Search the region
22509 stories
Alum tours Kaabong, Reviews Government Programmes
Read the full report from the original source.
RecentlyKabila Rebels Shoot Down DRC Fighter Jet
Read the full report from the original source.
RecentlyDAUDI YASSIN AMPONGEZA MCC ASAS KWA UJENZI WA OFISI ZA CCM ZA KATA MKOA WA IRINGA
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Daud Yassin, amempongeza Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas, kwa jitihada zake za kujenga ofisi za chama hicho katika kata mbalimbali za Mkoa wa Iringa. Yassin ametoa pongezi hizo Novemba 21, 2026, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kata za Makorongoni na Mlandege, ambako amekagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za CCM unaoendelea kutekelezwa kwa ufadhili wa Salim Asas. Amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa dhamira na ahadi ambayo Asas aliitoa mwaka 2022 alipoingia madarakani, akibainisha kuwa baadhi ya ofisi tayari zimekamilika huku ujenzi wa nyingine ukiendelea. “Nitumie nafasi hii kumpongeza MCC wetu, Ndugu Salim Asas Abri, kwa kazi nzuri ya ujenzi wa ofisi za CCM za kata. Alipanga na anatekeleza. Kila kata inajengwa ofisi na zipo ambazo ujenzi umekamilika. Tunamshukuru sana kwa moyo wake na upendo wake mkubwa kwa CCM,” amesema Yassin. Kutokana na mchango huo, Yassin amewataka wanachama wa CCM kuendelea kumuunga mkono Asas ili kumtia moyo na kuendeleza juhudi zake za kukijenga na kukiimarisha chama. Ziara hiyo ni sehemu ya shughuli za kawaida za Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Iringa, zinazolenga kuimarisha uhai wa chama, kufuatilia shughuli zake na kusimamia utekelezaji wa majukumu ya chama katika ngazi za chini.
Sun, 22 Nov 2026 11:28:33 +0000Simba Corporation launches MG in Kenya as It Targets a Lead Role In e-Mobility
Read the full report from the original source.
RecentlyChumi kuongoza Bodi ya Ushauri YIA
Read the full report from the original source.
RecentlyWAZIRI MKUU AIPONGEZA WHI KWA JUHUDI ZA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA MAKAZI NCHINI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameipongeza Watumishi Housing Investments (WHI) kwa juhudi zake za kuendeleza upatikanaji wa makazi bora na nafuu kwa Watanzania kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa katika mikoa tofauti nchini. Dkt. Mwigulu ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la WHI katika Ukumbi wa Super Dome, ambako yanafanyika Maonesho ya Jukwaa la Majadiliano ya Sekta ya Milki ya Makazi (Tanzania Real Estate Expo – TAREX 2026), jukwaa linalolenga kuwakutanisha wadau wa sekta ya milki na ujenzi pamoja na wananchi ili kujadili fursa na maendeleo ya sekta hiyo. Aidha, Waziri Mkuu ameihimiza taasisi hiyo kuendelea na juhudi hizo zenye mchango mkubwa katika kuboresha upatikanaji wa makazi nchini. “Nyie mnafanya kazi nzuri, tunaziona. Endeleeni,” alisema Dkt. Mwigulu. Dkt. Mwigulu amepata maelezo kuhusu shughuli na huduma mbalimbali zinazotolewa na WHI, ikiwemo utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika wilaya mbalimbali, huduma za kuuza na kupangisha nyumba kwa Watanzania, pamoja na usimamizi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja (Faida Fund). Akitoa maelezo kuhusu ushiriki wa WHI katika maonesho hayo, David Mwaipaja, Afisa Uhusiano kwa Umma wa Watumishi Housing Investments (WHI), amesema kuwa ushiriki wa taasisi hiyo katika TAREX 2026 ni sehemu ya juhudi za kutangaza huduma na fursa zake za uwekezaji, kuimarisha ushirikiano na wadau wa sekta ya milki, pamoja na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu fursa za kupata makazi bora na kuwekeza katika sekta ya Milki. Ameongeza kuwa kupitia jukwaa hilo, WHI inaendelea kutumia fursa ya kukutana moja kwa moja na wananchi na wadau mbalimbali kueleza huduma zake na mchango wa taasisi hiyo katika kukuza sekta ya Milki nchini.
Sun, 22 Nov 2026 11:25:08 +0000Voici comment annoncer cette nouvelle relation à ses enfants, selon deux expertes
Une situation qui peut être très enthousiasmante et source de bonheur peut se transformer en problème si nous ne gérons pas les choses avec prudence et tendresse.
RecentlyMbarara Regional Referral Hospital Gets Boost of Medical Sundries and Equipment Worth UGX 130m
Read the full report from the original source.
RecentlyMatiang’i rules out working with Gachagua
He said he is only willing to engage with leaders with whom he shared common ground and could work towards finding solutions to the country's challenges
RecentlyGachagua gives IEBC January deadline to address voter register audit
The former DP questioned IEBC's preparedness, saying the credibility of next year's election depended on addressing the concerns raised by political leaders
RecentlyMatiang’i rules out working with Gachagua as rift deepens
He said he is only willing to engage with leaders with whom he shared common ground and could work towards finding solutions to the country's challenges
RecentlyKWS deploys chopper, drones in search for missing Aberdare hiker
Read the full report from the original source.
RecentlyKiswahili kutumika CAF ni fursa nyingine ya ajira.
SPORTS AM | Mchambuzi wa soka, Philip Nkini anasema kiswahili kuidhinishwa kuwa moja ya lugha rasmi za Shirikisho la Kandanda Barani Afrika (CAF) baada ya kufanya mabadiliko madogo katika Katiba ya CAF ni hatua ambayo inaonesha kukua zaidi kwa lugha hiyo. Hatua hii inajiri baada ya Rais wa CAF Dkt. Patrice Motsepe kutangaza rasmi kuwa Kiswahili ni lugha rasmi ya CAF baada ya kupigiwa kura nyingi za kishindo na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 48 wa CAF uliofanyika Jijini Abuja, Nigeria. #SportsAM #PamojaAFCON2027 #Kiswahili
2026-11-22T10:36:14+00:00PM Nabbanja Orders Review of Telecom Loan Charges After Sanjay Tanna’s Probe
Read the full report from the original source.
RecentlySearch for missing Aberdare hiker David Kihuna enters day 9, no breakthrough
Read the full report from the original source.
RecentlyMabalozi wa Umoja wa Ulaya Kutembelea Tanga Kuimarisha Ushirikiano katika Ukuaji wa Uchumi Unaozingatia Utunzaji wa Mazingira na Uchumi wa Buluu
Ujumbe wa Mabalozi na Naibu Mabalozi 11 wanaowakilisha Umoja wa Ulaya (EU) na nchi wanachama wake nchini Tanzania utafanya ziara ya siku tatu mkoani Tanga kuanzia tarehe 23 hadi 25 Novemba 2026. Ziara hiyo italenga kuangalia fursa zilizopo mkoani humo za kukuza uchumi kwa njia endelevu, pamoja na namna ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na Tanzania unavyoweza kusaidia kufungua fursa mpya kwa wananchi na wafanyabiashara. Ushirikiano huo unajumuisha pia mpango wa Umoja wa Ulaya wa Global Gateway. Katika ziara hiyo, Mabalozi watakutana na viongozi wa serikali, wananchi wanaonufaika na miradi mbalimbali, wajasiriamali na wawakilishi wa sekta binafsi. Mikutano hiyo itawapa nafasi ya kujionea shughuli na miradi inayoendelea, kusikiliza uzoefu wa wananchi na kuelewa vipaumbele vya maendeleo vya Mkoa wa Tanga. Ujumbe huo unajumuisha wawakilishi kutoka Umoja wa Ulaya, Ubelgiji, Denmark, Finland, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Slovakia, Hispania na Sweden. Ziara hii ni sehemu ya utaratibu wa kila mwaka wa Mabalozi wa Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wake kutembelea kwa pamoja mikoa mbalimbali ya Tanzania. Mwaka jana, Mabalozi hao walitembelea Mkoa wa Kilimanjaro. Mabalozi Watakaoshiriki Katika Ziara: Umoja wa Ulaya: Jean-Marc Pisani – Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania (Kiongozi wa Ujumbe) Ubelgiji: Lot Debruyne – Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania Denmark: Jesper Kammersgaard – Balozi wa Denmark nchini Tanzania Finland: Anna Merrifield – Balozi wa Finland nchini Tanzania Ujerumani: Maximilian Mueller – Naibu Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Ireland: Nicola Brennan – Balozi wa Ireland nchini Tanzania Italia: Giuseppe Coppola – Balozi wa Italia nchini Tanzania Uholanzi: Marjo Crompvoets – Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Slovakia: Lancaric Ivan – Balozi wa Slovakia nchini Tanzania Hispania: Paloma Serra – Balozi wa Hispania nchini Tanzania Sweden: Sandra Diesel – Naibu Balozi wa Sweden nchini Tanzania
Sun, 22 Nov 2026 10:37:34 +0000RAIS SAMIA AELEKEA ETHIOPIA KUZINDUA MPANGO WA AFYA YA MAMA NA MTOTO
Sun, 22 Nov 2026 10:32:50 +0000Opposition leaders dismiss ‘Third Force’ claims
Karua dismissed claims of divisions, saying the Opposition's different engagements across the country were a coordinated effort to mobilise support.
RecentlySerikali kuhakikisha huduma ya maji Chalinze kwa asilimia 100
Read the full report from the original source.
RecentlyDk Mwigulu : Migogoro ya ardhi isichochee visasi
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 72 of 1126 · 22509 stories