Search the region
22818 stories
Manufacturers say peasant farming leaves Uganda’s factories short of raw materials
Manufacturers say peasant farming leaves Uganda's factories short of raw materials KAMPALA – Uganda's manufacturers say the country's reliance on small-scale peasant farming is leaving factories short of raw materials, w
RecentlyKindiki pushes smart farming in bid to boost yields
Deputy President says precision farming will reduce input wastage and improve productivity
RecentlyWAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO UONGEZAJI THAMANI MADINI ADIMU
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema ni muhimu kuendelea kuwekeza katika matumizi ya teknolojia itakayowezesha nchi kuongeza thamani ya madini adimu (critical minerals) badala ya kuyauza katika hali ghafi. Amesema hayo leo (Jumatano, Oktoba 7, 2026) wakati akipokea taarifa ya Utafiti ya uongezaji thamani na uchimbaji wa madini adimu iliyofanywa na wataalamu wa kampuni ya McKinsey ya Uingereza katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Hyatt, jijini London, Uingereza. Kikao hicho kimejadili matokeo ya utafiti huo, pamoja na fursa zinazoweza kutumiwa na Tanzania katika kuongeza thamani ya madini adimu nchini badala ya kuyauza katika hali ghafi. Aidha, wameangalia umuhimu wa matumizia ya teknolojia, uwekezaji na utaalamu katika kujenga uwezo wa ndani wa kuchakata na kuzalisha bidhaa zitokanazo na madini hayo. Dkt. Nchemba amesisitiza umuhimu wa Tanzania kutumia rasilimali zake za madini adhimu kama kichocheo cha uchumi na maendeleo ya viwanda, kwa kuweka mazingira wezeshi yatakayovutia uwekezaji na kuongeza manufaa kwa Taifa. Amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka mkazo katika tafiti, ubunifu na uwekezaji katika sekta ya madini ili kuhakikisha rasilimali hizo zinatumika kuongeza thamani, kutengeneza ajira na kukuza uchumi wa Tanzania.
Wed, 07 Oct 2026 18:21:30 +0000Interoperability, shared infrastructure key to scaling Uganda’s fintech sector, experts say
KAMPALA – Industry experts have urged Uganda's financial technology sector to adopt interoperable systems, shared digital infrastructure and common technical standards for data sharing if it is to move beyond fragmented.
RecentlyWadau Watakiwa Kugeuza Fursa Za Uchumi Wa Buluu Kuwa Biashara Zinazowekezeka
Na Karama Kenyunko Michuzi Tv NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Reuben Kwagilwa, amezitaka serikali, sekta binafsi, taasisi za fedha, watafiti, wabunifu, wajasiriamali na washirika wa maendeleo kushirikiana kufungua fursa za uwekezaji na biashara kwa ajili ya kujenga uchumi endelevu wa buluu katika Bahari ya Hindi ya Magharibi. Kwagilwa amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kubadilisha uwezo wa uchumi wa buluu kuwa fursa endelevu zinazoweza kuwekeza na kuchochea maendeleo, huku akisisitiza umuhimu wa kuunganisha uongozi wa bahari, hifadhi, biashara na uwekezaji. Akifungua Mjadala wa Jukwaa la Biashara kuhusu kufungua fursa za uwekezaji na biashara kwa ajili ya uchumi endelevu wa buluu katika Bahari ya Hindi ya Magharibi, amesema mjadala huo umewaleta pamoja wadau mbalimbali kujadili vikwazo na fursa za kiutendaji zinazokabili biashara katika sekta hiyo. Amesema mjadala huo umejikita katika namna ya kuunganisha rasilimali za bahari na masoko, huku jopo la kwanza likijadili uvuvi, mwani, jongoo wa bahari, uongezaji wa thamani, usimamizi wa baada ya mavuno na fursa za uchumi wa mzunguko. Amesema maeneo hayo yanaweza kuongeza thamani inayobaki kwa wazalishaji na kupunguza taka kupitia ubora wa usindikaji, teknolojia, vifaa vya usafirishaji na viunganishi vya soko. Kwagilwa amesema jopo la pili lilijadili fursa zinazoibukia za bioteknolojia ya buluu, kaboni ya buluu na utalii endelevu wa bahari na pwani, akieleza kuwa maeneo hayo yanaweza kuzalisha bidhaa mpya, huduma na vyanzo vya mapato. Amesema utekelezaji wa fursa hizo unahitaji sayansi, viwango vilivyo wazi, teknolojia inayofaa, hifadhi na ushirikiano kati ya watafiti, jamii, wajasiriamali na wawekezaji. Aidha, amesema jopo la tatu lilijadili ubunifu na ufadhili katika uwekezaji wa uchumi wa buluu, akisisitiza kuwa mawazo hayawezi kutimizwa bila utekelezaji. “Biashara na waendelezaji wa miradi wanahitaji usaidizi ili kuwa tayari kwa uwekezaji. Wafadhili wanahitaji mifano ya mapato inayoaminika, uongozi bora, na hatari zinazoweza kudhibitiwa. Na serikali zinahitaji kutoa mazingira ya biashara yanayotabirika na kuwezesha,” amesema. Amesema ufadhili mchanganyiko, dhamana, mtaji nafuu, ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi pamoja na mbinu nyingine za kugawana hatari zinaweza kusaidia kuziba pengo la ufadhili iwapo zitabuniwa vyema na kuoanishwa na vipaumbele vya kitaifa. Kwagilwa amesema serikali za nchi wanachama zina wajibu wa kutoa mwelekeo wa sera ulio wazi, udhibiti thabiti, takwimu za kuaminika, michakato ya wazi, mipango ya spatial ya bahari, hifadhi za mazingira na jamii pamoja na uratibu kati ya taasisi. Amesema sekta binafsi ina nafasi muhimu katika kuleta ubunifu, ufanisi, maarifa ya soko, mtaji wenye uwajibikaji na mifano ya biashara inayoweza kufanya kazi kwa kiwango kikubwa. “Taasisisi za fedha lazima zisaidie kuunda bidhaa zinazofaa kwa biashara za uchumi wa buluu, ikiwa ni pamoja na biashara ndogo na za kati. Wakati taasisi za utafiti zinapaswa kusaidia kuhamisha maarifa na teknolojia kutoka maabara kwenda miradi ya mfano hadi kwenye matumizi ya kibiashara,” amesema. Kwagilwa amesema kwa Tanzania Bara na Zanzibar, uchumi wa buluu ni sehemu muhimu ya ajenda ya maendeleo ya muda mrefu na umeelezwa katika Dira ya Maendeleo 2050, huku akikaribisha sekta binafsi kuchunguza fursa zilizopo. Amesema wakati Mkataba wa Nairobi ukiingia katika miaka yake mitatu ijayo, ni muhimu kuimarisha uhusiano kati ya uongozi wa bahari, hifadhi, biashara na uwekezaji. “Tujenge uchumi wa buluu wa Bahari ya Hindi ya Magharibi ulio na ushindani na ubunifu, lakini pia unaojumuisha wote, unaohimili mabadiliko ya tabianchi, na unaotegemea matumizi endelevu ya rasilimali za asili,” amesema. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo na Uratibu wa Uchumi Buluu, Wizara ya Uchumi Buluu na Uvuvi Zanzibar, Mondy Muhando, amewataka wadau wa Ukanda wa Bahari ya Hindi ya Kusini Magharibi kuacha kuzungumzia fursa za uchumi wa buluu kama uwezo wa rasilimali pekee, badala yake kuzibadilisha kuwa biashara endelevu zinazowekezeka na kuongeza thamani ya maliasili zilizopo. Amesema changamoto iliyopo si kugundua rasilimali na fursa zilizopo katika ukanda huo, bali namna ya kuzigeuza kuwa biashara zinazoweza kuvutia uwekezaji. Amesema ukanda huo una utajiri mkubwa wa maliasili, ukiwemo mwani, uvuvi, matumbawe, mikoko, bandari, rasilimali za utalii na njia za kimkakati za usafiri wa baharini. “Kwa hiyo, changamoto yetu si kugundua kile tulicho nacho au uwezo tulio nao. Badala yake, changamoto yetu ni jinsi gani tutabadilisha vyote tulivyo navyo kuwa biashara endelevu na zinazowekezeka,” amesema. Muhando amesema mwekezaji haangalii rasilimali pekee, bali huangalia mambo yanayoweza kujenga mnyororo wa thamani, ikiwemo masoko, miundombinu, vibali, vihatarishi na faida inayoweza kupatikana. Amesema fursa za uchumi wa buluu katika ukanda huo zipo katika sekta mbalimbali, zikiwemo uvuvi na ukulima wa viumbe vya majini, mwani, uhafidhina wa viumbe vya baharini, utalii endelevu wa pwani, bandari na usafirishaji, ubadilishaji wa taka kuwa thamani pamoja na kaboni buluu. “Hivyo tunapaswa kuacha kuonyesha tu fursa tulizonazo, badala yake tuzichukue fursa hizi pamoja na mifumo ya biashara, fedha, masoko, na utawala bora ili kutengeneza biashara zinazowekezeka,” amesema. Aidha, Muhando amesema dhana ya uchumi mzunguko inapaswa kutumika katika kuendeleza uchumi buluu kwa kubadili namna rasilimali zinavyotumika, ambapo taka inaweza kuwa malighafi ya kutengeneza bidhaa nyingine yenye thamani. Amesema uhifadhi wa mazingira haupaswi kuonekana kama kitu kinachoshindana na uwekezaji, bali vitu hivyo vinapaswa kwenda sambamba katika kuendeleza uchumi wa buluu.
Wed, 07 Oct 2026 18:14:30 +0000‘No leadership vacuum’: Kalonzo welcomes Uhuru’s resignation, says Ukombozi name reserved
Read the full report from the original source.
RecentlyCowrywise crosses 1 million stock trades as retail investing grows
Read the full report from the original source.
RecentlyUganda, South Sudan trade nears $800m as Kampala forum targets barriers
KAMPALA – Trade between Uganda and South Sudan has averaged between $700m and $800m a year in recent years, a senior Ugandan diplomat has said, as the two neighbours prepare to...
RecentlyEbola : le premier cas de décès au Kenya inquiète en RDC
Read the full report from the original source.
RecentlyTRAMEPRO YATOA WITO WA KUJENGA HISTORIA YA UTU, AMANI NA MAENDELEO
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam, Oktoba 7, 2026 Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania (TRAMEPRO) limeungana na Watanzania na jamii ya kimataifa kumkumbuka Askofu Mkuu Desmond Mpilo Tutu, aliyezaliwa Oktoba 7, 1931 nchini Afrika Kusini na kufariki dunia Desemba 26, 2021 akiwa na miaka 90. Tutu, aliyekuwa kiongozi wa dini na mtetezi wa haki za binadamu, amani na maridhiano, alitunukiwa Tuzo ya Nobel ya Amani mwaka 1984 kutokana na mchango wake katika mapambano dhidi ya Apartheid nchini Afrika Kusini. Katika kumbukizi hiyo, TRAMEPRO imesema urithi wa Tutu unapaswa kuwa somo kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutumia nafasi na taaluma walizonazo kuleta mabadiliko na kuacha alama kwa vizazi vijavyo. Shirika hilo limetumia pia kumbukizi hiyo kuhimiza Tanzania kutumia nafasi yake katika majukwaa ya kimataifa, ikiwemo Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), kutangaza fursa zilizopo katika afya, mazingira, utafiti na Tiba Asili. TRAMEPRO imesema Tanzania ina utajiri wa mimea tiba na maarifa ya jadi ambayo yanaweza kuchangia katika afya, utafiti, uhifadhi wa mazingira na uchumi, lakini maendeleo ya sekta hiyo yanapaswa kuzingatia usalama wa watumiaji, utafiti, ushahidi, ubora wa bidhaa, maadili ya kitaaluma na uhifadhi wa bioanuwai. Aidha, shirika hilo limewataka wataalamu wa Tiba Asili kuwa waaminifu kwa wagonjwa, kuepuka madai yasiyothibitishwa na kushirikiana na watafiti pamoja na wataalamu wengine wa afya. TRAMEPRO pia imewataka viongozi wa dini kuendelea kuwa sauti ya amani, utu na maridhiano, huku vyombo vya habari vikihimizwa kuelimisha jamii kuhusu afya, mazingira na matumizi salama ya Tiba Asili. Kwa upande wa wananchi, shirika hilo limesisitiza umuhimu wa kutambua kuwa afya ya binadamu inahusiana moja kwa moja na afya ya mazingira, hivyo kulinda misitu, maji, udongo na mimea tiba ni kulinda maisha ya kizazi cha sasa na kijacho. TRAMEPRO imesema kumbukizi ya Desmond Tutu inapaswa kuwa changamoto kwa kila mtu kufanya jambo litakalobaki kuwa na thamani katika jamii. “Umoja wetu ndiyo nguvu yetu. Huduma yetu ndiyo alama yetu. Matendo yetu ndiyo historia yetu.” BONIVENTURA MWALONGO. Katibu Mkuu & Mtaalamu wa Tiba Asili TRAMEPRO
Tue, 06 Oct 2026 21:00:00 +0000Audio — Journal 17:00 UTC (07.10.26)
To play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video
RecentlyKabudi avitaka vyama kutumia baraza kutatua tofauti
Read the full report from the original source.
RecentlyMinister calls for greater investment in girls as Tanzania prepares to mark International Day of the Girl Child
DAR ES SALAAM: MINISTER for Community Development, Gender, Women and Special Groups, Dkt. Dorothy Gwajima, has called for increased investment…
RecentlyUganda Turns to Domestic Investors as Public Debt Rises
Read the full report from the original source.
RecentlyRussia: WHO not able to 'fully' assess plague situation
Read the full report from the original source.
RecentlyTRAMEPRO YATOA WITO WA USHIRIKIANO KATIKA WIKI YA HUDUMA 2026
Katibu Mkuu wa Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania (TRAMEPRO), Boniventura Mwalongo, amewataka wataalamu wa Tiba Asili nchini kuendelea kutoa huduma kwa uadilifu, weledi, huruma na kuzingatia usalama wa wananchi. Akizungumza katika Wiki ya Huduma kwa wateja 2026, Mwalongo amesema huduma ni dhamana ya pamoja inayohitaji kujitolea, kusikiliza, kuheshimiana na kuwajibika, akisisitiza kuwa kila mgonjwa anayemtafuta mtaalamu wa Tiba Asili huja akiwa na imani na matumaini ambayo yanapaswa kulindwa. Amesema wataalamu wanapaswa kuzingatia usafi, ubora wa dawa, maadili ya taaluma na usalama wa wagonjwa, huku wakiepuka ulaghai, ramli, ushirikina na ahadi zisizo na msingi wa kitaalamu. Mwalongo amesisitiza pia uhusiano kati ya afya ya binadamu na afya ya mazingira, akiwataka wataalamu wa Tiba Asili kuwa mabalozi wa uhifadhi wa misitu, mimea tiba, maji na bioanuwai. Aidha, ametoa wito kwa wanachama, wataalamu wa afya, watafiti, taasisi za elimu, vyombo vya habari na wadau wa mazingira kuimarisha ushirikiano katika utafiti, elimu, usalama wa dawa, Tiba Asili na uhifadhi wa mazingira. “Tusijenge Shirika la viongozi pekee; tujenge Shirika la wanachama wote. Ushirikiano wetu ndio msingi wa kulifanya Shirika liwe na mchango mkubwa katika afya, mazingira na maendeleo ya jamii,” amesema. Amesisitiza kuwa Wiki ya Huduma kwa wateja isiishie katika maadhimisho pekee, bali iwe mwanzo wa utamaduni wa kudumu wa kuhudumia, kusaidiana, kuheshimiana, kulinda afya na kutunza mazingira. “Huduma ni wajibu wetu, upendo ni msingi wetu, afya na mazingira ni dhamana yetu.” BONIVENTURA MWALONGO Katibu Mkuu & Mtaalamu wa Tiba Asili – TRAMEPRO
Wed, 07 Oct 2026 17:17:27 +0000WHO releases first global guidelines on child obesity as cases surge
Read the full report from the original source.
RecentlyRaila Odinga's family calls for political ceasefire ahead of first anniversary
Read the full report from the original source.
RecentlyGovt steps up safety against cybersecurity and data privacy
Read the full report from the original source.
RecentlyMu rukiko abunganira Victoire Ingabire basabye umucamanza kububaha
Aba banyamategeko binubiye icyo bise kwihanangirizwa no gucibwa amafaranga bya hato na hato mu gihe cy'urubanza, icyo basanga ari ukubima uburenganzira bwo kunganira uko bikwiye uregwa.
RecentlyPage 805 of 1141 · 22818 stories