Search the region
22861 stories
UFAFANUZI KUHUSU UPATIKANAJI WA TIKETI ZA TRENI ZA SGR
Thu, 08 Oct 2026 15:02:04 +0000PMNCH’s Vice Chair calls on IPU to ensure adequate funding for healthcare services
ARUSHA: THE Vice Chair of the Partnership for Maternal, Newborn & Child Health (PMNCH), Dr Flavia Bustreo, has called on…
RecentlyMagoli | Mashujaa FC 2-1 Polisi Tanzania | NBC Premier League 08/10/2026
Mashujaa FC imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania, mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Lake Tanganyika Stadium, Kigoma. Mashujaa wametangulia kwa goli la Mishamo Daud, kabla ya Anuary Jabir kuchomoa kwa penati lakini Mashujaa nao wakapiga la ushindi kwa penati kupitia kwa Michael Joseph.
2026-10-08T14:51:56+00:00‘No plague case’ in Siberia, Russia tells WHO as assessments continue
Read the full report from the original source.
RecentlyRwanda Finance Minister received his Austrian counterpart Andreas Reichhardt
Read the full report from the original source.
RecentlyNyansaho, Chume sign pacts to cement Tanzania–Mozambique ties in defence and security
DAR ES SALAAM: THE Ministers of Defence of the United Republic of Tanzania and the Republic of Mozambique, Dr Rhimo…
RecentlyTANZANIA KUWA MWENYEJI WA KONGAMANO LA SACCOS AFRIKA, WASHIRIKI ZAIDI YA 1,000 KUTOKA NCHI 40 KUSHIRIKI
Na Janeth Raphael - MichuziTv Tanzania inatarajiwa kuwa kitovu cha mijadala kuhusu maendeleo ya vyama vya ushirika wa akiba na mikopo barani Afrika kupitia Kongamano la 26 la Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Afrika (SACCA Congress 2026), litakalofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 11 hadi 16, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC). Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo ,Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, amesema kongamano hilo linatarajiwa kuwakutanisha zaidi ya washiriki 1,000 kutoka nchi zaidi ya 40 za Afrika na maeneo mengine duniani, likilenga kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu katika sekta ya ushirika wa kifedha. Amesema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kongamano hilo lenye kaulimbiu isemayo “Building Trust, Driving Transformation: The Future of Financial Cooperatives in Africa”, inayosisitiza kujenga uaminifu na kuleta mabadiliko katika mustakabali wa vyama vya ushirika wa kifedha barani Afrika. Kwa mujibu wa Chongolo, kongamano hilo litaiwezesha Tanzania kujifunza mbinu bora za uendeshaji wa SACCOS, kuimarisha uwezo wa taasisi hizo na kufungua fursa mpya za uwekezaji. Ameeleza kuwa huduma za kifedha kupitia SACCOS zina nafasi muhimu katika kuwawezesha wakulima, vijana, wanawake na wafanyabiashara wadogo kupata huduma zinazoweza kuchochea shughuli zao za kiuchumi. Aidha, amesema Tanzania itanufaika na fursa za kutangaza utalii, utamaduni na mazingira ya uwekezaji kwa wageni watakaohudhuria kongamano hilo, hatua inayoweza kuongeza mwamko wa washiriki kuhusu vivutio na fursa zilizopo nchini. Kwa upande wake, Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dkt. Benson Ndiege, amesema maandalizi ya kongamano hilo yanaipa Tanzania nafasi ya kuimarisha uhusiano na wadau wa kimataifa, kuvutia uwekezaji na kujifunza uzoefu wa nchi nyingine katika kuendeleza vyama vya ushirika. Dkt. Ndiege amesema zaidi ya washiriki 600 wanatarajiwa kutoka nje ya Tanzania, jambo litakaloongeza fursa za kibiashara na kutoa mchango kwa sekta ya utalii kupitia matumizi ya huduma za hoteli, usafiri na biashara nyingine wakati wa kongamano hilo. Ameongeza kuwa wageni hao watapata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii, vikiwemo vilivyopo Dar es Salaam, Morogoro, Ngorongoro na Zanzibar, hali inayotarajiwa kuchochea shughuli za kiuchumi na kuitangaza Tanzania kimataifa. Amesema kongamano hilo pia litatoa fursa ya kujengeana uwezo kwa vyama vya ushirika nchini kupitia mijadala na mafunzo kuhusu utawala bora, usimamizi wa vyama na mikakati ya kuimarisha maendeleo ya SACCOS. Vilevile, Tanzania itapata jukwaa la kuonesha mafanikio iliyoyapata katika sekta ya ushirika na kujifunza maeneo yanayohitaji maboresho. Kwa mujibu wa Dkt. Ndiege, Tanzania kupewa nafasi ya kuandaa kongamano hilo ni ishara ya kutambulika kwa maendeleo ya sekta ya ushirika nchini na nafasi yake katika majukwaa ya kimataifa. Waziri Chongolo ametoa wito kwa wadau wa vyama vya ushirika, washiriki kutoka Afrika na sehemu nyingine duniani kushiriki kongamano hilo, akieleza kuwa litakuwa jukwaa muhimu la kujenga mitandao ya ushirikiano, kukuza uwekezaji, kutangaza utalii na kuimarisha mchango wa SACCOS katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Thu, 08 Oct 2026 14:55:37 +0000BINTI WA KITANZANIA AWEKA HISTORIA, ATOA MADA KUHUSU AFYA YA AKILI MKUTANO WA IPU
Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Arusha BINTI mdogo wa Kitanzania, Elizabeth Milaho(22), ameweka historia baada ya kupata nafasi ya kuwasilisha mada kuhusu afya ya akili mbele ya wajumbe wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), akitoa wito kwa Serikali na watunga sera kuwashirikisha vijana katika utengenezaji wa sera na sheria zinazolenga kukabiliana na changamoto za afya ya akili. Elizabeth, ambaye ni mratibu wa programu katika taasisi ya Akili Tulivu yenye makao yake makuu Jijini Dar es salaam, amesema ushiriki wa vijana katika mchakato wa utungaji wa sera ni muhimu kwa kuwa wao ni miongoni mwa makundi yanayoathirika kwa kiasi kikubwa na changamoto mbalimbali za afya ya akili. Akizungumza na wajumbe wa mkutano huo, Elizabeth amesema afya ya akili si suala linalowaathiri vijana pekee, bali linaweza kuathiri familia, uchumi na jamii kwa ujumla, hivyo linahitaji kushughulikiwa kuanzia ngazi ya chini hadi kitaifa. Elizabeth amesema kutokana na hali hiyo, Serikali inapaswa kuweka mazingira yatakayowawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika majadiliano na utengenezaji wa sera zinazohusu afya ya akili. “Tunatengeneza sera ambazo zitawasaidia vijana, lakini vijana nao wanapaswa kuwa miongoni mwa washiriki wa suala zima la utengenezaji wa sheria zetu,” amesema. Amesema vijana wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo shinikizo la kiuchumi, matatizo ya kifamilia na mazingira wanayoishi, mambo ambayo yanaweza kuwa na athari katika afya yao ya akili. Ameongeza kuwa maendeleo ya teknolojia za kidijitali yameleta changamoto nyingine, kwa kuwa vijana ni miongoni mwa watumiaji wakubwa wa teknolojia hizo na hukutana na mazingira mbalimbali yanayoweza kuathiri ustawi wao wa kisaikolojia. Elizabeth amesema taasisi ya Akili Tulivu ilianzishwa Tanzania kwa lengo la kuwasaidia vijana kukabiliana na changamoto za afya ya akili, huku mpango huo ukiendelea kupanuka na kufikia maeneo mbalimbali duniani. “Akili Tulivu inatoa jukwaa salama na lenye faragha linalowawezesha vijana kueleza changamoto wanazopitia na kutafuta msaada unaohitajika kwa kutumia Kiswahili au Kiingereza,” amesema Amesema fursa ya kuwasilisha mada hiyo katika Mkutano wa IPU imemuwezesha kufikisha ujumbe wa vijana mbele ya viongozi na wawakilishi wa mabunge kutoka mataifa mbalimbali duniani. Kwa mujibu wa Elizabeth, viongozi hao wana nafasi muhimu katika kutengeneza sera na sheria, hivyo ni muhimu wao kuelewa changamoto halisi zinazowakabili vijana katika masuala ya afya ya akili. Amesema ujumbe uliowasilishwa kupitia Akili Tulivu umepokelewa vyema, huku akieleza matumaini kwamba hatua zaidi zitachukuliwa kuweka mazingira bora ya kushughulikia changamoto za afya ya akili kabla hazijawa kubwa na kusababisha madhara zaidi katika jamii. Elizabeth amesema sababu kubwa ya kuanza na vijana ni kwamba kundi hilo ndilo linalotarajiwa kuwa viongozi, watunga sera na waamuzi wa masuala mbalimbali ya nchi katika siku zijazo. “Tunategemea vijana hawa baadaye kuwa viongozi, kutengeneza sera na kuwa watu watakaokuwa wanaongoza nchi yetu. Kwa hiyo tunahitaji kuanza kuwasaidia mapema,” amesema. Amewataka vijana kutokuwa na hofu ya kuzungumza kuhusu changamoto wanazopitia, akisisitiza umuhimu wa kutafuta watu sahihi wa kuwaeleza pale wanapokabiliwa na changamoto za afya ya akili. Amesema vijana wanapaswa kutumia fursa zilizopo katika shule, vyuo vikuu na ngazi nyingine za jamii kuzungumzia changamoto zinazowakabili, ili kujenga jamii inayotambua afya ya akili kama sehemu muhimu ya maendeleo ya kizazi cha sasa na kijacho.
Thu, 08 Oct 2026 14:57:40 +0000Max Dowman avunja rekodi
Read the full report from the original source.
RecentlyPep Guardiola kuishuhudia Man City Etihad
Read the full report from the original source.
RecentlyPedro Rodriguez atupa taulo
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Hispania, Pedro Rodriguez, ametangaza kustaafu soka akiwa na miaka 39 baada ya kumaliza safari ya miaka 20 katika mchezo huo.
RecentlyRonaldo ampa kongole Messi
CRISTIANO Ronaldo ameweka pembeni ushindani wake wa muda mrefu na Lionel Messi, akimtumia ujumbe wa heshima baada ya nyota huyo wa Argentina kufunga rasmi ukurasa wake wa miaka 21 akiwa na timu...
RecentlyHigh Court suspends 2026 National Youth Council elections
Read the full report from the original source.
RecentlyQui est Bally Bagayoko, le maire de Saint-Denis qui s'est retrouvé au milieu des étudiants manifestants en France ?
Dans une vidéo qui fait le buzz sur les réseaux sociaux, Bally Bagayoko, maire de la ville française de Saint-Denis, en banlieue parisienne, se tient face aux forces de l'ordre lors d'une manifestation à Paris mardi. Pro
RecentlySénégal-Rwanda : une coopération bilatérale renforcée et une dynamique de diplomatie économique
Read the full report from the original source.
RecentlyEquity Bank Uganda recognises 80 customers during Customer Service Week
Equity Bank Uganda has recognised 80 customers for loyalty, business growth, community work and their long-standing relationship with the bank, as it marked Customer Service Week 2026 under the theme "Going...
RecentlyEU envoy in China to avert trade war
Read the full report from the original source.
RecentlyHELB releases funds for five student loan batches
The board urged students whose batch numbers appear in the latest update to confirm the status of their funds through the HELB student portal
RecentlyDr Tulia drums for the laws to protect health rights for women, children, youth
Read the full report from the original source.
RecentlyLe Rwanda gagne neuf places et réalise la plus forte progression du dernier classement FIFA
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 782 of 1144 · 22861 stories