Search the region
22951 stories
Why your knees may hurt more at night
Wear and tear can cause discomfort after a long day
RecentlyKabogo wants chiefs who fail to fight illicit brews sacked
Read the full report from the original source.
RecentlyBANDARI YA TANGA YAVUKA LENGO LA SHEHENA, YAPUNGUZA MUDA WA MELI KUSUBIRI
Na Oscar Assenga, Tanga BANDARI ya Tanga imevuka lengo la kuhudumia shehena kwa mwaka wa fedha 2025/2026 baada ya kuhudumia tani milioni 2.179 dhidi ya lengo la tani milioni 1.65, ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na tani milioni 1.3 zilizohudumiwa mwaka wa fedha 2024/2025. Aidha, bandari hiyo imepunguza muda wa meli kusubiri huduma kutoka wastani wa siku 10 hadi 20 katika mwaka uliopita wa fedha hadi kati ya siku sifuri na tano katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka mpya wa fedha. Meneja wa Bandari ya Tanga, Salehe Mbega, alisema hayo alipokuwa akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja, akieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na maboresho yaliyofanyika katika utoaji wa huduma. Alisema maboresho hayo hayajalenga kuongeza idadi ya meli pekee, bali pia yameongeza uwezo wa bandari kushughulikia shehena kwa ufanisi. Kwa mujibu wa Mbega, mojawapo ya changamoto kubwa iliyokuwa ikiikabili bandari hiyo ni meli kukaa nje ya bandari kwa muda mrefu zikisubiri kuingia gati, hali iliyosababisha malalamiko ya wateja kuhusu kuchelewa kwa mizigo yao. “Katika mwaka uliopita nilikuwa napokea simu nyingi sana za wateja wakilalamika kwamba meli zimekaa muda mrefu zikisubiri kuingia nangani au magari yao yamefika lakini mizigo haijapakiwa. Kwa miezi hii mitatu tangu kuanza mwaka huu wa fedha, simu hizo zimepungua sana,” alisema. Alisema uongozi wa bandari ulifanya tathmini kubaini maeneo yaliyokuwa yakisababisha ucheleweshaji na kuyafanyia maboresho, hatua ambayo imeanza kuleta matokeo chanya katika utoaji wa huduma. Mbega alibainisha kuwa katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2026, zaidi ya asilimia 70 ya meli zilizohudumiwa katika bandari hiyo zilianza kupata huduma bila kusubiri, huku muda wa kusubiri kwa ujumla ukipungua hadi kati ya siku sifuri na tano. Aliongeza kuwa maboresho hayo yameambatana na kupungua kwa muda ambao meli hutumia zikiwa gati, ambapo nyingi sasa huhudumiwa ndani ya siku tatu hadi tano, na katika baadhi ya mazingira muda huo unaweza kufikia siku saba. Kwa upande wa meli za mafuta, alisema muda wa kusubiri nao umepungua, huku baadhi ya meli zikiingia katika eneo la kuhudumiwa ndani ya chini ya siku mbili kabla ya kukamilisha shughuli zake na kuondoka. Akizungumzia utendaji wa bandari hiyo, Mbega alisema katika mwaka wa fedha 2025/2026 ilihudumia meli 166 dhidi ya lengo la meli 163, ikilinganishwa na meli 150 zilizohudumiwa mwaka wa fedha 2024/2025. Alisema mafanikio hayo yanatoa matumaini ya kufanya vizuri zaidi katika mwaka wa fedha unaoendelea, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kampuni za meli, mawakala wa forodha, wateja na taasisi nyingine zinazohusika na shughuli za bandari. “Tumeshanza kwenda extra mile kwa vitendo. Ufanisi huu hauji kwa sababu ya TPA pekee, bali ni matokeo ya ushirikiano wa wadau wote. Tunaamini tukiendelea kushirikiana, tutafanya vizuri zaidi kuliko mwaka uliopita,” alisema. Hata hivyo, Mbega alisema bado kuna meli zinazolazimika kusubiri nje ya bandari kabla ya kuingia, lakini muda wa kusubiri umepungua ikilinganishwa na ilivyokuwa awali. Alizitaka kampuni na wadau wengine kuendelea kutumia huduma za Bandari ya Tanga na kutoa mrejesho wanapokutana na changamoto, akieleza kuwa TPA itaendelea kuboresha huduma ili kuhakikisha meli na shehena zinahudumiwa kwa wakati. Naye Meneja wa Seafront Shipping katika Bandari ya Tanga, Amri Sufiani Kagembe, alisema kampuni hiyo imeshuhudia maboresho ya huduma za bandari, akibainisha kuwa kupungua kwa changamoto zilizokuwapo awali kumeongeza ufanisi katika kuhudumia meli na wateja. Alisema Seafront imeendelea kuhudumia idadi kubwa ya meli katika bandari hiyo, jambo alilolitaja kuwa ishara ya imani waliyonayo katika huduma zinazotolewa. “Tunathamini sana ‘extra mile’ inayofanywa katika Bandari ya Tanga kwa vitendo. Tunaamini huduma bora kwa mteja si kwa sababu tu ni wajibu wetu, bali kwa sababu mteja anastahili huduma bora zaidi. Hapa Tanga, tunaona hilo likitekelezwa kwa vitendo,” alisema Kagembe. Kwa upande wake, Meneja wa CHICASA ICDV, Sofia Mfinanga, alisema wanajivunia huduma wanazopata katika Bandari ya Tanga, akieleza kuwa maboresho hayo yamechangia kuongezeka kwa wateja wanaotumia huduma za kituo hicho cha kuhifadhi na kushughulikia makontena pamoja na shughuli za biashara kwa ujumla. “Tunajivunia sana huduma tunazozipata hapa Tanga chini ya uongozi wa Meneja wa Bandari, Salehe, na timu yake. Pia tunajivunia jinsi tunavyopata wateja na kuona ongezeko la shughuli. Tunawakaribisha wadau kutumia huduma za Bandari ya Tanga kwa sababu huduma zake ziko vizuri,” alisema Mfinanga.
Sun, 11 Oct 2026 13:04:48 +0000TCB KUONGEZA KIWANGO CHA UNYWAJI WA KAHAWA.
BODI ya Kahawa Tanzania (TCB) imelenga kuongeza kiwango cha unywaji wa kahawa nchini kutoka asilimia saba ya sasa hadi asilimia 15, ili kupanua soko la ndani na kuongeza matumizi ya kahawa inayozalishwa na wakulima wa Tanzania. Mkurugenzi Mkuu wa TCB, Primus Kimaryo, alisema hayo wakati wa Tamasha la Saba la Kahawa lililofanyika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, akibainisha kuwa tangu tamasha hilo lilipoanzishwa mwaka 2019, kiwango cha unywaji wa kahawa nchini kimeongezeka kutoka chini ya asilimia tatu hadi kufikia asilimia saba. Kimaryo alisema lengo la bodi hiyo ni kuendelea kuhamasisha Watanzania kunywa kahawa inayozalishwa nchini, hatua itakayosaidia kukuza soko la ndani na kuongeza fursa za kibiashara kwa wakulima na wadau wengine katika mnyororo wa thamani wa zao hilo. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava, aliwataka wadau wa kahawa kuongeza juhudi za kuhamasisha matumizi ya kahawa ya Tanzania, huku akisisitiza kuwa maafisa ugani wanapaswa kuacha kukaa maofisini na badala yake kwenda mashambani kuwaongoza wakulima kutumia kanuni bora za kilimo na miche bora iliyofanyiwa utafiti na Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI). Alisema matumizi ya miche bora inayovumilia ukame na kustahimili magonjwa, pamoja na kufuata kanuni bora za kilimo, yataongeza uzalishaji na tija, huku akiwataka wadau kuongeza thamani ya kahawa kupitia usindikaji, ufungashaji na utengenezaji wa bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi. Mnzava pia aliitaka TCB kuendelea kuwashirikisha vijana na wanawake katika uzalishaji na shughuli za kuongeza thamani ya kahawa, akisisitiza umuhimu wa kujenga soko la uhakika litakalowanufaisha wakulima na wadau wengine. Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCB, Profesa Aurelia Kamuzora, alisema matumizi ya mifumo ya kidijitali, ikiwemo miamala kupitia simu za mkononi na mifumo ya ufuatiliaji wa uzalishaji na biashara ya kahawa, yamechangia kuongeza imani ya wakulima, wakiwemo vijana, katika shughuli za uzalishaji. Alisema TCB inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutangaza chapa ya kahawa ya Tanzania ili kuongeza ushindani wake katika masoko ya kimataifa. Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Denis Mahulu, alisema maonyesho ya mwaka huu yalishirikisha washiriki zaidi ya 40, hali inayoonesha kuendelea kukua kwa tamasha hilo na ushiriki wa wadau wa kahawa.
Sun, 11 Oct 2026 13:09:29 +0000Mosiria declares Nairobi gubernatorial bid
Mosoria cited his experience working in different departments within the county
RecentlyThree dead, more than 40 rescued as vessel catches fire on Lake Nyasa
Read the full report from the original source.
RecentlyMangungu afichua siri ya kuifunga Yanga
Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, ametaja siri ya ushindi wao wa jana, Jumamosi, Oktoba 10, 2026, dhidi ya Yanga kuwa ni kudhibiti kile alichokiita ‘mauzauza’ ya wapinzani wao.
RecentlyL'attaque de l'aéroport de Riyad, un autre moment dangereux dans un conflit déjà tendu
Les Houthis ont intensifié leurs attaques sur le sol saoudien, et bien que les dégâts matériels puissent être rapidement réparés, la réputation de stabilité du pays est fortement mise à mal.
RecentlyCoop Bank yaunga mkono Kongamano la SACCA 2026
Read the full report from the original source.
RecentlyTumaini jipya ujenzi shule ya kimataifa Zanzibar ukianza
Read the full report from the original source.
RecentlyUmunya-Tanzania Jihan Mohin Dimachk yegukanye ikamba rya Miss Grand International
Read the full report from the original source.
RecentlyPope Leo to undergo lung surgery
The 71-year-old pontiff said his medical team "believe it would be right to intervene"
RecentlyTwo arrested over woman’s murder, link suspect to two other killings
MASAKA — Police in Masaka have arrested two suspects over the murder of Natukunda Jackline, a resident of Lukaya, with investigators linking the prime suspect to two other killings reported in...
RecentlyPapa Leo XIV agiye kubagwa ikibyimba kiri ku bihaha
Read the full report from the original source.
RecentlySakaja: Most El Niño hotspots in Nairobi cleared
The governor attributed the progress to joint efforts by county departments and national government
RecentlyMamelodi Sundowns yaichapa Orlando Pirates yatwaa taji
Read the full report from the original source.
RecentlyYanga wameutafuta mpira kwa tochi, mpaka sasa hawajauona
Soma zaidi hapa
RecentlyStanbic Bank Employees Donate ICT Equipment to Strengthen Modern Policing in West Nile district
YUMBE, Uganda — Stanbic Bank Uganda has donated Information and Communication Technology (ICT) equipment worth UGX 30 million to Ikafe Police Training School in Yumbe District, strengthening the school’s capacity…
RecentlyMasaka Murder Probe: Two Arrested Over Alleged Shs2m Human Body Parts Deal
Police in Masaka East have arrested two suspects in connection with the murder of Natukunda Jackline, a resident of Lukaya, as investigations into the killing and two other suspected murder…
RecentlyCHIMP SPORT: Kitara edge Kataka for Maiden Away Win
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 729 of 1148 · 22951 stories