sur le diesel russe

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

New CoG Chair Njuki vows to stand up to Ruto

News · 4 hours ago

Recently
Uncategorized · Capital FM

IEBC sued over changes to ballot paper security features

Business · 4 hours ago

Recently
Uncategorized · Capital FM

Shikangwa Hits Hat-Trick as Starlets Seal Record 22-0 Aggregate Win Over Seychelles

Latest · football

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

PEMA EVENT, MS ONE AGENCY KUHAMASISHA ELIMU KUHUSU MENOPAUSE

Mtumishi wa Mungu, Isaac Paul Hammoud (IPM) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 12, 2016. Mkurugenzi wa PEMA Event, Khairat Ndassiwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 12, 2016. Na Mwandishi Wetu PEMA Event kwa kushirikiana na MS One Agency wameandaa tukio maalumu la kutoa elimu kuhusu mabadiliko ya mwili na homoni yanayotokea wakati wa premenopause, menopause na postmenopause, wakilenga kuongeza uelewa kwa wanawake, wanaume na Wanandoa nchini Tanzania na kuondoa hofu pamoja na imani potofu zinazohusishwa na hatua hizo za maisha. Wadau hao wamesema ukosefu wa elimu kuhusu mabadiliko hayo umekuwa ukisababisha baadhi ya wanawake kuishi kwa hofu, huku wengine wakihusisha hali wanazopitia na kulogwa, kuingiliwa au maradhi mengine badala ya kutafuta elimu na ushauri sahihi wa kitaalamu. Akizungumza leo, Oktoba 12, 2026, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa PEMA Event, Khairat Ndassiwa, amesema tukio hilo litafanyika Oktoba 31, mwaka huu, katika ukumbi wa ghorofa wa Golden Jubilee, jijini Dar es Salaam, likiwa na lengo la kuelimisha jamii kuhusu menopause na changamoto zinazowakabili wanawake katika hatua hiyo ya maisha. Amesema tukio hilo ni sehemu ya juhudi za PEMA Event kwa kushirikiana na MS One Agency kuhamasisha mazungumzo ya wazi kuhusu masuala ambayo bado hayajaeleweka ipasavyo katika jamii, huku wanawake wakipewa nafasi ya kueleza uzoefu wao na kupata ushauri unaofaa. Kwa upande wake, Mtumishi wa Mungu, Isaac Paul Hammoud (IPM), amesema jamii inapaswa kutambua umuhimu wa elimu kuhusu masuala ya maisha na afya badala ya kuyatafsiri kwa mitazamo isiyo sahihi. “Elimu haina mwisho. Usifanye unajua kila kitu, bado unajifunza,” amesema IPM, akisisitiza kuwa elimu kuhusu menopause inapaswa kuwahusisha wanawake na wanaume kwa kuwa wote ni sehemu ya familia na jamii. Amesema wanaume wana nafasi muhimu ya kuwasaidia wanawake wanaopitia mabadiliko hayo, hivyo wanapaswa kupata uelewa utakaowawezesha kutoa msaada unaohitajika. Amewahimiza wananchi, hususan wakazi wa Dar es Salaam, kushiriki katika tukio hilo ili kupata maarifa yatakayowasaidia kuelewa menopause na changamoto zake. Naye Mkurugenzi Mwenza wa PEMA Event, Imelda Mtema, amesema elimu kuhusu mabadiliko ya homoni kwa wanawake ni muhimu katika kuwasaidia kuelewa kinachoendelea katika miili yao na namna ya kukabiliana na mabadiliko hayo. Amesema baadhi ya wanawake hukosa uelewa wa kutosha kuhusu vipindi vya premenopause, menopause na postmenopause, hali inayoweza kuwafanya kudhani kuwa wana magonjwa mengine au kuhusisha mabadiliko hayo na imani potofu. Mtema amesema kupitia tukio hilo, PEMA Event kwa kushirikiana na MS One Agency wanalenga kujenga uelewa mpana kwa wanawake, wanafamilia, waajiri na jamii kwa ujumla ili kuwapa wanawake wanaopitia mabadiliko hayo heshima, uelewa na msaada unaostahili. Amesisitiza kuwa ni muhimu jamii kutafuta maarifa mapema badala ya kusubiri changamoto zitokee, akieleza kuwa tukio la Oktoba 31 litatoa nafasi kwa wanawake na wanaume kujifunza, kuzungumza na kubadilishana uzoefu kuhusu menopause na masuala yanayohusiana nayo.

Mon, 12 Oct 2026 14:26:08 +0000
Health · Issa Michuzi

BoT, NHIF, TIRA, UHAMIAJI NA TBL WASHIRIKI KONGAMANO LA MISA TANZANIA KUJADILI MAENDELEO YA SEKTA YA HABARI

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tanzania), Edwin Soko, amevitaka vyombo vya habari nchini kuimarisha uwezo wao wa kiuchumi ili viweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi huku vikiendelea kuchochea maendeleo ya jamii. Soko ameyasema hayo jijini Mwanza wakati wa Kongamano la MISA Tanzania na wadau lililofanyika leo, Oktoba 12, 2026, likiwa na kaulimbiu ya “Uhuru wa Vyombo vya Habari Kiuchumi.” Kongamano hilo limewakutanisha wanachama 60 wa MISA Tanzania kutoka Kanda ya Ziwa, inayojumuisha Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara na Kagera; Kanda ya Magharibi yenye mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi; pamoja na Kanda ya Kati inayojumuisha Singida na Dodoma. Aidha, mkutano huo umehudhuriwa na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za umma na binafsi, zikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Idara ya Uhamiaji, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Ushiriki wa taasisi hizo ni sehemu ya mkakati wa MISA Tanzania wa kutekeleza mpango kazi wake wa mwaka, unaolenga kuimarisha mahusiano na ushirikiano kati ya vyombo vya habari na wadau wa maendeleo. Akizungumza katika kongamano hilo, Soko alisisitiza kuwa vyombo vya habari vinapaswa kujenga misingi imara ya kiuchumi huku vikizingatia weledi na maadili ya taaluma katika kutekeleza wajibu wake kwa jamii. Alionya kuhusu tabia ya baadhi ya wanahabari kukimbilia kuchapisha habari bila kufanya uchunguzi wa kina, akisema ni muhimu kuzingatia ukweli, maadili na weledi ili kuepusha upotoshaji wa umma na taarifa zinazoweza kuchochea uchonganishi. Kwa mujibu wa Soko, ushirikiano wa karibu kati ya vyombo vya habari na sekta nyingine ni muhimu katika kujenga tasnia imara inayoweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kutoa mchango katika maendeleo ya Taifa. Kongamano hilo limekuwa fursa ya kuwakutanisha wanahabari na wadau wa sekta mbalimbali kujadili umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari kiuchumi na nafasi ya ushirikiano katika kuimarisha tasnia ya habari nchini.

Mon, 12 Oct 2026 14:26:15 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

RC NYONGO APIGA MARUFUKU WANAFUNZI KUBEBESHWA MAKOSA YA WAZAZI

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani MKUU wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, amepiga marufuku tabia ya wanafunzi kufukuzwa au kurudishwa nyumbani kwa kushindwa kuchangia chakula shuleni, akiwataka walimu kuacha kuwaadhibu watoto kwa makosa yanayohusiana na wazazi wao. Nyongo alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake katika Kata ya Msata, Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, alipokutana na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero zao. Alisema mtoto hapaswi kunyimwa fursa ya kupata elimu kwa sababu mzazi au mlezi ameshindwa kutimiza mchango wa chakula, akisisitiza kuwa walimu wanapaswa kufuata utaratibu unaofaa katika kushughulikia changamoto hizo bila kumuathiri mwanafunzi. Hata hivyo, Nyongo aliwataka wazazi na walezi kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha watoto wanapata chakula shuleni, akieleza kuwa pamoja na Serikali kutoa elimu bila ada, jamii ina wajibu wa kushiriki katika mahitaji mengine ya wanafunzi, yakiwemo sare na chakula. Alisema wazazi wanaokataa kuchangia chakula wanapaswa kubainishwa ili suala hilo lifuatiliwe na kushughulikiwa, badala ya kuwaadhibu watoto ambao hawana uwezo wa kuamua kuhusu michango hiyo. “Tusiendekeze haya,Wazazi wenzangu, tujifunze na kuzoea kuchangia, Kama mzazi hutaki kuchangia, unataka mtoto akale chakula cha nani?” alihoji Nyongo. WAZAZI WALALAMIKIA MICHANGO Agizo hilo limekuja wakati baadhi ya wazazi katika eneo hilo wakilalamikia wingi wa michango ya shule, wakisema hali hiyo inawaongezea mzigo wa gharama za elimu, hasa kwa familia zenye kipato cha chini. Mmoja wa wakazi wa Msata, Daniel Mkali, alisema wazazi wamekuwa wakikabiliwa na michango mbalimbali inayohusisha ulinzi, mitihani, chakula, majaribio na masomo ya ziada, hali inayowafanya baadhi yao kushindwa kumudu gharama hizo. Alisema wakati mwingine wazazi hutakiwa kuchangia kiasi tofauti kwa mahitaji mbalimbali, huku gharama za masomo ya ziada kwa wiki zikifikia Sh6,000, jambo alilodai kuwa ni gumu kwa familia zenye kipato kidogo. “Unakuta mtoto anarudishwa shule. Sasa kosa lake ni nini? Kama kuwajibishwa niwajibishwe mzazi kwa ujinga wangu,” alisema Mkali. DC NDEMANGA AWAOMBA WAZAZI KUSHIRIKIANA NA WALIMU Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga, aliwataka wazazi kushirikiana na walimu kutafuta suluhisho la changamoto zinazojitokeza shuleni, ikiwemo suala la michango. Ndemanga alisema baadhi ya wazazi wamekuwa wakipuuza michango ya shule, huku akibainisha kuwa katika shughuli nyingine za kijamii, ikiwemo sherehe ,mahafali, baadhi yao hushiriki kuchangia fedha. Alitoa rai kwa wazazi kutumia mikutano ya shule kujadili na kukubaliana kuhusu mahitaji ya wanafunzi ili kuepusha migogoro na kuhakikisha watoto wanaendelea na masomo bila vikwazo visivyo vya lazima. WANANCHI WATAJA KERO ZA BARABARA NA MAJI Katika mkutano huo, wakazi wa Msata, akiwemo Chocha Chocha na Yusuph Ramadhani, waliwasilisha malalamiko kuhusu changamoto za barabara na upatikanaji wa maji, wakiiomba Serikali kuzifanyia kazi. Nyongo alisema dhamira ya ziara zake ni kuwafikia wananchi katika maeneo yao, kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo na kushirikiana na viongozi pamoja na mamlaka husika kutafuta ufumbuzi wa kero hizo.

Mon, 12 Oct 2026 14:29:11 +0000
National · Issa Michuzi

TOSCI YAHIMIZA MATUMIZI YA MBEGU BORA KUIMARISHA USALAMA WA CHAKULA

Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imeendelea kutoa elimu kwa wakulima kuhusu umuhimu wa kutumia mbegu bora, ikieleza kuwa hatua hiyo ni msingi wa kuongeza uzalishaji wa mazao na kuimarisha usalama wa chakula nchini. Akizungumza Oktoba 12, katika Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika kuanzia Oktoba 10 hadi 16, 2026, mkoani Tanga, Aleti Kibalazo, Mtafiti na Mkaguzi wa Mbegu kutoka TOSCI, amesema matumizi ya mbegu bora ni hatua muhimu katika kuhakikisha wakulima wanazalisha chakula cha kutosha na chenye ubora. Kibalazo amesema usalama wa chakula unaanzia kwenye mbegu bora, akieleza kuwa bila kuhakikisha wakulima wanatumia mbegu zinazokidhi viwango, jitihada za kuongeza uzalishaji wa chakula haziwezi kufikia matokeo yanayotarajiwa. Amesema Serikali imewekeza katika tasnia ya mbegu, huku TOSCI ikiendelea na mikakati ya kuhakikisha mbegu bora zinapatikana kwa wingi, zinawafikia wakulima kwa urahisi na zinakuwa na gharama nafuu. Ameeleza kuwa mikakati hiyo inazingatia mambo matatu muhimu yanayojulikana kama A3, ambayo ni Availability (upatikanaji wa mbegu), Accessibility (urahisi wa kuzipata) na Affordability (uwezo wa wakulima kumudu gharama zake). Kwa mujibu wa Kibalazo, upatikanaji wa mbegu pekee hautoshi iwapo wakulima wanashindwa kuzifikia kutokana na umbali au gharama za usafiri. Hivyo, TOSCI inaendelea kusajili mawakala wa kusambaza mbegu hadi vijijini ili kurahisisha upatikanaji wake na kupunguza muda na gharama ambazo wakulima hutumia kuzitafuta. Amesema kuongezeka kwa upatikanaji wa mbegu bora kunatarajiwa kusaidia wakulima kuzipata kwa urahisi zaidi, huku ongezeko la upatikanaji na matumizi yake likitarajiwa kuchangia kupunguza gharama kulingana na hali ya soko na mahitaji. Kibalazo amesema TOSCI inaendelea kutoa elimu moja kwa moja kwa wakulima kupitia maonesho na kampeni mbalimbali ili kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa kutumia mbegu zinazokidhi viwango, amesisitiza kuwa elimu hiyo haihusu mbegu za zao moja pekee, bali inajumuisha mazao mbalimbali, pamoja na miche na vipando. Amesema kwa mwaka 2026, TOSCI imeweka makadirio ya matumizi ya mbegu bora kufikia tani 120,000, na hadi sasa kiwango kilichofikiwa tayari kimevuka nusu ya lengo hilo. Kwa muda mrefu, taasisi hiyo inalenga matumizi ya mbegu bora kufikia tani 250,000 ifikapo mwaka 2030. Ameeleza kuwa maendeleo hayo yanahusishwa na kampeni zinazoendelea za kuhamasisha matumizi ya mbegu bora, huku ushiriki wa TOSCI katika Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani ukiwa sehemu ya juhudi za kukutana na wakulima moja kwa moja, kuwapatia elimu na kuwahamasisha kutumia mbegu bora katika shughuli zao za kilimo.

Mon, 12 Oct 2026 14:21:49 +0000
Uncategorized · Chimpreports

dfcu Foundation Calls on SMEs to Build Better Records to Unlock Financing

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Chimpreports

CHIMP SPORT: Naiga, Mutesi Conquer Commonwealth

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Muthomi Njuki elected Council of Governors chairperson, Lusaka named deputy

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

MP Millie Odhiambo breaks silence on alleged rift with Wanga

Read the full report from the original source.

Recently

Page 705 of 1150 · 22984 stories