Unganishwa

Search the region

22984 stories

Uncategorized · Issa Michuzi

UMAHIRI WA WAHITIMU WA VETA WANG’ARA WIKI YA VIJANA SUMBAWANGA

Banda la Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) limekuwa kivutio katika Maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Nduwa, mjini Sumbawanga, mkoani Rukwa, kutokana na umahiri wa vijana wahitimu na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya VETA, hususan wenye ulemavu, wanaoonesha ujuzi walioupata kupitia mafunzo ya ufundi stadi. Maonesho hayo yaliyoanza Oktoba 8 na yanayotarajiwa kuhitimishwa Oktoba 14, 2026, yanafanyika chini ya kaulimbiu “Mazingira Tofauti, Fursa Sawa kwa Vijana,” ambayo imetafsiriwa kwa vitendo kupitia ushiriki wa vijana wenye ulemavu wanaotumia ujuzi wao kubuni na kutengeneza bidhaa mbalimbali. Miongoni mwa vijana wanaovutia ni Francis Madanganya, mhitimu wa TEHAMA kutoka VETA Kipawa na Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro, mwenye ubunifu wa kifaa cha kuhifadhi na kusambaza umeme kwa kompyuta mpakato (laptop); Gonsalva Lungu na Riziki Ndumba, wahitimu wa Ubunifu, Ushonaji na Teknolojia ya Nguo kutoka VETA Songea; Imelda Kanyengele, mwanafunzi wa fani hiyo VETA Nkasi; pamoja na Ernest Mashiku Igobeko, mhitimu wa useremala kutoka VETA Tanga ambaye ana ulemavu wa uoni. Umahiri wa vijana hao umevutia wadau mbalimbali, wakiwemo wawakilishi wa Benki ya CRDB, ambao wamenunua bidhaa zao na kuwachangia fedha kwa ajili ya kukuza mitaji ya shughuli zao. Meneja wa Mahusiano na Taasisi za Serikali wa benki hiyo, Paskalina Diu, amesema wataangalia namna ya kuwawezesha vijana hao kupata mikopo na huduma za kifedha zitakazosaidia kukuza shughuli zao za kiuchumi. Amesema kupitia CRDB Bank Foundation, benki hiyo ina fursa za kuwawezesha vijana kiuchumi, ikiwemo mitaji wezeshi isiyo na riba, ameeleza kuwa kliniki ya taasisi hiyo itatumika kuangalia namna bora ya kuwasaidia vijana wenye ujuzi wa ufundi stadi kujiajiri na kuendeleza shughuli zao. Kwa upande wake, Imelda Kanyengele amesema mafunzo anayopata VETA Nkasi yamemwezesha kushona aina mbalimbali za nguo na kutengeneza batiki, akiwahimiza vijana wenzake, hususan wenye ulemavu, kutokata tamaa katika kutafuta elimu na ujuzi utakaowawezesha kujitegemea. Maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Mon, 12 Oct 2026 14:17:36 +0000
Uncategorized · Issa Michuzi

NAESA KUWAJENGEA UWEZO MAAFISA UGANI KUTAFSIRI UTABIRI WA MVUA.

Wakala ya Taifa ya Huduma za Ugani (NAESA), kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, umejipanga kutoa mafunzo kwa maafisa ugani katika mikoa 14 inayopata misimu miwili ya mvua, yakilenga kuwajengea uwezo wa kutafsiri taarifa za utabiri wa mvua na kuzitumia katika kutoa ushauri kwa wakulima. Akizungumza Oktoba 12, mara baada ya Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde kutembelea Banda la NAESA katika Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika kuanzia Oktoba 10 hadi 16, 2026, mkoani Tanga, Kaimu Meneja wa Sehemu ya Masoko na Uongezaji Thamani, Esther Mwaisango, amesema mafunzo hayo yanalenga kuimarisha uwezo wa maafisa ugani kuelewa taarifa za hali ya hewa na kuwafikishia wakulima elimu itakayowasaidia kupanga shughuli zao za kilimo. Amesema maafisa ugani wana nafasi muhimu katika kuwaunganisha wakulima na taarifa za kitaalamu zinazohitajika katika uzalishaji, huku NAESA ikiendelea kuratibu na kusimamia huduma za ugani nchini kwa kutoa mafunzo kwa maafisa ugani, kuratibu mafunzo katika vyuo vya kilimo na kuandaa miongozo ya utoaji wa elimu ya ugani. Aidha, Mwaisango amesema NAESA imeshirikisha wawakilishi wa vyuo vya kilimo katika maonesho hayo ili kuonesha teknolojia mbalimbali zinazofundishwa kwa maafisa ugani, zikiwemo mbinu za uchakataji na uongezaji thamani wa mazao, ameongeza kuwa zaidi ya wakulima 5,000 wamesajiliwa katika mfumo wa usajili wa wakulima, huku zoezi hilo likiendelea. Kwa upande wake, Nyagesera, mkufunzi kutoka Chuo cha Kilimo Uyole, amesema wakulima wanapaswa kuachana na mtazamo wa kuuza mazao ghafi pekee na badala yake kuangalia fursa za kuyachakata na kutengeneza bidhaa zinazoweza kuwaongezea kipato. Amesema bidhaa zinazooneshwa katika banda la NAESA zimetokana na mazao ya kilimo na zinalenga kuwapa wakulima mifano ya namna wanavyoweza kutumia mazao yao kutengeneza bidhaa mbalimbali, ikiwemo bidhaa za lishe. Nyagesera ametoa mfano wa parachichi ambayo baadhi yake yanapotokidhi vigezo vya soko huishia kutupwa, akieleza kuwa wakulima wanapaswa kuona fursa ya kutumia mazao hayo kutengeneza bidhaa zenye thamani badala ya kuyaacha bila matumizi. Ameongeza kuwa mazao ya kilimo yanaweza kutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali, ikiwemo mafuta yanayotokana na nta ya nyuki, akisisitiza umuhimu wa wakulima kutambua fursa za uongezaji thamani ili kunufaika zaidi na shughuli za kilimo.

Mon, 12 Oct 2026 14:19:48 +0000
National · Issa Michuzi

RAIS DKT. SAMIA KUWA MGENI RASMI KILELE CHA MBIO ZA MWENGE KITAIFA RUKWA.

Jane Mwakyoma RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 mkoani Rukwa. Maadhimisho hayo yatafanyika Oktoba 14, 2026 katika Uwanja wa Nelson Mandela uliopo katika Mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais na maendeleo ya vijana Joel Nanauka akizungumza katika kikao na wanahabari kilichofanyika mjini Sumbawanga leo ambacho pia kilihudhuriwa na Waziri wa vijana,ajira na uwekezaji Zanzibar Ali Suleiman Ameir . Alifafanua kuwa maadhimisho ya kilele hicho yanaenda sambamba na kuzimwa rasmi kwa Mwenge wa Uhuru Kitaifa ambao uliwashwa Zanzibar Aprili 04 mwaka huu na Rais na Mwenyekiti wa Mapinduzi ya Nzanzibar Ali Hassan Mwinyi ambapo umekumbizwa katika Halmashauri 195 zilizopo katika mikoa 31 Bara na Visiwani. Aliongeza kuwa kuelekea maadhimisho hayo Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda kwa niaba ya Waziri Mwigulu Nchemba akifungua wiki ya Vijana Kitaifa Oktoba 10 mwaka huu ambayo ilianza rasmi Oktoba 08 katika Uwanja wa Ndua mjini hapa na itahitimishwa 0ktoba 14. Aidha maadhimisho ya kilele cha Mwenge wa Uhuru Kitaifa kitaendana na ibada takatifu ya kumbukizi ya miaka 27 ya kifo cha baba wa Taifa mwalimu Julias Kambarage Nyerere itakayo fanyikana katika kanisa Katoliki la mtakatifu Epifani saa 12:00 asubuhi mjini Sumbawanga. Aidha Nanauka amewaalika wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia maadhimisho hayo.

Mon, 12 Oct 2026 14:12:44 +0000
Uncategorized · DW Afrique

Les Houthis accentuent la pression sur l'Arabie Saoudite

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · BBC Afrique

5 technologies qui transforment les humains en demi-machines

Voler dans l'espace est depuis longtemps un rêve humain, du mythe grec d'Icare aux voitures volantes des films de science-fiction comme Blade Runner.

Recently
Uncategorized · Capital FM

DPP asks Supreme Court to uphold 20-Year jail term for Ex-Venezuelan Diplomat

Latest · News

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

TikToker Gitonga Archives remanded in extortion case

Gitonga has denied the allegations and previously pleaded not guilty

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

US Homeland Security chief defends plan to livestream execution

Homeland has defended a plan to livestream the execution of convicted killer Nidal Hasan

Recently
Uncategorized · Business Daily Africa

New Zealand, US tourists biggest daily spenders in Kenya

Read the full report from the original source.

Recently
National · Mwananchi

Polisi: Msisingizie Mungu ajali zinazotokana na uzembe

Jeshi la Polisi limewataka madereva kuacha kuhusisha ajali za barabarani na mapenzi ya Mungu, likisema nyingi husababishwa na makosa ya kibinadamu yanayoweza kuzuilika kwa kuzingatia sheria na...

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Kindiki issues tough warning to political violence sponsors ahead of 2027 polls

DP vows peaceful campaigns as 2027 race intensifies

Recently
Uncategorized · DW Afrique

L’empreinte chinoise gagne du terrain économique au Togo

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Le pouvoir burundais expose 13 présumés espions au profit du Rwanda et désigne les Banyamulenge à la vindicte

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Lecturers’ strike escalates as talks with govt collapse

EDUCATION · 4 hours ago

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

State rolls out e-birth notification system to end delays

CS Kipchumba Murkomen says the digital reform is part of wider efforts to streamline public services.

Recently
Uncategorized · Business Daily Africa

Inside a 500 species collector’s garden

Read the full report from the original source.

Recently
Sports · Mwanaspoti

Barker afichua alivyoigomea Simba kisa Maema

Soma zaidi hapa

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Rwanda and China strengthened aviation cooperation

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · PML Daily

Police impound 275 bags of charcoal in northern Uganda crackdown

AMURU — Police and other security agencies have impounded 275 bags of charcoal in Amuru and Pakwach districts and arrested two suspects as enforcement of a government ban on charcoal burning...

Recently
Uncategorized · KBC

King Mohammed VI of Morocco urges new MPS to prioritize action over titles

Read the full report from the original source.

Recently

Page 706 of 1150 · 22984 stories