Unganishwa

Search the region

22901 stories

Uncategorized · Kigali Today

RDC iri mu kaga, kuyirokora ni inshingano yihutirwa - Joseph Kabila

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Standard

Cabinet approves tougher penalties for quack surveyors, architects

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

MAKADA CCM RUVUMA WANOLEWA KUHUSU ITIKADI YA CHAMA

Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma wameanza kushiriki semina maalumu ya itikadi ya Chama hicho, inayolenga kuwaongezea uelewa kuhusu misingi, maadili na masuala mbalimbali yanayohusu Chama. Mafunzo hayo yameanza leo, Oktoba 9, 2026, na yanatarajiwa kuendelea hadi Oktoba 25, mwaka huu, yakihusisha makada kutoka wilaya mbalimbali za mkoa huo, ikiwa ni sehemu ya mafunzo yanayoendelea kutolewa kwa wanachama wa CCM nchini kote. Akizungumza kwa niaba ya wanachama wanaoshiriki mafunzo hayo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Kiliani Mwisho, amesema wamepokea mafunzo hayo kwa furaha, akieleza kuwa baadhi ya wanachama wamekuwa wakikosa fursa za kupata mafunzo ya aina hiyo kwa muda mrefu. Mwisho, ambaye ameshiriki mafunzo hayo kama mwanafunzi katika darasa lililopo Kata ya Mjimwema, Wilaya ya Songea Mjini, ameipongeza CCM kwa kuandaa mafunzo hayo yanayolenga kuwajengea wanachama uelewa kuhusu itikadi na masuala ya Chama. Pia, amempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha mafunzo hayo kufanyika nchi nzima, huku akimpongeza Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM, Kenani Laban Kihongosi, kwa uratibu wa mafunzo na maandalizi ya walimu wanaoyatoa kwa wanachama. Kwa upande wake, Mratibu wa mafunzo hayo Mkoa wa Ruvuma, Edna Lameck, ambaye ni afisa wa Idara ya Itikadi na Uenezi kutoka Makao Makuu ya CCM, ametembelea madarasa mbalimbali yanayoendesha mafunzo hayo mkoani humo ili kujionea namna yanavyotolewa. Lameck amesema ameridhishwa na hali ya utoaji wa mafunzo hayo kwa makada wanaoshiriki katika madarasa hayo mkoani Ruvuma. Mafunzo hayo yanatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 25, 2026, yakiwa na lengo la kuendelea kuwajengea uwezo viongozi, makada na wanachama katika kufahamu itikadi, siasa na misingi ya Chama Cha Mapinduzi.

Fri, 09 Oct 2026 17:41:54 +0000
Sports · Azam TV Videos

Mbeya City 1-3 Kagera Sugar | Highlights | NBC Premier League 09/10/2026

#NBCPL MAGOLI YOTE: Tazama Kagera Sugar walichowafanya Mbeya City wakianza kwa header ya Emmanuel Mvuyekure, kabla ya Mudathir Said Abdullah kupiga mawili makali… La kufutia machozi nalo lilikuwa la moto kutoka kwenye guu la Hassan Ali Cheda. FT: Mbeya City 1-3 Kagera Sugar #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi #MbeyaCity #KageraSugar #MbeyaCityKageraCity

2026-10-09T17:19:56+00:00
Uncategorized · Citizen Digital

Nairobi court denies man accused of threatening magistrate bail

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

US report links Gov’t officials to recruitment of Kenyans into Russian-Ukraine war

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Ankole Times

UHRC Chairperson Wangadya Takes Human Rights Campaign Directly to Ugandans at UMA Exhibition

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Afrique

Pays pétrolier en manque de carburant, le paradoxe gabonais

Read the full report from the original source.

Recently
Health · Issa Michuzi

MADAKTARI BINGWA WA BMH WAHITIMISHA KAMBI YA MATIBABU NCHINI MALAWI, 64 WAFANYIWA UPASUAJI, 49 WAPEWA RUFAA BMH

Akifunga kambi hiyo Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Malawi, Bw. Bestone Chisamile. amesema Hospitali ya Benjamin Mkapa inatekeleza kwa vitendo ushirikiano wa matibabu ya kibingwa "Ushirikiano wa Afya kati ya Malawi na Tanzania unatekelezwa kupitia kambi ya matibabu ya kibingwa nchini Malawi. Hata hivyo tumeanza Majadiliano, yataangazia manufaa ya kambi hiyo kwa wagonjwa pamoja na umuhimu wa kurasimisha ushirikiano mpana zaidi unaojumuisha huduma za matibabu, mafunzo ya wataalamu, masuala ya dawa na rufaa za wagonjwa." amesema Bw. Chisamile Timu ya wataalamu kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa nchini Tanzania imefanya upasuaji kwa wagonjwa 64 haya yote yamewezekana chini ya ushirikiano uliopo kati ya Serikali za nchi hizi mbili. "Madaktari na wataalamu kutoka Tanzania walileta ujuzi na uzoefu katika fani mbalimbali za matibabu na kubadilishana maarifa na wenzao wa Malawi, pale Mzuzu katika hospitali ya Mzuzu na hapa Lilongwe katika Hospitali Kamuzu" Bw. Chisamile Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mhe. Agnes Kayola amesema hii imekuwa ni fursa kubwa kwa wanchi wa malawi na madaktari "Kambi hii imewanufaisha wagonjwa zaidi ya 810,katika hao 64 wamefanyiwa upasuaji 49 wamepewa rufaa ya kwennda Hospitali ya Benjamin Mkapa faida nyingine ya kambi hii imewezesha pia kujifunza na kubadilishana uzoefu wa kitaaluma kati ya wataalamu wa afya wa nchi hizi mbili." Amesema Balozi Kayola Kambi hii ilianza tarehe 28/09/2026 na imehitimishwa leo ikiwa ni ushirikiano wa BMH,SOTAC na MSD, kambi hii inamagari ya kisasa yenye chumba chaupasuaji inayowezesha kutoa matibabu katika mazingira yoyote.

Fri, 09 Oct 2026 17:15:35 +0000
Uncategorized · BBC Afrique

Christa Pike pourrait-elle être exécutée à nouveau, et selon quelle méthode ?

La meurtrière Christa Pike a survécu à l'injection létale, ce qui soulève des questions quant à la possibilité que le Tennessee tente à nouveau sa chance.

Recently
Uncategorized · BBC Afrique

Partout dans le monde, des trésors culturels sont détruits. Pourquoi personne n'est-il sanctionné ?

Partout dans le monde, les conflits bouillonnent, et des monuments culturels sont détruits. Ces personnes luttent contre cela.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

China, EU reach deal to 'moderate' China's car exports to EU

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Issa Michuzi

HESLB YATAKA MIFUMO IMARA KUDHIBITI UDANGANYIFU WA MIKOPO

Na Janeth Raphael - MichuziTv Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetaka kuimarishwa na kuunganishwa kwa mifumo ya taarifa za taasisi mbalimbali ili kudhibiti matumizi ya taarifa za kughushi, kupunguza makosa na kuhakikisha mikopo inatolewa kwa wanafunzi wanaostahili kwa wakati. Wito huo umetolewa leo, Oktoba 9, 2026, jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia, wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, HESLB pamoja na Wathibiti Ubora wa Elimu kutoka mikoa yote 26 ya Tanzania Bara. Dkt. Kiwia amesema upatikanaji wa taarifa sahihi na zinazoweza kuhakikiwa ni msingi muhimu katika kuboresha mchakato wa utoaji mikopo, ikiwemo kupanga bajeti na kuhakikisha fedha zinagawiwa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wanafunzi. Ameeleza kuwa taarifa kuhusu matokeo ya mitihani, hali ya uyatima, ulemavu na mahitaji maalumu ya wanafunzi zina nafasi muhimu katika kutambua waombaji wanaostahili kupata mikopo na msaada wa kifedha. Aidha, amesema kuunganisha mifumo ya taarifa za taasisi husika kutarahisisha ukusanyaji na uhakiki wa taarifa, kupunguza usumbufu kwa waombaji na kusaidia wanafunzi kupata mikopo au fedha zao kwa wakati wanaporipoti katika vyuo wanavyopangiwa. Katika hatua nyingine, Dkt. Kiwia amesema Serikali imetenga Shilingi Bilioni 787.4 kwa ajili ya mikopo na msaada kwa wanafunzi katika mwaka huu, huku zaidi ya wanafunzi 292,400 wakitarajiwa kunufaika. Amesema wanufaika hao wanajumuisha wanafunzi wapya zaidi ya 81,300, wanafunzi 160,738 wanaoendelea na masomo pamoja na zaidi ya wanafunzi 11,000 wa ngazi ya stashahada. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ephraim Simbeye, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi zinazohusika katika kuhakikisha taarifa za wanafunzi zinakusanywa na kuhakikiwa kwa usahihi. Amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha mikopo inawafikia wanafunzi wanaokidhi vigezo, huku ukisaidia kuimarisha ufanisi na uwazi katika mchakato wa utoaji mikopo ya elimu ya juu.

Fri, 09 Oct 2026 17:11:10 +0000
Uncategorized · The Standard

Kalonzo to Ruto: You have no numbers

The united opposition will deal President William Ruto a humiliating defeat in next years general election, Wiper Party leader Kalonzo Musyoka has predicted.

Fri, 09 Oct 2026 20:04:21 +0300
Uncategorized · KBC

Ghana approves formal application to join BRICS

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · UN News Burundi

Afghanistan: Women face fresh dress code arrests amid record refugee returns

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · BBC Afrique

Des voleurs ont dérobé 30 000 bouteilles de vin d'une valeur de 5 millions d'euros en Italie, selon les médias locaux

Le vol commis dans ce domaine viticole florentin est considéré comme l'un des plus importants de ce type en Italie.

Recently
Business · Issa Michuzi

CMSA YAFIKISHA ELIMU YA UWEKEZAJI KWA WATU WENYE ULEMAVU

Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imesisitiza umuhimu wa kuhakikisha elimu ya uwekezaji inawafikia wananchi wote bila kujali hali zao za kimwili au uwezo wa kiuchumi, ili kuongeza ushiriki wa wananchi katika masoko ya mitaji nchini. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha kwa watu wenye ulemavu, Mkuu wa Uhusiano wa Umma wa CMSA, Charles Shirima, amesema kuwa kuwawezesha wananchi kupata maarifa ya kifedha ni hatua muhimu katika kuongeza akiba za ndani na kukuza uchumi jumuishi. "kampeni hii ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Wawekezaji Duniani (World Investor Week), mpango wa kimataifa unaoratibiwa na Shirika la Kimataifa la Tume za Dhamana (IOSCO) kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu uwekezaji salama na wenye taarifa sahihi",amesema Shirima Amesema kuhamasisha wananchi wengi zaidi kushiriki katika uwekezaji ni muhimu katika kujenga utajiri binafsi na kuimarisha uchumi wa taifa. Shirima amesema kuwa CMSA imeshirikiana na Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kutoa mafunzo yatakayowawezesha washiriki kuelewa fursa mbalimbali za uwekezaji na namna ya kuzitumia kuboresha maisha yao. "Mafunzo hayo yamejikita katika namna masoko ya mitaji yanavyofanya kazi, utaratibu wa kununua hisa pamoja na mbinu bora za kusimamia fedha binafsi",amesema Shirima Aidha, Shirima amesema CMSA hutumia njia mbalimbali kufikisha elimu hiyo kwa wananchi, zikiwemo warsha za ana kwa ana, semina za mtandaoni na mitandao ya kijamii, huku makundi yanayolengwa yakijumuisha wanafunzi, walimu, viongozi wa maeneo na wananchi kwa ujumla. Amesema lengo ni kujenga mazingira jumuishi ya uwekezaji kwa kuhakikisha wananchi wa makundi mbalimbali wanapata maarifa na fursa za kushiriki katika masoko ya mitaji. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa SHIVYAWATA, Jonas Mbago, amesema mafunzo hayo yamesaidia kurahisisha dhana za kifedha ambazo awali zilionekana kuwa ngumu kueleweka, huku yakiwafahamisha washiriki njia mbadala za kusimamia na kukuza akiba zao. Mbago amesema watu wengi katika jamii wamekuwa na mazoea ya kuhifadhi fedha majumbani au kwenye akaunti za benki zenye riba ndogo, hali inayoweza kupunguza fursa za kukuza fedha zao. “Mafunzo haya yametutambulisha katika njia mpya za uwekezaji zinazoweza kuboresha usalama wetu wa kifedha,” amesema, huku akiiomba Serikali kupanua programu kama hizo ili kuwafikia wananchi wengi zaidi nchini. Naye Mwenyekiti wa chama kinachowakilisha watu wenye 'Psoriasis', ugonjwa sugu wa ngozi unaosababisha kutokea kwa mabaka mazito yenye magamba, Dorothy Malechela, amesema wananchi wanapaswa kuachana na tabia ya kuhifadhi fedha bila kuzizalisha na badala yake kujifunza fursa za uwekezaji zinazodhibitiwa kisheria. Amesema mipango sahihi ya kifedha inaweza kuwasaidia watu kukuza biashara zao, kuimarisha usalama wa kifedha na kufikia malengo yao ya muda mrefu.

Fri, 09 Oct 2026 17:02:14 +0000
Uncategorized · Mwananchi

Jeni azikwa, Askofu Shoo atoa ujumbe kwa wanandoa

Soma zaidi...

Recently
Uncategorized · SoftPower News

Museveni Sets June 2027 Target for Uganda’s Economy to Reach $74 Billion

Read the full report from the original source.

Recently

Page 754 of 1146 · 22901 stories