Unganishwa

Search the region

22846 stories

Uncategorized · CEO East Africa

Under Pressure From all Sides: Is Platinum Credit Rethinking its Funding Model to Stay Sustainable?

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Atwoli Tells Youth to Reject Political Hate as He Praises Ruto’s Leadership

NATIONAL NEWS · 4 hours ago

Recently
Uncategorized · Chimpreports

CHIMP SPORT: Uganda Improve in Latest FIFA Rankings

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Mwangi joins global commission on future of North-South development ties

Latest · Business

Recently
Sports · Issa Michuzi

Kombe la EPL Kutua Tanzania, Guinness Kuwapa Mashabiki Fursa ya Kulishuhudia Dar es Salaam

Mashabiki wa Ligi Kuu ya England nchini Tanzania wanajiandaa kushuhudia tukio la kipekee baada ya Kombe la Ligi hiyo kutua rasmi nchini kwa mara ya kwanza kupitia Guinness, Mdhamini Mkuu wa Bia wa Ligi Kuu ya England. Kombe hilo litawasili nchini Ijumaa, Oktoba 9, 2026, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya saa tatu asubuhi, kabla ya kuzungushwa katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam ili kuwapa mashabiki fursa ya kuliona kwa karibu. Hivyo, kwa mashabiki wa EPL ambao wamezoea kuliona Kombe hilo likikabidhiwa baada ya msimu kumalizika kupitia televisheni, safari hii litakuwa mbele yao na katika jiji lao. Baada ya kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, Kombe hilo litahamia The Super Dome, Masaki, ambako kutakuwa na hafla maalum kwa wageni na mashabiki kupata fursa ya kuliona kwa karibu zaidi na kupiga picha nalo. Akizungumzia ujio wa Kombe hilo, Mkurugenzi wa Ubunifu na Masoko wa Serengeti Breweries Limited (SBL), Henry Esiaba, alisema Guinness inaleta uzoefu wa EPL karibu zaidi na mashabiki wa soka nchini. “Mashabiki wa Tanzania wana mapenzi makubwa na Ligi Kuu ya England na kila wiki wanafuatilia mechi, wanajadili timu zao na kusherehekea pamoja. Safari hii tunataka kuwapa nafasi ya kuona Kombe lenyewe kwa karibu na kuwa sehemu ya tukio hili. Ni fursa kwa mashabiki kupata uzoefu tofauti na ule wanaoupata wanapotazama mechi kwenye televisheni,” alisema Esiaba. Burudani ya soka itaendelea Jumamosi, Oktoba 10, ambapo mashabiki watakutana katika Uwanja wa KMC, Mwenge, kwa Guinness Matchday. Katika tukio hilo, mashabiki watapata fursa ya kushuhudia kwa pamoja mechi za Ligi Kuu ya England kupitia skrini kubwa, ikiwemo mchezo wa Arsenal dhidi ya Leeds pamoja na Manchester United dhidi ya Tottenham Hotspur. Lakini kwa kuwa soka Tanzania lina ladha yake, siku hiyo pia mashabiki watapata nafasi ya kushuhudia Dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga mubashara kupitia skrini kubwa zitakazowekwa katika eneo la tukio. Hiyo itakuwa fursa ya mashabiki wa soka kukutana sehemu moja, kufuatilia mechi za Ligi Kuu ya England na wakati huohuo kushuhudia moja ya mechi zinazovuta hisia kubwa zaidi katika soka la Tanzania. Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kampuni wa SBL, Juanita Mramba, alisema ujio wa Kombe hilo unalenga kuwaleta pamoja mashabiki na wadau wa soka kupitia uzoefu unaounganisha soka la kimataifa na shauku ya mashabiki wa Tanzania. “Soka linawajumuisha watu wengi na Tanzania ni moja ya nchi ambazo mashabiki wake wanaishi kwa karibu sana na mchezo huu. Kupitia ujio wa Kombe la EPL, tunataka mashabiki wapate nafasi ya kuliona kwa macho yao, kupiga picha nalo na kushiriki katika matukio yatakayowakutanisha pamoja. Hii ni nafasi ya kusherehekea soka na mashabiki ambao wamekuwa sehemu muhimu ya utamaduni wa mchezo huu,” alisema Juanita. Mbali na kutazama mechi, mashabiki watakaohudhuria Guinness Matchday watapata pia fursa ya kupiga picha na Kombe la Ligi Kuu ya England, huku wakifurahia burudani na mazingira ya pamoja ya kusherehekea soka. Ujio wa Kombe hilo Tanzania unaifanya Dar es Salaam kuwa sehemu ya ziara maalum ya Kombe la Ligi Kuu ya England katika Afrika Mashariki, huku Guinness ikiendelea kutumia nafasi yake kama Mdhamini Mkuu wa Bia wa Ligi hiyo kuwaleta mashabiki karibu na mchezo wanaoupenda. Kwa siku mbili, Oktoba 9 na 10, macho ya mashabiki wa soka yataelekezwa Dar es Salaam, kuanzia ujio wa Kombe hilo JNIA, safari yake katika maeneo mbalimbali ya jiji, hafla ya Super Dome Masaki hadi Guinness Matchday katika Uwanja wa KMC, Mwenge. Kwa mashabiki wa EPL na soka kwa ujumla, hii ni nafasi ya kuliona Kombe la Ligi Kuu ya England kwa karibu na kusherehekea soka pamoja na mashabiki wengine.

Thu, 08 Oct 2026 03:00:00 +0000
Uncategorized · BBC Afrique

Christa Pike marche désormais après l'échec de son exécution aux États-Unis, a déclaré son avocat à la BBC

Un avocat affirme que la meurtrière de Colleen Slemmer se déplace dans sa chambre d'hôpital après avoir survécu à deux injections mortelles.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Ogamba: Poverty, early sex drive teenage pregnancies among schoolgirls

Education Ministry says it lacks comprehensive data to establish the exact number of learners affected.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Margaret Hamilton, scientist on NASA's Apollo program, dies

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

NMB yaimarisha ujumuishi wa kifedha, yazindua dawati maalumu kwa watu wenye ulemavu

Katika jitihada za kuongeza ujumuishi wa kifedha nchini, Benki ya NMB imezindua Dawati Maalumu la Huduma kwa Wateja Wenye Ulemavu, likiwa na huduma ya mawasiliano ya video inayosaidiwa na wakalimani wa lugha ya alama, hatua inayolenga kuondoa vikwazo vya mawasiliano na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa watu wenye ulemavu. Dawati hilo lililoanzishwa katika Kituo cha Mawasiliano cha NMB litahudumia wateja wenye ulemavu wa kusikia, kuona na viungo. Wateja wanaweza kupata msaada kupitia namba ya simu ya bure 0800 002002, huduma ya video kupitia WhatsApp inayosaidiwa na wakalimani wa lugha ya alama, pamoja na matawi ya NMB nchini. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alisema huduma hiyo inalenga kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata huduma za kibenki kwa heshima na usawa, huku wakilindwa faragha zao na kupunguziwa utegemezi wa watu wengine wanapohitaji msaada. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Nemes Temba, aliipongeza NMB kwa kuanzisha dawati hilo, akisema hatua hiyo itasaidia kupunguza vikwazo vya mawasiliano na kuwawezesha watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika matumizi ya huduma za kifedha nchini.

Thu, 08 Oct 2026 09:00:20 +0000
Uncategorized · Citizen Digital

Woman arrested for allegedly subjecting daughter to FGM in Dandora

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

Kikwete tasks public servants to transfer SHIMIWI Games spirit to workplaces

KILIMANJARO: THE Minister of State in the President’s Office, Public Service Management and Good Governance, Ridhiwani Kikwete, has urged public…

Recently
Uncategorized · Daily News

Envoy Eunju hailed for cementing Tanzania-Korea’s diplomatic,economic ties

Read the full report from the original source.

Recently
Business · Issa Michuzi

TANZANIA YAZINDUA AJENDA YA MIAKA MITANO MAENDELEO YA MAFUNDI,UCHUMI WA UBUNIFU

Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Arusha TANZANIA imezindua Ajenda ya Kitaifa ya Maendeleo ya Mafundi na Uchumi wa Ubunifu, inayolenga kuweka mazingira bora kwa mafundi na wasanii kukuza shughuli zao, kufungua masoko mapya na kuchangia zaidi katika uchumi wa taifa. Aidha kupitia ajenda hiyo, Tanzania inalenga kutengeneza zaidi ya ajira 600,000 na kuzalisha mapato ya dola za Marekani milioni 500 kwa mwaka ifikapo 2032. Akizungumza katika uzinduzi wa ajenda hiyo jijini Arusha,Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania International Tourism Festival, Ibrahim Othman Jama, amesema ajenda hiyo ya miaka mitano inalenga kuunganisha sekta ya sanaa, utamaduni, biashara na utalii ili kuhakikisha kazi za mafundi na wasanii zinakuwa sehemu muhimu ya uchumi wa Tanzania. Amesema ajenda hiyo imejengwa juu ya nguzo sita, ikiwemo kurasimisha, kusajili na kuweka mfumo wa kutambua mafundi na wasanii nchini, pamoja na kutumia teknolojia na mifumo ya kidijitali katika kukuza uchumi wa sekta hiyo. Kwa mujibu wa Jama, nguzo nyingine ni kufungua masoko mapya ndani na nje ya Tanzania, kulinda haki miliki za mafundi na wasanii pamoja na kuendeleza urithi wa vitendo na ubunifu unaotokana na tamaduni mbalimbali za Watanzania. Amesema ajenda hiyo pia inalenga kuunganisha kikamilifu kazi za mafundi na wasanii katika uchumi wa utalii wa Tanzania, akisisitiza kuwa hadithi ya utalii wa Tanzania haiwezi kutenganishwa na hadithi ya ubunifu, sanaa na utamaduni wa Watanzania. Jama amesema kupitia ajenda hiyo, Tanzania inalenga kusajili takribani mafundi 50,000, kuzalisha mapato ya dola za Marekani milioni 500 kila mwaka kutoka katika sekta hiyo na kutengeneza ajira 600,000 katika uchumi wa ubunifu ifikapo mwaka 2032. Amesema malengo hayo pia yamezingatia usawa wa kijinsia na kuongeza nafasi za vijana kushiriki katika uchumi wa ubunifu, akieleza kuwa kundi hilo limekuwa likihitaji fursa zaidi za kuonyesha vipaji, kupata masoko na kujenga maisha kupitia kazi zao. Ameeleza kuwa Tanzania International Tourism Festival ilianzishwa kwa lengo la kujenga majukwaa yanayokutanisha utamaduni, biashara na jamii, huku tamasha hilo likiwa sehemu ya utekelezaji wa dhamira hiyo kwa kuwaunganisha mafundi na wasanii kutoka maeneo mbalimbali nchini na wanunuzi, wawekezaji na wadau wengine. Jama amesema zaidi ya wasanii na mafundi 100 wamepata nafasi ya kushiriki katika tamasha hilo, akibainisha kuwa thamani kubwa ya tukio hilo haiishii kwa washiriki waliopo Arusha bali inapaswa kuonekana katika mabadiliko ya maisha ya mafundi walioko vijijini na kwenye warsha mbalimbali nchini. Amesema mafundi kama washonaji, wachongaji, wachoraji, wasusi na wanaofanya kazi za vyuma wamekuwa wakibeba historia na utamaduni wa Tanzania kupitia kazi zao, lakini mara nyingi hawapati kutambuliwa wala kulipwa kulingana na thamani ya kazi wanazozifanya. Katika hatua nyingine, Jama ameiomba Serikali na wadau wa sanaa kuweka mifumo itakayowawezesha wasanii na mafundi kushiriki katika matukio ya kimataifa ili kupata fursa za kuonyesha kazi zao, kujenga mitandao ya kibiashara na kutafuta masoko nje ya Tanzania. Amesema mabalozi na balozi za Tanzania katika nchi mbalimbali zinaweza kuwa sehemu muhimu ya kufungua fursa hizo kwa kuwaunganisha wasanii na mafundi wa Tanzania na masoko ya kimataifa, huku akisisitiza umuhimu wa BASATA na taasisi nyingine za sanaa katika kuratibu fursa hizo. Ameishukuru Serikali, Serikali ya Mkoa wa Arusha, viongozi wa Wilaya, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), COSOTA, Bodi ya Filamu, BRELA, taasisi za fedha, washirika wa maendeleo na wadau mbalimbali kwa kushirikiana katika kufanikisha tamasha hilo na ajenda hiyo. Amesema katika kipindi cha siku tano za tamasha hilo, Arusha itakuwa mwenyeji wa maonesho ya sanaa, biashara, warsha, mikutano ya kibiashara kati ya wafanyabiashara na wawekezaji (B2B), pamoja na filamu na shughuli zinazolenga kuonyesha utamaduni wa Tanzania. Jama ametoa wito wa kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi, wasanii, mafundi, taasisi za fedha na wadau wa utalii ili ajenda hiyo iweze kutekelezwa na kutoa fursa kwa Watanzania wengi zaidi, hasa vijana, wanawake na jamii zinazotegemea kazi za ubunifu kama chanzo cha kipato. Mgeni rasmi katika uzinduzi wa tamasha hilo, Mkurugenzi Msaidizi wa Sanaa za Ufundi kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bona Leoni Masenge, amewataka vijana na wanawake nchini kutumia vipaji vyao katika sanaa na ubunifu kama fursa ya kujiajiri na kuongeza kipato, badala ya kuuchukulia ubunifu kama njia ya burudani pekee. Masenge amesema sanaa na ubunifu vina uwezo wa kuzalisha ajira na kujenga biashara, hivyo vijana wanapaswa kutumia vipaji walivyonavyo kuanzisha shughuli zinazoweza kuwapatia kipato na kuchangia maendeleo ya familia na jamii. Amesema mtu anayeshona nguo, kufuma, kuchonga, kuchora, kupaka rangi, kutengeneza bidhaa za ngozi, kufua chuma, kubuni mavazi au kuhifadhi mbinu za jadi za sanaa siyo fundi pekee, bali ni mjasiriamali, mbunifu na mtunzi wa utamaduni wa Tanzania.

Thu, 08 Oct 2026 08:51:18 +0000
Uncategorized · BBC Afrique

S'agissait-il de la peste ? Les versions contradictoires concernant la mort d'une technicienne de laboratoire russe

Le décès d'une technicienne de laboratoire russe dans un centre de recherche sur la peste en Sibérie a alimenté les spéculations quant à une possible fuite de données au sein du laboratoire.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Uhuru in Rwanda for DRC peace talks

Latest meeting comes as regional and continental efforts continue to find lasting peace in eastern DRC.

Recently
Business · Daily News

TADB awards 13 SUA students for excellence in agriculture-related fields

MOROGORO: THE Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) has awarded 13 students from Sokoine University of Agriculture (SUA) for outstanding academic…

Recently
Sports · Issa Michuzi

GUINNESS YALETA KOMBE LA LIGI KUU YA UINGEREZA NCHINI TANZANIA

Kombe la Ligi Kuu ya Uingereza limewasili Tanzania, kwa mara ya kwanza, likiashiria kuanza kwa ziara yake ya Afrika Mashariki. Kombe hilo limeletwa na bia ya Guinness, ambayo ni mmoja wa wadhamini wa vinywaji wa Ligi Kuu hiyo kubwa ya soka duniani. Kuwasili kwa Kombe hilo kunaashiria kuanza kwa sherehe za siku mbili zitakazounganisha hadhi ya Ligi Kuu ya Uingereza na utamaduni wa soka Tanzania. Kwa Guinness, kuwasili kwa Kombe hili si suala la kuleta tu moja ya alama zinazotambulika zaidi katika soka duniani, ni kutengeneza tukio ambalo linaunganisha soka la kimataifa na mapenzi, nguvu na utamaduni wa soka la Tanzania. Kuhusu ujio huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Serengeti Breweries Dk. Obinna Anyalebechi alisema: “Ligi Kuu ya Uingereza tayari ina nafasi kubwa katika mioyo na mazungumzo ya mamilioni ya mashabiki wa soka, wakiwemo Watanzania. Kinachofanya tukio hili kuwa tofauti ni kwamba sasa Kombe lenyewe limefika hapa, likikutana na mashabiki mahali ambapo mapenzi yao kwa soka yanaishi. Tunataka kuandaa tukio ambalo lina ladha ya Tanzania na kuipa dunia nafasi ya kuona kinachotokea pale soka la kimataifa linapokutana na nguvu, ubunifu na mapenzi yetu wenyewe kwa mchezo huu.” Kuwasili kwa Kombe hilo pia kumeingia moja kwa moja kwenye utamaduni mkubwa wa soka nchini, huku mashabiki wa Simba SC na Young Africans (Yanga) wakiwa sehemu ya hamasa hiyo. Klabu hizi mbili ni miongoni mwa makundi makubwa zaidi ya mashabiki nchini, huku wengi wao pia wakifuatilia kwa karibu Ligi Kuu ya Uingereza. Mkurugenzi wa Masoko na Ubunifu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Henry Esiaba alisema: “Tanzania ina utamaduni mkubwa sana wa soka, na kulileta Kombe la Ligi Kuu ya Uingereza hapa kumetupa nafasi ya kuona mapenzi hayo kwa karibu. Tanzania ikiwa sehemu ya safari hii ya Afrika Mashariki, tunataka Kombe hili liwe sehemu ya tukio halisi la soka la Tanzania tukio hili liongozwe na mashabiki, simulizi zao na namna wanavyosherehekea ujio wa Kombe hili na mchezo wa soka kwa ujumla.” Kwa jamii ya soka Tanzania, tukio hili pia linaunganisha utamaduni unaokua wa soka nchini na ulimwengu mpana wa soka la kimataifa. Mwakilishi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Aaron Nyanda alisema: “Kuwasili kwa Kombe la Ligi Kuu ya Uingereza kunaonyesha uhusiano mkubwa uliopo kati ya jamii yetu ya soka na soka la kimataifa. Kuanzia hamasa inayozunguka klabu zetu hadi Ligi Kuu ya Uingereza na mashindano ya kimataifa, mashabiki wa Tanzania wanafuatilia soka katika ngazi mbalimbali. Tukio hili linaunganisha mapenzi hayo na kuwapa mashabiki wetu nafasi ya kukutana na soka la kimataifa kwa namna tofauti.” Umuhimu wa tukio hili unaenda zaidi ya soka, kwa kuunganisha michezo, burudani, utamaduni na vijana, huku Tanzania ikipata nafasi ya kuionyesha dunia mapenzi na utamaduni wake wa soka. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, aliyehudhuria tukio hilo alisema: “Michezo huwaleta watu pamoja, hutengeneza fursa kwa vijana na kutoa nafasi kwa nchi kuonyesha utamaduni na utambulisho wake. Kwa hiyo, kuwasili kwa Kombe la Ligi Kuu ya Uingereza si tukio kwa mashabiki wa soka pekee, bali pia ni fursa ya kuonyesha nafasi kubwa ambayo michezo inaendelea kuwa nayo katika jamii yetu.” Baada ya Tanzania, Kombe hilo litaendelea na safari yake nchini Uganda tarehe 11 hadi 13 Oktoba na kumaliza safari yake nchini Kenya. Kuhusu Ligi Kuu ya Uingereza Ligi Kuu ya Uingereza ni miongoni mwa ligi zinazotoa ushindani mkubwa na soka linalovutia zaidi duniani. Kupitia umaarufu wake duniani, ligi hii pamoja na vilabu vyake huwafikia na kuwahamasisha mashabiki, jamii na washirika mbalimbali nchini Uingereza na maeneo mengine duniani. Ligi hiyo inawaleta pamoja watu kutoka katika makundi na asili mbalimbali, na ni mashindano yanayolenga kila mtu, kila mahali. Kwa sasa, mashindano haya yanawafikia watazamaji katika kaya milioni 920 katika nchi 189 duniani.

Thu, 08 Oct 2026 08:39:42 +0000
Uncategorized · The Standard

Court certifies urgent fresh petition challenging Dangote Lamu refinery

The High Court has certified urgent a fresh petition seeking disclosure of key agreements and public commitments surrounding the Sh2.2 trillion Dangote oil refinery in Lamu.

Thu, 08 Oct 2026 11:33:59 +0300
Uncategorized · DW Afrique

Le Bénin réclame à la France 35 biens culturels spoliés

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

CDH launches 2026 guide on labour laws across Africa

Latest · Africa

Recently

Page 792 of 1143 · 22846 stories